BAADA YA BARUA YA MHUSIKA KUWA IMEGONGWA MUHURI NA HATIMAYE KUHAKIKISHIWA KUWA HAIKUWA NA TATIZO TENA
Mhusika rasmi likizo yake ya siku 28, ALHAMIS ya tarehe 08/09/2022 badala ya tarehe J3 ya tarehe 05/09/2022 na ilipofika J3 ya tarehe 03/10/2022 mhusika aliripoti idarani kama barua hiyo ilivyokuwa imeagiza
YALE YALIYOJIRI MUDA MFUPI BAADA YA MHUSIKA KURUDI KUTOKA LIKIZO YAKE YA MWAKA ILIYOANZIA TAREHE 05/09 NA KUISHIA TAREHE 02/10/2022
J5 ya tarehe 05/10/2022, mhusika alilipoti pia kwenye ofisi husika iliyopo jengo la CA. Kawaida alitakiwa aripoti kwenye ofisi hii ya pili siku hiyo hiyo ya J3 ya tarehe 03/10/2022 lakini alisita kufanya hivyo kutokana na sababu ambazo kwa sasa hawezi kuziweka wazi sana humu jukwaani
Ukizingatia matukio yale yaliyojiri muda mfupi kabla mhusika hajaenda likizo, mhusika hakupendelea sana kuingia ndani ya jengo la CA siku ya kwanza tu baada ya kuwa ametoka likizo; na
possibly uamuzi wake huu ulikuwa sahihi zaidi
BAADHI YA MATUKIO MUHIMU YALIYOJIRI SIKU HIYO YA J5 YA TAREHE 05/10/2022 BAADA YA MHUSIKA KUINGIA TENA NDANI YA JENGO HILO LA “CA” (KWA MARA YA TATU SASA NDANI YA KIPINDI CHA TAKRIBANI MWEZI MMOJA) AKIWA ANAENDA KURIPOTI; BAADA YA KUTOKA LIKIZO
Baada ya mhusika kufika kwenye eneo lilipo jengo la “CA”, pale nje kwenye
security chek point safari hii alimkuta security officer ambaye naye kwa mara nyingine tena, alimruhusu mhusika aingie ndani ya jengo la CA pasipo kuwa amemfanyia (mhusika) security scan.
Mpaka hapa ikawa sasa ni mara ya tatu ndani ya kipidi cha takribani mwezi mmoja, mhusika akiwa anaingia ndani ya jengo la CA na pasipo kufanyiwa security scan
Baada ya mhusika kufika kwenye ofisi husika, aliwapatia nakala ya barua yake ya likizo, na baada ya maofisa hao kuwa wameweka rekodi sawa, walimrudishia barua hiyo na kumruhusu aondoke
- Kabla hajaondoka, mhusika aliulizia kuhusu malipo ya likizo yake
- Mmojawapo wa maofisa husika wa ofisi hiyo, alimuomba tena mhusika barua yake na baada ya kuiangalia; ofisa huyo alimwelekeza mhusika sehemu husika
Baada ya hapo, mhusika alitoka ofisini hapo na kuanza kuelekea kwenye ofisi nyingine husika aliyokuwa ameelekezwa akaulizie malipo hayo ya likizo yake
Huko alifika na maelezo alipewa kuwa asubirie kidogo malipo hayo hadi wiki ijayo (yaani wiki hii tuliyonayo sasa)
- Baada ya mhusika kutoka kwenye ofisi hiyo ya pili, kwa maamuzi yake mwenyewe na pasipo maelekzo ya mtu mwingine yeyote yule, aliamua sasa kuelekea kwenye ofisi nyingine, ofisi ile kuu inayohusika na maswala ya fedha.
- Nia ilikuwa ni kwenda kuulizia ule mchakato ambao siku kadhaa nyuma, uliwahi kugongana na swala la likizo yake na hatimaye kupelekea barua yake ya likizo kuchelewa.
- Huko mhusika alitamani kujua mchakato huo umefikia wapi na alitamani pia kuonana na boss wake (mhusika) anayeshikilia ofisi hiyo
Ilikuwa ni bahati nzuri kwamba alimkuta Katibu Muhtasi wa boss na ambaye baada ya kuongea naye, mama huyu aliridhia mhusika aweze kuonana na kuongea na boss wake
Hata hivyo ilionekana kuwa kwa muda huo, boss alikuwa anaongea na mtu mwingine ndani na hivyo mhusika kuombwa aketi kidogo kwenye kiti ili asubirie mtu huyo atoke kwanza. Mhusika aliketi kwenye mojawpo ya viti vya wageni na kuanza kusubiria
YALE MUHIMU TU YALIYOJIRI PINDI MHUSIKA ALIPOKUWA OFISINI HAPO AKIWA ANASUBIRIIA MTU ATOKE ILI NAYE AINGIE NDANI OFISINI AKAONGEE NA BOSS WAKE
GHAFLA KIJANA MMOJA WA KIUME ALIYEKUWA AMEBEBA BEGI MGONGONI, MIAKA ISIYOZIDI 30, ALIINGIA OFISINI HAPO!
- Kijana huyu alikuwa anatetemeka kwa hasira, na alikuwa karibia anataka kulia
- Baada ya kuingia ofisini, alienda akasimama kwenye kaunta karibu na mahali alipokuwa amekaa Katibu Muhtasi (KMH)
- Kijana huyu alianza kulalamika kuwa alikuwa chumba namba 200, ametokea huko na ambako kuna “binti mweupe” ambaye ana majibu mabaya. Kijana alikuwa amejibiwa vibaya na “binti mweupe”
Baada ya maeongezi mafupi ya kijana huyo na KMH, kijana alitoka nje ya ofisi na baada ya sekunde kadhaa, KMH naye alitoka pia huku akiuacha mlango wa ofisi yake nusu wazi, hakuufunga.
- Mhusika alibaki hapo mbele ya mapokezi peke yake huku kwenye ofisi mbili zlizokuwa kulia na kushoto mwa veranda ya mapokezi kukiwa na watu ndani; na mojawapo ya ofisi hizo ilikuwa ni ile ambayo mhusika alikuwa anasubiria kuingia
- Baada ya muda kidogo, mtu mwingine binti aliingia ofisini hapo akiwa ameshika handbag, akiwa anamuulizia KMH
- Mhusika hakumjibu binti huyu kwa sababu hata kwa kutumia macho yu, ofisi yenyewe ilikuwa inamjibu.
- Binti huyu hakukaa sana; hakumaliza hata nusu dakika; alitoka nje
Wakati huo wote mhusika alikuwa amebaki peke yake pale mbele ya mapokezi ya ofisi ya KMH, mlango wa ofisi hiyo ukiwa uko nusu wazi na kulikuwa na watu wengi tu ambao mhusika alikuwa anawaona wakiwa wanapita kwenye korido
Baada ya kuwa zimepita takribani dakika 7-10, KMH alirudi ofisini huku huyu mtu aliyekuwa anaongea na Boss wakati mhusika anawasili ofisini hapo, akiwa bado hajatoka nje ya ofisi ya Boss
Baada ya takribani dakika 2 tangu KMH arudi, mtu huyu alitoka na KMH aliingia ofisini kwa Boss, kwenda kuona kama alikuwa bado ana muda wa kufanya maongezi na mtu mwingine
Muda siyo mrefu KMH alitoka nje ya ofisi ya boss na hatimaye kumruhusu mhusika aingie ndani
Mhusika aliingia ndani kwa boss na baada ya hapo, ilipita kama nusu dakika hivi kabla mhusika hajasalimiana na kuongea na boss kwa sababu alimkuta akiwa anaongea na simu
KITAMBO KIFUPI KABLA MHUSIKA NA BOSS WAKE HAWAJAANZA MAONGEZI; KIPINDI BOSS ALIPOKUWA BADO ANAONGEA NA SIMU
Mhusika alifanya tathmini na kugundua kuwa aliyemkuta ofisini hapo si boss yule wa siku zote (PERMANENT) ambaye yeye (mhusika) anamfahamu siku zote
- Zaidi ni kuwa boss huyu mpya alikuwa ni kijana miaka si zaidi ya 35, kitu ambacho hata kama angekuwa ni boss mpya kwenye ofisi, ni nadra sana kwa ofisi hiyo kubwa mno kushikiliwa na mtu wa umri huo kwa sababu mara zote huwa inahitaji watu wenye uzoefu wa miaka si chini ya 15 kwenye eneo la utaalamu wa maswal ya fedha
- Kwa kijana huyu kuwa na uzoefu wa miaka hiyo na kupelekea aweze kuaminiwa kwenye ofisi kubwa namna hiyo, maana yake ni kwamba mtu huyu atakuwa alianza kazi akiwa na umri usiozidi miaka 20
Mpaka hapa ruling ya mhusika kichwani kwake ikamwambia kuwa aliyekuwepo ofisini hapo alikuwa ni
ACTING, japo mhusika aliingia akiwa hajaelezwa kuwa aliyekuwepo ofisini siku hiyo alikuwa ni
ACTING
BAADA YA BOSS KUMALIZA KUFANYA MAONGEZI KWENYE SIMU
Mhusika alimweleza boss wake shida yake kwamba alikuwa anaomba kujua mchakato wa malipo yake ya muda mrefu uliouacha ukiwa unaendelea alipokuwa anaondoka kwenda likizo, kuwa ulikuwa umefikia hatua gani hadi siku hiyo
- Baada ya mhusika kuwasilisha ombi lake kwa boss wake huyo, yalifuatia majadiliano ya muda mfupi, na baada ya majadiliano hayo, boss huyo aliamua kupiga simu kwenye mojawapo ya ofisi zilizo chini yake. Baada ya maongezi mengine mafupi kwenye simu, boss alimwelekeza mhusika aende ofisi namba 315 na akamuone mtu ambaye alimtajia jina
- Mhusika aliondoka ofisini hapo kwa boss, akielekea chumba alichotajiwa na kwa mtu aliyekuwa ametajiwa jina lake
Ofisi aliyokuwa ameelekezwa aende ilikuwa jirani, mkabala tu na ofiisi ile ya mwanzo alipoanzia mhusika wakati anawasilisha nyaraka zake zilizohusiana na maswala yake ya kuripoti kutoka likizo
- Ofisi ilikuwa wazi huku mlango wake ukiwa umeachwa nusu wazi, isipokuwa mtu (binti) aliyekuwepo ofisini pale muda huo si yule ambaye mhusika alikuwa ameelekezwa akamuone
- Baada ya mhusika kuongea na binti aliyekuwepo kwenye ofisi hiyo muda huo, binti alimjulisha mhusika kuwa yule ambaye mhusika alikuwa ameelekezwa kwake alikuwa ametoka kidogo
- Binti huyu alienda mbali zaidi kutaka kujua shida ya mhusika ili (binti) aone kama anaweza kusaidia
- Kusikia hivyo, mhusika naye hakusita kumweleza binti shida yake na hivyo kulazimika kujieleza tena ila kwa kifupi sana
Baada ya binti kuisikia shida ya mhusika, aliamua kumpigia simu huyu ambaye alikuwa amepelekea mhusika afike ofisini hapo lakini kwa bahati mbaya hakuwepo ofisini, alikuwa ametoka kidogo
Huku binti huyu akiwa amemkaribisha mhusika kwenye kiti; mhusika akiwa tayari amekaa kwenye kiti;
binti aliamua kutoka nje ya ofisi huku akipiga simu ili akaongee na simu akiwa yuko nje.
HITIMISHO
Kwenye ofisi hiyo, mhusika alikuwa amekaa pembezoni mwa mlango wa kutokea nje wa ofisi hiyo,
na kilichotokea ni kwamba wakati binti anajiandaa atoke nje huku akiwa anaashiria dalili za kutaka kuongea na simu (alikuwa hajaanza kuongea) mhusika naye alinyanyuka kwenye kiti alichokuwa amekaa na hivyo kupelekea mhusika na binti; wote wawili kwa pamoja kupita pale mlangoni wakiwa wamejipanga kama askari wawili walio kwenye mstari wa kwata
Baadaye, kilichoendelea baada ya hapo huku mhusika akiwa kwenye korido nje ya ofisi hiyo, kilikuwa ni kile tu ambacho mhusika hakuweza tena kukielewa
Muda mfupi baadaye, hatimaye mhusika alitoka maeneo zilipo ofisi hizo, akatoka nje ya jengo la CA na kurudi idarani kwake.
MUBARIKIWE TENA NA BWANA