Mkasa wa Afande Mwasifiga alivyopoteza kazi baada ya kubishana na hayati Rais Magufuli

Mkasa wa Afande Mwasifiga alivyopoteza kazi baada ya kubishana na hayati Rais Magufuli

Kes
yaan alichukua pesa bila sababu ? huyo Rugemalila mm namjuaa binafsi nje na ww unamsoma na kumuona kweny Tv , alikuwa mpigaj sana acha mengine tusiyataje humu , hao walioporwa pesa bank ni wale walipiga pesa za serikali , mf hospital ya mbagala inayojengwa ss hv ilitolewa pesa kitambo sn enz za Jakaya ila watu walipiga zile na kukimbia wachache walikamatwa pesa zikachukuliwa.

HV UNAEZA NTAJIA TAJIR AMBAYE HAJAIBIA SERIKALI HAPA TANZANIA ?

KIPIND JPM ANAINGIA MADARAKAN UNAKUMBUKA YALE MADENI YA KODI ALIKUWA ANAYATAJA ? ULIKUWA HUNA RADIO YAKO YA ANTENA KIPIND HIKO ?

UNAHITAJ MAOMBEZ UNASHABIKIA UJINGA UNAOUJUAVKIUNDANI ILA UMECHAGUA KUWA MNAFIK
Kwa nini Mahakama kwa miaka yote ya Urais wa Magufuli ilishindwa kumkuta na hatia Rugemalira kama kweli alikuwa ni mpigaji ??

Umaskini wenu na Magufuli wenu usiwe chanzo cha kuwachukia wenye akili na utajiri wao.
 
We ulijuaje ilikuwa jumanne tulivu tu?
Uliskia wapiii??? 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Wewe hujui tofauti ua "uamini" na "huamini".

Huwa siwaamini watu wasiojua kuweka h kwenye sehemu inayotakiwa katika Kiswahili.

Pamoja na wanaochanganya l na r.

Huna hata lugha ya kuweza kufanya mjadala na mimi.

Hawa watu wengi ni Walugaluga wasiojua hata Kiswahili, siwezi kufanya nao mjadala wa kimantiki.
Na kuna mazuzu bado wanakuona great thinker kwa huu utumbo.
Hapo umetumia logic fallacy gani!? au ndio logic yenyewe.
Hapo unajadili hoja au mtoa hoja!? na wewe tukuandikie aina ya fallacy great thinker!?
 
Mimi mtu asiyejua tofauti ya zambi na dhambi siwezi kufanya mjadala naye wa kimantiki.

Kama hajui tofauti ya zambi na dhambi kiswahili atajuaje logical fallacy kilatini?

Kutojua tofauti ya zambi na dhambi ni ishara ya umbumbumbu na mimi sitaki mijadala na mbumbumbu.
Mkuu kwaiyo asingemtumbua ndio angeendelea kuishi ama
 
Magufuli kajitapa kuvua watu manyota lakini na yeye kavuliwa uhai hakuweza kuzuia kuvuliwa uhai.

Cheo ni dhamana, usinyanyase watu kwa cheo.

Najua wewe ngumbaru huwezi kuelewa somo, uwezo huo wa juelewa huna kwa sababu wewe guluguja huna ubongo wala uti wa mgongo.

Ila kuna watu wataelewa.
Kwahiyo ukiwa kiongozi hutakiwi kumwajibisha mtu ili usife?
 
Huwezi kujuwa kwa vile wewe siyo ndugu wa Ben Saanane au Azory Gwanda au ndugu ya walionyang'anywa fedha zao na task force
Hitler dunia nzima inajua aliyoyafanya, sasa kumbe huyo Magufuli hata dunia haimtambui kwa hayo maovu halafu ndio useme hata Shetani anamuogopa?
 
Kes

Kwa nini Mahakama kwa miaka yote ya Urais wa Magufuli ilishindwa kumkuta na hatia Rugemalira kama kweli alikuwa ni mpigaji ??

Umaskini wenu na Magufuli wenu usiwe chanzo cha kuwachukia wenye akili na utajiri wao.
Vitu vingine haviitaj akil nying piga mahesabu vyanzo vyake vya mapato vs matumizi yake , unajuww watu wangese km ww ndo mnatunza Hawa wabadhilifu wanapambanaa kuharibu mifumo ya elimu ili watoto wake mtaani wawaajili kwenye viwandq au mashamba Yao Kwa mshahara wa mbuzi

Sa100 ametoa pikipiki nchi nzima , nikuulize swali zile pesa zimetoka wap ? Je bunge limehoji ? Taasisi ya mapato imetoka kauli yoyote kutaka kujua pesa unatoka wap ? kesho atakuja kiongozi makin atalivalia njuga hili swala na mtasema ni chuki kumbe hili swala lilipaswa kuchukuliwa hatua mapema tu

Hao matajir wamehusika kwenye kuhihujumu nchi Kwa miaka ming tu , mf walificha mafuta yote ya kula na ya kuendesha vyombo vya moto lengo likiwa kupandisha bei hiyo bidhaa , hii kwako ilikuwa sw ? hao wafanya biashara wamekuwa hawalipi Kodi na kuingiza mizigo Yao kwa njia za PANYA na serikali inqjuq ila walishikwa , wajinga kama ww unakuja na hoja zako kuwa ana ugomvi mq mqtajiri

Muda mwingine tuache uswahili , hili narq ili lipige hatua lzm tudeql na Hawa matajir maana ndo kikwazo Kwa nchi yetu
 
Nitajia mhaya jeuri.

Mi nakutajia nyakyusa.
1.sugu
2. Tulia
3. Mwambukusi.
4. Wachungaji na mashekh sijui akina nani

5. Marafiki na.maboss zangu maeneo ya kazi
Kwenye siasa Cfahamu ,Maana wao wanapenda vyeo mfano kwenye taasisi za elimu,Mabenki mtaani ...Mm nachukulia sifa zao zinapitiliza zinakuwa dharau
 
Hili an
Leo nimekumbuka mkasa mmoja uliotokea enzi ya awamu ya tano!

Ilikuwa ni Julai 16 ya mwaka 2019 Jumanne tulivu tu ndani ya jiji la Mwanza, ghafla Gereza Kuu la Butimba likapata ugeni wa Amiri Jeshi Mkuu, Rais Magufuli.

Basi baada ya maofisa wa juu kutonywa kuwa Rais angeweza kufika pale, wakajipanga kumpokea.

Punde si punde, hayati Magufuli akawasili na bila kupoteza muda akaomba kuongea na wafungwa ili asikie matatizo yao kama ilivyoada yake.

Wafungwa walifurahi sana kumuona Rais, basi wakaambiwa watoe kero zao. Wakazungumza wengi mpaka ilipofika kwa mfungwa mmoja aliyeamua kumwaga mchele kwenye kuku wengi.

Mmoja ya wafungwa waliopata nafasi ya kuongea na hayati Magufuli alikuwa ni Kalikenye Thomas Nyamboge, mfungwa mwenye ulemavu wa ngozi, aliyekuwa anatumikia kifungo cha Miaka 30 jela.

Mfungwa Kalikenye yeye akatoa kero yake kuhusu Afisa Usalama wa Gereza hilo, Afande Mwasifiga kuwa anashirikiana na wafungwa wengine kwa kuwapa simu waongee na watu wa nje ya Gereza kinyume na utaratibu uliowekwa lakini pia anashirikiana na baadhi ya wafungwa wenye hela kuingiza simu kwenye Gereza hilo la Butimba.

Mfungwa wa miaka 30 Jela, Bwana Thomas Kalikenye akaendelea kumsagia kunguni Afande kuwa, msako ukipita simu hazionekani na wao akina Thomas wasiohusika na kuingiza simu wanamwagiwa vitu vyao kama vile Karanga, Sukari, Sabuni na saa nyingine vinachukuliwa kwa nguvu na team ya Afande Mwasifiga.

Ghafla hayati Magufuli anabadilika na kuuliza yuko wapi huyo Afande Mwasifiga? Afande anatokea na kupiga saluti na kuanza kujibu shutuma.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Afande Mwasifiga anaanza kubishana na Rais Magufuli kuhusu suala la uwepo wa simu kwa wafungwa katika Gereza la Butimba.

Afande Mwasifiga katika ubishani wake akamuambia Rais Magufuli, “huyu alitaka kuniinua” Maneno hayo yalimchefua sana Rais.

Magufuli akamwambia afande kuwa”inaonekana una dharau sana wewe” akawa ameshakasirika huku wasaidizi wa Rais wakimtonya Afande Mwasifiga aombe msamaha kwa Rais. Kweli akaomba msamaha huku akipiga saluti, lakini haikusaidia kitu.

Kama utani Rais Magufuli akamwambia ninaweza nikang’oa hizo nyota zako hapo (huyu Afande alikuwa na nyota mbili).

Basi Rais akaachana nae akamalizia kuongea na wafungwa kama alivyopanga ana akatoa agizo kwa Mkuu wa Gereza la Butimba, ole wake mfungwa yoyote aliyetoa kero anyanyaswe, basi atachukua hatua mara moja. Akamaliza akaaga akaondoka zake.

Usiku wake, Afande Mwasifiga akapokea maelekezo kuwa ameondolewa Gereza la Butimba na kupewa uhamisho wa kwenda Ukerewe.

Sambamba na hilo, akavuliwa nyota yake moja alitoka kuipata siku chache kabla ya kubishana na Rais. Hivyo basi akabaki na nyota moja tu badala ya mbili kama hatua ya kinidhamu iliyochukuliwa dhidi yake.

Kama haitoshi, baada ya miezi sita akiwa katika kituo chake kipya cha kazi, akastaafishwa kwa maslahi ya umma na utumishi wake ndani ya Jeshi la Magereza ukawa umefikia kikomo.

Ikumbukwe alipewa miaka mitano ya ziada jeshini baada ya kupewa nyota ya pili kabla ya kuipoteza nyota hiyo kutokana na kubishana na Rais.

Ukawa ndio mwisho wa Afande Mwasifiga, aliyepata kuwa Mkuu wa Usalama ndani ya Gereza la Butimba na waliopata kufanya nayr kazi wanakwambia alikuwa ni mjivuni, kiburi kwelikweli.

Kwasasa amerudi kwao Mbeya akiwa ni mkulima akiendeleza maisha baada ya kustaafishwa kwa maslahi ya Umma!View attachment 3164402
Andiko zuri ,ila lipo kimkakati ,kwamba mtu flani akitimiza majukum na kwa sababu mtu flani hajapenda atakuondolea vyeo vyako sio ,vyeo unaweza chukua cha msingi tunaishi, interview ya uyu bwana niliiangalia vizuri , sikuona kosa ,na kumbuka JPM alikua na shida sana kuleta vitisho hasa kwa hawa maafisa vyombo vya ulinzi , hata kule songwe au ukanda ule wakati wa ziara moja hivi ,alisikika akimwambia afisa mmoja kwamba akiamua anafikili hivyo vyeo atakua navyo ,clip ipo you tube.
 
Na kuna mazuzu bado wanakuona great thinker kwa huu utumbo.
Hapo umetumia logic fallacy gani!? au ndio logic yenyewe.
Hapo unajadili hoja au mtoa hoja!? na wewe tukuandikie aina ya fallacy great thinker!?
Great thinker ni tusi kwangu.

Wewe bado hujui tofauti ya "umetumia logic fallacy" na "umetumia logical fallacy".

Jifunze Kiingereza kwanza kabla ya kubishana na mimi.
 
Mkuu kwaiyo asingemtumbua ndio angeendelea kuishi ama
Wapi nimesema hivyo?

Logical non sequitur fallacy.

Point kubwa kwamba cheo ni dhamana na wote tutakufa, tuache kujimwambafy kwa cheo kuwaambia watu "unanijua mimi nani, nitakuvua nyota" ni ugangwe wa kishamba ambao unamuonesha rais anayependa kujionesha yeye yuko juu kuliko kufuata haki na kuchunguza tatizo kimantiki.

Hii approach inanyima taifa hata nafasi ya kujua vizuri tatizo, pale kulikuqa na fursa ya kujua matatizo ya kinfumo na kuyatatua kqa nchi nzima, lakini rais kaishia kumvua nyota mtu mmoja tu, hata kama mtu huyo kakosea rais naye kakosea.

Kwa nini somo hili dogo linakuwa gumu sana kuelewa nyie watu?
 
Wewe hujui tofauti ua "uamini" na "huamini".

Huwa siwaamini watu wasiojua kuweka h kwenye sehemu inayotakiwa katika Kiswahili.

Pamoja na wanaochanganya l na r.

Huna hata lugha ya kuweza kufanya mjadala na mimi.

Hawa watu wengi ni Walugaluga wasiojua hata Kiswahili, siwezi kufanya nao mjadala wa kimantiki.
Jf huwa ipo na watu ajabu sana ,ili sio jukwaa lakufundisha mwandiko ,mbona mchina mnampa kazi tz hajui lugha yenu na project zinaenda ,mtu akijibu kwa kukosoa lugha yako ambayo wengi tunaizungumza tu kisa ni lugha mama ,ipo shida gani ,why usifungue jukwaa la kufundisha lugha tajwa wanaotaka waje, bali wajimwambafai kwenye majukwaa ya watu walioyanzisha kwa dam na jasho, pole mkuu acha jibizana na upeo mdogo
 
Jf huwa ipo na watu ajabu sana ,ili sio jukwaa lakufundisha mwandiko ,mbona mchina mnampa kazi tz hajui lugha yenu na project zinaenda ,mtu akijibu kwa kukosoa lugha yako ambayo wengi tunaizungumza tu kisa ni lugha mama ,ipo shida gani ,why usifungue jukwaa la kufundisha lugha tajwa wanaotaka waje, bali wajimwambafai kwenye majukwaa ya watu walioyanzisha kwa dam na jasho, pole mkuu acha jibizana na upeo mdogo
Mchina kama hajui lugha yetu ni sawa kwa sababu si yake.

Ila Mchina kama hajui lugha yake hiyo ni alama hajaelimika.

Huelewi wapi?
 
Back
Top Bottom