Makanyaga
JF-Expert Member
- Sep 28, 2007
- 11,129
- 7,321
- Thread starter
- #541
BAADA YA BARUA ZA MHUSIKA KUPITIA MKONDO WA ZAMANI KUWA ZINARUDI: WALICHOONGEA MHUSIKA NA KAIMU MKUU WA IDARA (K-MWI) OFISINI KWA MKUU HUYO
……………..inaendelea
KMH alifika ofisini kwa mhusika na kumjulisha kuwa K-MWI alikuwa anamhitaji waongee ofisini. K-MWI huyu hakuwa yule wa siku zote, yule wa siku zote alikuwa yuko safarini
Tangu tarehe hiyo hadi J3 nyingine tena ya tarehe 01/03/2021 hapakuwa na chochote kile kisichokuwa cha kawaida isipokuwa kuanzia J4 ndiyo kukaanza kujitokeza pilika pilika zisizokuwa za kawaida na kupelekea mhusika kuamua kufuatilia kuona kama barua yake ya kwanza ilifika kule alikokuwa ameielekeza, kwa sababu hiyo ndiyo ilikuwa barua pekee iliyosemekana kutumia mkondo sahihi wa mawasilano. Barua hiyo aliikuta haijafika huko. Hata hivyo ile ambayo alidhani kuwa ilitumia mkondo usio sahihi, na ambayo alikuja kuiandika nyuma ya ile ya kwanza, yenyewe pekee ndiyo aliikuta imeshafika kunakohusika
MUBARIKIWE TENA NA BWANA
……………..inaendelea
KMH alifika ofisini kwa mhusika na kumjulisha kuwa K-MWI alikuwa anamhitaji waongee ofisini. K-MWI huyu hakuwa yule wa siku zote, yule wa siku zote alikuwa yuko safarini
- Mhusika alitikia wito huo na kuelekea ofisi ya MWI kwa ajili ya maongezi hayo
- K-MWI alimweleza mhusika kuwa barua zake anazoandika kupitia mkondo wa mawasiliano wa zamani zinarudi
- Zaidi K-MWI alimuuliza swali mhusika kuwa “sasa tufanyeje?”
- Mhusika alimjibu K-MWI kuwa inabidi hilo zoezi tulisitishe kwanza, akimaanisha kuwa aache kwanza kushughulika na swala la barua hizo kwa sababu lilikuwa linamletea utata kwa kuwa na mawasilano ambyao ni ya aina mbili
- K-MWI alimjibu mhusika akisema kuwa “hizi hela ni za kwako, inabidi uzipate. Leo upo kesho haupo”
- Mhusika alimjibu bosi wake huyo kwamba hela hizo atazipata. Vile vile alimweleza kuwa hakuna haja ya kuwa na haraka kiasi hicho kwa sababu zimekaa muda mrefu muno