Mkasa wa Afande Mwasifiga alivyopoteza kazi baada ya kubishana na hayati Rais Magufuli

Magufuli alikuwa mpuuzi sana kwenye ubishiubishi na watendaji.

Najua serikalini wapigaji wengi na rais anatakiwa kukomaa, ila Magufuli alikuwa anabishana kwa ligi. Hataki kushindwa.

Ila kiboko yake ni yule jamaa aliyebishana naye kuhusu kuweka lift hospitali, Magufuli akamuuliza kwani wewe nyumbani kwako kuna lift? Jamaa akamjibu nyumbani kwangu si hospitali.

Halafu jamaa hata hakujibu kwa kiburi, ni kama alikuwa anamuelewesha rais tu kitaalamu lift hospitali ni muhimu, kuna wagongwa wataihitaji. Magufuli na ushamba wake hataki kuelewa somo.

Pale wenye akili walimuona Magufuli mjinga sana kulinganisha hospitali na nyumbani kwa mtu.
Hii naikumbuka na alikuwa cool hana papara
 
Kufa kwa Magufuli haku justify tabia mbovu za huyo afande aliyestaafishwa.
Na hakuna niliposema kuwa kufa kwa Magufuli kuna justify tabia mbovu za huyo afande aliyestaafishwa.

Labda hujaweza kusima kwa ufahamu tu.

Ni hivi, inawezekana Watanzania wote mna tabia mbovi tu.

Huyo afande alikuwa na tabia mbovu ya kuruhusu simu gerezani, na Magufuki alikuwa na tabia mbovu ua kujimwambafy kutumia maguvu isivyotakiwa na kuendek3za kutumia cheo sehemu inayotakiwa kutumia mantiki kuchambua hoja.

Ila, wabongo wezi that is too much to process.

Mmezoea kufikiri kwa one track mindset.

Yani mnaona ama Magufuli mzuri na huyu afande mbaya, ama huyu afande mzuri na Magufuli mbaya.

Yani hamuwezi hata kuona kuwa, hata kama afande kakosea, Magufuki kujimwambafy vile kwa summary execution bila kufuata die process nako no kitu kibaya.

Mshazoea zike zake za "nitymbue nisitumbueee?" Mnajibu "Tumbuaaaaa".

"Apigwe asipigweeee?" Mnajibu "Apigweee".

Bila kujali mizani na due process na haki za watu.

Yani hamuelewi kuwa hata kama Afande alikosea, Magufuli hakutakiwa kujimwambafy vile kwa maneno ya "naweza kukuvua nyota" kama lile ni suala lake personal.
 
Kiranga au
Huyu jamaa miaka yangu ya mwanzo Jamiiforums early 2010 nilikuwa namuona wa maana sana alikuwa na namna fulani ya uwasilishaji wa hoja ukisoma unamuelewa but kadiri nilivyozidi kukutana nae majukwaani taratibu nikaanza kumuona kumbe hayupo sawa upstairs.

Bahati mbaya sana binadamu tumeumbiwa kiburi,kwa alipofikia ilikuwa bora ajirudi hata kwa kukaa kimya but jinsi anavyodhani anaboresha hoja yake ya mwanzo ndiyo amezidi kuharibu.
 
Magufuli alikuwa mpuuzi sana kwenye ubishiubishi na watendaji.

Najua serikalini wapigaji wengi na rais anatakiwa kukomaa, ila Magufuli alikuwa anabishana kwa ligi. Hataki kushindwa.

Ila kiboko yake ni yule jamaa aliyebishana naye kuhusu kuweka lift hospitali, Magufuli akamuuliza kwani wewe nyumbani kwako kuna lift? Jamaa akamjibu nyumbani kwangu si hospitali.

Halafu jamaa hata hakujibu kwa kiburi, ni kama alikuwa anamuelewesha rais tu kitaalamu lift hospitali ni muhimu, kuna wagongwa wataihitaji. Magufuli na ushamba wake hataki kuelewa somo.

Pale wenye akili walimuona Magufuli mjinga sana kulinganisha hospitali na nyumbani kwa mtu.
Msaada wa hiyo clip ndugu
 
Watu wengi hawajui story ya "who will rid me of this troublesome priest?", inafundisha viongozi kuwa makini na kauli zao wakati wana hasira, zinaweza kuwa na madhara makubwa.

Ninavyokumbuka jamaa alijibu "nilijua utaniinua" akimaanisha kuinuliwa kujibu swali.... Sasa mkuu akadhani, anamanaisha atampandisha chati.... Ndio mwisho ukawa hivyo
Lugha gongana.

Na ziara kama zile zinakuwa zishasukwa tayari pale rais anakuja kufanya show for public consumption tu.
 
Msaada wa hiyo clip ndugu

Link pekee nimeikuta Facebook.

Magufuli anabishia hospitali kuwekewa lift kweli kabisa?

View: https://www.facebook.com/share/v/14Rx9GUaTx/

Siku hizi nimeanza kuzi download hizi naziweka kwenye server yangu ya nyumbani maana nyingine wanaziondoa Youtube.

Ile clip inatakiwa kuwekwa kwenye somo la kuwafundisha viongozi wasijibizane na watendaji sana maswali ya hapo kwa papo kwa sababu watendaji wanaoelewa mengi sehemu zao za kazi na rais akija kichwakichwa anaweza kuadhirika sana.
 
Leo nimekumbuka mkasa mmoja uliotokea enzi ya awamu ya tano!

Ilikuwa ni Julai 16 ya mwaka 2019 Jumanne tulivu tu ndani ya jiji la Mwanza, ghafla Gereza Kuu la Butimba likapata ugeni wa Amiri Jeshi Mkuu, Rais Magufuli.

Basi baada ya maofisa wa juu kutonywa kuwa Rais angeweza kufika pale, wakajipanga kumpokea.

Punde si punde, hayati Magufuli akawasili na bila kupoteza muda akaomba kuongea na wafungwa ili asikie matatizo yao kama ilivyoada yake.

Wafungwa walifurahi sana kumuona Rais, basi wakaambiwa watoe kero zao. Wakazungumza wengi mpaka ilipofika kwa mfungwa mmoja aliyeamua kumwaga mchele kwenye kuku wengi.

Mmoja ya wafungwa waliopata nafasi ya kuongea na hayati Magufuli alikuwa ni Kalikenye Thomas Nyamboge, mfungwa mwenye ulemavu wa ngozi, aliyekuwa anatumikia kifungo cha Miaka 30 jela.

Mfungwa Kalikenye yeye akatoa kero yake kuhusu Afisa Usalama wa Gereza hilo, Afande Mwasifiga kuwa anashirikiana na wafungwa wengine kwa kuwapa simu waongee na watu wa nje ya Gereza kinyume na utaratibu uliowekwa lakini pia anashirikiana na baadhi ya wafungwa wenye hela kuingiza simu kwenye Gereza hilo la Butimba.

Mfungwa wa miaka 30 Jela, Bwana Thomas Kalikenye akaendelea kumsagia kunguni Afande kuwa, msako ukipita simu hazionekani na wao akina Thomas wasiohusika na kuingiza simu wanamwagiwa vitu vyao kama vile Karanga, Sukari, Sabuni na saa nyingine vinachukuliwa kwa nguvu na team ya Afande Mwasifiga.

Ghafla hayati Magufuli anabadilika na kuuliza yuko wapi huyo Afande Mwasifiga? Afande anatokea na kupiga saluti na kuanza kujibu shutuma.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Afande Mwasifiga anaanza kubishana na Rais Magufuli kuhusu suala la uwepo wa simu kwa wafungwa katika Gereza la Butimba.

Afande Mwasifiga katika ubishani wake akamuambia Rais Magufuli, “huyu alitaka kuniinua” Maneno hayo yalimchefua sana Rais.

Magufuli akamwambia afande kuwa”inaonekana una dharau sana wewe” akawa ameshakasirika huku wasaidizi wa Rais wakimtonya Afande Mwasifiga aombe msamaha kwa Rais. Kweli akaomba msamaha huku akipiga saluti, lakini haikusaidia kitu.

Kama utani Rais Magufuli akamwambia ninaweza nikang’oa hizo nyota zako hapo (huyu Afande alikuwa na nyota mbili).

Basi Rais akaachana nae akamalizia kuongea na wafungwa kama alivyopanga ana akatoa agizo kwa Mkuu wa Gereza la Butimba, ole wake mfungwa yoyote aliyetoa kero anyanyaswe, basi atachukua hatua mara moja. Akamaliza akaaga akaondoka zake.

Usiku wake, Afande Mwasifiga akapokea maelekezo kuwa ameondolewa Gereza la Butimba na kupewa uhamisho wa kwenda Ukerewe.

Sambamba na hilo, akavuliwa nyota yake moja alitoka kuipata siku chache kabla ya kubishana na Rais. Hivyo basi akabaki na nyota moja tu badala ya mbili kama hatua ya kinidhamu iliyochukuliwa dhidi yake.

Kama haitoshi, baada ya miezi sita akiwa katika kituo chake kipya cha kazi, akastaafishwa kwa maslahi ya umma na utumishi wake ndani ya Jeshi la Magereza ukawa umefikia kikomo.

Ikumbukwe alipewa miaka mitano ya ziada jeshini baada ya kupewa nyota ya pili kabla ya kuipoteza nyota hiyo kutokana na kubishana na Rais.

Ukawa ndio mwisho wa Afande Mwasifiga, aliyepata kuwa Mkuu wa Usalama ndani ya Gereza la Butimba na waliopata kufanya nayr kazi wanakwambia alikuwa ni mjivuni, kiburi kwelikweli.

Kwasasa amerudi kwao Mbeya akiwa ni mkulima akiendeleza maisha baada ya kustaafishwa kwa maslahi ya Umma!View attachment 3164402
Yote maisha...
 
Hivi jeshini inaruhusiwa kuuliza order ya afande kwanini imekaa hivyo?
 
Unaweza kujitapa sana kwamba unaweza kumvua mtu manyota wakati wowote lakini huyo unayemvua manyota akaendelea kuishi na wewe na tambo lako lote la kumvua manyota ukafa ukamuacha.

Cheo ni dhamana, tusipende sana kujimwambafy kwa dhamana ya cheo.

Magufuli angeweza kumsikiliza Afande na kuamua kesi kwa busara bila kujimwambafy kwamba anaweza kumvua manyota.
Kwahiyo tuogope kutenda haki kisa twaogopa kifo? Tuogope kufanya maamuzi kisa twaogopa Kifo?
Hoja yako ni dhaifu, Haijustify maamuzi na Kifo!
 
Binafsi kwa mtazamo wangu Kuna watu wakipewa mamlaka hugeuka kua MA GODFATHER.

Afande alikua mtu jeuri na mwenye kunyanyasa wafungwa na alikua na mtandao mkubwa na mpana.

Real life story.
Kuna ndugu yangu alipata kesi ya mauaji so AKAWA gereza moja gumu mkoa wa Tabora..Enzi za utawala wa mzee Benja

Siku moja kiongozi mkubwa alitembelea gerezani wakapewa nafasi wameelezea kero na shida zao ndugu yangu akanyoosha mkono na kuanza kueleza..

Yaan mahindi yalikua yanakobolewa na kwenda kuuzwa wao wanapikiwa mapumba. Alieleza mambo mengi Sanaa yalivyo kua hayaendani na haki za wafungwa

Viongozi baada ya kuondoka maaskari walimpiga Sana na kumvunja mguu mmoja kumbe ki Siri Siri aliachiwa code akipata tatizo ajulishe kipenyo mmoja

All in all,
After that saga alitibiwa vizuri na alipewa uangalizi wa Vvip AKIWA gerezani na wale askari walio mpiga walishuhurikiwa na akaanza kuogopewa na maaskari walio wengi pia welfare za gerezani zilifanyiwa some improvement

Alitumikia gerezani kwa miaka 7 na Alikujaga kutoka kwenye utawala wa kikwete mwanzoni kwa msamaha wa Raisi (prerogative of mercy) yupo uraiani Sasa.
 
Hakuna haki ya "naweza kukuvua nyota mimi" hiyo ni show ya kibabe tu.

Ila wabongo wengi ndicho mnachopenda, mkiona show za kibabe ndiyo mnaita haki.

Wabongo wengi ni sadists, na Magufuli mlimpenda sana kwa sababu alikuwa Sadist In Chief.

Hata kama Afande alikosea, rais angeweza kumuadhibu kwa kufuata due process si kwa kuonesha umwamba wa summary execution.
 
Kuna mtu nilikuwa nafuatiliaga sana comment zake huwa anaonheaga vitu vya msingi sana.....leo nimeshangaa kwenye huu uzi ame comment mashudu tupu
Kuna wimbo wa harmonizer hapa kibwagizo nasikia kinasema..... 🎵 🎶 KAMA UNA MJUA MTAJEEE....WANASEMA KAMA UNAMJUA MTAJEEEE....😊😊😊
 
Binafsi kwa mtazamo wangu Kuna watu wakipewa mamlaka hugeuka kua MA GODFATHER.

Afande alikua mtu jeuri na mwenye kunyanyasa wafungwa na alikua na mtandao mkubwa na mpana.

Real life story.
Kuna ndugu yangu alipata kesi ya mauaji so AKAWA gereza moja gumu mkoa wa Tabora..Enzi za utawala wa mzee Benja

Siku moja kiongozi mkubwa alitembelea gerezani wakapewa nafasi wameelezea kero na shida zao ndugu yangu akanyoosha mkono na kuanza kueleza..

Yaan mahindi yalikua yanakobolewa na kwenda kuuzwa wao wanapikiwa mapumba. Alieleza mambo mengi Sanaa yalivyo kua hayaendani na haki za wafungwa

Viongozi baada ya kuondoka maaskari walimpiga Sana na kumvunja mguu mmoja kumbe ki Siri Siri aliachiwa code akipata tatizo ajulishe kipenyo mmoja

All in all,
After that saga alitibiwa vizuri na alipewa uangalizi wa Vvip AKIWA gerezani na wale askari walio mpiga walishuhurikiwa na akaanza kuogopewa na maaskari walio wengi pia welfare za gerezani zilifanyiwa some improvement

Alitumikia gerezani kwa miaka 7 na Alikujaga kutoka kwenye utawala wa kikwete mwanzoni kwa msamaha wa Raisi (prerogative of mercy) yupo uraiani Sasa.
Wewe angalau umeongea cha kueleweka kiasi kwamba mtu akisoma anaelewq nini umemaanisha
 
Hakuna haki ya "naweza kukuvua nyota mimi" hiyo ni show ya kibabe tu.

Ila wabongo wengi ndicho mnachopenda, mkiona show za kibabe ndiyo mnaita haki.

Wabongo wengi ni sadists, na Magufuli mlimpenda sana kwa sababu alikuwa Sadist In Chief.

Hata kama Afande alikosea, rais angeweza kumuadhibu kwa kufuata due process si kwa kuonesha umwamba wa summary execution.
Maafrika mengi mpaka uya deal perpendicular Tena by IRON & BLOOD Ila ukitaka discussion, debating mtu mweusi ni kumshuhurikia Kama hayati alivyo kua anafanyaa..

Tena Mimi ndio ntakuwa zaidi ya hayati nikipata nafasi maana sisi majority ni wavivu, wazembe, wakwepa majukumu & everything.
 
Back
Top Bottom