A MUST READ POST
KUNA AKILI KUBWA IMETUMIKA HAPA IWAPO TU MATUKIO HAYA YALIYOELEZEWA HAPA YATAKUWA SIYO COINCIDENCES
…………………………..inaendelea
MAELEZO KAMILI YA TUKIO LENYEWE
J4 ya tarehe 19/01/2021 mhusika alipofika ofisini alikuta kuna mafundi ujenzi wanaendelea na shughuli za ukarabati wa jengo kwa nje, usawa wa mojawapo ya madirsiha ya ofisi yake iliyoko ghorofa ya kwanza. Kutokana na pilika pilika zilizokuwa zikiendelea, aliamua atoke kidogo ofisini akafuatilie maswala mengine ya muhimu kwake kwa kutarajia kuwa mpaka atakapokuwa manarudi, mafundi hao wanaweza kuwa wamesogea sehemu nyingine na hivyo kelele hizo zitakuwa zimepungua
Mhusika aliamua kutoka ofisini na kuelekea sehemu nyingine kwa ajili ya kufuatilia swala la maji ambayo yalikatwa tangu Novemba 2018 pamoja na umeme uliopungua nguvu kwenye baadhi ya sehemu ndani ya nyumba yake. Mara ya mwisho alifanya hivyo ilikuwa mwanzoni mwa mwezi Desemba 2020. Kwa hiyo alienda kukumbushia maswala hayo mawili ili aweze kupata msaada wa haraka kama inawezekana
Baada ya kuwa ametoka huko, kipindi fulani akiwa juu ghorofa ya kwanza akiwa anapunga upepo, alibahatika kumuona office mate na swahiba wake akiwa anatembea chini kuelekea kwenye parking.. Office mate huyu ni mpya kiasi pale ofisini na kabla ya hapo alikuwa anafanya kazi ofisi ya mkuu wa taasisi aliyepita, yaani yule ambaye kwa sasa ni mstaafu. Huyu office mate akiwa yuko chini nje ya jengo, (ground floor) alimjulisha mhusika kuwa kuna mtu XXX alikuwa anamtafuta mhusika. Mhusika alishukuru kwa ujumbe huo na kumjulisha office mate kuwa atajitahidi kuhakikisha kuwa anafanya mawasiliano na mtu huyo XXX
Siku moja kabla ya siku hiyo, mafundi wawili walifika ofisini kwa mhusika wakijitambulisha kuwa kuna kazi wanatakiwa wafanye na walimtaja mtu anayehusika ndani ya jengo ambaye wameelekezwa kwake, walimytaja YYY.Baadaye tena YYY allisema anayehuiska ni XXX, ambaye kwa J3 hiyo mhusika hakuweza kuonana naye na ndiyo maana ilibidi waonane J4
Zaidi ni kuwa wiki jana kwenye J5 au Alhamis, mhusika alikwa tayari ameshaanza pilika pilika za kuandaa barua ya kwa ajili ya kudi maslahi yake, akionekana akipita kwenye korido na nakala za vielelezo muhmi kwa ajili ya mpango wake huo
Tukirudi tena kwenye mtiririko wa mada yetu. Hatimaye mhusika alitoka hapo kwenye korido ghorofani akawa anaelekea ofisini kwake
- Office ya XXX iko njiani kabla haujafika ofisini kwa mhusika
- Alipofika usawa wa pale ilipo ofisi ya XXX, mhusika alijaribu kufungua kitasa cha mlango,lakini ulikuwa umefungwa,
- Kwa hiyo XXX hakuwamo ofisini na hata wenzake wawili ambao huwa yuko nao humo siku zote nao pia hawakuwamo
- Mhusika akaendelea mbele kuelekea ofisini kwake
- Jirani kabisa mkabala na ofisi yake upande wa kushoto ukiwa unaelekea ofisini kwake, kuna chumba kingine kinaitwa MICROSCOPE.
- Kabla mhusika hajaingia ndani ofisini mwake, walikutana ghafla na XXX kwenye korido ndogo inayotenganisha chumba hiki na ofisi ya mhusika
- Kumbe XXX alikuwa ndani ya chumba hicho tajwa kwa muda akwa anamsubiria mhusika
- Kwa wakati huo, mhusika hakuweza kujiuliza swali la kwa nini XXX hakuwa amekaa ofisini kwake akamsubiria mhusika humo, na badala yake aliaamua kwenda kumsubiria kwenye chumba hicho ambacho ni nadra sana kwake XXX kuonekana humo
Mpaka hapa, kuna coincidenceskadhaa zinajitokeza wazi kwenye tukio hili au kama sivyo basi kulikuwa na super plan. Hii ni kutokana na ukweli kuwa kwenye korido la floor hiyo kuna kamera. Hivyo basi:
- Iwapo mhusika angemkuta XXX ofisini kwake halafu baada ya hapo wakaongozana wote kuelekea ofisini kwa mhuiska ili wakaongee kuhusiana na swala lile lililomfanya XXX amtafute mhusika pindi alipokuwa ametoka kidogo, korido hiyo ina Kamera ambayo ingewaonyesha wawili hao wakiwa wanaongozana kuelekea ofisini kwa mhusika
- Iwapo kwa upande mwingine kama mhusika angemkuta XXX akiwa ndani ofisini kwake, Kamera hiyo vile vile ingemwonyesha mhusika akiingia ofisini kwa XXX, na baada ya muda kadhaa kupita, ingemwonyesha akiwa anatoka tena ofisini humo aidha peke yake au wakiwa wawili na XXX
- Kamera hiyo ingeonyesha pia “lapse of time” ambayo mhusika angeitumia akiwa ndani ya ofisi ya XXX na hadi muda ambao alitoka humo ofisini kwa XXX
- Muda huo pamoja na matukio mengine ambayo yangekuja kuwahusisha wawili hawa baadaye, ungedhihirsha wazi kuwa kulikuwa na muda fulani waliutumia aidha kwa maongezi fulani maalumu possibly kwa ajili ya kazi fulani maalum ambayo walipangiwa kuifanya kwa ushirikiano
Hata hivyo, mpaka muda huu na baada ya matukio mengi kupita, kwa sasa,
INAONYESHA KAMA Kitendo cha XXX kuwa ndani ya chumba cha MICROSCOPE akiwa anamsubiria mhusika kwa ajili ya maongezi, badala ya kuwepo ofisini kwake, akikitumia chumba hicho kama
“shield” ya yeye kujikinga na Kamera iliyoko kwenye Korido.
- Chumba hiki kimekaa katika namna ambayo ukifungua mlango wake, anayeelekea ofisini kwa mhusika hawezi kupita kwanza mpaka pale utakapofunga
- Mlango huu una uwezo wa kumkinga mtu aliye ofisini kwa mhusika asionekane na watu walioko kwenye korido
- Malngo huu huwa unafunguka kwa nje ya kikorido kidogo na hivyp mhusika anaweza kupita tu kuelekea ofisini kwake pindi mlango huu unapokuwa katika position ya kufunga, na si katika position ya kufungua
- Mlango huu unapokuwa umefunguliwa una uwezo wa kumkinga mtu anayeingia ofisini kwa mhusika asionekana na Kamera ya kwenye Korido
- Kamera ya kwenye korido huwa inarekodi matukio hadi ofisini kwa mhusika hata kama mlango wa ofisi yake umefunga kwa sababu mlango huo una nusu kioo kwa juu
Zaidi ni kuwa sehemu ambayo mhusika huwa anakaa siku zote ndani ya ofisi hiyo, iko accessible na Kamera iliyoko kwenye korido kwa sababu kioo kilicho kwenye mlango huo. Kwa hiyo ni likely (hana uhakika) kwamba Kamera hii huwa imekaa imemumulika muda wote pindi anapokuwa yupo ofisini kwenye meza yake
Baada ya XXX kuwa wamekutana na mhusika katika mazingira hayo, XXX alimweleza mhuiska kuwa kuna matengenezo ambayo inabidi yafanyike siku hiyo ofisini kwake, na hivyo itabidi kwa muda abadilishe sehemu ya kukaa, kuwapisha nafundi ili waweze kufanya kazi yao. Hata hivyo ilikuwa ni ghafula mno ila mhusika hakuwa na pingamizi lolote lile katika hilo kwa sababu
- XXX alionekana kuwa amepewa maelekezo kutoka ngazi ya juu na hivyo kwa wakti huo XXX alivaa koti la la wakuu wa kazi wa mhusika
- Mhusika hakuwa na chochote cha ziada cha kuhoji isipokuwa kuruhusu kazi ziweze kuendelea
Kabla ya kazi kuanza, mhusika hakuona sababu ya kubadilisha sehemu ya kukaa, alisubiri mafundi waje waanze kazi kwanza halafu ndiyo abadilishe sehemu ya kukaa. Aliendelea kukaa pale pale ambapo watu wote huwa wanapita kwenye korido na kumuona amekaa kupita kioo cha mlango wa ofisi yake hiyo
Kama angeamua kubadilisha sehemu ya kukaa kabla mafundi hawajaanza kazi, baadhi ya watu anbao wameshazoea kumuona akiwa amekaa mahali pale siku zote wangeweza kudhani kuwa hayumo ofisini, ametoka. Vile vile hata kwenye kamera asingeweza kuonekana pia
Mapema siku hiyo, kuna wakati XXX aliwaleta rasmi mafundi hao na kuwatambulisha rasmi kwa mhusika, mmoja wao akiwa ni yule ambaye jana yake aliwahi kufika tena ofisini ila wakati huo ilionekana kuwa XXX hakuwepo
Baada ya utambulisho huo, mafundi hawa waliondoka na baada ya masaa kadhaa kupita, walirudi na kuja kuchomeka nyaya kwenye socket ya umeme na kuondoka tena
- Baada ya hapo ndipo sasa mhusika alipolazimika kubadilisha sehemu ya kukaa
- Alihamisha meza yake na baadhi ya vitu na kusogea ndani zaidi pamoja, sehemu ambayo watu waliozoea kumuona kutokea kwenye korido, wasingeweza kumuona tena na wengine walidhani kuwa pengine hakuwamo ofini mwake, lila alikuwemo
Baada ya hapo, mafundi waliondoka tena na baada ya masaa kadhaa kupita tena na kabla hawajarudi,
umeme ulikatika
Umeme ulirudi mida ya karibia saa 10, na baada ya hapo
- XXX alifika tena ofisini kwa mhusika akiwa ameambatana na fundi aliyechomeka nyaya asubuhi kabla ya umeme kukatika
- XXX akashauri mafundi waanze kazi muda huo, lakini mhusika akatoa udhuru kwamba muda wa kuondoka kwake ofisini ulikuwa umekaribia na hivyo akashauri kazi ianze kesho yake
- XXX akamshauri mhusika awaachie funguo zake za ofisi ili waendelee na kazi yeye atakapokuwa anaondoka baada ya saa kumi
- Mhusika naye tena akamshauri XXX akachukue funguo za akiba za ofisi hiyo, ambazo huwa zipo muda wote ofisini kwa Mkuu wa Idara, watumie hizo
- XXX akafanya hivyo lakini baadaye alirudi mikono mitupu akisema kuwa hapakuwepo na funguo za ziada
Mhusika akashangaa kusikia hilo kwa sababu funguo hizo zimekuwepo siku zote, miaka yote. Hata hivyo walishauriana hatimaye wakakubaliana kazi ianze kesho yake kwa sababu muda ulikuwa umeenda, na muda rasmi wa masaa ya kazi ulikuwa unaisha. Vile vile umeme nao pia ulionekana kuwa umerudi sehemu sehemu, kiasi kwamba socket zote hazikuwa na umeme
Hiyo siku ikawa imepita hivyo, ambayo sasa hii ndiyo J4 ya wiki hii
……………………..inaendelea