UPDATE: MONDAY, 12 AUGUST 2020
Inaendelea………………………..
NAMA MHUSIKA ALIVYOWEZA KUKUTANA NA KUMKARIBISHA MHUBIRI/ KIONGOZI MGENI NYUMBANI KWAKE NA YALIYOJIRI KATIKA MAONGEZI YAO
Katika kuelezea kwa kifupi mazingira ambayo yalipelekea mhusika kukutana na Mtumishi Mgeni wa Mungu (MMM), mhusika anaomba awarudishe nyuma wasomaji hadi muda kipindi alipokuwa
uhamishoni Kanisa B
Ni kwaba ilikuwa ilikuwa J2 moja mhusika akiwa bado uko huko uhamishoni Kanisa B, ndipo alipobahatika kutana na MMM.
- IJ2 hiyo MMM alipewa nafasi ya kuhudumu Kanisani hapo
- Baada ya huduma Ibada kuu J2 hiyo, MMM alifanya mambo mawili makubwa yafuatayo
- MOJA: Alipitisha harambee kwa muda mfupi sana ambayo ilimuwezesha kukusanya kiasi cha fedha taslimu kisichopungua TZS 400,000/= (laki nne)
- PILI: Aliwaita mbele ya madhababhu akina mama wajane, kwa ajili ya kuwatamkia baraka. Wakati wakiwa wanajiandaa kwa ajili ya kuitikia wito huo, akahisi kama wanataka kukwepa wito wake, kitu kilichopelekea awakaripie kwa kuwaambia “NIMESEMA AKINA MAMA WAJANE WAPITE MBELE, ……, KWA SABABU WEWE HATA UKIJIFICHA NI MJANE TU
Maneno hayo yaliyo kwenye bold, hayakumfurahisha sana mhusika kwa sababu hayakuwa yamekaa kiroho sana, na possibly ndiyo yalisababisha amkariri sura MMM tangu siku hiyo, ukizingatia kuwa aliokuwa anawaita kwa ajili ya mibaraka, lilikuwa ni kundi la watu ambao halitakiwi kuburuzwa kwa namna yoyote ile na mtu yeyote yule bila kujali mburuzaji ni mtumishi wa Mungu ama la
Zaidi ni kuwa siku hiyo MMM alijitambulisha pia kwa umri wake akisema kuwa ana miaka zaidi ya 80. Hapa sasa ilikuwa ni kabla ya April 2017
BAADA YA MHUSIKA KURUDI TENA KANISA A AKITOKEA UHAMISHONI KANISA B
APRIL 2017:
Ilitokea kwa mara nyingine tena, MMM akaonekana na akapewa nafasi ya kutoa huduma kwenye Ibada kuu, safari hii sasa kwenye Kanisa jingine, yani Kanisa A
- Hiyo sasa ilikuwa ni August /Septemba 2018
- Ilikuwa ni zaidi ya mwaka tangu mhusika akutane kwa mara ya kwanza na MMM
- Mhusika alimkumbuka MMM
- Wakati wa huduma kanisani hapo, MMM aliuliza akitaka kujua ni waumini wangapi waliokuwa wanamfahamu
- Baadhi ya waumini walinyosha mikono, mhusika akiwa ni mmoja wao
- Baada ya huduma J2 hiyo, safari hii MMM hakufanya harambee kama alivyofanya kule Kanisa B, wala hakuombea wajane isipokuwa alitoa namba yake ya simu kwa Kanisa zima
- Namba hii ilikuwa ni kwa wale watakaohitaji msaada kutoka kwake
- Mhusika naye alichukua namba hiyo ya simu
- Ndani ya wiki iliyofuata, mhusika aliwasiliana na MMM kutaka kujua kama alikuwa na nafasi; alikuwa anahitaji msaada kutoka kwa MMM kwenye mambo kadhaa yayokuwa yakimtatiza kwa kipindi hicho
- MMM alikubali kuwa nafasi anayo, na mhusika aliwasha gari na kuanza safari ya kumfuata sehemu aliyokuwa amefikia, kwani yeye alikuwa ni mgeni hapa dare s Salaam
- Kwa maelezo yake, MMM alisema kuwa anachunga Kanisa moja huko Kongwa, Dodoma
- Alikuwa amefikia Moshi Hotel iliyopo Manzese Tip Top
Mhusika hakupata shida ya kumfuata kwa sababu yeye amekulia meneo hayo, na kuna rafiki yake ambaye ana ofisi maeneo, nyuma ya hiyo Moshi Hotel. Walikubaliana kukutana kwenye kituo cha mafuta kilichopo karibu, na mhusika alifika hapo kwa muda waliokubaliana na kumchukua MMM. Kitu cha pekee alichokiona kwa MMM siku hiyo ni kuwa alikuwa amevaa kofia. Na kwa sababu mara mbili zote alizowahi kukutana na MMM huyo ilikuwa ni katika mazingira ya Kanisani, mhusika hakuweza kujua kama MMM alivaa kofia kwa siku hiyo tu au huwa anavaa siku zote. Hili swala la kofia ni muhimu kulijua kwa sababu wakati mwingine limekuwa likitumiwa na watu kama comouflage ya wao kujificha ili wasijulikane kirahisi na watu wasiohusika, especially wanapokuwa wapo kwenye secret mission. Kwa mfano mstaafu ambaye mhusika amewahi kumwongelea huko nyuma, yule aliyewahi kukaribishwa katika mazingira ya ofisini kwa mhusika na kuendesha kikao ambacho kilithibitisha ulipwaji wa maslahi ambayo mhusika amekuwa akiyadai kwa miaka kadhaa pasipo mafanikio, naye pia alivaa kofia siku hiyo, ilhali katika kipindi chote ambacho mhusika alipata kumfahamu mtu huyu (kabla ya kustaafu kwake), hakuwahi hata siku moja kumuona akiwa amevaa kofia, kwa kipindi cha takribani zadi ya miaka 15. Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa mhusika siku hiyo kumuona mtu huyu naye akiwa amevaa kofia pia
Wakiwa ndani ya gari wakielekea nyumbani, mhusika ilibidi aweke wazi mambo kadhaa kwa MMM akimweleza kuwa yeye (mhuiska)
- Anahitaji msaada wa kiroho lakini si mafundisho ya kwenye Biblia wala si maombezi
- Anahitaji kuelekezwa tu namna ya kutatua baadhi ya mambo ya kiroho ambayo yamemtatiza
- Alisisitiza kuwa HAHITAJI KULISHWA SAMAKI, ANAHITAJI KUFUNDISHWA NAMNA YA KUVUA SAMAKI. Kwa hiyo alisisitiza sana kuwa msaada aliuohitaji kutoka kwa MMM unatakiwa uwe kwenye mfumo wa namna hiyo
Baada ya MMM kuwa amesikia hitaji la mhusika, yeye alijibu kwa kifupi tu akisema
NGOJA KWANZA TUFIKE NYUMBANI
Baada ya MMM kufika nyumbani, mhusika alieleza kwa kina kilichokuwa kinamsibu.
- lilikuwa ni tatizo la bidhaa alizokuwa ananunua kurushiwa mapepo lakini kwa wakati huo, alikuwa hajui kama hata bidhaa nazo zinaweza zikarushiwa au zikawa na mapepo.
- Alikuwa anaona madhara na kujua kuwa yanatokana na bidhaa hizo, lakini alikuwa hajui kama ni mapepo, na alikuwa hata hajui hata namna ya kulitatua tatizo hilo
- Yeye kwa wakati huo, alikuwa anajua kuwa ni binadamu tu anayeweza akarushiwa pepo na si bidhaa au kiumbe kingine tofauti na binadamu
Mhusika atalielezea kwa kina swala hili atakapokuwa anatoa wasifu wake wa nyuma wa kiroho kwenye sehemu itakayofuata. Kwa sasa itoshe tu kueleza kuwa alikuwa ananunua bidhaa ambazo akishakuwa nazo ndani nyumbani kwake au akishaanza kuzitumia, zinaonyesha kuwa haziko kawaida, na kwamba alikuwa na uwezo wa kujua hilo tu lakini pasipo kuwa na ujuzi wa namna ya kulirekebisha
Kwa hiyo, kwa kifupi tu ni kwamba mhusika alimkaribisha MMM ili ampe msaada wa namna ya kutatua tatizo hilo na kama ikiwezekana, apate msaada wa mafungu kutoka kwenye Maandiko Matakatifu yanayoweza kumsaidia kuziwekea kinga ya kiroho, bidhaa hizo alizokuwa akinunua
Baada ya mhusika kuwa amemweleza MMM hayo yote wakiwa tayari wapo nyumbani kwa mhusika:
- MMM akawa hatoi majibu yanayoeleweka, au majibu ya moja kwa moja
- Akawa anauliza uliza maswali zaidi, halafu mhusika akiyajibu, MMM anarukia tena kwenye kitu kingine au anauliza swali jingine tofauti
Hatimaye wawili hawa walipoteza FOCUS yao ya kufundishana KUVUA SAMAKI, badala yake waliingia kwenye KULISHANA SAMAKI, na ilipofikia hatua hiyo, mhusika alistukia anamuona MMM anasimama na kuanza kufanya maombi ya kimya kimya huku akigusa:
- Kila kitu kilichokuwa sebuleni kuanzia viti meza, meza ya TV, TV yenyewe, Radio n.k
- Kuta za nyumba huku akiwa anatembea, mikono akiwa ameiweka juu ya kuta mithili ya mtu aliyewekwa ukutani akisechiwa na Polisi baada ya kuwa amekamatwa
MMM akiwa amebadilika na kuwa katika mood ya namna hiyo, angeweza hata kufungua mlango wa kuingia master bedroom, ili aendelee na maombi hayo ila aligundua kuwa mhuiska hakuwa tayari kwa hili
Kwa ufupi tu ni kwamba, mpaka hapa MMM:
- Hakufanya kile alichokuwa amemwahidi mhuiska kuwa atafanya, maana wakiwa bado wako njiani mhusika baada ya kuwa ameeleza hitaji lake kwa MMM, mwenyewe alijibu kwa kusema NGOJA KWANZA TUFIKE NYUMBANI
- Kufika nyumbani kwa mhusika kwake ilikuwa muhimu zaidi kuliko kufanya kile ambacho mhusika alikuwa amemwitia / ameomba asaidiwe. Target kubwa ya MMM ilikuwa kufika nyumbani kwa mhuiska
- Alianza kufanya maombi ya kimya kimya nyumbani kwa mhusika, kitu ambacho mhusika hakuwa anahitaji
- Hakuweza kumwonyesha mhusika tiba halisi ya tatizo alilokuwa nalo, bidhaa alizokuwa akinunua na hatimaye kupelekea matatizo anapozitunia
- Hakufanya kile ambacho aliitiwa, alifanya kile alichotaka kufanya mwenye, na hakufanya hivyo kwa bahati mbaya au kwa kupitiwa
As a temporary measure, yeye (mhusika) chochote kile kilichokuwa kinamletea matatizo alikuwa anakitupa bila kujali gharama. Kuna kipindi aliwahi kuchana na kutupa kiatu kipya ambacho alikinunua kwa TZS 180,000/= . Pia ni bidhaa nyingi tu za thamani ambazo alikuwa akizitupa, mostly sabuni za kuogea na vitu kama kahawa au majani ya chai
Wakati MMM anakaribia kuondoka, ndiyo mhusika akaomba angalau amwachie pia mafungu ya kwenye Biblia, na ndipo MMM alipomtajia kutoka kichwani, mafungu ambayo tayari ameshayaongelea hapo juu, ambayo ndiyo yalipelekea sasa mhusika kuona pattern nyingine kwenye mafungu aliyokuwa natumia Kiongozi Mkuu wakati akifundisha mafundisho yenye kichwa SISI NI WATU WA NENO pamoja na LUPENDO KATIKA UTUMISHI WETU.
Vile vile, wakati mhusika anamchukua MMM kumrudisha Hotelini, mtu huyu alirudia kufanya kosa jingine tena. Aliuliza swali akisema HILI GARI NI LA KWAKO AU LA OFISINI?
Hili swali lilimpa indicator nyingine tena mhusika kwa sababu MMM
- Alifika nyumbani kwa mhuiska na kukiri kuwa kuna majirani zake na mhusika anawafahanu, na kwamba alishawahi kufika nyumbani kwao
Hawa walikuwa ni wale ambao kwa sasa ni wastaafu na kwa muda huu walishahama. Kipindi hicho walikuwa bado wapo, ila walikuwa wameshabadilisha nyumba ya Ibada kutoka Kanisa A na kuhamia Changanyikeni
- Alikuwa anajua kuwa nyumba hizo ni za watumishi wa umma
- Si mtu ambaye uelewa wake uko katika kiwango (au hata kukarinbiana tu na kile) cha kutoweza kutofautisha kati ya namba za usajili za gari ambalo ni la umma na lile ambalo ni la mtu binafsi
- Alikuwa ameziona namba za gari la mhusika kipindi mhusika anampokea MMM na kumchuka pale kituo cha mafuta Shekilango
….itaendelea
2Wakorintho 5:14
2Wakorintho 5:15
2Wakorintho 5:17
2Wakorintho 5:14
14 Maana, upendo wa Kristo watubidisha; maana tumehukumu hivi, ya kwamba mmoja alikufa kwa ajili ya wote, basi walikufa wote;
2Wakorintho 5:15
15 tena alikufa kwa ajili ya wote, ili walio hai wasiwe hai tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa akafufuka kwa ajili yao.
2Wakorintho 5:17
17 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.
MUBARIKIWE TENA NA BWANA
NEXT: 1 Yale ambayo mhusika alikuja kuyabainisha kuwa MMM alikuwa ametumwa kuja kuyafanya nyumbani kwake mhusika
2 Wasifu wa kiroho wa mhusika tangu aanze kuwa muumini wa kanisa A hadi siku wanakutana na MMM
MwiH
elly obedy