IBADA YA KUSIFU NA KUABUDU
Ibada ya Kusifu na Kuabudu ilianza na baadaye ilihitimishwa kwa sala na Kiongozi wa zamu.
Sala iliyohitimisha Ibada hiyo ilimalizia kwa neno
AMINA na baada ya hapo waumini walishangilia kwa kupiga makofi; kitu ambacho ni kawaida kabisa
- Hata hivyo, baada ya makofi hayo kupigwa, Kiongozi wa zamu aliwaomba waumini waliokuwa tayari wameshakaa wasimame juu na mhusika naye pia alifanya hivyo
- Baada ya waumini kusimama, Kiongozi wa zamu aliwaomba waumini wapige makofi mengine tena; makofi ambayo safari hii mhusika hakufanikiwa kupata nafasi ya kuyapiga.
WAKATI WA MAHUBIRI
Baada ya waumini kupiga makofi ya pili na hatimaye kuombwa wakae, Kiongozi wa Zamu alimkaribisha mhubiri au mwalimu wa somo la siku hiyo
Baada ya mwalimu wa somo kukaribishwa na hatimaye kutoa salaamu zake kwa waumini, alitambulisha somo lake lililokuwa na kichwa chenye kusisitiza
heshima na/ adabu ndani ya NYUMBA YA BWANA
Somo hilo lilikuwa zuri mno na lilifundishwa vizuri mno, ukizingatia kuwa kichwa chake kilikuwa kinazidi kutambua uwepo wa
NYUMBA YA BWANA, tofauti na lile jingine llililowahi kufundishwa hapo awali siku ya J2 ya tarehe 04/09/2022
Kama ambavyo mhusika aliwahi kugusia hivi karibuni, pamoja na uzuri wa namna lilivyofundishwa somo lile la mwanzo J2 ya tarehe 04/09/2022
bado somo hilo halikutambua uwepo wa nyumba ya Bwana kwa sababu lilitumia mafungu ya Biblia yaliyosema kuwa Bwana hakai kwenye majengo yaliyojengwa kwa mikono ya wanadamu
Kwa hiyo, kwa upande mwingine somo la J2 ya tarehe 06/11/2022 lilikuja na kitu kingine cha ziada na kikubwa zaidi, na hivyo lilifanya kazi ya ku-OVERWRITE baadhi ya mambo ambayo hayakuwa yamewekwa vizuri sana kwenye somo la J2 ya Septemba 2022
Kwa ujumla somo hilo lilikuwa zuri mno na lilifundishwa vizuri sana; mwalimu wa somo alikuwa mzuri mno
BAADA YA KIPINDI CHA SOMO KUU LA IBADA YA SIKU HIYO KUPITA NA HATIMAYE KUINGIA KIPINDI CHA MATANGAZO
Matangazo ya awamu ya kwanza yalitoka ofisi ya wazee
Kiongozi wa zamu aliyehusika na matangazo hayo; japo mwenyeji wa miaka mingi kwenye ofisi hiyo:
- Kwa kipindi cha kuanzia Desemba 2021 Ibada zilipohamia kwenye Kanisa jipya hadi J2 hiyo ya matangazo, mhusika anakumbuka kumuona Kiongozi huyu mara moja tu akiwa amesimama kwenye madhabahu na kusimama huko haikuwa kwa ajili ya kutoa matangazo
- J2 pekee hiyo ambayo mhusika aliwahi kumuona kiongozi huyu akiwa amesimama madhabahuni (mhusika hakumbuki kama ilikuwa ni wakati wa Ibada ya pili au ya kwanza; mara chache chache mhusika amekuwa akilazimika kubadilisha ratiba na hivyo wakati mwingine kuhudhuria Ibada ya kwanza badala ya Ibada ya pili), ilikuwa ni kwa ajili ya salaam kwa waumini baada ya kuwa amerudi kutoka safari ambayo ilipelekea asiwepo Kanisani kwa muda fulani wa kutosha
Hata hivyo
mara nyingi sana mhusika amekuwa akimsikia Kiongozi huyu akiwa anatajwa kwenye RATIBA ya matangazo ya J2, kuwa J2 inayofuata angekuwa zamu lakini siku za Ibada husika zilipokuwa zinawadia, zamu hizo zimekuwa zikichukuliwa na viongozi wengine na hivyo kwa muda mwingine wote ulipoita, viongozi wengine tu na si yeye, ndiyo wale ambao wamekuwa wakisimama kwenye zamu zake
Takwimu hizi hasa ni kwa mujibu wa Ibada za pili tu za Kanisa A ambazo mhusika ndiyo huwa anahudhuria.
Anachokijua mhusika kuhusu Kiongozi huyu ni kwamba kwenye RATIBA YA ZAMU huwa yupo kama kawaida na kwenye matangazo ya zamu kwa kila J2 huwa anatajwa kama kawaida ila linapofikia swala la kusimama madhabahuni kama ratiba ambavyo imekuwa ikisomwa, Kiongozi huyu amekuwa haonekani madhabahuni
Kwa hiyo J2 iliyopita
ilikuwa mara ya kwanza kwa Kiongozi huyu kusimama madhabahuni kutoa matangazo wakati wa Ibada ya Pili
Mbali na huyu, kuna kiongozi mwingine tena ambaye naye pia anaangukia kwenye scenerio hii na ambaye wako pamoja idara moja na huyu wa sasa. Huyu ni DR yule ambaye alikaribishwa na KM-A kusimama madhabahuni kusalimia waumini J2 ya tarehe 30/10/2022
Huyu naye pia pamoja na kuwa mara kwa mara jina lake limekuwa likitajwa kwenye matangazo ya zamu,
ni mara moja tu mhusika amemuona kiongozi huyu akisimama madhabahuni kusoma matangazo wakati wa Ibada ya pili
Kwa Ibada za kwanza, mhusika hana details za mtu huyu isipokuwa labda za kwenye J2 moja tu ambayo mhusika alibahatika kuwahi sana Kanisani na kukuta Ibada ya kwanza haijaimalizika, kitendo kilichopelekea kubahatika pia kumkuta Kiongozi huyu akiwa anamalizia kutoa matangazo ya Ibada ya kwanza.
Kwa hiyo, kwa Ibada za pli, viongozi hawa wawili wamekuwa mara kwa mara wakitajwa kwenye ratiba lakini ni mara moja tu mhusika amebahatika kumuona kila mmoja wao akisimama kwenye zamu hizo kama zinavyotolewa kwenye matangazo ya kila J2.
Hiki kitu kimetokea mara baada tu ya kuhamia kwenye Kanisa jipya, yaani kuanzia Desemba 2021
Mhusika hana ukakika zaidi ila anachokumbuka pia ni kwamba J2 ya tarehe 21/08/2022 Ibada ilipohamishiwa kwa dharaula kwenye Kanisa la zamani, siku hiyo DR alisimama kusoma matangazo. Baada ya Ibada kurudi tena kwenye Kanisa jipya DR alipotea tena madhabahuni, hadi leo hii
Hata hivyo mhusika anazidi kusisitiza kuwa kwa Ibada za kwanza, kabisa mhusika hana details za kutosha za viongozi hawa isipokuwa kwa Ibada za pili tu!
………………..inaendelea