#COVID19 Mkasa wa kipekee kuhusu pilikapilika za kujikinga na COVID-19

#COVID19 Mkasa wa kipekee kuhusu pilikapilika za kujikinga na COVID-19

KILE AMBACHO WAGENI HAO WALIWAHI KUMTONYA MHUSIKA WALIPOFIKA OFISINI KWA MARA YA PILI NA AMBACHO KILIPELEKEA MHUSIKA KUANZA KUWAONA KUWA PENGINE HAWAKUWA NA NIA NJEMA

Ikumbukwe kuwa MG-MF aliporudi kwa mara ya pili idarani kwa mhusika, aliambatana pia na boss wake mwingine ambaye hakuwa ameambatana naye kwenye safari ile ya mwanzo

Kwenye safari ile ya mwanzo, MG-MF alifika idarani kwa mhusika akiwa amembatana na subordinates wake tu

Kwa hiyo, baada ya MG-MF kurudi safari ya pili akiwa na boss wake,

  • MG-MF alimweleza mhusika kuwa boss huyo alikuwa amekuja kwa ajili ya kukiona kifaa kilichokuwa kinatakiwa kwenda kufanya kazi na hivyo mhusika alilazimika kuwapeleka mahali kilipokuwepo kifaa hicho ili boss huyo aweze kukiona
  • Kifaa kilikuwa ground floor, na hivyo ilibidi ashuka nao wote huko ground floor
Baada ya kuwa wamezimaliza tu ngazi zinazoshuka chini (kabla hawajaingia kwenye sehemu kifaa kile kilipokuwa, wakiwa bado wapo kwenye veranda)

Wakiwa katika configuration ya kumzunguka hivi, walisiama na kumtonya mhusika kuwa kazi hiyo ilikuwa anaambatana na hela nyingi za pembeni na kama ataamua, mhusika anaweza kutengeneza hela nyingine kwa kutumia mgongo wa nyuma na bila ya taasisi yake anayofanyia kujua hilo.

I see! Hapa napo ndipo walipomtibua tena mhusika kwa mara nyingine!


Hapa mhusika aliwajulisha wageni hawa kuwa miezi kadhaa tu iliyokuwa imepita nyuma, kuna gari jipya la mamillion ya fedha alilokuwa ameagiza kutoka Japan, ambalo amewaachia watu kwenye gereji baada ya kuwa wamefanya upumbavu. Wakati huo, gari hilo ndiyo lilikuwa lina takribani miezi sita tangu aliache pale gereji

Mhusika aliwajulisha kuwa madili ya kijinga huwa hafanyi na walimwelewa kwa hili na hawakuweza kulirudia tena katika maongezi yao yote yaliyofuata baada ya pale

Mhusika hana kumbukumbu nzuri kuhusiana na kiasi cha fedha aliyopata kwenye kazi, lakini haikuzidi TZS 700,000/=

Labda MWI ndiyo anaweza kuwa pengine alipata kitu ch maana kwa sababu kwenye kazi ile ya kwanza ambayo set-up yake inaonekana kufanana mno na hii, alisemekana kuwa alikamata million 10 (TZS 10,000,000/=); hana uhakika sana na hili

Set-up ya kwenye kazi hii ya million 10 na ambayo mhusika aliielezea mwanzo, inafanana kabisa na hii ya pili ambayo mhusika alishindwa kufanya kazi mwenyewe na kuamua kuwapa watu wengine waifanye

Kikubwa tu ambacho wasomaji wa taarifa hizi inabidi wakielewe ni kwamba SAFARI ZOTE HIZI ZA HATARI ZILIANZA KUJITOKEZA MARA TU BAADA YA SENIOR MSATAAFU WA KIUME (SMME) KUPANDA CHEO NA KUFIKIA KWENYE NGAZI YA PILI KWA UKUBWA NDANI YA TAASISI

MUBARIKIWE TENA NA BWANA

UPNEXT: SAFARI YA NNE, NJE YA NCHI; AFRIKA KASKAZINI (JUNE-JULY 2012)


  • Hii ni safari ile ambayo hakufanikiwa kuifanya
  • Angefanikiwa kuifanya, angeondoka idarani akimwacha MWI–A na angerudi idarani na kukuta kuna MWI mwingine B
  • Safari ilikuwa ni ya kiofisi; ila ya hiari
  • Theme yake ilikuwa inahusiana na data za matetemeko ya ardhi
  • Ni safari ambayo alishauriwa kuifanya na MWI na siyo Boss X
……………….inaendelea
 
Kwenye safari hizi nne ambazo maelezo yake yamekuwa yakiendelea, hizi mbili za mwisho mhusika alishawahi kuwasilisha maelezo yake kwa “SPECIALIST” mwaka 2016
 
WTF huyu jsmaa analipwa na JF au!?.. what a special privilege!?

Kinda like Days of our lives au isidingo the need.

Fascinating!!?
 
UPDATE:TUESDAY 21ST JUNE 2022

SAFARI YA NNE: SAFARI YA MOROCCO-JUNE-JULY 2012 (HAKUIFANYA)


Safari hii ilikuja siku kadhaa tu baada ya mhusika kurudi kutoka kwenye safari ya kiofisi ya ndani ya nchi ambayo ameieleza hapo juu.

Ikumbukwe kuwa kwenye safari hiyo, alienda akauktana na kufahamiana na watu wa Afrika ya Kaskazini, na mara baada tu ya kutoka huko ndiyo akawa ame-passiwa safari hii nyingine ya kwenda Morocco

Safari hii ilikuwa ya Morocco ililetwa kama surprise kwake kwa sababu taarifa zake zilikuwa ni za ghafla sana na ambazo hazikuhusiha maongezi yoyote ya ana kwa ana kati yake na Mkuu wa Idara (MWI) wa wakati huo. Safari hii ilitakiwa ifanyike ndani ya miezi miwili ya kati ya June na July 2012 na ilikuwa ni ya wiki nne

“PLOT

Asubuhi moja (ilikuwa mwezi April/May) mhusika akiwa ndiyo anaingia ofisini, alikuta kijikaratasi mlangoni; chini kwenye grill ya mlango

Kikaratasi hicho kilikuwa na mwandiko wa MWI, na kilionyesha anwani ya kwenye mtandao (website address) iliyohusiana na mkutano wa data za matetemeko ya ardhi uliokuwa unafanyika Morocco kwa muda wa wiki nne; ndani ya miezi ya June na July 2012

Hata hivyo, MWI huyu aliyekuwa amemwandikia mhusika ki-note hicho, muda wake wa utawala kwa awamu nyingine ya pili ya miaka mitatu; ulikuwa unaishia 30 June 2012

  • Kuanzia 01 July 2012, MWI mwingine mpya alikuwa anatarajiwa kuingia ofisini
  • Kwa hali hiyo, kama mhusika angeamua kusafiri; angeondoka idarani akiacha kukiwa na MWI-A tuseme; na kama angebahatika kupata bahati ya kurudi salama, basi angerudi na kukuta kuna MWI mwingine, tuseme MWI-B
Safari hii ilikuwa ni optional na hivyo mhusika aliamua kutokuifanya, na badala yake kuna mtu mwingine ambaye alihudhuria safari hiyo; mwanafunzi wa ngazi ya juu aliyekuwa anafanya masomo ya juu chini ya usimamizi wa Boss X

PROGRAM YA MOROCCO ILIKUWA PIA NA KIPENGELE CHA KUTEMBELEA OBSERVATORIES

Kipengele cha pekee kilichokuwepo kwenye ratiba ya program hii ya Mororcco ambacho hakikuwahi hap awali hakikuwahi kuwepo kwenye program nyingine zote ambazo mhusika alikuwa amewahi kuhudhuria ni kwamba washiriki wote walikuwa wanatakiwa pia kutembelea OBSERVATORIES. Hizi ni research centres ambazo zinakuwa tailor-made kwa ajili ya intensive research kwenye nchi husika. Mshiriki aliyebahatika kuhudhuria mkutano huo alisema kuwa walipokuwa wanatembelea observatories hizi, wakati mwingine walikuwa wanalazimika kusafri kwa mabasi wakipita kwenye mapori mazito, na kwa umbali mithili ya ule wa kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza

MABADILIKO YA UONGOZI YALIYOWAHI KUTOKEA IDARANI KWA MHUSIKA KUANZIA 01 JULY 2012

Ilipofika 01 July 2012, MWI mwingine mpya aliingia madarakani na mara baada tu ya kuanza kazi: alianza mkakati wa kusuka tuhuma kwa mhusika possibly ili afukuzwe kazi; huku akiwa anashirikiana na Boss X

  • Baada ya mhusika kugundua mbinu hizo; siku moja wakiwa wapo kwenye mojawapo ya kikao ambacho MWI-B alikuwa amemwita mhusika ofisini kwa MWI ili kujibu tuhuma zilizokuwa zimepelekwa kwake (MWI-B) na Boss X; kwenye kikao hicho siku hiyo, mhusika alishauri tuhuma zake zote zinazomkabili ziwekwe kwenye maandishi ili na yeye aweze kuzijibu kwa maandishi
  • Hapa ilikuwa ni baada ya mhusika kuwa tayari ameshagundua kuwa kuna maneno ya majungu yaliyokuwa yanatembea chini chini kuhusiana naye, na ambayo yalikuwa yamekusudiwa ku-trigger vikao kadhaa vya tuhuma za mara kwa mara kwa mhusika, ili hatimaye wamfukuze kazi huku uthibitisho ukiwa ni zile minutes za vikao hivyo na kwa tuhuma za kutembea mdomoni mwa watu tu
Kwa hiyo baada ya mhusika kugundua hilo alitamani sana kwamba tuhuma hizo sasa ziwekwe kwenye maandishi, badala ya kuwa zinatembea kwenye midomo ya watu tu na ambao alikuwa na uhakika kabisa kuwa hawakuwa na nia njema naye

  • MWI-B huyu ndiye pia alishiriki kupanga safari ya mhusika kwenda Entebbe, Uganda mwezi Desemba 2012 ambayo nayo pia hakufanikiwa kuifanya
  • Baada ya kuwa amepanga safari hiyo, pale zilipokaribia tarehe zile ambazo mhusika alitakiwa kusafiri, MWI-B huyu naye aliamua kusafiri na kukamimisha mamlaka ya ukuu wa idara kwa mtu mwingine
Kwa hiyo kama mhusika angesafiri, ruhusa ya safari yake ingepitishwa na Kaimu MWI ambaye alikuwa ameachiwa ofisi kwa wakati huo

  • Huyu Kaimu MWI hakuwa mwingine bali yule aliyekuwa amemaliza muda wake 30 June 2012
  • Mbali na hilo, MWI huyu mpya ndiye alikuja sasa aka-facilitate swala la mhusika kushushwa cheo na hatimaye kukatwa mshahara tangu June 2014, na kuanzia pale mshahara huu haukuwahi kuongezeka; ukiwa unalipwa kwake underpaid hadi kufikia mwaka juzi Oktoba 2021 uliporekebishwa tena kwenye salary slip tu na si kwa barua yoyote.
  • Wakati mshahara wa mhusika unakatwa, MWI-B alikuwa amekamisha tena ukuu wa Idara kwa mtu yule yule ambaye ametajwa hapo juu na ulikuwa ni wakati wa kukamilisha kujaza OPRAS za mwaka wa 2011/2012.
  • Kwa hiyo wakati OPRAS hizi zinajazwa, MWI-B hakuwepo idarani; ila alikuwa amekaimisha tena madaraka kwa yule waliyewahi kupishana naye wakati yeye (MWI-B) anaingia madarakani
Zaidi ni kuwa tangu pale mhusika hakuwahi kupanda cheo tena hadi leo

HITIMISHO

KUHUSIANA NA SAFARI AMBAZO MHUSIKA HAKUWAHI KUZIFANYA


Safari pekee ambazo mhusika hakuwahi kuzifanya ni mbili tu

  • Safari ya Morocco June-July 2012
  • Safari ya Entebbe, Uganda; Desemba 2012
Hii ya Entebbe ndiyo ile ambayo ndege ilikuwa inaingia huko kuanzia saa 5:00 usiku, baada ya kuwa imepitia nchi nyingine jirani kwanza

KUHUSIANA NA NCHI SHIRIKI KWENYE MIKUTANO YA KUCHAKATA DATA ZA MATETEMEKO YA ARDHI AMBAYO MHUSIKA ALIWAHI KUSHIRIKI

Ukiondoa nchi jirani ambazo zilikuwa si washiriki kwenye mikutano ya aina hii ambazo ni Rwanda, Burundi na DRC; kwenye mikutano kadhaa ambayo mhusika aliwahi kushiriki, ni mikutano miwli tu ambayo Msumbiji iliwahi kushiriki ambayo ni

  • Mkutano wa Entebbe Uganda uliowahi kufanyika Desemba 2009
  • Mkutano wa Dar es salaam Tanzania uliowahi kufanyika Septemba 2017 na ambao ulikuwa uliambatana pia na field ya kwenda Kigamboni.
Mkutano huu pia, ndiyo ulikuwa wa pekee ulioambatana kipendele cha kwenda field. Kwenye mikutano mingine yote ya aina hii ambayo mhusika aliwahi kuhudhuria ndani na nje ya nchi hapo kabla, hapakuwahi kuwa na mkutano mwingine uliokuwa na kipengele cha aina hii ambacho washiriki wake walitakiwa kwenda field pia

MUBARIKIWE TENA NA BWANA
 
UPDATE:TUESDAY 05TH JULY 2022

TUKIO LA MAFUNDI WASIOJULIKANA KAMA NI WAFANYAKAZI WA TAASISI YA MHUSIKA LAJIRUDIA TENA.

NI BAADA YA MHUSIKA MWENYEWE, SAFARI HII KULAZIMIKA KWENDA KUOMBA MSAADA WA MAFUNDI ILI WAWEZE KUFIKA NYUMBANI KWAKE KWA AJILI YA MSAADA


NB: Kwa wasomaji wa siku zote wa uzi huu; kabla ama baada ya kuwa wamesoma maelezo yaliyopo hapa chini; wanaombwa pia kupitia maelezo yaliyoko wenye post hii hapa #728 ambayo ina maelezo ya tukio jingine tofauti lakini linaloshahibian sana na tukio hili la sasa

Tukio hili la sasa limetokea ndani ya siku mbili za kazi zinazofuatana mfululizo ila zilizo kwenye wiki mbili tofauti, na limehusisha jumla ya matukio mawili yaliyotukia kwenye siku mbili zilizotofautiana

MAELEZO YA UTANGULIZI

OMBI LA MSAADA WA KWANZA KUTOKA KWA MAFUNDI WA MILIKI ZA NYUMBA

Tukio la ombi la
kwanza limetokea Ijumaa ya tarehe 01 July 2022; na ambayo ni siku ya mwisho kabisa ya kazi ya wiki. Hili lilisababishwa na mambo kadhaa kama ifutavyo hapa chini

  • Mfumo wa ndani ya nyumba wa sink la maji taka ya jikoni wa nyumbani kwa mhusika uliziba ghafla
  • Kwa miaka kadhaa nyuma, mara zote na kwa mara nyingi sana, mhusika amekuwa akiuzibua mwenyewe kwa kutumia kifaa alichonacho lakini safari hii ilishindikana
Hiyo sasa ilikuwa J5 wiki jana

Hata hivyo, ilipofika Alhamis tarehe 30 July 2022

  • Mhusika alijaribu kuchemsha maji ya moto kwanza ili kuyeyusha mafuta ambayo alidhani pengine yanaweza kuwa yameingia kwenye mfumo huo, lakini bado ilishindikana kabisa kuuzibua
  • Baada ya hapo mhusika alilazimika sasa kwenda kuomba nsaada wa mafundi kutoka miliki ya nyumba ili waje wamsaidie
Kilichotokea sasa baada ya mhusika kuanza mchakato huo wa kupata mafundi ili wakamsaidie kazi nyumbani kwake, ndiyo hicho kinachopelekea haya yote kuandikwa humu

Ikumbukwe pia kuwa mwaka jana kwenye wakati na majira yanayoelekea na haya, uliwahi kutokea mchakato mwingine tena uliohusisha mafundi waliofika nyumbani kwa mhusika kwa ajili ya kurudisha maji ambayo yalikuwa yamekatwa kwa takribani miaka mitatu

Mchakato wa kurudisha maji hayo uligubikwa na mambo mengi yenye utata; kubwa zaidi likiwa ni ugeni wa watu waliokuwa wamefika kwenye ghorofa analoishi mhusika na kuanza kuishi kwenye nyumba mojawapo iliyo juu kabisa ambayo kwa kipindi kirefu sasa imekuwa wazi pasipo kupangiwa mkazi yoyote kuishi ambaye ni mfanyakazi wa taasisi

Ukihusianaisha na tukio hilo la mwaka jana na hili la sasa, safari hii pia kuna ugeni mwingine kwenye nyumba hiyo; na hivyo kuna watu wengine pia kwa sasa wanaoonekana kuishi kwenye nyumba hiyo na ambao si wafanyakazi wa taasisi

Kitu unique sana kwenye ombi hili la msaada wa kwanza ni kwamba

  • Mara ya mwisho mhusika kuomba msaada wa tatizo la aina hii ilikuwa takribani miaka mine iliyopita
  • Safari hii, baada ya tatizo hilo kuwa limetatuliwa siku hiyo ya Ijumaa asubuhi (wiki jana), hadi kufikia jioni tatizo hilo lilikuwa limerudi tena sawia kabisa kama lilivyokuwa awali
  • Tatizo hilo lilirudi likiwa limebeba sifa zote/ zile zile za awali kiasi kwamba hapakuwa na uwezekano wowote wa mhusika kulitatua kwa njia zake zile ambazo amekuwa akizitumia siku zote
OMBI LA MSAADA WA PILI KUTOKA KWA MAFUNDI WA MILIKI ZA NYUMBA

Ombi la pili limetokea J3 ya tarehe 04 July 2022 (wiki hii); na kwenye siku ambayo ni ya mwanzo kabisa ya kazi ya wiki

  • Tatizo hili la pili lilijitokeza J2 asubuhi, huku tatizo lile la Ijumaa iliyokuwa imepita nyuma yake nalo likiwa tayari limesharudi na hivyo kupelekea uwepo wa matatizo mawili kwa wakati mmoja
  • Kwa hiiyo, msaada wa ombi la siku ya kwanza ulikuwa ni kwa ajili ya kutatua tatizo lililokuwa limejitokeza nyumbani kwake yeye mhusika AMBALO LILITATULIWA SIKU HIYO HIYO LAKINI BAADAYE TENA JIONI HIYO, TATIZO HILO LIKAWA LIMERUDI KAMA LILIVYOKUWA AWALI
  • Kwa upande mwingine, msaada wa ombi la siku ile ya pili ilikuwa ni kwa ajili ya kutatua tatizo kwenye nyumba ya juu ya jirani yake ambaye wanachangia mfumo mmoja wa maji taka
  • Hii ilikuwa ni baada ya jirani huyo kukataa kwenda kuwaita mafundi, ILA KWA TATIZO LILILOKUWA LIKISUMBUA NYUMBANI KWA MHUSIKA
Kwa mara ya kwanza, mhusika aliliripoti tatizo Ijumaa. Baada ya kuripoti fundi mmoja alitumwa nyumbani kwa mhusika kwa ajili ya kushughulika tatizo hilo asubuhi hiyo na alilitatua ila kwa sababu zilizo nje ya upeo wa mhusika hadi kufikia jioni siku hiyo ya Ijumaa, tatizo hilo likawa limerudi tena pale pale.

NA KWA SABABU

  • Hapo hapo kulikuwa pia na TATIZO JINGINE TENA LA NYONGEZA nyumbani kwa mhsika na amblo lilikuwa ni KUBWA ZAIDI lililojitokeza kwa siku mbili mfululizo za J2 na J3 asubuhi; na likiwa limesbabishwa na nyumba ya jirani iliyo juu ya ile ya mhusika;
  • Jirani mwenye kusababisha tatizo nyumbani kwa mhusika alidai kuwa yeye hawezi kwenda kuwaita mafundi kwa sababu tatizo linalolisababisha matatizo nyumbani kwa mhusika, halikuwa linasabbisha matatizo nyumbani kwake yeye;
LOGIC inayojitokeza kutoka kwenye vipengele hivi viwili ni kwamba ilikuwa ni lazima tu mhusika angeenda kuripoti matatizo hayanyote mawili, yaani lile la mwanzo kabisa lililojirudia; baada ya kuwa limetatuliwa Ijumaa asubuhi halafu Ijumaa jioni likawa limerudi tena pamoja na hili la pili lililokuwa limejitokeza asubuhi za simku mbili za J2 na J3. Katika hali ya awaida, hiyo, isingekuwa rahisi sana mhusika aende akaripoti tatizo dogo lile ambalo linatokana na nyumba anayoishi, halafu aache lile la kufurika mavi nyumba nzima; kisa tu kufurika mavi hayo kunasababishwa na jirani yake ambaye amekataa kwenda kuriripoti kwenye mamlaka husika. Logically; ilikuwa ni lazima tu mhusika arudi tena kwenda kuripoti na wakati anafanya hivyo, angeripoti matatizo yote mawili kwa wakati mmoja, likiwemo lile ambalo jirani yake alitakiwa kuwa ameriripoti wiki kadhaa zilizokuwa zimepita nyuma

……………………..inaendelea
 
HISTORIA FUPI YA MATUKIO YA AINA HII UKIYAHUSIANAISHA NA JIRANI WA MHUSIKA

Kwa kipindi kisichozidi miaka mitano (au sita), ilikuwa ni mara ya pili kwa jirani huyu kusababisha tatizo la aina hiyo hiyo nyumbani kwa mhusika; kulingana na taarifa za kitaalamu ambazo zimekuwa zikitolewa na mafundi ambao wamekuwa wakifika kwenye ghorofa hilo kwa ajili ya kutatua tatizo hilo na ambao wamefanikiwa kutatua matatizo yote mawili; yaani lile la awali, na hili la wiki hii yaani jana J3

Kwa mara ya kwanza, dalili za tatizo hili la pili zilianza kuonekana takribani wiki nne zilizopita, hali iliyopelekea mhusika kufika nyumbani kwa jirani huyo kumjulisha kuwa kuna tatizo kama lile la awali lilikuwa lianelekea kujitokeza tena na hivyo kumuomba jirani huyo achukue hatua kabla halijafikia kwenye hatua kama ile ya kipindi cha nyuma. Ukichukulia ukweli kuwa wote wawili, yaani mhusika na jirani mwenye nyumba inayosababisha matatizo nyumbani kwa mhusika wanajua fika kabisa kuwa tatizo hili lilishawahi kujitokeza huko nyuma na siyo geni; baada ya mhusika kuwa amezifikisha taarifa hizo kwa jirani, (mhusika) aliamini kabisa kuwa jirani huyu angeshughulikia tatizo hili haraka iwezekanavyo, ukizingatia hatari ya kiafaya inayoambatana na tatizo hilo. Tofauti na mhusika alivyotarajia, jirani huyu hakufanya hivyo. Mbali na hivyo, jirani huyu hakuchukua hata hatua ya kumjulisha mhusika kuwa hakuwa na mpango wa kulishughullikia tatizo hilo kama mhusika alivyokuwa ametoa taarifa, bali aliamua kukaa kimya tu na pasipo kumjulisha mhusika uamuzi wake huo juu ya swala hilo.

Kutona na hali hiyo basi:

  • Hadi kufikia asubuhi ya J2 ya tarehe 03 July 2022; mhusika akiwa anajiandaa kuoga ili aende Kanisani, alikuta hali mbaya bafuni kwake na chooni kwake pia
  • Sink la kuogea lilikuwa limefurika mavi yaliyokuwa yanatoka juu nyumba ya jirani
  • Mbali na bafu, choo nacho pia kikawa kinafurika mavi kutoka nyumba hiyo hiyo ya juu ya jirani
Kumbe jirani huyu hakuwa ameripoti tatizo hili kwa wahusika na aliamua kukaa kimya pasipo kumjulisha mhusika, huku mhusika naye akiwa anadhani kuwa tatizo hilo lilishashughulikiwa kwa sababu kwa kipindi cha takribani wiki nne tangu pale mhusika alipobaini uwepo wake na kuamua kwenda kumjulisha jirani yake, , TATIZO HILI HALIKUWAHI KUJITOKEZA TENA HATA SIKU MOJA isipokuwa kwa siku hizo tajwa tu

Baada ya tatizo kuwa kubwa, ndipo mhusika alipoamua tena kurudi kwa jirani yake akimjulisha kuwa maji taka kutoka nyumbani kwake yakiwa yameambatana na kinyeshi, tayari yalikuwa yameshaanza kufurika nyumbani kwake (mhusika), na hapa ndipo alipobaini kuwa jirani hakuwa ameripoti tatizo hilo baada ya mhusika kupokea majibu mazuri kutoka kwenye mdomo wa jirani huyo

KABLA YA KUENDELEA ZAIDI:

MAELEZO MAFUPI YA TATIZO LA AWALI LINALOSHAHIBIANA NA HILI LA SASA


Kwa mara ya kwanza, tatizo hili lilitokea takribani miaka mitano iliyopita. Na kama alivyosema hapo juu kwamba kutokana na ukweli kuwa mhusika na jirani walishawahi kulishuhudia tukio hili huko nyuma, mhusika aliamini kuwa jitrani huyu angelishughulikia tatizo hilo ipasavyo na kwa uharaka wa kipekee sana. Ukiongezea na ukweli mwingine kuwa tangu mhusika amjulishe jirani dalili za uwepo wa tatizo hilo, zilifuatia wiki zingine kama nne hivi pasipo mhusika kuona dalili zingine zozote mbaya za nyongeza. Hadi hapo mhusika alikuwa ameamini fika kabisa kuwa jirani alikuwa tayari ameshashughulikia tatizo hilo. Kumbe hapana

  • Ni kwenye asubuhi ya J2 ya tarehe 03 July 2022 ndipo mhusika alipobaini tena sink la kuogea pamoja na choo, vyote viwili vikifurika tena mavi kutoka nyumba ya jirani huyo
  • Mbali na hivyo, asubuhi nyingine tena ya siku iliyofuata, yaani J3 ya tarehe 03 July 2022, mhusika alivishuhdia tena sink na choo vikifurika tena mavi kutoka nyumba ya jirani huyo; safari hii kwa kiwango cha juu zaidi kuliko kile cha siku ile ya kwanza
Bahati nzuri (bado kwake yeye mhusika anaona ni bahati nzuri kwa sababu mziki wake ulio kamili; yaani ule wa tukio lile la kwanza, anaujua vizuri zaidi) aliyokuwa nayo mhusika ni kwamba mavi hayo yalikuwa hayajaanza kuvuka ukingo wa choo na ule wa sink la bafu la kuongea hivyo yalikuwa bado hayajaanza kumwagika kwenye sakafu ya nyumba; kitu ambacho kama kingetokea, kingepelekea mavi hayo kuenea nyumba nzima na hatimaye yangeenda kutokea kwenye ngazi ambazo huwa wanapita wakazi wote wa ghororfa hilo ikiwa ni pamoja na watu wote ambao huwa wanafika kwenye ghorofa hilo

KILE AMBACHO KIMEKUWA KIKIFANYIKA KWENYE NYUMBA YA MAJIRANI HAO NA AMBACHO KIMEKUWA KIKIPELEKEA TATIZO HILI LA MFUMO WA MAJI TAKA KUZIBA

Hii ni kulingana na amaelezo ya wataalamu ambao wamekuwa wakifanya kazi ya kuurekebisha mfumo huu kwa awamu zote mbili, ile ya mwanzo na hii ya sasa

Maelezo ya kitaalamu yanadai kuwa mfumo wa maji taka (ya chooni na bafuni pia) wa nyumba ya jirani huwa unaziba na hivyo kupeleka maji taka yasiweze kusafiri kuelekea kwenye septic tank. Hali hii ikishatokea uchafu huo huwa unaamua kutafuta njia mbadala na hivyo ku-divert njia na hivyo kulazimika kupitia bafuni na chooni kwa mhusika ambaye nyumba yake iko chini ya ile ambao mfumo wake huwa unaziba. Hali hii ikisharokea, hupelekea nyumba nzima ya mhusika kufurika mavi yaliyochanganyikana na maji, na ambayo hatimaye husambaa nyumba nzima hadi kwenda kutokea mlanngoni kwenye ngazi za kushuka chini.

Mfumo wa maji taka wa nyumba hii huwa unaziba baada ya vitu kama pampers zikiwemo taulo za kike, kuwa zimetupwa chooni, kitu kinachopelekea pampers hizo kujazana kwenye unene wa bomba la kupitisha maji machafu na kusababisha bomba hilo kutopitisha uchafu wote kama inavyotakiwa.

Zaidi ni kuwa kitu pekee ambacho huwa kinasababisha mafundi hawa kufanya ruling ya aina hii kitaalamu ni kwamba huwa wanafanya test ya kumwaga maji kwenye choo cha kila nyumba, iliyo juu (ya jirani) na iliyo chini (ya mhusika), kabla ya kuanza kazi.

  • Wakimwaga maji kwenye choo cha nyumba ya juu (ya jirani) peke yake, maji yake huwa yanatokea kwenye bafu na choo cha mhusika
  • Wakimwaga maji kwenye choo cha nyumba ya mhusika peke yake, maji yake yanakwenda chini moja kwa moja kama kawaida pasipo kurudi juu au kufurika kwenye sink la choo cha nyumba hiyo
Vile vile pale inapotokea maji yakamwaga bafuni kwa mhusika pekee, maji hayo nayo pia huwa yanakwenda chini moja kwa moja yakipita kwenye mfumo wake pasipo kutuama kwenye sink, huwa yanapita pasipo shida yoyote

…………………….inaendelea
 
REFERENCE YA NYUMA YA TATIZO LA AINA HII LILILOWAHI KUTOKEA MARA YA KWANZA TAKRIBANI MIAKA MITANO ILIYOPITA

Tatizo la awali la aina hii liliwahi kutokea siku moja ambayo ilikuwa ni ya mwanzo wa weekend, yaani Ijumaa jioni baada ya masaa ya kazi.

Siku hiyo mhusika alirudi nyumbani jioni akitokea ofisni na kukuta nyumba yake nzima ikiwa imefurika kinyesi kilichochanganyikana na maji

Hapo ndipo alipoamua kumfuata nyumbani kwake mtu anayeitwa Wilson ambaye walikuwa wanaishi eneo jirani kwenye nyumba zilizoko ndani ya eneo la tasisi wanayofanyia kazi

Baada ya kumweleza tatizo lake, Wilson aliamua kumpa msaada mhusika kutokana na uzito wa swala lilivyokuwa na ambalo lilionekana lisingeweza kusubiri hadi J3 ya wiki iliyokuwa inafuata ukizingatia kuwa kesho yake tu ilikuwa bado ni Jumammosi; ambayo nayo pia haikuwa siku ya kazi, ukiachilia mbali J2 ya wiki hiyo

Baada ya mhusika kuongea na Wilson; bwana huyu alimpigia simu kijana mmoja akaja na kuanza kufanya kazi akimsimamia, kuanzia tuseme saa 12:30 hadi saa 3:00 au saa 3:30 usiku na baada ya hapo kila kitu kikawa kimtengemaa. Jirani wenye nyumba ambayo imekuwa ikiziba mfuno huu nao pia walikuwepo pamoja na mke wake, tangu mwanzo wa zoezi la urekebishaji wa mfumo hadi kumalizika.

Tukirudi kwenye tatizo la sasa au la pili; hili nalo pia limetokea siku ya weekend; mara ya kwanza limetokea J2 asubuhi wakati wa maandalizi ya kuelekea Kanisani, na mara ya pili tena J3 asubuhi (jana)

MAELEZO MAFUPI KUHUSIANA NA MATATIZO HAYA MAWILI

Tukianza na lile la zamani lililowahi kutokea mwanzoni mwa siku ya weekend au siku ya Ijumaa jioni; siku hiyo mhusika aliamua kuongea na huyo mfanyakazi mwenzake wanayefahamiana; anayefanya kazi kwenye miliki ya nyumba anayeitwa Wilson

Baada ya kazi, mhusika kwa hiari yake yake aliamua kumlipa Wilson TZS 20,000/= na fundi aliyehusika na kazi ya kurekebisha mfumo wa maji taka naye pia alimlipa TZS 60,000/=

Baada ya mafundi kuwa wamemaliza kufanya kazi; Wilson alisema kuwa kuziba kwa maji taka nyumba ya juu kulisababishwa na pampers za kike kuwa zinatupwa chooni.

Hata hivyo tukirudi kwenye post hii hapa #728 ya Julai 29, 2021 (mwaka jana) kwa jicho jingine mtu mwingine anaweza kuona kuwa tatizo kubwa liliosababisha haya yote kutokea, ni ILE NYUMBA ILIYO JUU KABISA KWENYE BLOCK LA MHUSIKA, NA AMBAYO HAIKALIWI NA MFANYAKAZI YEYOTE WA TAASISI KWA SASA

Kwa siku za hivi karibuni, mhusika amebaini uwepo wa watu wageni kwenye nyumba hiyo na ambao si wafanyakazi wa taasisi, huku akiwa hajui ni sababu ipi hasa inayopelekea watu hao kuishi kwenye nyumba hiiyo

Vile ukizingatia post hiyo hapo tajwa, kwenye kipindi tajwa cha post hiyo, paliwahi pia kutokea mafundi wa kurudisha maji ambayo yaliyokuwa yamekatwa nyumbani kwa mhusika kwa kipindi cha takribani miaka mitatu

  • Mafundi hao walifika kufanya kazi kwenye ghorofa analoishi mhusika, siku ya Ijumaa baada ya saa za kazi
  • Mojawapo ya mambo ambayo walifanya siku hiyo ni kwamba mafundi hao walim-prompt mhusika kupandisha juu summit, baada ya kuonekana kuwa bado kulikuwa na maji yaliyokuwa yanaendelea kuvuja nyumbani kwa mhusika mara baada ya mafundi hao kuwa wamekamllisha kazi yao
  • Mafundi hao walidhani kuwa maji hayo yalikuwa yanavuja kutoka nyumba ya jirani huyu wa sasa ambaye kinyesi kutoka kwenye nyumba yake kimekuwa kikimwagikia nyumbani kwa mhusika
  • Baada ya mafundi kupandisha juu kwenye nyumba hiyo, walifanya ubashiri mwingine kuwa maji hayo yatakuwa yalikuwa yanatoka juu summit
  • Mhusika alikuwa ameambatana nao hadi kwenye nyumba ya jirani, na baada ya hapo hakuambatana nao tena baada ya wao kuamua kuelekea juu summit
Zaidi ni kuwa; Mafundi hawa na ambao baadaye ilikuja kudhihirika kuwa hawakuwa wafanyakazi wa taasisi

Walikuja kufanya kazi katika muda ambao nyumba ya juu kabisa kwenye ghorofa hilo, na ambayo imekuwa tupu pasipo kukaliwa na mfanyakazi wa taasisi kwa kipindi kirefu mno hadi sasa; ilikuwa inakaliwa na wageni ambao walikuwa wamengia kwenye myumba hiyo siku chache kabla ya siku hiyo ya kazi, na ambao hawakuwa wafanyakazi wa taasisi vile vile

Kwa kipindi hiki vile vile, mhusika akiwa yupo ofisini, alipelekewa nyumbani kwake mafundi ambao nao pia wamefanya kazi katika mazingira kama haya, huku Supervisor wao Wilson mbaye mara zote huwa anaambatana nao siku zote akiwa siyo mmoja wao

Mhusika hana uhakika kama mafundi hawa walikuwa wafanyakazi wa taasisi kwa sababu walifika nyumbani kwake na kuanza kufanya kazi tu pasipokuwa wametambulishwa kwake au kujulishwa kwake kwa majina yao na uhusika wao kwenye kazi hiyo

Aidha mafundi hao hawakuwa wamevaa vitambulisho vya aina yoyote. Mhusika ataliongelea zaidi hili kwenye kipengele kingine cha namna mafundi hawa walivyoweza kufika nyumbani kwake na kuanza kazi huku Wilson akiwa si mmoja wao

Siku hiyo ya Ijumaa, mhusika alikuwa ofisini na nyumbani kwake alimuacha mgeni; huyo ndiyo amekuwa akiwapokea.

Alichokuwa amekifanya mhusika Ijumaa hiyo ni kumpa maelekezo tu mgeni kuwa mafundi wakija ampigie ili arudi nyumbani na kukutana nao kwa ajili ya kuwahakiki kama kweli ni wafayakazi wa taasisi ama la.

Siku hiyo ya Ijumaa kweli mhusika alipigiwa simu kujulishwa kuwa kuna fundi alikuwa amefika nyumbani kwake; ila aliporudi nyumbani hakumkuta fundi huyo;

Fundi huyo alikuwa ametoka kidogo na kazi iliyokuwa imemleta tayari alikuwa ameshaimaliza, huku akiwa ameacha pale nyumbani makaratasi ya kazi zake ambayo alikuwa amesema atakuja kuyapitia baadaye

Mhusika alijaribu kumsubiria kidogo fundi huyo kwa sababu makaratasi yake yalikuwa pale lakini hakufanikiwa kurudi hadi mhusika alipoamua kurudi tu ofisini kwake pasipo kuonana na na fundi huyo

Baada ya kufika ofisini, mhusika alipigiwa simu kujulishwa kuwa fundi huyu alikuwa amesharudi

Mhusika aliongea na fundi ambaye kwa jina alijitambulisha kuwa anaitwa Mood.

Huyu Mood (tumwite MD) ndiye aliyefanya kazi Ijumaa asubuhi sink likazibuka na hatimaye jioni likaziba tena na pasipo uwezekano wa mhusika kulizibua tena

Inasemekena kuwa MD wa Ijumaa, ndiye aliambatana na fundi mwingine tena wa pili kwa ajili ya kufanya kazi nyumbani kwa mhusika J3 ya tarehe 04 Julai 2022

Maelezo zaidi kuhusiana na mafundi hawa yanafuata muda siyo mrefu

MD ni fundi aliyetumwa nyumbani kwa mhusika kwa mara ya kwanza Ijumaa iliyopita na alitumwa na mtu anayeitwa MR SAHANI (tumwite SHN)

…………………..inaendelea
 
TATIZO LA KWANZA: KUZIBA KWA SINK LA MAJI YA JIKONI:

NAMNA ULIVYOKUWA MCHAKATO WA KUWAPATA MAFUNDI WA KULIREKEBISHA


Kwa mara ya kwanza kabisa katika kipindi cha hivi karibuni, sink hili liliziba J5 ya tarehe 29 July 2022

  • Mhusika alijaribu kulirekebisha lakini hakufanikiwa
  • Kesho yake Alhamis ya tarehe 30 July 2022, mhusika aliamua kuchemsha maji ya moto na kuyamwaga kwenye sink na hatimaye kuanza kuyasukuma kwa nia ya kulizibua
  • Bado sink hilo halikuweza kuzibuka
Baada ya hapo kesho yake Ijumaa ya tarehe 30 July 2022, mhusika akiwa anaelekea ofisini, aliamua kupitia kwanza ofisi za miliki ya nyumba kwa ajili ya kujaza fomu ili aweze kupatiwa masaada stahiki

Kwenye ofisi husika alimkuta swahiba wake wa siku nyingi sana MR SHN

  • MR SHN alimjulisha mhusika kuwa tatizo lake lingeshughulikiwa muda huo huo kwa sababu fundi anayehusika na tatizo hilo alikuwepo around maeneno yale
  • Mhusika hakuyaamini sana maeno hayo matamu kutoka kwa swahiba wake kwa sababu ni mara chahe mno kupata response ya haraka namna hiyo kutokana ukweli kwamba kwa muda huo mara nyingi mafundi wengi huwa wanakuwa tayari wameshakwenda site
  • Vile vile, mhusika alikiri kabisa kimoyomoyo kuwa kile alichokisema MR SHN siku hiyo kingekuwa kweli, basi ilikuwa ni rekodi ya pekee kutokana na ukweli kuwa ingekuwa ni mara yake ya kwanza a kabiskupata response ya namna hiyo katika kipindi chake chote ambacho amekuwa akihitaji misaada inayofanana na huo wa siku hiyo
Baada ya kujaza fomu akiwa nje ya ofisi ila mbele ya mapokezi (kwenye sehemu ile ya ndani ambamo mara zote watu huwa wanakaa wakiwa wanajaza fomu hizo hapakuwa na mtu), mhusika aliipitisha fomu hiyo dirishani na hatimaye kuanza kurudi ofisini kwa MR SHN kwenda kumjulisha kuwa alikuwa tayari ameshakamilisha zoezi la kujaza fomu

  • Kwa bahati mbaya kumbe MR SHN alikuwa tayari ameshatoka kidogo kwa muda huo
  • Kwa bahati nzuri mhusika alibahatika kumuona MR SHN kwa mbali kidogo akiwa anarudi ofisini kwake na alimweleza kwa kumpayukia kuwa tayari alikuwa ameshajaza fomu husika
Kwa kumweleza hayo, mhusika alidhani kuwa pengine MR SHN angeshauri mhusika amchukue fundi ili ende naye moja kwa moja nyumbani kwake ili akakamilishe kazi lakini MR SHN hakufanya hivyo

Aidha mhusika naye pia hakupenda kutoa ombi hilo kwa MR SHN; maadam yeye (MR SHN) alikuwa amesema kuwa fundi huyo alikuwepo around na angemtuma muda huo huo, mhusika naye aliona ni hekima kuendelea kumwamini MR SHN kuwa atafanya kama alivyokuwa amesema na kweli MR SHN alifanya sawia kabisa na maneno yake

  • Baada ya hapo mhusika aliondoka maeneo ya ofisino kwa akina MR SHN na kunyoosha moja kwa moja kuelekea ofisini kwake
  • Baada ya muda kupita, mgeni aliyekuwa nyumbani kwa mhusika alimjulisha mhusika kuwa fundi alikuwa tayari ameshafika kwa ajili ya kazi.
  • Muda huo huo mhusika alianza safari ya kuelekea nyumbani na alipofika huko, alikuta fundi tayari ameshamaliza kazi na kila kitu kwenye sink kilikuwa kinafanya kazi kama kawaida
  • Mgeni alimjulisha mhusika kuwa fundi alikuwa ametoka kidogo huku akiwa ameacha makaratasi yake ambayo angerudi kuyapitia.
  • Mhusika alimsubiria fundi kwa dakika kama kumi hivi lakini hakufanikiwa kurudi.
  • Hatimaye mhusika aliamua kurudi ofisini, na baadaye tena fundi naye alirudi tena mhusika kiwa tayari amesharudi ofisini
  • Walipoongea mhusika na fundi, ndiyo fundi alipojitambulisha kuwa yeye anaitwa MD
Baada ya maongezi hayo, mhusika aliendelea na kazi zake ofisini hadi jioni. Baadaye aliporudi nyumbani jioni alikuta sink hilo hilo likiwa limeziba tena sawa sawa kabisa kama lilivyokuwa limeziba awali kabla ya fundi hajaja kulirekebisha

Baada ya kuona hivyo, mhusika alimuuliza mgeni kuwa fundi yeye alifanyaje kulizibua asubuhi ile na mgeni alijibu kwamba yeye alizunguka pia kule nje na baada ya pale maji yalianza kuserereka bila tatizo lolote.

Huu mtego ni wa siku nyingi na mhusika anaujua na hivyo hakuthubutu kwenda kuangalia ni nini kilikuwa kikisababisha bomba lenye unene wa mkono wa mtu mzima, kushindwa kupitisha maji machafu ya jikoni na hivyo kupelekea maji kutuama kwenye sink irrespective of the effort made to unblock the pipe.

Mhusika anaujua tego huu tangu siku nyingi nyuma na hivyo hakuthubutu kabisa kushuka chini kwenda kuangalia kwenye mdomo wa bomba hilo kulikuwa na kitu gani kilichokuwa kinapelekea bomba hilo kuziba.

By the way,
watu wawili walikuwa wamekuja kukaa karibu na mhusika asubuhi hiyo ya Ijumaa wakati mhusika alipokuwa anajaza fomu ya maombi siku hiyo. Watu hawa atapenda kuwaongelea angalau kwa kifupi tu hapo baadaye. Mmoja anahusika na mambo ya umeme na pia wanaongea lugha moja na mhusika, na mwingine ni swahiba na jirani wa mhusika wa siku nyingi ambaye naye pia huwa anahusika na maswala ya miundo mbinu ya maji taka

………………….itaendelea
 
UPDATE: 06TH JULY 2022: MHUSIKA ALIPOKUWA YUPO NJE MBELE YA OFISI YA MAPOKEZI AKIJAZA FOMU YA MAOMBI KWA AJILI YA KUREKEBISHIWA SINK LA JIKONI LILILOKUWA LIMEZIBA

Mhusika akiwa anajaza fomu ya maombi, watu wawili anaofahamiana nao tangu kipindi kirefu nyuma walifika pale alipokuwa amekaa

  • Wote wawili waliwahi kuwa majirani zake kwenye makazi ya taasisi kwenye miaka ya mwanzoni ya 2000
  • Mmoja ni fundi umeme na huwa wanaongea lugha moja ya kuzaliwa na mhusika
  • Mwingine ni subordinate wa Wilson.
  • Wilson huyu ndiye jamaa yake na mhusika ambaye aliwahi kumuokoa mhusika kwenye janga la kinyesi cha mavi kilichowahi kutapakaa nyumba nzima miaka kadhaa iliyopita
Subordinate wa Wilson alijaribu kumhoji mhusika kuwa kwa nini asingekuwa amempigia simu kumwambia yeye (subordinate wa Wilson) na akaenda akashughulikia tatizo hilo la sink nyumbani kwa mhusika

  • Mhusika alimjibu mtu huyo kuwa swala la sink kuziba lilikuwa la kiofisi zaidi na ndiyo maana alikuja kujaza fomu ya maombi
  • Baada ya maongezi haya mafupi, mhusika aliondoka akielekea kwenye ofisi ya MR SHN huku akiwaacha staff hao wakiwa wamekaa kwenye viti.
Hapa ndipo alipofanikiwa kumuona kwa mbali MR SHN akirudi ofisini na alimpayukia kwa mbali kuwa fomu ya maombi ameshajaza tayari. Baada ya hapo, mhusika aliondoka eneo la miliki za nyumba na kuelekea ofisini ( kwa siku hiyo, mhusika alikuwa bado hajaripoti ofisni hadi muda huo) ambako baadaye ndiyo alikuja kupewa taarifa kuwa fundi wa kurekebisha sink alikuwa ameshafika nyumbani kwake. Baada ya kupokea taarifa hiyo, mhusika alirudi tena nyumbani lakini hakufanikiwa kuonana na fundi huyo. Hiyo siku ikapita; yaani Ijumaa ya tarehe 01 July 2022

Siku ya Jumamosi tarehe 02 July 2022 nayo pia ikapita.

Ikumbukwe kuwa hadi siku hii ya Jumamosi, sink hilo lilikuwa bado limeziba. Ni kwa sababu lilizibuliwa Ijumaa asubuhi na kufikia Ijumaa jioni likawa limeshaziba tena, na katika namna ambayo ilikuwa ni beyond servicing ya mtu yeyote yule ambaye si professional; mhusika akiwa mmoja wao

……………………………..inaendelea
 
KILE KILICHOTOKEA KUANZIA SIKU YA J2 TAREHE 03 JULY 2022

Kilichotokea siku hii tayari mhusika ameshatoa maelezo yake hapo juu; choo na bafu vilifurika mchanganyiko wa mavi na maji kutoka nyumba ya jirani iliyo juu ya ile ya mhusika.Muda wa mafuriko haya ilikuwa ni saa moja asubuhi

Mafuriko haya yalikuja kujirudia tena asubuhi ya siku iliyofuata, yaani J3 ya tarehe 03 July 2022

Mafuriko ya J2 yalipotokea, mhusika alipandisha juu nyumba ya jirani na kuwakumbusha utaratibu uliotakiwa kufuatwa kabla tatizo halijawa kubwa kama lilivyowahi kuwa kipindi kile cha nyuma

Baada ya mafuriko ya pili kutokea tena J3 hiyo, mhusika alipandisha tena nyumba ya jirani na kuuliza ni nini kilikuwa kinaendelea, na hapa ndipo BABA MWENYE NYUMBA (tumwite BMN) alipoamua kufunguka kwa mara ya kwanza na kwa ufasaha wa akili ya mtu mzima mwenye akili timamu

  • BMN alidai kuwa yeye hajaenda kuripoti kwa sababu tatizo la mafuriko haliko kwake
  • Ikumbukwe kuwa hadi hapa, BMN alikuwa anajua fika kabisa kuwa kuna tatizo jingine la aina hii ambalo liliwahi kutokea huko nyuma na ambalo Wilson alilithibitisha kwake kuwa lilisababishwa na mchakato wa mambo ya usafi yaliyokuwa yanafanyika nyumbani kwake
Zaidi BMN alimlaani sana mhusika kuwa jana yake J2 alimweleza mtoto mdogo kuwa nyumba yake inavuja mavi na siyo maji, kitu ambacho kilikuwa si kizuri sana kumweleza mtoto maneno makali ya namna hiyo

Kitendo hiki cha mhusika kumweleza mtoto maneno haya kilikuwa kimetokea jana yake siku ya J2, baada ya BMN kushindwa kuonana na mhusika

Ilikuwa ni baada ya mhusika kutaka kuonana na BMN asubuhi hiyo kwa nia ya kumjulisha kuwa kulikuwa na kinyesi kilichokuwa kinavuja nyumbani kwa mhusika; kikiwa kinatokea nyumbani kwake BMN

Siku hiyo ya J2, BMN alidai kuwa asingeweza kuonana na mhusika kwa sababu alikuwa na udhuru na hivyo alikituma kitoto kidogo ambacho pia ni kirafiki chake na mhusika ili kimweleze mhusika kuwa yeye (BMN) alikuwa na udhuru hapo ndani nyumbani kwake na hivyo alikuwa hawezi kuja sebuleni kwa ajili ya kumsilkiliza mhusika

Kitoto hicho kilifikisha ujumbe kwa mhusika na baada ya hapo mhusika naye alikipatia ujumbe kitoto hicho ili kimpelekee baba, na baada ya hapo mhusika aliondoka na kurudi nyumbani kwake

Kumbe ujumbe aliokipatia (mhusika) kitoto, ulikuwa una madhara zaidi kuzidi madhara ya mavi kutoka nyumbani kwa BMN, kujaa nyumbani kwa mhusika. Nadhani hapa kwa akili ya BMN, mhusika alitakiwa akieleze kitoto hicho kuwa “nyumbani kwake (mhusika) kulikuwa na MABOMBA YA SODA yalikuwa yanavujisha soda kutokea nyumbani kwao kwenda nyumbani kwake (mhusika) kwa kupitia chooni na bafuni”

Kwa hiyo mpaka hapa, BMN alivyokuwa na akili ndefu, akawa ametengeneza mazingira ya shutuma kwa mhusika; kwamba just in case of anything successful on his side basi aweze kuja kudai kuwa:

  • “Jana (yaani Jumapili ile ambayo BMN na mhusika hawakupata nafasi ya kuongea) mhusika alikuwa ameghafirika kiasi cha kumtamkia mtoto wangu mdogo maneno makali yasiyostahili, hali ambayo huwa si ya kawaida sana kwake”
  • “Isitoshe leo tena J3 mhusika amefika tena nyumbani kwangu akiwa ameghafirika swa na alivyokuwa J2”
Baada ya kusikia maneno hayo kutoka kwa BMN J3 hiyo, mhusika alianza kudhani kuwa pengine labda BMN ana jambo jingine ndani ya roho yake ambalo anaona njia pekee ya kulitatua ni kwa kutumia ujanja wa kuhamishia mzigo wake kwa mhusika kwa njia ya kmtegeshea (mhusika) ili aghafirike halafu baada ya hapo ionekane kuwa mhusika ndiyo mwenye matatizo na si yeye BMN

Hadi hapa, mhusika aliona pasipo shaka kabisa kuwa BMN alikuwa amejiandaa sana katika hili na hivyo alikuwa ana “plot” ambayo alikuwa amepanga kuikamilisha

Baada ya hapo, mhusika aliondoka nyumbani kwa BMN na kushuka chini, akawasha gari na kuanza kuelekea ofisi za miliki ya nyumba ili akajaze tena fomu ya maombi ya marekebisho yaliyokuwa yanayohitajika; safari hii sasa ikiwa ni kwa mambo mawili makubwa ambayo ni

  • Sink ilililozibuliwa Ijumaa asubuhi na kuziba tena Ijumaa jioni
  • Mavi ambayo yameanza kuvuja yakitokea kwenye nyumba ya BMN yakipitia kwenye sink la choo na la bafu la mhusika, na ambayo hatima yake ni baadaye kufurika nyumba nzima ya mhusika
………………………inaendelea
 
BAADA YA MHUSIKA KUONDOKA NYUMBANI KWA BMN J3 YA TAREHE 03 JULY 2022

Mhusika alinyoosha moja kwa moja hadi kwenye ofisi za miliki ya nyumba, na muda ulikuwa ni majira ya saa 1:30 asubuhi

“PLOT”

Pale mapokezi ambapo ndiyo sehemu fomu huwa zinatolewa na kujazwa; alimkuta dada wa usafi akiwa anafanya usafi nje ya ofisi ya kkaribu na ofisi hiyo ya mapokezi. Kwa muda ule watu wengi walikuwa bado hawajafika ofisini

  • Dada wa usafi alimshauri mhusika aingie ofisini ajaze fomu; kitu ambacho mhusika hakukiafiki
  • Baadaye dada huyu alimjulisha mhusika kuwa “Afisa Tawala” alikuwa tayari ameshafika ofisini na alikuwepo ofisini kwake; na kweli mhusika aliona mlango mmoja ukiwa wazi ghorofa ya kwanza
  • Dada wa usafi alimshauri mhusika kwenda kumuona ofisa huyo; kitu ambacho mhusika alikiafiki
Mhusika alipandisha juu na kwenda kumona boss huyu na hatimaye kumweleza shida yake kuanzia sink lililozibuka na kuziba tena Ijumaa ya wiki iliyopita, hadi lile la mavi kuanza kuvuja kwenye masink ya choo na bafu la mhusika

Mara ya mwisho mhusika wanakutana na ofisa huyu, ilikuwa August 2018 kipindi ambacho ofisa huyu alikuwa akifanya kazi kama msaidizi wa Ofisa wa Nyumba wa sasa

Baada ya ofisa huyu kumsikiliza mhusika, alimtuma tena kwenye ofisi ya akina MR SHN

Kwenye ofisi hiyo aliwakuta watu wawili tu ambao walikuwa wameshafika ofisini muda huo

  • Mmoja wanafahamiana na mwingine wa pili hakuweza kumfahamu kwa sababu ilikuwa ni mara yake ya kwanza kumuona kwenye ofisi hiyo; alikuwa ni mzee wa makamo na aliyekuwa amevaa kibaraghashia
  • Wanayefahamiana alikuwa ni boss wake na MR SHN na ambaye ndiye overall incharge wa ofisi hiyo; yeye ndiyo mkuu kabisa wa kitengo hicho (tumwite MKTE)
  • Yule ambaye hakumfahamu alionekana kama mmojawapo wa wataalamu kadhaa waliopo kwenye kitengo hicho (tumwite MTLM)
Baada ya hapo, mhusika alianza kumweleza MKTE historia ya matatizo yote mawili nyumbani kwake, MTLM naye akiwa anasikiliza

Baada ya MKTE kumsikiliza mhusika, MKTE alimpatia fomu mbili mhusika ili ajaze. Kitu hiki kilikuwa unique sana kwake kwa sababu katika maisha yake yote ya utumishi kwenye taasisi anayofanyia kazi Ilikuwa ni mara ya kwanza kabisa kwake kujaza fomu hizi akiwa ofisini nyingine tofauti na pale ambapo huwa anajazia siku zote; yaani mapokezi. Hapo awali; mara zote fomu hizi amekuwa akizipewa na kuzijaza kwenye sehemu moja tu ambayo ni pale mapokezi

Kati ya fomu hizo mbili, moja ilikuwa ni kwa ajili ya sink na nyingine kwa ajili ya mavi yaliyokuwa yanavuja kutoka nyumba iliyo juu yakipitia bafuni na chooni nyumbani kwa mhusika

  • Baada ya kuzijaza na kuzikabidhi tena kwa MKTE, mhusika alianza safari ya kurudi nyumbani kwake kwenda kuwasubiria mafundi ambao aliambiwa wangefika pale nyumbani kwake muda siyo mrefu
  • Baada ya kuwasubiria mafundi kwa takribani dakika 45 bila kuonekana, mhusika aliamua kumpigia simu MKTE kutaka kujua ni nini kilikuwa kimewachelewesha, lakini simu ya MKTE haikuwa na majibu
  • Mhusika aliamua kubadilisha namba na kupiga kwenye namba nyingine ya MKTE lakini nayo pia haikuwa na majibu
KWA MARA YA KWANZA KABISA, KATIKA MAISHA YAKE YOTE YA UIJIRANI WAO HATIMAYE BMN AGONGA NYUMBANI KWA MHUSIKA

Baada ya muda kidogo, mtu aligonga kwenye mlango wa nyumba ya mhusika

Mhusika alidhani kuwa ndiyo mafundi wamefika kwa ajili ya kuanza kazi lakini kumbe siyo, hawakuwa mafundi bali BMN; jirani anayekaa nyumba iliyo juu ya ile ya mhusika

BMN aliingia na kumpa ujumbe mhusika kuwa tayari alikuwa ameshaongea kwa simu na fundi ambaye amekubali kuja kurekebisha tatizo hilo

Pamoja na BMN kukataa kwenda kujaza fomu kwa ajili ya marekebisho ya mfumo wa maji taka yaliyokuwa yanavuja kutoka nyumbani kwake na kuingia nyumbani kwa mhusika, safari hii BMN alikuja akiwa na habari njema sana kwa mhusika. Zaidi BMN alikuwa na uso unaofariji, tofauti na ule aliokuwa nao asubuhi hiyo alipokuwa akimlalamikia mhusika kutamka maneno makali kwa mtoto mdogo aliyempa ujumbe kuupeleka kwa (baba yake) BMN

TUKIRUDI NYUMA KIDOGO KUHUSIANA NA MUDA AMBAO WATU HAWA WAWILI WAMEKUWA NI MAJIRANI

Kwa kifupi tu ni kwamba BMN alihamia kwenye makazi hayo anayoishi hadi sasa mwaka 2016

Katika kipindi hiki chote cha miaka sita, ilikuwa ni mara yake ya kwanza BMN kuingia nyumbani kwa mhusika tangu ahamie hapo mwaka 2016

Ni kitu kizuri sana kutokuwa na tabia ya kugonga gonga majumbani kwa watu ila pia kwa upande mwingine ikumbukwe kuwa, itakapokuja kutokea siku ukagonga kwa mara ya kwanza nyumbani kwa mtu na ndani ya kipindi kirefu sana, chances ni kwamba lazima utakuwa una ujumbe ambao ni mzito mno na ambao siyo wa kawaida.

Ujumbe wa aina hiyo hauwezi kulingana na ujumbe wa kutoa tu taarifa kuwa kuna fundi anaykuja, na ambaye hapo kabla ulikuwa umekataa kwenda kumjulisha tatizo kubwa kiofisi, linalomkabili jirani yako na ambalo umelisababisha wewe; kwa kudai kuwa tatizo hilo haliko kwako

Angalau BMN angekuja na ujumbe kuwa pamoja na kwamba mhusika alienda kwenda kufanya utaratibu wa fundi kuja kurekebisha tatizo, yeye naye amefuata procedure hizo hizo za kiofisi na hivyo kuna fundi ambaye amepewa jukumu hilo na anakuja kushughulikia tatizo

Ujumbe wa BMN kwa mhusika haukuwa unaangukia kwenye maudhui ya mambo haya yaliyotajwa hapa juu. Yeye BMN alidai tu kuwa kuna fundi amempigia simu na anakuja kufanya kazi

Kwa hali hiyo BMN alikuwa anafanya kzai kwa timing; kwamba alitegea kwanza mhusika aende ofisi za miliki ya nyumba ili aone kwanza matokeo yake yatakuwaje. Baada ya kuona matokeo yake, ndiyo sasa akaja na “PLAN B ya kugonga nyumbani kwa mhusika akiwa amebeba habari zilizo njema mno kwa mhusika huku akiwa amebeba uso wa kibinadamu

Kwa hali hiyo, BMN hakuwa ameenda ofisi za miliki ya nyumba kwenda kujaza fomu ya marekebisho ya tatizo lililokuwa limejitokeza bali alikuwa amempigia fundi anayemfahamu kuja kufanya marekebisho hayo

  • Mhusika alimuuliza BMN kuwa fundi huyo ni mfanyakazi wa taasisi, na BMN naye alijibu kuwa ndiyo
  • Baada ya hapo, mhusika alimjulisha BMN kuwa tayari ameshaenda kujaza fomu ofisi ya miliki za nyumba na hivyo mafundi walikuwepo njiani wanakuja.
Zaidi mhusika alimjulisha BMN kuwa kama fundi huyo aliyempigia ni mmoja wa wale ambao watakuwa wametumwa na MKTE kuja kufanya kazi basi anakaribishwa pasipo tatizo lolote. Vinginevyo kama si mmoja wa wale waliotumwa na MKTE, basi fundi huyo hatakiwi kuingia kufanya kazi ndani nyumbani kwa mhusika

Baada ya hapo, mhusika alimuongoza BMN kwenye mlango wa kutokea, akamfungulia mlango na kutoka

Hili likawa tukio la pili kati ya mhusika na BMN, la kwanza likiwa ni ile argument ya ujumbe mkali kuwasilishwa kwa mtoto aupeleke kwa baba (BMN)

………………..inaendelea
 
KUMBUKUMBU ZA IJUMAA ILIYOKUWA IMEPITA KUHUSIANA NA FUNDI ALIYEFIKA NYUMBANI KWA MHUSIKA SIKU HIYO, ZAPELEKEA MHUSIKA AELEKEE OFISINI BADALA YA KUENDELEA KUWASUBIRI MAFUNDI NYUMBANI KWAKE J3 HIYO

Baada ya BMN kuondoka, mhusika alikumbuka kuwa siku ya Ijumaa ya wiki iliyopita, pamoja na jitihada zake kubwa, mhusika hakufanikiwa kabisa kumjua fundi alyefika nyumbani kwake kufanya kazi siku hiyo

Kwa kuzingatia hilo, mhusika aliamua kuondoka kwanza nyumbani ili kuona kama mafundi hao wangeweza kuja ukizingatia kuwa mwenye kuwatuma ambaye ni MKTE alikuwa hapokei kabisa simu za mhusika

Hapa ilikuwa ni mara baada tu ya BMN kuwa ameondoka nyumbani kwa mhusika

  • Mhusika aliamua kuondoka nyumbani kuelekea ofisini ikiwa ni kabla ya ujio wa mafundi hao
  • Alipofika ofisni, alijaribu kumpigia tena MKTE lakini simu yake bado iliendelea kutokuwa na majibu
Baadaye mhusika aliamua kwenda kufanya muamala wa Bima ya gari kwa kutumia wakala aliye ndani ya taasisi

  • Baada ya muamala huo, akiwa njiani anatoka huko kwenye ofisi hizo za Bima, MKTE ndiyo sasa alimpigia simu mhusika akimjulisha kuwa mafundi walikuwa tayari wameshaelekea nyumbani kwake
  • Baada ya hapo, mhusika alirudi na kupitiliza moja kwa moja kwenye parking bila kufika ofisini kwake, akawasha gari na kuanza kuelekea nyumbani
Alipofika nyumbani pale kwenye parking alimkuta mtu aliyeonekana kama fundi, alikuwa amesimama akiwa anazugazuga nje kwenye parking za gari

Mhusika akiwa anapandisha ngazi kuelekea juu nyumbani kwake, mtu huyu naye aliamua kumfuata mhusika huku akijitambulisha kuwa yeye ndiye fundi aliyewahi kufika pale nyumbani Ijumaa na kwamba kulikuwa tayari na mwenzake mule ndani nyumbani kwake na mhusika

Scenerio inayojidhihirsha mpaka hapa ni kwamba wakati mhusika anatoka kule Bima, alipigiwa simu na MKTE akijulishwa kuwa mafundi walikuwa tayari wameshaenda nyumbani kwake.

  • Baada ya kutoka huko mhusika aliwasha gari na kuanza kuelekea nyumbani, na pale kwenye parking zao alimkuta mtu akiwa anamsubiri, na ambaye walipandisha naye juu huku akijitambulisha kuwa yeye ni fundi pia
  • Kwa observer wa kawaida aliyekuwa anamu-observe mhusika siku hiyo; scenario hii ingeweza kuleta tafsiri kuwa aliyempigia simu mhusika alipokuwa anatoka kule Bima si MKTE bali ni huyu fundi ambaye alimkuta yupo nje kwenye parking akiwa anamsubiria.
Hii ni kutokana na ukweli kuwa mhusika alipigiwa simu na baada ya hapo aliwasha gari haraka haraka kuelekea nyumbani na ambako alikuta mtu akiwa anamsubiria nje kwenye parking na ambaye walipandisha naye juu na kwenda kuingia naye ndani nyumbani kwake

Fundi huyu anaonekana kama alimpigia simu mhusika; ametengeneza mazingira ya namna hiyo ila kiuhalisia hakuwa amempigia simu mhusika, na wala hawakuwa wamewahi kuonana na mhusika hata siku moja

  • Siku hiyo, mhusika alipigiwa simu na MKTE na hatimaye fundi huyu naye kuigiza kama ndiye aliyempigia simu mhusika
  • Baada ya mhusika kuingia ndani wakiwa wameambatana na huyu fundi (tumwite MOOD) ndani walimkuta fundi mwingine wa plii (tumwite FUNDI-B) akiwa yupo bafuni
Ikumbukwe kuwa katika maongezi yao na BMN, mhusika alimjulisha BMN kuwa asingependa kupokea nyumbani kwake fundi ambaye atakuwa hajatoka kwenye mikono ya MKTE

  • Huyu MOOD aliyekuwa amekaa kwenye parking akimsubiria mhusika arudi nyumbani, inaonekana kama ndiyo yule ambaye aliripotiwa na BMN kuwa angekuja pale siku hiyo
  • Kwa upande mwingine FUNDI-B ndiye ambaye mhusika alimkuta ofisini kwa MKTE asubuhi hiyo.
  • Fundi huyu alikuwa yupo chooni muda wote akiwa amesimama pamoja na kifaa cha kurekebishia maji taka wakati mhusika na MOOD walipokuwa wanaingia ndani
MOOD naye baada ya kuingia nyumbani kwa mhusika, aliongoza moja kwa moja hadi bafuni, kule alikokuwa amesimama FUNDI-B, na baada ya sekunde kadhaa, MOOD aliaga na kusema inabidi atoke nje ili akaangalie kuna nini huko

Baada ya MOOD kuondoka, FUNDI-B, aliendelea kubaki bafuni

MOOD AONEKANA KAMA KUPOTELEA NJE

Muda mrefu kidogo ulipita MOOD akiwa yupo nje na hatimaye mhusika aliamua kushuka chini kwenda kumwangalia alikuwa anafanya kitu gani

  • FUNDI-B naye aliamua kutoka nje lakini yeye hakushuka chini; alitoka nje akawa amebaki somewhere kwenye ngazi
  • Mhusika alimkuta MOOD akiwa amesimama kwenye parking tu na hakuna kitu alichokuwa anafanya
Muda uliokuwa umepita zilikuwa takribani dakaika 20 hivi

Baadaye tena MOOD alimshauri mhusika kuwa warudi ndani nyumbani kwake

Mhusika alianza kuongooza njia, na pale kwenye ngazi kabla hawajafika nyumbani kwa mhusika, FUNDI-B naye aliwa-join tena, mhusika akawa yuko mbele halafu mafundi wawili wakimfuata kwa nyuma

Hapo kidogo MOOD na FUNDI-B walisimama kwa ajili yakujadiliana kitu, huku mhusika akiwa anaendelea na hatua zake za kupandisha juu bila kuwajali

Mhusika alifika kwenye mlango wa nyumba yake akafungua kitasa cha mlango na kuingia ndani akijua kuwa mafundi wanajadiliana kitu kwa sekunde kadhaa tu kwenye ngazi na baada ya hapo wataingia tena ndani nyumbani kwake mhusika

Baada ya kuingia ndani, mhusika aliwasubiria mafundi hao kwa dakika kadhaa bila kuwasikia wakigonga mlango na alipochunguia nje kwenye ngazi, hakuwaona tena mahali pale walipokuwa wamesimama wakiongea

Baada kuona hivyo, mhusika hakuamua kuwatafuta kutaka kujua walielekea wapi, kuokana na experience aliyonayo hadi muda huu

Mhusika alianza kunywa chai na baada ya kama dakika 10 hivi, mafundi hao walirudi tena; wakachukua vifaa vyao na kutoka nje

Katika kipindi chote hiki, mafundi hawa walikuwa tayari wameshalishughulikia tatizo la sink na wakati mhusika anarudi nyumbani, alilikuta likiwa tayari sink likiwa limeshakaa sawa. MOOD ndiyo yule aliyekuwa amefika siku ya Ijumaa kurekebisha sink hilo ambalo lilikuja kuziba tena jioni ya siku hiyo hiyo

NB Kuna nyumba iko kwenye ghrorofa analoishi mhusika haina watu; mambo yote yako kwenye nyumba hiyo

…………………….inaendelea
 
UPDATE: FRIDAY 08TH JULY 2022

KUHUSIANA NA WATU WAWILI WALIOMSOGELEA MHUSIKA WAKATI ANAJAZA FOMU YA MAOMBI KULE OFISI ZA MILIKI YA NYUMBA:


  • BAADA YA MHUSIKA KUFIKA NYUMBANI KWAKE JIONI NA KUKUTA BOMBA LILILOZIBULIWA ASUBUHI HIYO LIKIWA LIMEZIBA TENA:
  • IWAPO KAMA MHUSIKA ANGEAMUA KUSHUKA CHINI SIKU HIYO KWENDA KUONA NI NINI KILIKUWA KIMEPELEKEA KUZIBA TENA KWA BOMBA LA MAJI MACHAFU MARA BAADA TU KUWA LIMEZIBULIWA ASUBUHI SIKU HIYO
  • ASSUMING KUNGETOKEA CHOCHOTE CHA HATARI KWAKE WAKATI ANAJARIBU KULICHUNGUZA BOMBA HILO HUKO CHINI
Assuming kungetokea chochote cha hatari Ijumaa hiyo, watu hao wawili waliofika sehemu ya mapokezi wakati mhusika anajaza fomu ya maombi wangeweza kuwa mashahidi wazuri sana kwenye tukio hilo.

Hii ni kutokana na ukweli kuwa

  • Mmojawapo wa wawili hao, ukiacha yule ambaye ni fundi umeme, ndiye hasa huwa anashughulika kurekebisha MABOMBA YA NJE na mazingira yote ya nje yenye matatizo ya kuziba
  • Tatizo la mhusika lilihusisha bomba la ndani na hivyo kwa vyovyote vile, fundi huyu alijua fika kuwa hata ingekuwa ni kwa makubaliano binafsi, bado mhusika asingeweza kumchukua yeye
Kwa hiyo kiilichokuwa kimepelekea fundi huyu kumfuata mhusika (huku akiwa ameambatana na shahidi wa pili) na kumshauri kuwa angeweza kumpa yeye kazi ya ufundi huo ili aifanye, ilikuwa ni kujenga mazingira ya ushahidi wa baadaye kwa kile ambacho fundi huyu alikuwa anakijua na hivyo kukitarajia, na ambacho kwa muda huo maongezi yao, mhusika mwenyewe alikuwa bado hajakifahamu

Fundi huyu anaonyesha kuujua pasipo shaka, mtego ambao hatima yake ungepelekea mhusika atoke nje na kwenda kukagua kile kilichokuwa kimesbabisha bomba lililokuwa limezibuliwa asubuhi; kuziba tena jioni ya siku hiyo hiyo

Assuming mhusika angetoka nje na hatimaye kumtokea chochote cha hatari akiwa anakagua bomba hilo la nje, fundi huyu angeweza kusema kuwa “MIMI MWENYEWE NILIMUOMBA NIKAIFANYE KAZI HIYO LAKINI YEYE ALIKATAA; ILIKUWAJE TENA YEYE AKAAMUA KWENDA KUIFANYA MWENYEWE?”

Rafiki yake waliyekuwa naye ambaye ni fundi umeme, ndiye sasa angepigilia msumari kwa kusema kuwa hata yeye alikuwepo wakati fundi na mhusika wanafanya maongezi hayo

…………………..inaendelea
 
MAFUNDI BOMBA WAWILI WA J3 TAREHE 04TH JULY 2022

……………….inaendelea


Mafundi bomba waliingia ndani na kuchukua vifaa vyao ili wakafanye kazi nje

Hapa sasa walikuwa tayari wameshafanya ruling kwamba tatizo halikuwa nyumbani kwa mhusika ila kwenye nyumba ile ya jirani

Baada ya kuwa wamefanya kazi kwa takribani dakika 10, walirudi tena na kugonga nyumbani kwa mhusika, wakimuomba mhusika awafuate nje

Mhusika alikubali kutoka nje

BAADA YA MHUSIKA KUTOKA NJE

Mafundi walimweleza kuwa tatizo lililopo ni kubwa zaidi na hivyo hawawezi kulitatua wao peke yao na kwa vifaa walivyokuwa navyo

  • Hapo hapo mhusika akawa amepata shida kwenye maelezo hayo kwa sababu hapakuwa na sababu ya kutoka nje kwenda kumweleza haya; wangeweza kumweleza tu akiwa ndani nyumbani kwake, pasipo kumhitaji atoke nje
  • Baada ya kusikia hayo, mhusika aliwauliza ni nini ambacho wao kama wataalamu, walikuwa wanashauri kutokana na hali waliyokuwa wameiona
Mafundi walisema wanahitaji kuongea na MKTE ili aongeze watu wengine zaidi ikiwa ni pamoja na vifaa zaidi vya kufanyia kazi

Implication ya maoni yao ilikuwa ni kwamba walihitaji sasa mhusika awachukue kwenye gari lake na kuwarudisha ofisi za miliki ya nyumba ili wakachukue vifaa zaidi possibly pamoja na extra manpower

Hapo hapo mhusika aliwaomba wapandishe juu nyumbani kwake ili mhusika akajaribu tena kumpigia simu MKTE na kuona kama safari hii anaweza kupokea simu

Baada ya kuingia ndani; mhusika aliwajulisha mafundi hao kwanza conditions mbili muhimu sana kwamba

  • Kwanza huwa kila inapotokea yeye (mhusika) amempigia simu boss wao MKTE; MKTE huwa mara zote hapokei simu za mhusika kwa kipindi kirefu sasa
  • Kutokana na hali hiyo, mhusika aliwajulisha mafundi hao kwamba; angependa kujaribu kumpigia simu MKTE muda huo ili waongee naye kwanza kuhusiana na kile ambacho walidhani kuwa anaweza kuwasaidia
  • Mhusika aliendelea kuwajulisha kuwa kama MKTE atapokea simu, basi mhusika atawachukua mafundi hao kwa gari lake kuwarudisha ofisi za miliki ya nyumba ili wakachukue vifaa vya ziada walivyosema kuwa wanavihitaji
  • Kwa upande mwingine, mhusika aliwajulisha kuwa kama MKTE hapatokea simu; basi hatawachukua mafundi hao kwenye gari lake kwa sababu alikuwa hawajui
Zaidi mhusika aliwajulisha mafundi hao kuwa anawafahamu kwa kina sana MR SHN pamoja MKTE namna walivyo kwake na hivyo asingependa sana kuonekana anaambatana na mafundi hao ambao walikuwa wanafanya kazi chini ya maelekezo nusu nusu ya MR SHN na MKTE; assuming MKTE hatapokea simu ya mhusika

NAMNA ULIVYOKUWA MCHAKATO WA KUMPIGIA SIMU MKTE ILI AWAONGEZEE MAFUNDI HAO WAWILI MANPOWER PAMJA NA VIFAA VINGINE VYA KAZI

Baada ya hapo, mhusika alijaribu kupiga namba ya MKTE na safari hii MKTE alipokea simu

  • Tangu maji yakatike nyumbani kwa mhusika March 2018 hadi siku hiyo, Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa MKTE kupokea simu ya mhusika
  • Kwa hiyo MKTE alikuwa na zaidi ya miaka mine hajawahi kupokea simu ya mhusika
  • Baada ya MKTE kupokea simu hiyo, mhusika aliwaachia mafundi wake ili waongee naye
  • MKTE na mafundi waliongea na kukubaliana kuwa MKTE inabidi aje hapo nyumbani kwa mhusika muda huo aili ajionee hali halisi yeye mwenyewe
  • Baada ya muda mpango huo ulibadilika tena na kuwa Wilson ndiyo inabidi aje badala ya MKTE
Yeyote yule ambaye angeweza kuja kati ya wawili hawa, bado ilikuwa ni faraja kubwa sana kwa mhusika kwa sababu wao ndiyo wanaolifahamu zaidi tatizo la kuziba kwa bomba hili la maji machafu ya bafuni na chooni. Vile vile, ndio wanaofahamu pia kama kuziba huko kuna siri zilizojificha nyuma yake ama la, na kama zipo, basi wawili hawa ndiyo wanaozijua vizuri sana siri hizo

Baada ya maongezi hayo, mafundi hawa walitoka nje na kuanza kazi, bila kifaa kingine cha nyongeza na pasippo MKTE au Wilson kuja kwenye site ya kazi

  • Muda huo huo tena, mhusika aliamua kurudi ofisini akiacha maagizo nyumbani kuwa mafundi hawatakiwi tena kuingia ndani nyumbani kwake kwa sababu tatizo halikuwa nyumbani kwake na kama watahitaji tena kuingia ndani, basi inabidi mhusika ajulishwe kwa simu huko ofisini.
  • Mhusika alitoka nje na kuwasha gari akiwa anaelekea ofisini.
Pale nje alimkuta fundi MOOD akiwa kwenye eneo la kazi ilipo mifereji ya maji hayo, huku FUNDI B yeye akiwa ameinama kwenye parking za gari akiwa ameelekeza uso wake upande ule ilipokuwa imepaki gari ya mhusika, akiwa ameficha uso wake. FUNDI B alikuwa ameinama chini kwenye parking mithili ya mtu aliye kwenye Ibada anaswali

Mhusika hakuwasemesha mafundi hawa na aliwasha gari lake na kurudi ofisini

………………..inaendelea
 
DAKIKA KADHAA BAADA YA MHUSIKA KUWASILI OFISINI: MHUSIKA APIGIWA SIMU KUJLISHWA KUWA MAFUNDI WALIHITAJI TENA KUINGIA NDANI NYUMBANI KWAKE

Ikumbukwe kuwa siku hiyo mhusika alikuwa anashughulikia pia muamala wa Bima

  • Wakati anapigiwa simu ya kujulishwa kuwa mafundi walihitaji kuingia tena nyumbani kwake, muda huo alikuwa yupo ndani Benki akiwa sasa anajiandaa kutoka nje, baada ya kuwa amemaliza kufanya malipo ya Bima
  • Mhusika alipotoka Benki, alinyooosha moja kwa moja hadi kwenye parking, akwasha tena gari lake na kurudi nyumbani
Alipokuwa yuko kama mita 50 hivi nyuma kutoka ilipo kona ya kukatiza kutoka njia kuu na kuingia yalipo makazi yao, kwa mbele kidogo alimuona fundi MOOD akiwa tayari yupo barabara kuu, akitembea upande wa kulia wa barabara (kulia kwake mhusika, kushoto kwake yeye fundi), kuelekea uelekeo ule ambao mhusika alikuwa anatokea; possibly alikuwa yuko njia moja akirudi ofisini kwake
  • Mhusika alijaribu kuvunga kama hajamuona na kuacha kumpungia achilia mbali kusimama, kutaka kuona nini angeweza kufanya baada ya hapo
  • Mhusika alipofika eneo la makazi yake; alipark gari lake na kulizima
Wakati anashuka kwenye gari, fundi MOOD naye akawa tayari ameshafika tena mahali pale baada ya kuwa aligeuza njia baada ya kuwa ameliona gari la mhusika

  • Fundi MOOD alifika hadi pale alipokuwa amesimama mhusika na kumpa maelezo kuwa alikuwa yuko njiani anaondoka ila amerudi baada ya kuiona gari
  • Baada ya hapo, fundi MOOD alimuongoza mhusika hadi pale ulipokuwa mfereji wa maji taka na kumwonyesha mhusika kitu ambacho alikiona ni maigizo, na asingependa sana kukiongelea humu
Kitu hicho kilikuwa kinajaribu ku-justify system ya maji hayo kuziba pasipo kuwa kumechangiwa na jitihada zozote au makosa yoyote ya kibinadamu

Mhusika hakuona haja yoyote ya yeye kuonyeshwa kitu hicho ili athibitishe sababu za bomba kuziba, yeye alichokuwa anahitaji ni kuona kuwa bomba limezibuliwa na linafanya kazi sawsawa na si vinginevyo

  • Kitu hiki kilionyesha kama fundi MOOD alikuwa ame-caclcuate kupanda kwenye gari la mhusika kutokea pale bararabarani walipopishania, kurudi mahali pale, assuming mhusika angesimama na kuongea naye pale barabarani.
  • Kulikuwa na uwezekano kwamba MOOD angeomba apande kwenye gari halafu arudi akamuonyeshe kitu mhusika eneo lile ambalo fundi alikuwa amelifanyia kazi
Wakati huo FUNDI B yeye wala hakuwepo kabisa maeneo hayo na mhusika hajui fundi huyu aliondoka ondokaje mahali pale

…………………….inaendelea
 
HITIMISHO:

Tukio la mwaka jana la mafundi waliowahi kuja kufanya kazi ya kurudisha maji yaliyokuwa yamekatwa kwa makusudi nyumbani kwa mhusika ambalo sehemu tu ya taarifa yake imeongelewa kwenye post hii hapa #728 LILIBEBA BAADHI ya mambo kadhaa yafuatayo

  • Lilihusisha mafundi wageni kabisa ambao hapo awali, mhusika alikuwa hajawahi kukutana nao hata mara moja, na ambao hawakuwa wametambulishwa kwa mhusika
  • Lilihusisha fundi ambaye walijitambulisha kwa mhusika kwa kumu-approach mhusika akiwa kwenye ngazi
  • Lilihusisha MAJI MACHAFU kuvuja kutoka nyumba juu ya jirani yule yule wa sasa na kuingia nyumbani kwa mhusika kwa kupitia jikoni
  • Lilihusisha mafundi kupandisha juu kutokea nyumba ya mhusika kuelekea juu nyumba ya jirani ambayo ilikuwa inavujisha maji machafu na kuingia nyumbani kwa mhusika
  • Lilihusisha nyumba ya juu kabisa kwenye ghorofa hilo analoishi mhusika (ambayo imekuwa haina wakazi kwa kipindi kirefu sana) kukaliwa kwa muda mfupi na watu ambao si wafanyakazi wa taasisi, na ambao walifika ghafla na kupewa hifadhi kwenye nyumba hiyo, siku chache tu kabla ya ujio wa mafundi wa maji
Akijaribu kuangalia ulinganifu wa matukio haya ya MAJI MACHAFU, lile la mwaka jana na la mwaka huu, msomaji ataona kuwa matukio yote mawili yamefanana isipokuwa tufauti ndogo tu iliyopo ni kwamba TUKIO LA MAJI MACHAFU YA MWAKA JANA LILIHUSISHA MAJI MACHAFU YALIYOKUWA YAKIVUJA JIKONI KWA MHUSIKA WAKATI LILE LA MWAKA HUU LIMEHUSISHA MAJI MACHAFU YALIYOKUWA YAKIVUJA BAFUNI /CHOONI KWA MHUSIKA

Matukio yote haya mawili yakiwa yanahusisha maji machafu kuvuja na kuingia ndani nyumbani mwa mhusika, huku yakiwa yanatoka kwenye nyumba ile ile moja ya jirani ambaye nyumba yake iko juu ya ile ya mhusika

MUBARIKIWE TENA NA BWANA
 
UPDATE 15TH JULY 2022

Coming up next:

YALE YA MUHIMU TU YALIYOJIRI KUANZIA J2 YA TAREHE 10 JULY 2022 HADI JANA ALHAMIS YA TAREHE 14TH JULY 2022

Stay tuned
 
UPDATE 15TH JULY 2022

YALE YA MUHIMU TU YALIYOJIRI KUANZIA J2 YA TAREHE 10 JULY 2022 HADI JANA ALHAMIS YA TAREHE 14TH JULY 2022


Kwa muda huu, yale yote yaliyojiri siku ya J2 anaomba ayaache kwanza, atakuja kuyaongelea baadaye. Hapa ameyataja tu katika namna ya kuweka kumbukumbu akimaanisha kuwa lazima tu atakuja kuyaongelea huko mbele ya safari

YAJILYOJIRI OFISINI ASUBUHI SIKU YA J4 TAREHE 12/07/2022

Akiwa yupo ofisini asubuhi hiyo, mtandao wa computer yake ulikatika.

Kukatika kwa mtandao huu ndiyo jambo analoliona kuwa lina uhusiano sana na baadhi ya matukio machache tu yaliyotokea J2 ya wiki kabla ya J4 hiyo, pindi alipokuwa yupo Kanisani. Machache haya ndiyo yale ambayo asingependa sana kuyaongelea kwa sasa, bali hapo baadaye. Anachokisema hapa anakijua na ana uhakika nacho na kwa hali hiyo wasomaji wa taarifa hizi wanazidi kuombwa kuendelea kusoma kile kilichopo hapa muda huu

NAMNA AMBAVYO MTANDAO WAKE WA OFISINI UMEKUWA UKIKATIKA KWA MARA NYINGI KWA KIPINDI KIREFU SASA

Kikubwa kuzidi yote, mtandao huu huwa unakatika kwenye Kompyuta yake yeye peke yake, halafu baada ya muda (siku kadhaa au masaa kadhaa wakati mwingine), mtandao huu huwa unarudi na pasipo kufanyiwa marekebisho na mtu yeyote yule

  • Kuna siku hadi aliwahi kutoa details humu jukwaani za namna mtandao wake ambavyo huwa unakatika
  • Kila unapokuwa umekatika, mhusika huamua kutumia bundle ya kununua kwa cellular network ISP’s na hutumia hiyo hadi pale ule wa ofisini kwake unapokuwa umerudi
Hata hivyo, J4 hii hakuwa na bundle na hivyo aliamua kwenda kumuona mtaalamu wa maswala haya ya mtandao; na baada ya kuongea naye; kilichoendelea baada ya maongezi hayo ndiyo sasa kikawa kimepa mwanga wa kuunganisha na yale machcahe yaliyokuwa yamejiri Kanisani siku ya J2, na hatimaye kupelekea haja ya angalau kuleta kitu humu jukwaani.

  • Hii inamaanisha kuwa iwapo kama asingepata nafasi ya kuongea na huyu mtaalamu wa IT, haya matukio machache anayoyataja kuwa yalijiri kanisani J; strictly yasingeweza kuleta maana yoyote kwake.
  • Kwa hiyo ni baada tu ya kuongea na huyu mtaalamu wa IT, ndiyo matukio yale ya Kanisani yaliweza kuleta maana kwake
Kwa kifupi tu ni kwamba kule kanisani kulifanyika tricks mbili ambazo zilikuwa zimelenga kumfanya mhusika aonekane kuwa ameghafirika; mojawapo ya matukio yanayoshahibiana na lile lililotokea nyumbani kwake hivi karibuni baada ya kinyesi kufurika bafuni na chooni

Kwa hiyo J4 ndiyo mtandao ulikatika tena na hivyo kumpelekea safari hii alazimike kwenda kumuona mtaalamu wa maswala ya mtandao ofisini kwake

BAADA YA KUWA AMEFIKA OFISINI KWA MTAALAMU HUYO

Lawama nyingi zilirudi kwake yeye mhusika kuwa hajawahi kuripoti matukio ya aina hiyo pindi yanapokuwa yamemkabili. Mhusika aliona ni bora tu akubaliane na lawama hizo ili aweze kupata mdsaada, japo, hajawahi kuona policy yoyote ambayo ilishatolewa ikiwa inaelezea namna utartibu huo ulivyo kama ulivyokuwa ukitajwa mdomoni na mtaalaamu wa IT.

Utaratibu aliokuwa anaujua yeye (mhusika) hadi siku hiyo na ambao umekuwa ukitumika enzi na enzi, ni aidha kumpigia simu mtaalamu kwa kutumia hela iliyoko kwenye simu yako ya mkononi au kumfuata na kwenda kuongea naye physically ofisini kwake

  • Mtaalamu huyu vilevile, alimjulisha mhusika kuwa utaratibu uliopo kwa sasa ni kwa kuandika email kwenda kwake na baada ya hapo mteja hupewa namba (unique ID) inayohusiana na tatizo lake.
  • Mtaalamu alienda mbali zaidi na kumuomba mhusika wakati huo huo wa maongezi yao, a-login kwenye official email yake na baada ya hapo mtaalamu huyo alimsaidia mhusika kuandika email ya kuwasilisha tatizo lake kwake (mtaalamu)
BAADA YA HAYO YOTE KUWA YAMEJIRI; MHUSIKA AOMBA SASA KUELEWESHA KWA MAELEZO YA KITAALAMU; NINI HASA KIMEKUWA KIKISABABISHA KOMPYUTA YAKE PEKE YAKE TU KUKATIKIWA MTANDAO JENGO ZIMA

Mtaalamu alijibu kuwa sababu zinaweza kuwa nyingi tu na zinaweza kufika hata 20 ila mojawapo ya zile alizozitolea mfano alisema ni kama OS ya workstation kukosa updates zinazohitajika au FIREWALL SETTINGS za anti-virus zilizowe kwenye workstation husika.

Baada ya kusikia maelezo hayo, mhusika aliziondoa sababu hizi kwa sababu kama zingekuwa valid, basi asingeweza pia kupata mtandao kwa kutumia bundles za cellular ISP’s. Hadi hapa mhusika akajua kuwa mtaalamu huyu alikuwa anaijua vizuri sababu hiyo isipokuwa tu alikuwa hataki kuiweka wazi kwa mhusika

……………………..inaendelea
 
PINDI MHUSIKA ALIPOKUWA AKIFANYA MAONGEZI YAKE NA MTAALAMU WA IT (tumwite MT-IT)

Kijana mwingine ambaye alionekana kuwa ni subordinate wa MT-IT; aliingia ofisini na kukuta maongezi yao yakiwa yanaendelea

  • Kijana huyu alichukua kiti na kukaa na hatimaye kuanza kusikiliza maongezi kati ya mhusika na MT-IT hadi mwisho; mithili ya ilivyokuwa kwa yule fundi bomba aliyefika nyumbani kwa mhusika siku J3 wiki jana
  • Huyu naye (fundi bomba) alikuwepo wakati mhusika na MKTE wakifanya maongezi yao ila wawili hawa, yaani fundi bomba na mhusika hawakutambulishwa
  • Baada ya hapo, mhusika alimkuta fundi bomba tayari yupo nyumbani kwake akiwa anafanya kazi
Hii scenerio ya wiki jana inafanana sana na hii ya wiki hii

J5 hii vilevile, MT-IT hakuwatambulisha mhusika na SMT-IT na lakini baada ya hapo, SMT-IT alifika kwenye jengo ilimo ofisi ya mhusika, akimtaka mhusika waongozane naye kutokea hapo kwenye veranda, ili SMT-IT akafanye kazi ofisini kwa mhusika

TUKIRUDI NYUMA TENA KWENYE SIKU YA MAONGEZI YA KWANZA KATI YA MT-IT NA MHUSIKA

Baada ya maongezi, mhusika alihakikishiwa kuwa kuna mtu atafika ofisini kwake kuja kushughulikia tatizo hilo, kuona ni nini hasa huwa kinaendelea kwenye computer yake

  • Baada ya mhusika kuachana na MT-IT siku hiyo, alirudi ofisini na kukuta mtandao ukiwa tayari umesharudi
  • Aidha J4 hiyo hakuona mtu yeyote aliyefika ofisini kwake kuona kama tatizo lake lilikuwa bado lipo ama la
Kesho yake J5 mtandao ulikuwepo siku nzima haukukatika

YALE YA MUHIMU AMBAYO HASA YAMEPELEKEA TAARIFA HIZI KULETWA KWENU
:

KABLA MTAALAMU KUTOKA OFISI YA MT-IT HAJAJA KUANGALIA KAMA TATIZO LA MTANDAO WA MHUSIKA LIMESHAKWISHA AMA LA:

MAONGEZI MENGINE KATI YA MHUSIKA NA WATU HAWA WAWILI YAANI SUBORDINATE WA MT-IT PAMOJA NA MT-IT MWENYEWE YAFANYIKA NDANI YA JENGO ILIMO OFISI YA MHUSIKA, BAADA YA MHUSIKA KUONANA NA WATU HAWA KILA MMOJA KWA WAKATI WAKE PASIPOKUWA AMETARAJIA


Mhusika aliongea na watu hawa wawili kila mmoja kwa wakati wake na kwa siku mbili tofauti ambazo ni J5 na Alhamis za wiki hii. Zaidi ni kuwa mhusika hakuwatafuta watu hawa ili aongee nao bali ilitokea kwa bahati tu wakaonana naye wakiwa wametembelea kwenye jengo ilimo ofisi yake

  • Maongezi ya mhusika na Subordinate wa MT-IT (tumwite SMT-IT) yalifanyika J5 kwenye mhusika akiwa yupo kwenye veranda na SMT-IT akiwa kwenye ngazi
  • Ikumbukwe kuwa kwa maongezi ya aina hii mmoja akiwa amesimama kwenye ngazi na mwingine akiwa kwenye veranda, ni yule aliyekuwa kwenye veranda tu ambaye alikuwa anaonekana na CCTV camera
  • Yule aliyekuwa kwenye ngazi, au SMT-IT hakuwa anaonekana na camera, isipokuwa angeweza kuonekana tu pindi wawili hao wakiwa wanatembea kwenye corridor, iwapo mhusika angeamua kuongozana naye (SMT-IT) kuelekea ofisini kwake (mhusika)
Kwa upande mwingine, maongezi ya mhusika na MT-IT yalifanyika Alhmis kwenye korido pia. Tangu J4 baada ya maongezi na MT-IT, mtandao wa mhusika ulikuwa sawa ila ulikuja kukatika tena mara tu baada ya kuwa ameongea na MT-IT siku ya Alhamis

NAMNA MAONGEZI YA MHUSIKA NA WATU HAWA WAWILI YALIVYOTOKEA (SIYO YALIVYOFANYIKA)

J5 kwenye majira kama ya saa 8 hivi, mhusika alitoka ofisini akiwa anaelekea washroom

  • Baada ya kutoka huko, kama ilivyo kawaida yake siku zote, mhusika aliamua kupumzika kidogo akinyoosha viungo kwenye veranda iliyoko ghorofa ya kwanza
  • Akiwa yuko pale, ghafla alitokea SMT-IT akitokea chini anapandisha juu; na hatimaye kusimama kwenye ngazi
  • SMT-IT alimuomba mhusika kama wanaweza kuongozana kutokea pale kuelekea ofisini kwake ili akashughulikie tatizo la mtandao wake
Mhusika alimweleza SMT-IT kuwa mtandao wake ulikuwa tayari umesharudi na hivyo hapakuwa na haja ya kupoteza muda wa SMT-IT kuongozana naye kuelekea ofisini kwake (mhusika).

Hayo yakawa ndiyo maongezi ya kwanza na mafupi sana kati ya mhusika na SMT-IT. Hiyo siku ikapita

Ikumbukwe kuwa wakati SMT-IT anaongea na mhusika, alikuwa amesimama kwenye ngazi na hivyo alikuwa haonekani na CCTV camera

JANA ALHMIS TAREHE 14/07/2022


Maongezi mengine mafupi yalifanyika kati ya mhusika na MT-IT mwenyewe.

  • Wakati maongezi haya yanafanyika, ofisi ya mhusika yenye mlango unaoelekeana na korido nzima ya ghorofa ya kwanza ilikuwa iko mlango wazi
  • Ilikuwa ni majira ya mchana kati ya saa 7 na 8 mchana, MT-IT alifika kwenye jengo ilimo ofisi ya mhusika
  • MT-IT alikuwa anaelekea ofisini kwa Mkuu wa MAJOR UNIT; ofisi ambayo iko si zaidi ya mita 10 kutoka pale ilipo ile ya mhusika
  • Muds huo MT-IT akiwa anajaribu ku-access kwa mkono wake kitasa cha mlango wa ofisi ya Mkuu wa MAJOR UNIT, alisalimiana na mhusika
  • Baada ya hapo MT-IT alimuuliza mhusika kama tatizo la J4 bado lipo au limeshaisha ili kama halipo aende akaifunge case yake
  • Mhusika alimjibu kuwa tatizo liliiisha siku hiyo hiyo na pasipo mtu yeyote kuja kulishughulika
  • Mhusika aliongezea kwa kumuomba MT-IT amjulishe SMIT-IT asiwe anamvizia (mhusika) kwenye korido wakati issue ni official; asiwe anafanya kazi kama mtu ambaye ni invader kwenye jengo
MT-IT alimjulisha mhusika kuwa ujumbe huo umefika na ataufanyia kazi ipasavyo

Baada ya hapo, MT-IT aliingia ofisini kwa Mkuu wa MAJOR UNIT, na maongezi yao yakawa yameishia hapo. Haya yakawa sasa ni maongezi ya pili kati ya MT-IT na mhusika

HITIMISHO:

Mara tu baada ya maongezi ya mhusika na MT-IT kumalizika, mtandao wa mhusika ulikatika tena

  • Baada ya takribani dakika 10 mtandao ukiwa hauna dalili zote za kurudi, mhusika alitoka ofisini na kwenda kubarizi tena kidogo kwenye veranda ya ghorofa ya kwanza
  • Baada ya kuwa hayupo ofisini kwa takribani dakika 15, mhusika alirudi ofisini na kukuta mtandao umesharudi tena
Cha muhimu zaidi alichokiona mhusika kwenye tukio hili ni kuwa kitendo cha SMT-IT kutaka kwenda kufanya kazi ofisini kwa kupitia njia ya kumvizia mhusika akiwa kwenye veranda kinashahibiana sana na kile cha mafundi wa wiki jana waliofika ofisini kwa mhusika kwa ajili ya kushughulikia maji yaliyokuwa yanavuja na kupita sehemu isiyo sahihi
MUBARIKIWE TENA NA BWANA
 
UPDATE 19TH JULY 2022

TATIZO LA KIFAA MUHIMU KUSHINDWA KUFANYA KAZI LILILOWAHI KUMPATA MHUSIKA SEPTEMBA 2020 (MWAKA JUZI) LAJIRUDIA TENA MWAKA HUU (2022), KWENYE KIFAA KINGINE KIPYA CHA AINA HIYO NA KATIKA MAZINGIRA YANAYOFANANA SANA


Mnamo Septemba 2020 (mwaka juzi) mhusika alipatwa na tatizo la kifaa chake cha nyumbani kushindwa kufanya kazi ambacho kwa sasa asingependa akitaje ni kifaa gani

  • Wakati kifaa hicho kinashindwa kufanya kazi, wanafunzi walikuwa tayari wameshaondoka mazingira ya kazini, walikuwa wako field
  • Mwishoni mwa mwezi jana (JUNE 2022), mhusika aliamua tena kwenda kununua kifaa kingine kipya cha aina ile ile kama kile kilichowahi kushindwa kufanya kazi mwaka 2021, na kwenye duka lile lile alilowahi kununua kile cha mwanzo
  • Kifaa hiki kipya mara ya mwisho kilitumika kikiwa kiko sawasawa, asubuhi ya J2 iliyopita ya tarehe 17/07/2022
  • Baada ya kutumika asubuhi J2 hiyo, mhusika aliondoka kuelekea Kanisani
  • Alivyorudi kutoka Kanisani J2 hiyo muda wa saa 8 mchana, mhusika alikuta kifaa hicho hakifanyi kazi tena na katika namna iko sawa kabisa na ile ya kile cha awali
Zaidi ni kuwa Ijumaa iliyopita ya tarehe 15/07/2022 wanafunzi walimaliza mitihani yao na possibly, baadhi yao ndiyo ilikuwa siku ya mwisho kuwepo katika mazingira ya ofisini kwa mhusika

HITIMISHO:

Kifaa kile cha awali kiliharibika ndani ya muda ambao wanafunzi hawakuwepo kwenye mazingira ya ofisini kwa mhusika wakati hiki cha sasa kimeharibika siku ya pili tu baada ya wanafunzi hao kuwa wamemaliza mitihani yao na hivyo kupelekea wengi wao wasiwepo kwenye mazingira ya ofisini ya mhusika

Kifaa hiki cha sasa alikinunua tarehe 24/06/2022 kutoka kwenye duka moja maarufu sana na linaloaminika sana hapa jijini Dar es Salaam

MUBARIKIWE TENA NA BWANA
 
Back
Top Bottom