Mkasa wa Afande Mwasifiga alivyopoteza kazi baada ya kubishana na hayati Rais Magufuli

Mkasa wa Afande Mwasifiga alivyopoteza kazi baada ya kubishana na hayati Rais Magufuli

Hakuna haki ya "naweza kukuvua nyota mimi" hiyo ni show ya kibabe tu.

Ila wabongo wengi ndicho mnachopenda, mkiona show za kibabe ndiyo mnaita haki.

Wabongo wengi ni sadists, na Magufuli mlimpenda sana kwa sababu alikuwa Sadist In Chief.

Hata kama Afande alikosea, rais angeweza kumuadhibu kwa kufuata due process si kwa kuonesha umwamba wa summary execution.
kwa katiba ya wabongo Rais ana mamlaka ya kumpandisha/Kumshusha cheo askari yeyote bila kuhitaji justification yoyote.

Tukirudi Gerezani it seems ya kwamba askari husika ni kweli alikuwa akiumiza wafungwa.. Kwahivyo tutende haki bila kukiogopa kifo!

Kufa tutakufa tu!
 
Binafsi kwa mtazamo wangu Kuna watu wakipewa mamlaka hugeuka kua MA GODFATHER.

Afande alikua mtu jeuri na mwenye kunyanyasa wafungwa na alikua na mtandao mkubwa na mpana.

Real life story.
Kuna ndugu yangu alipata kesi ya mauaji so AKAWA gereza moja gumu mkoa wa Tabora..Enzi za utawala wa mzee Benja

Siku moja kiongozi mkubwa alitembelea gerezani wakapewa nafasi wameelezea kero na shida zao ndugu yangu akanyoosha mkono na kuanza kueleza..

Yaan mahindi yalikua yanakobolewa na kwenda kuuzwa wao wanapikiwa mapumba. Alieleza mambo mengi Sanaa yalivyo kua hayaendani na haki za wafungwa

Viongozi baada ya kuondoka maaskari walimpiga Sana na kumvunja mguu mmoja kumbe ki Siri Siri aliachiwa code akipata tatizo ajulishe kipenyo mmoja

All in all,
After that saga alitibiwa vizuri na alipewa uangalizi wa Vvip AKIWA gerezani na wale askari walio mpiga walishuhurikiwa na akaanza kuogopewa na maaskari walio wengi pia welfare za gerezani zilifanyiwa some improvement

Alitumikia gerezani kwa miaka 7 na Alikujaga kutoka kwenye utawala wa kikwete mwanzoni kwa msamaha wa Raisi (prerogative of mercy) yupo uraiani Sasa.
Tatizo la Watanzania wengi ni sadists. Unaweza kukuta Magereza wanaonea watu ki sadist, lakini hata rais anayekuja kuangalia kero za wafungwa na yeye badala ya kumulika ubaya wa sadism kwa kufuata due process kuhukumu maafisa wa Magereza, anawakomoa wale Magereza ki sadist kwa summary execution.

Na Watanzania wengi wanafurahia wale Magereza kukomolewa ki sadist, kwa sababu wao wanaona wale Magereza wanaonea wafungwa wanyonge, sasa na wao zamu yao ya kuonewa na rais kigangwe imefika.

Bila ya kuelewa kuwa wanashangilia tatizo lile lile la sadism tu.

Yani Watanzania wengi hawaelewi tofauti ya justice na revenge, wanaona revenge ndiyo justice.
 
Kuna uonevu wa kiaina ulifanywa mwingi sana,tatizo tukimpenda hata marehemu,hatupendi aambiwe ukweli,au akosolewe.Kuna doctor pale Tabora alishughukiwa kisa alienda hospital binafsi kufuata maslah kwa ajili ya maisha yake.Baba akasahau aliacha ualimu akaingia kwenye siasa.Tuamini ya Mungu ni mengi
Angeacha kupokea mshahara wa serikali akiwa nje ya kazi hiyo private imlipe
 
Kiranga una chuki kubwa sana na magufuli tangu zamani sana

Hii haifai
Hapana mkuu,

Wewe una uvivu fulani hivi ambao unakufanya ushindwe kutofautisha chuki na tofauti za kifalsafa.

Mimi nina tofauti za kifalsafa si tu na Magufuli, bali na Watanzania wengi sana.

Kwa mfano, mimi nathamini due process na justice.

Watanzania wengi, hususan wa JF kwenye uzi huu, hamthamini due process wala justice, mnataka show ya kibabe, summary execution na revenge.

Sasa nikianza kuelezea tofauti za misimamo miwili hii kifalsafa, wengi wenu hamna uwezo wa kuelewa, mnaishia kuona chuki binafsi tu.

Mkuu,

Magufuli katupa famikia yangu nyumba Oysterbay. Magufuli anajuana na Baba yangu tangu hajawa rais. Baba yangu alimpa maneno yake Mkapa kuhusu ubinafsishaji wa mashirika ya umma, maneno ambayo mawaziri wengi walitaka kusema lakini wakamuogopa Makapa. Baba yangu akausema wazi.

Kesho yake Magufuli akampigia simu baba yangu na kumshukuru sana kwa maneno yake yale kwamba kama amesema kwa niaba ya kina Magufuli waliotaka kusema wakashindwa.

Sasa huyo mtu ambaye kwetu tunamjua personally, kabla hajawa rais, si mtu wa kumsoma magazetini tu, mtu kama huyo mini naanzaje kumchukia kwa chuki binafsi?

Magufuli katupa jumba la serikali la US $ 3 million Oysterbay.

Sasa mimi namchukiaje huyo mtu kwa chuki binafsi?

Ukienda kwa habari binafsi mimi nilitakiwa kuwa namuimbia mapambio ya uchawa Magufuli.

Hizi ni tofauti za kifalsafa, si chuki binafsi.

Familia yangu inakula rent ya jumba la Oysterbay alilotupa Magufuli mpaka leo.

Sasa namchukiaje Magufuli kwa chuki binafsi hapo?

Ni yofauti za kifalsafa tu, ila wengi zimewapita kimo.
 
nimecheka sana kumbe Kiranga huwa anaamini kuwa mungu yupo 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣

Kumbe kuna watu humu wanatulisha upepo dah
Mkuu,

Nikiandika inabidi usome huku kichwa kimetulia.

Maana ni rahisi kutoelewa ninachoandika.

Nimeandika Mungu anasingiziwa kwa sababu siamini kuwa yupo.

Watu wanaisingizia ile character ya Mungu kuivika mambo yao mengi, wakati huyo Mungu mwenyewe hata hayupo.

Mtu kashindwa mtihani kwa sababu hajajiandaa kusoma, anasema kirahisi tu "Mungu hakuniwezesha".

Mungu anasingiziwa tu.

Ushaelewa?
 
Magufuli alikuwa mpuuzi sana kwenye ubishiubishi na watendaji.

Najua serikalini wapigaji wengi na rais anatakiwa kukomaa, ila Magufuli alikuwa anabishana kwa ligi. Hataki kushindwa.

Ila kiboko yake ni yule jamaa aliyebishana naye kuhusu kuweka lift hospitali, Magufuli akamuuliza kwani wewe nyumbani kwako kuna lift? Jamaa akamjibu nyumbani kwangu si hospitali.

Halafu jamaa hata hakujibu kwa kiburi, ni kama alikuwa anamuelewesha rais tu kitaalamu lift hospitali ni muhimu, kuna wagongwa wataihitaji. Magufuli na ushamba wake hataki kuelewa somo.

Pale wenye akili walimuona Magufuli mjinga sana kulinganisha hospitali na nyumbani kwa mtu.
Sijui kama huyo dr. Atakuwepo kazini hadi sasa. Atakuwa alishatenguliwa muda mrefu. Ile mauti Mungu aliiruhusu kwa sababu.
 
Leo nimekumbuka mkasa mmoja uliotokea enzi ya awamu ya tano!

Ilikuwa ni Julai 16 ya mwaka 2019 Jumanne tulivu tu ndani ya jiji la Mwanza, ghafla Gereza Kuu la Butimba likapata ugeni wa Amiri Jeshi Mkuu, Rais Magufuli.

Basi baada ya maofisa wa juu kutonywa kuwa Rais angeweza kufika pale, wakajipanga kumpokea.

Punde si punde, hayati Magufuli akawasili na bila kupoteza muda akaomba kuongea na wafungwa ili asikie matatizo yao kama ilivyoada yake.

Wafungwa walifurahi sana kumuona Rais, basi wakaambiwa watoe kero zao. Wakazungumza wengi mpaka ilipofika kwa mfungwa mmoja aliyeamua kumwaga mchele kwenye kuku wengi.

Mmoja ya wafungwa waliopata nafasi ya kuongea na hayati Magufuli alikuwa ni Kalikenye Thomas Nyamboge, mfungwa mwenye ulemavu wa ngozi, aliyekuwa anatumikia kifungo cha Miaka 30 jela.

Mfungwa Kalikenye yeye akatoa kero yake kuhusu Afisa Usalama wa Gereza hilo, Afande Mwasifiga kuwa anashirikiana na wafungwa wengine kwa kuwapa simu waongee na watu wa nje ya Gereza kinyume na utaratibu uliowekwa lakini pia anashirikiana na baadhi ya wafungwa wenye hela kuingiza simu kwenye Gereza hilo la Butimba.

Mfungwa wa miaka 30 Jela, Bwana Thomas Kalikenye akaendelea kumsagia kunguni Afande kuwa, msako ukipita simu hazionekani na wao akina Thomas wasiohusika na kuingiza simu wanamwagiwa vitu vyao kama vile Karanga, Sukari, Sabuni na saa nyingine vinachukuliwa kwa nguvu na team ya Afande Mwasifiga.

Ghafla hayati Magufuli anabadilika na kuuliza yuko wapi huyo Afande Mwasifiga? Afande anatokea na kupiga saluti na kuanza kujibu shutuma.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Afande Mwasifiga anaanza kubishana na Rais Magufuli kuhusu suala la uwepo wa simu kwa wafungwa katika Gereza la Butimba.

Afande Mwasifiga katika ubishani wake akamuambia Rais Magufuli, “huyu alitaka kuniinua” Maneno hayo yalimchefua sana Rais.

Magufuli akamwambia afande kuwa”inaonekana una dharau sana wewe” akawa ameshakasirika huku wasaidizi wa Rais wakimtonya Afande Mwasifiga aombe msamaha kwa Rais. Kweli akaomba msamaha huku akipiga saluti, lakini haikusaidia kitu.

Kama utani Rais Magufuli akamwambia ninaweza nikang’oa hizo nyota zako hapo (huyu Afande alikuwa na nyota mbili).

Basi Rais akaachana nae akamalizia kuongea na wafungwa kama alivyopanga ana akatoa agizo kwa Mkuu wa Gereza la Butimba, ole wake mfungwa yoyote aliyetoa kero anyanyaswe, basi atachukua hatua mara moja. Akamaliza akaaga akaondoka zake.

Usiku wake, Afande Mwasifiga akapokea maelekezo kuwa ameondolewa Gereza la Butimba na kupewa uhamisho wa kwenda Ukerewe.

Sambamba na hilo, akavuliwa nyota yake moja alitoka kuipata siku chache kabla ya kubishana na Rais. Hivyo basi akabaki na nyota moja tu badala ya mbili kama hatua ya kinidhamu iliyochukuliwa dhidi yake.

Kama haitoshi, baada ya miezi sita akiwa katika kituo chake kipya cha kazi, akastaafishwa kwa maslahi ya umma na utumishi wake ndani ya Jeshi la Magereza ukawa umefikia kikomo.

Ikumbukwe alipewa miaka mitano ya ziada jeshini baada ya kupewa nyota ya pili kabla ya kuipoteza nyota hiyo kutokana na kubishana na Rais.

Ukawa ndio mwisho wa Afande Mwasifiga, aliyepata kuwa Mkuu wa Usalama ndani ya Gereza la Butimba na waliopata kufanya nayr kazi wanakwambia alikuwa ni mjivuni, kiburi kwelikweli.

Kwasasa amerudi kwao Mbeya akiwa ni mkulima akiendeleza maisha baada ya kustaafishwa kwa maslahi ya Umma!View attachment 3164402

View: https://www.youtube.com/watch?v=z1Oq2b0lFhs
 
Maafrika mengi mpaka uya deal perpendicular Tena by IRON & BLOOD Ila ukitaka discussion, debating mtu mweusi ni kumshuhurikia Kama hayati alivyo kua anafanyaa..

Tena Mimi ndio ntakuwa zaidi ya hayati nikipata nafasi maana sisi majority ni wavivu, wazembe, wakwepa majukumu & everything.
You are proving my point.

Thanks for being honest in your monstrous sociopathy.
 
kwa katiba ya wabongo Rais ana mamlaka ya kumpandisha/Kumshusha cheo askari yeyote bila kuhitaji justification yoyote.

Tukirudi Gerezani it seems ya kwamba askari husika ni kweli alikuwa akiumiza wafungwa.. Kwahivyo tutende haki bila kukiogopa kifo!

Kufa tutakufa tu!
Sikusema hana mamlaka na wala sikujadili katiba.

Kwa katiba ya Bongo rais ana mamlaka ya kuuza ardhi ya nchi nzima, lakini je, afanye hivyo?
 
Mtu gani? Mtaje tu.

Inawezekana katoa mashudu yenye virutubisho vingi vya protein ni wewe tu hujaelewa.

Halafu,

Usimfuatilie mtu, fuatilia hoja.

Ukimfuatilia mtu ndiyo mwanzo wa kujifunga kwa mahaba na mtu hata akikosea usione makosa yake kwa sababu una mahaba naye.
Nilikuwa nafuatilia anchokiandika sio yeye....ila leo kaandika ukurutu sijategemea aisee
 
Mwisho wa siku mfungwa aliendelea kubakia mfungwa, askari akaendelea kuwa askari na Rais akaendelea kuwa Rais...

Tujitahidi kurekebisha mifumo na sio watu, maana mfumo ukiwa thabiti sisi watu tutaishi tukihakikisha tunaufuata...
 
Mimi mtu asiyejua tofauti ya zambi na dhambi siwezi kufanya mjadala naye wa kimantiki.

Kama hajui tofauti ya zambi na dhambi kiswahili atajuaje logical fallacy kilatini?

Kutojua tofauti ya zambi na dhambi ni ishara ya umbumbumbu na mimi sitaki mijadala na mbumbumbu.
Sasa Dada yangu mmmmm!!! Ila una Kilanga wewe, umri uliokuwa nao bado unajikita kwenye spelling kikubwa ni kuelewa dada yangu mpendwa.

Angalia attachment yako, neno la kiongozi wa nchi uwa linaanza na herufi kubwa Rais na sio rais au kwa kuwa ni nyani ndio maana hauoni kundule.
 

Attachments

  • Screenshot_20241128_201218_Chrome.jpg
    Screenshot_20241128_201218_Chrome.jpg
    348.6 KB · Views: 1
Back
Top Bottom