Mkasa wa Afande Mwasifiga alivyopoteza kazi baada ya kubishana na hayati Rais Magufuli

Mkasa wa Afande Mwasifiga alivyopoteza kazi baada ya kubishana na hayati Rais Magufuli

You are proving my point.

Thanks for being honest in your monstrous sociopathy.
Nyinyi huko ulaya civilization ime advance Sana hata GENES zenu zime be civilized 😊☺️

*Mtu anaenda kun'goa miundombinu ya barabara, reli na kwenda kuuza vyuma chakavu.

*Mtu anaiba public funds na kwenda kuzificha uswisi

*Wanaiba madawa ya serikali na kwenda kuyapeleka kwenye maduka yao binafsi

*Pesa ya ujenzi wa shule,kituo Cha afya, mahakama,soko, barabara wanajenga Chini ya kiwango

*Dhuruma,rushwa, wizi, ubadhilifu na everything dirty

*Kama msimamizi wa kituo Cha kupigia kura ana cheat kwa kuingiza kura za muruhani zaidi ya 200..

HAPO HAPO AKIPATIKANA MTU WA KUNYOOSHA PALIPO PINDA KWA MKONO WA CHUMA...TENA HATA KWA KUVUNJA KATIBA.. BINAFSI MIMI NAONA HUO NDIO UZALENDO WA KWELI.
 
Sasa Dada yangu mmmmm!!! Ila una Kilanga wewe, umri uliokuwa nao bado unajikita kwenye spelling kikubwa ni kuelewa dada yangu mpendwa.

Angalia attachment yako, neno la kiongozi wa nchi uwa linaanza na herufi kubwa Rais na sio rais au kwa kuwa ni nyani ndio maana hauoni kundule.
Wewe Mlugaluga hata tofauti ya l na r hujui.

Unaniletea shombo tu hapa nakupeleka ignore list kuanzia hapa sitaona unachoandika.
 
Logical non sequitur fallacy.

Hataishi milele ila Magufuli katangulia kufa kamuacha afande analifaidi jua bado.

Magufuli na mabobish yake yote ya "Naweza kukuvua manyota" hayakumsaidia kukishinda kifo.

Cheo ni dhamana, usikitumie kujimwambafy na kutishia watu.

Duniani wote tunapita tu.
Inasemekana afande pia ashafariki.
Rais akisema mbona manyasi yameota sana
Hapo haulizi bali ni amri hayo manyasi yapaliliwe, Mpo hapo?

Aliposema naweza nikaziondoa hizo nyota maana yake ilikuwa ashushwe cheo
Daa naikumbuka hiyo ziara
 
Rais alikufa usisahau.

Pamoja na kujimwambafy sana "naweza kukuvua manyota".

Yes...

Aliamua kudeal na mtu badala ya kuangalia ni namna gani ya kutatua tatizo kama lipo kwa magereza yote na sio Butimba pekee...
 
Huu mkasa umenikumbusha siku Ile spika wa bunge jobu ndugai aliposema ipo siku Nchi hii itapigwa mnada.Alipoisikia mama hiyo kauli alichukia sana na kuanza kumfokea jobu ndugai na hatimaye kufukuzwa usipika pamoja na kuwa mhimili wa bunge Huwa tunaamimishwa kuwa ni huru
 
You are proving my point.

Thanks for being honest in your monstrous sociopathy.
Nyinyi huko ulaya civilization ime advance Sana hata GENES zenu zime be civilized.

*Mtu anaenda kun'goa miundombinu ya barabara, reli na kwenda kuuza vyuma chakavu.

*Mtu anaiba public funds na kwenda kuzificha uswisi

*Wanaiba madawa ya serikali na kwenda kuyapeleka kwenye maduka yao binafsi

*Pesa ya ujenzi wa shule,kituo Cha afya, mahakama,soko, barabara wanajenga Chini ya kiwango

*Dhuruma,rushwa, wizi, ubadhilifu na everything dirty

*Kama msimamizi wa kituo Cha kupigia kura ana cheat kwa kuingiza kura za muruhani zaidi ya 200..

HAPO HAPO AKIPATIKANA MTU WA KUNYOOSHA PALIPO PINDA KWA MKONO WA CHUMA...TENA HATA KWA KUVUNJA KATIBA.. BINAFSI MIMI NAONA HUO NDIO UZALENDO WA KWELI
 
Huu mkasa umenikumbusha siku Ile spika wa bunge jobu ndugai aliposema ipo siku Nchi hii itapigwa mnada.Alipoisikia mama hiyo kauli alichukia sana na kuanza kumfokea jobu ndugai na hatimaye kufukuzwa usipika pamoja na kuwa mhimili wa bunge Huwa tunaamimishwa kuwa ni huru
Ahaaa ila job alifeli
 
Nyinyi huko ulaya civilization ime advance Sana hata GENES zenu zime be civilized.

*Mtu anaenda kun'goa miundombinu ya barabara, reli na kwenda kuuza vyuma chakavu.

*Mtu anaiba public funds na kwenda kuzificha uswisi

*Wanaiba madawa ya serikali na kwenda kuyapeleka kwenye maduka yao binafsi

*Pesa ya ujenzi wa shule,kituo Cha afya, mahakama,soko, barabara wanajenga Chini ya kiwango

*Dhuruma,rushwa, wizi, ubadhilifu na everything dirty

*Kama msimamizi wa kituo Cha kupigia kura ana cheat kwa kuingiza kura za muruhani zaidi ya 200..

HAPO HAPO AKIPATIKANA MTU WA KUNYOOSHA PALIPO PINDA KWA MKONO WA CHUMA...TENA HATA KWA KUVUNJA KATIBA.. BINAFSI MIMI NAONA HUO NDIO UZALENDO WA KWELI
Baso ondoeni tu hiyo katiba tujue moja, acheni unafiki.
 
NENDA UHAYANI KAFANYE KAZI...FROM EXPERIENCE WAHAYA NILISHUHUDIA WAKITU DISCUSS KIHAYA KUMBE RAFIKI YANGU NI MZINZA😊☺️ AKAWA ANASIKIA WANAVYO TUSEMA 😅😅
Wahaya hawawafikii Wanyakyusa. Angalia.
1. Ulimboka
2. Sativa
3. Rais wa CHAMA CHA WANASHERIA
4. Kijana aliyechoma picha ya Rais
5. Askofu wa Moravian
6. Mponjoli.

Hili kabila ni hatari halifai. Wajeuri na wanajiamini sana.
 
Leo nimekumbuka mkasa mmoja uliotokea enzi ya awamu ya tano!

Ilikuwa ni Julai 16 ya mwaka 2019 Jumanne tulivu tu ndani ya jiji la Mwanza, ghafla Gereza Kuu la Butimba likapata ugeni wa Amiri Jeshi Mkuu, Rais Magufuli.

Basi baada ya maofisa wa juu kutonywa kuwa Rais angeweza kufika pale, wakajipanga kumpokea.

Punde si punde, hayati Magufuli akawasili na bila kupoteza muda akaomba kuongea na wafungwa ili asikie matatizo yao kama ilivyoada yake.

Wafungwa walifurahi sana kumuona Rais, basi wakaambiwa watoe kero zao. Wakazungumza wengi mpaka ilipofika kwa mfungwa mmoja aliyeamua kumwaga mchele kwenye kuku wengi.

Mmoja ya wafungwa waliopata nafasi ya kuongea na hayati Magufuli alikuwa ni Kalikenye Thomas Nyamboge, mfungwa mwenye ulemavu wa ngozi, aliyekuwa anatumikia kifungo cha Miaka 30 jela.

Mfungwa Kalikenye yeye akatoa kero yake kuhusu Afisa Usalama wa Gereza hilo, Afande Mwasifiga kuwa anashirikiana na wafungwa wengine kwa kuwapa simu waongee na watu wa nje ya Gereza kinyume na utaratibu uliowekwa lakini pia anashirikiana na baadhi ya wafungwa wenye hela kuingiza simu kwenye Gereza hilo la Butimba.

Mfungwa wa miaka 30 Jela, Bwana Thomas Kalikenye akaendelea kumsagia kunguni Afande kuwa, msako ukipita simu hazionekani na wao akina Thomas wasiohusika na kuingiza simu wanamwagiwa vitu vyao kama vile Karanga, Sukari, Sabuni na saa nyingine vinachukuliwa kwa nguvu na team ya Afande Mwasifiga.

Ghafla hayati Magufuli anabadilika na kuuliza yuko wapi huyo Afande Mwasifiga? Afande anatokea na kupiga saluti na kuanza kujibu shutuma.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Afande Mwasifiga anaanza kubishana na Rais Magufuli kuhusu suala la uwepo wa simu kwa wafungwa katika Gereza la Butimba.

Afande Mwasifiga katika ubishani wake akamuambia Rais Magufuli, “huyu alitaka kuniinua” Maneno hayo yalimchefua sana Rais.

Magufuli akamwambia afande kuwa”inaonekana una dharau sana wewe” akawa ameshakasirika huku wasaidizi wa Rais wakimtonya Afande Mwasifiga aombe msamaha kwa Rais. Kweli akaomba msamaha huku akipiga saluti, lakini haikusaidia kitu.

Kama utani Rais Magufuli akamwambia ninaweza nikang’oa hizo nyota zako hapo (huyu Afande alikuwa na nyota mbili).

Basi Rais akaachana nae akamalizia kuongea na wafungwa kama alivyopanga ana akatoa agizo kwa Mkuu wa Gereza la Butimba, ole wake mfungwa yoyote aliyetoa kero anyanyaswe, basi atachukua hatua mara moja. Akamaliza akaaga akaondoka zake.

Usiku wake, Afande Mwasifiga akapokea maelekezo kuwa ameondolewa Gereza la Butimba na kupewa uhamisho wa kwenda Ukerewe.

Sambamba na hilo, akavuliwa nyota yake moja alitoka kuipata siku chache kabla ya kubishana na Rais. Hivyo basi akabaki na nyota moja tu badala ya mbili kama hatua ya kinidhamu iliyochukuliwa dhidi yake.

Kama haitoshi, baada ya miezi sita akiwa katika kituo chake kipya cha kazi, akastaafishwa kwa maslahi ya umma na utumishi wake ndani ya Jeshi la Magereza ukawa umefikia kikomo.

Ikumbukwe alipewa miaka mitano ya ziada jeshini baada ya kupewa nyota ya pili kabla ya kuipoteza nyota hiyo kutokana na kubishana na Rais.

Ukawa ndio mwisho wa Afande Mwasifiga, aliyepata kuwa Mkuu wa Usalama ndani ya Gereza la Butimba na waliopata kufanya nayr kazi wanakwambia alikuwa ni mjivuni, kiburi kwelikweli.

Kwasasa amerudi kwao Mbeya akiwa ni mkulima akiendeleza maisha baada ya kustaafishwa kwa maslahi ya Umma!View attachment 3164402
Alikosea Sheria namba moja ya maisha. Never outshine the master.
 
Back
Top Bottom