Mkasa wa Afande Mwasifiga alivyopoteza kazi baada ya kubishana na hayati Rais Magufuli

Mkasa wa Afande Mwasifiga alivyopoteza kazi baada ya kubishana na hayati Rais Magufuli

Walugaluga ni watu wa makabila tofauti waliofikia sehemu fulani, hawajui hata lugha ya pale vizuri, ndiyo maana wanaitwa "walugaluga".

Hao Walugaluga original walichukuliwa jeshi la Wanyamwezi kutoka makabila tofauti kama Wakonongo, Wanubi etc wakalowea kwa Wanyamwezi.

Sasa hawa walugaluga wa siku hizi nao hawajui Kiswahili wanatuharibia lugha yetu.
Hawa watoto wa siku hizi tuwaite "wagoloko"
 
Karibu JF!!
If you ask me, kati ya kuheshimiwa na watu na uhuru wangu wa kujieleza, nachagua uhuru wangu wa kujieleza.

Heshima nyingine za watu zinakufunga usiweze kujieleza kwa uhuru wako.

Na kama mtu hanielewi, hanielewi tu, sihitaji heshima yake.

I am here to shine my light, I am not here to make friends.

Zaidi, nafikiri hoja nzima ya kumtazama mtu badala ya hoja zinazotolewa ni ujinga.

Watanzania wengi sana, kwa kuangalia uzi huu, hawawezi kuangalia hoja bila kumuangalia mtoa hoja.

Wanaishia kufanya ad hominem logical fallacy kumjadili mtoa hoja badala ya hoja.

Mtu anaishia kusema "kuna mtu nilikuwa namujeshimu sana lakini hapa katoa mashudu matupu".

Kauli hii inaonesha matatizo mengi ya Watanzania.

Hatutaki kujadili hoja. Tunamjadili mtoa hoja.

Hatutaki kuwa wawazi, huyo mtu nani? Mashudu yake yapi? Kwa nini mashudu?

Yani hata JF kwenye anonimity pamekuwa sehemu za "kuna mtu" bila kumtaja huyo mtu na "mashudu" bila kuelezea yapi, kwa nini ni mashudu. Hawa watu hawawezi kutetea hoja zao.

Dalili za maongezi ya watu wajinga na waoga ambao hawawezi kujadili hoja toe by toe.
 
Leta hapa death certificate ya Afande Mwasifiga, wacha kuleta "habari za nasikia"

Utakufa wewe UCD ukaungane na mungu wenu Magufuli na utaniacha
Kufa ni kawaida kama ulivyozaliwa. Vipi wewe unaogopa kufa? Tusipokufa basi hata wakuzaliwa hatakuwepo hiyo ndio maana ya "reproduction"
 
Link pekee nimeikuta Facebook.

Magufuli anabishia hospitali kuwekewa lift kweli kabisa?


View: https://www.facebook.com/share/v/14Rx9GUaTx/

Siku hizi nimeanza kuzi download hizi naziweka kwenye server yangu ya nyumbani maana nyingine wanaziondoa Youtube.

Ile clip inatakiwa kuwekwa kwenye somo la kuwafundisha viongozi wasijibizane na watendaji sana maswali ya hapo kwa papo kwa sababu watendaji wanaoelewa mengi sehemu zao za kazi na rais akija kichwakichwa anaweza kuadhirika sana.

Magu alikuwa Mbabe sana .
 
Wahaya na wanyakyusa ni Walewale tu. Sema tu wahaya siyo.jeuri kama nyakyusa
Wewe utakuwa muhaya bila shaka. Nchi hii kama kuna kabila linakngoza kwa sifa (zingine zikiwa za kijinga) ni watu wa Bukoba.

Kuna uzi huku jamaa aliandika(ga) miaka mingi imepita eti "kufika mwaka 2012 Bukoba kuipiku dubai kwa miundombinu." Hadi leo hii imepita miaka 12 bado Bukoba hata stendi ya maana hakuna
 
Leo nimekumbuka mkasa mmoja uliotokea enzi ya awamu ya tano!

Ilikuwa ni Julai 16 ya mwaka 2019 Jumanne tulivu tu ndani ya jiji la Mwanza, ghafla Gereza Kuu la Butimba likapata ugeni wa Amiri Jeshi Mkuu, Rais Magufuli.

Basi baada ya maofisa wa juu kutonywa kuwa Rais angeweza kufika pale, wakajipanga kumpokea.

Punde si punde, hayati Magufuli akawasili na bila kupoteza muda akaomba kuongea na wafungwa ili asikie matatizo yao kama ilivyoada yake.

Wafungwa walifurahi sana kumuona Rais, basi wakaambiwa watoe kero zao. Wakazungumza wengi mpaka ilipofika kwa mfungwa mmoja aliyeamua kumwaga mchele kwenye kuku wengi.

Mmoja ya wafungwa waliopata nafasi ya kuongea na hayati Magufuli alikuwa ni Kalikenye Thomas Nyamboge, mfungwa mwenye ulemavu wa ngozi, aliyekuwa anatumikia kifungo cha Miaka 30 jela.

Mfungwa Kalikenye yeye akatoa kero yake kuhusu Afisa Usalama wa Gereza hilo, Afande Mwasifiga kuwa anashirikiana na wafungwa wengine kwa kuwapa simu waongee na watu wa nje ya Gereza kinyume na utaratibu uliowekwa lakini pia anashirikiana na baadhi ya wafungwa wenye hela kuingiza simu kwenye Gereza hilo la Butimba.

Mfungwa wa miaka 30 Jela, Bwana Thomas Kalikenye akaendelea kumsagia kunguni Afande kuwa, msako ukipita simu hazionekani na wao akina Thomas wasiohusika na kuingiza simu wanamwagiwa vitu vyao kama vile Karanga, Sukari, Sabuni na saa nyingine vinachukuliwa kwa nguvu na team ya Afande Mwasifiga.

Ghafla hayati Magufuli anabadilika na kuuliza yuko wapi huyo Afande Mwasifiga? Afande anatokea na kupiga saluti na kuanza kujibu shutuma.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Afande Mwasifiga anaanza kubishana na Rais Magufuli kuhusu suala la uwepo wa simu kwa wafungwa katika Gereza la Butimba.

Afande Mwasifiga katika ubishani wake akamuambia Rais Magufuli, “huyu alitaka kuniinua” Maneno hayo yalimchefua sana Rais.

Magufuli akamwambia afande kuwa”inaonekana una dharau sana wewe” akawa ameshakasirika huku wasaidizi wa Rais wakimtonya Afande Mwasifiga aombe msamaha kwa Rais. Kweli akaomba msamaha huku akipiga saluti, lakini haikusaidia kitu.

Kama utani Rais Magufuli akamwambia ninaweza nikang’oa hizo nyota zako hapo (huyu Afande alikuwa na nyota mbili).

Basi Rais akaachana nae akamalizia kuongea na wafungwa kama alivyopanga ana akatoa agizo kwa Mkuu wa Gereza la Butimba, ole wake mfungwa yoyote aliyetoa kero anyanyaswe, basi atachukua hatua mara moja. Akamaliza akaaga akaondoka zake.

Usiku wake, Afande Mwasifiga akapokea maelekezo kuwa ameondolewa Gereza la Butimba na kupewa uhamisho wa kwenda Ukerewe.

Sambamba na hilo, akavuliwa nyota yake moja alitoka kuipata siku chache kabla ya kubishana na Rais. Hivyo basi akabaki na nyota moja tu badala ya mbili kama hatua ya kinidhamu iliyochukuliwa dhidi yake.

Kama haitoshi, baada ya miezi sita akiwa katika kituo chake kipya cha kazi, akastaafishwa kwa maslahi ya umma na utumishi wake ndani ya Jeshi la Magereza ukawa umefikia kikomo.

Ikumbukwe alipewa miaka mitano ya ziada jeshini baada ya kupewa nyota ya pili kabla ya kuipoteza nyota hiyo kutokana na kubishana na Rais.

Ukawa ndio mwisho wa Afande Mwasifiga, aliyepata kuwa Mkuu wa Usalama ndani ya Gereza la Butimba na waliopata kufanya nayr kazi wanakwambia alikuwa ni mjivuni, kiburi kwelikweli.

Kwasasa amerudi kwao Mbeya akiwa ni mkulima akiendeleza maisha baada ya kustaafishwa kwa maslahi ya Umma!View attachment 3164402
Wabongo bana. So point yako nini mkuu
 
Aliwaweka watu jela kama Rugemalira, Kitilya wa TRA, Mwaimu wa NIDA. Akapora mapesa ya wafanya biashara wengi benki.

Wewe pimbi ni masikini kajamba nani huwezi juwa kwa vile hukuwa na frdha benki
yaan alichukua pesa bila sababu ? huyo Rugemalila mm namjuaa binafsi nje na ww unamsoma na kumuona kweny Tv , alikuwa mpigaj sana acha mengine tusiyataje humu , hao walioporwa pesa bank ni wale walipiga pesa za serikali , mf hospital ya mbagala inayojengwa ss hv ilitolewa pesa kitambo sn enz za Jakaya ila watu walipiga zile na kukimbia wachache walikamatwa pesa zikachukuliwa.

HV UNAEZA NTAJIA TAJIR AMBAYE HAJAIBIA SERIKALI HAPA TANZANIA ?

KIPIND JPM ANAINGIA MADARAKAN UNAKUMBUKA YALE MADENI YA KODI ALIKUWA ANAYATAJA ? ULIKUWA HUNA RADIO YAKO YA ANTENA KIPIND HIKO ?

UNAHITAJ MAOMBEZ UNASHABIKIA UJINGA UNAOUJUAVKIUNDANI ILA UMECHAGUA KUWA MNAFIK
 
Back
Top Bottom