“KANISA B”, “KANISA B”, “KANISA B”, “KANISA B”, “KANISA B”
MZEE KIONGOZI WA KANISA B (MZK-B)
MATUKIO MUHIMU SANA AMBAYO MZK-B AMEWAHI KUYAFANYA KIPINDI MHUSIKA ALIPOKUWA KANISA B
TUKIO MUHIMU –I: MAELEZO YA UTANGULIZI YA TUKIO LENYEWE
Ikumbukwe kuwa mhusika alihamia Kanisa B tarehe 14 April 2017, kwa hiyo hadi kufikia tarehe 7 Julai 2017, mhusika alikuwa hajakamilisha hata miezi mitatu akiwa yupo Kanisa A. Na kwa hali hiyo basi, hadi kufikia kipindi hicho, Kiongozi Mkuu wa Kanisa B (KM-B) alikuwa bado hajamfahamu vizuri mhusika, pamoja na watu wengiine baadhi, ukiondoa kikundi lmaalumu chini ya MZK-B ambacho chenyewe kumbe klilikuwa tayari kimeshafnaya
“phishing’ ya taarifa zake kutoka kwa wale wanamfahamu,yaani kule alikokuwa ametokea, Kanisa A
MWANZONI MWA JULAI 2017: MHUSIKA APATA WAZO LA KIBIASHARA AKIWA YUPO OFISINI KWAKE ANAFANYA KAZI
Siku moja akiwa yuko ofisini, Julai 2017, mhusIka alijiwa na wazo fulani la kibiashara na kuamua kulifanyia kazi.
Baada ya wazo hilo kuwa limemjia
- Aliamua kuingia kwenye website ya Kampuni ambayo ilikuwa inahusiana na wazo lake hilo na akafanikiwa kupata mawasiliano ya simu ya Kampuni hiyo
- Alivyowapigia akitaka kujua zaidi juu ya details za bidhaa zao, kampuni hiyo walifurahi sana na wakaenda mbali kwa kumuuliza yeye anaishi maeneo gani hapa Dar es Salaam
- Alipowatajia sehemu anayoishi, ikaonekana kuna wakala wao mwingine ambaye anaishi maeneo jirani na eneo analoishi mhusika, na wakamwahidi kuwa wakala wao huyo anaweza akapata nafasi ya kumpitishia mhusika brochure zao katika moja ya safari zake atakapokuwa anarejea nyumbani jioni akitokea ofisini
Maongezi hayo hatimaye kweli yalipelekea siku moja ndani ya wiki hiyo, wakala wa kampuni hiyo kufika nyumbani kwa mhusika akiwa na brochure za kampuni yao kwa ajili ya kumkabidhi mhusika. Baada ya hapo wakala huyu aliaga kuelekea nyumbani kwao, na kwa sababu hakuwa na gari, mhusika aliamua kumepeleka angalu kituo cha mwisho cha karibu na anapoishi
- Wakala huyu alikuwa ni binti umri kati ya miaka 24-26
- Wakati wa maongezi yao na mhusika, binti huyu alimjulisha mhusika kuwa weekend hiyo wangekuwepo pia Mlimani City kwa ajili ya matangazo zaidi ya bidhaaha zao, ikiwa ni pamoja na kugawa brochure kwa watu mbalimbali ambao huwa wanafika hapo
- Binti huyu alimkaribisha mhusika aweze kufika pia Mlimani City Jumamosi ya wiki hiyo, na mhusika alikubali
Ilipofika Jumamosi, kweli mhusika alifika mlimani city na akawa amefanikiwa kufika kwenye banda la Kampuni hiyo, na huyu binti akiwa ni mmoja wa waliokuwepo kwenye banda hilo siku hiyo.
Kumbe huku nyuma kulikuwa na watu wanafuatilia mienendo hiyo na hadi kufikia hatua hii, wakawa wame-conclude kwamba mhusika na binti huyu wameshakuwa na mahusiano.
- Baada ya hapo taarifa hizi zikapelekwa kwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa B (KM-B)
- Zaidi ya kupelekewa taarifa hizi, KM-B, akashauriwa pia kuwa kesho yake (yaani Jumapili) wakati wa Ibada, aitishe wazinzi wapite mbele madhabahuni
Kesho yake mhusika akiwa yupo kanisani, alistukia mara KM-B anasimama na kuanza kuita watu wazinzi wapite mbele. KM-B aliita mpaka akachoka, pande kuu nne za Kanisa, hakuna mtu aliyejitokeza. Kwa kifupi ni kwamba siku hiyo KM-B hakupata mtu yeyote ambaye aliitikia wito wa tuhuma hizo, hapakuwa na mtu hata mmoja. Mzee wa watu alionekana wazi kabisa kuaibika baada ya kukosa mtu hata mmoja, wakati kwa kumwamngalia tu wakati anasimama na kuanza kuita watu, alikuwa na uhakika kabisa kuwa lazima kulikuwa na mtu mmoja. Hakuwa amepewa maono na Roho Mtakatifu bali alikuwa maeelezwa na chanzo ambacho alikiamini kuwa ni cha uhakika na ambacho hakiwezi kumdanganya
Hapa vijana wa kisasa huwa wanasema “aliingizwa uchaka” mithili ya siku ile ya tangazo la MABOMU YA MAREKANI. Siku hii nayo pia alikuwa ameshauriwa kuwatambulisha baadhi ya watu mbele ya kundi la watu wengi wageni kanisani hapo, mhusika akiwa mmoja wao, kitu ambacho hapo awali, mhusika na KM-B walikuwa wamekubaliana kuwa wasiwe wanakifanya, unless kama kuna ulazima wa sana wa kufanya hivyo.
……………..inaendelea
NEXT:
MARA YA KWANZA MHUSIKA AGUNDUA WALAKINI KWENYE TANGAZO LA UZINZI LA KM-B NA KUANZA KUONA KUWA KUNA UWEZEKANO LILIKUWA LIMEPIKWA
- Ni baada ya kupata taarifa kutoka kwa MKE WA “KIONGOZ-XB”
- “KIONGOZ-XB” ni yuke ambaye aliwahi kuwa mwenyeji wa Kiongozi Mkuu wa Kanisa A, siku kiongozi huyo (KM-A) alipozuru Kanisa B,
- Vile vile, huyu “KIONGOZ-XB” ndiye aliyewahi kumtuhumu mhusika mbele ya KM-A kuwa alihama Kanisa A na hakumuaga KM-A kwa kusema “kumbe huyu mtu aliondoka na hakukuaga!”
Kwa wasomaji wa tangu mwanzo wa taarifa hizi, hawawezi kupata shida kumjua “KIONGOZ-XB” japo huko nyuma mwandishi anaweza akawa amemtaja kwa jina tofauti
- Kwa hiyo hints hizi ambazo alianza kuzipata mhusika, zilikuwa zinatoka kwa MKE WAKE na “KIONGOZ-XB” na si kwake yeye “KIONGOZ-XB”
- Baada ya kupata taarifa za walakini wa tangzao hilo lililowahi kutolewa na KM-B, mhusika kwa mara ya kwanza aliona walakini kutoka kwa kiongozi wake huyo
Hata hivyo kwa sasa anaelewa vizuri kilichotokea, ni MZK-B alikuwa kazini na yote yaliyokuwa yametokea yalikuwa ni mapishi kutoka kwa MZK-B