Mkasa wa kweli, kuhusu visa vya kushangaza nilivyokutana navyo katika kazi za Udalali

Mkasa wa kweli, kuhusu visa vya kushangaza nilivyokutana navyo katika kazi za Udalali

Me nna swali moja.. sasa maisha yalivyokupiga, why hukuwaza kuurudia udalali? Maana niliona ni simple zaidi kurudi kule huku ukijipanga kwa mengine
DALALI MKUU
Udalali una mambo mengi sana. afu ukishatoka sehemu ukirudi unaanza tena upya unarudi kama mgeni.

hata hivyo sikuwa natamani tena hiyo kazi
 
Hivi kumbe Mtu pasipo kujali Hali Yako ya kiroho Unaweza kuandaa programu ya maombi katika jambo lako na majibu yakapatikana pasipo msaada wa watumishi wa Kisasa!? Kama Jeni alipata watoto Kwa njia ya Imani(maombi binafsi)...
Maombi ni Imani yako binafsi mkuu.

Watumishi mara nyingi ni kutuongoza tu ila kimsingi unaweza kuwa na program yako binafsi na ukatoboa ili mradi ujue tu jinsi ya kuomba
 
Hii roho mmepewa wanaume siwezi kushangaa ila sio sie wanawake, hamjufunzi kwa Adam aliletewa sijui tunda akapokea na akala kilichomkuta ni laana ya kifo na nyinginezo tunazoishi nazo mpaka kiama
kuna wakati hata sisi wanaume huwa tunakwama na tunapeda watu wa karibu watusaidie hata kwa kidogo,ila utashangaa mwanamke unayemhudumia kila siku hawezi hata jiongeza,kuna wanawake wanafikiri walivoambiwa wawe wasaidizi wanafikiri wnatakiwa kufua soksi kama vile sisi hatuji kufua
 
EPS 1

Heshima Kwenu Wakuu,

Niliwaahidi Kwamba Nitawaletea Mkasa Kuhusu safari au Hekaheka zangu nilizozipata wakati nafanya Shughuli zangu za Udalali Jiji la Dar es salaam na maeneo ya jirani.

Mwaka 2017 Nilitoka kwenye wilaya Niliyokuwa Ninaishi nikaamua Kuhami Jiji La Dar es salaam kwenda Kufanya Kazi zangu binafsi nikiamini Kwamba nitatoboa Kimaisha, Nilikuja Dar es salaam baada ya kufanya akzi maeneno tofauti tofauti Mkoa wa Kilimanjaro.

Nilipofika Dar maisha Yalikuwa magumu sana kwakweli, kuna sehemu nilipata Kazi nilikuwa nalipwa 40k kwa wiki haikuwa inatosha Chochote, Lakini kazi Pia ilikuwa na mateso sana. Nilikuwa nafanya kazi kwenye Kampuni Fulani Binafsi inajihusisha na Masuala ya Matangazo ilikuwa ni kazi ya mteso sana, nilikuwa naingia kazini Asubuhi saa moja natoka saa 12 Jioni.

Nikitoka nakuwa nimechoka sana kiasi kwamba siwezi hata Kufanya shughuli nyingine na mshahara ndio huo kwa wiki unalipwa elfu arobaini tu ukitoa hapo nauli na hela ya kula kwa wiki unabaki na deni au ukijibana sana useme ule mlo mmoja tu unabaki na elfu Kumi.

Kodi nilikuwa nalipa eldu thelathini kwa mwezi maji elfu kumi umeme elfu Kumi jumla Kodi kwa mwezi ni elfu hamsini na kila wiki nikijibana sana kwa mwezi nakuwa na Akiba ya Elfu arobaini yaani kila iki elfu Kumi.

Hapo nilipokuwa nakaa ilifika wakati kodi ikaisha nikawa sina hata Mia mbovu akiba yote nilikuwa nimeitumia kutokana matatizo yaliyojitokeza, Mwenye nyumbaalikuwa haelewi Kitu zaidi ya kutaka hela yake.Yule mzee alinisumbua sana nikaongea nae Anivumilie akanipa Muda wa wiki nikaanza kupiga Bei vitu vyangu vya ndani ila kupata wateja ndio ikawa shida sana, kila nikinidai Mitandaoni hakuna mteja zaidi watacoment watu wanaulizia Uko wapi na bei gani tu.

Aisee nilichanagnyikiwa sana Wakuu Wiki ikakata nikapata ile hela ya wiki Elfu arobain nikakusanya kusanya kwa wadau nilikuwa naapiga Vizinga nikapata elfu sabini nikampa mwenye nyumba ili inayobaki nitamlipa.

Kuna watu ana Roho mbaya sana Yule Mzee akaniambia hapokei Kodi hata kama Imebaki Buku Hapokei na kama siwezi kumpa hela yake nijiandae kuhama nikatafute Chumba sehemu Nyingine.

Pale pale akaanza Kupiga simu anamtafuta Dalali ili amtafutie mpangaji mwingine, Hela yangu ameikataa nilirudi ndani nikawaza sana mambo mengi mno nilipiga simu kwa wadau lakini kila ninayemkopa ananielezea matatizo yake makubwa zaidi nikaamua kuachana nao.

Nikiwa ndani Yule Mzee nikamsikia anaongea na watu anamuonyesha Chumba Changu na wanakubaliana bei afu anamwambia Kuna mtu ndnai ila nitamwmabia afungue uingie ndani ukiangalie.
Nyumba za kupanga ni ngumu sana
 
kuna wakati hata sisi wanaume huwa tunakwama na tunapeda watu wa karibu watusaidie hata kwa kidogo,ila utashangaa mwanamke unayemhudumia kila siku hawezi hata jiongeza,kuna wanawake wanafikiri walivoambiwa wawe wasaidizi wanafikiri wnatakiwa kufua soksi kama vile sisi hatuji kufua
Wanawake wana ufala sana.
 
Hivi kumbe Mtu pasipo kujali Hali Yako ya kiroho Unaweza kuandaa programu ya maombi katika jambo lako na majibu yakapatikana pasipo msaada wa watumishi wa Kisasa!? Kama Jeni alipata watoto Kwa njia ya Imani(maombi binafsi)...
Mtumishi ana nafasi yake,na muombaji ana nafasi yake.Kwani yule mama aliyekuwa anatokwa na damu kwa miaka 12 aliombewa na nani?,si alichukua hatua za imani mwenyewe na akapona?
 
kuna wakati hata sisi wanaume huwa tunakwama na tunapeda watu wa karibu watusaidie hata kwa kidogo,ila utashangaa mwanamke unayemhudumia kila siku hawezi hata jiongeza,kuna wanawake wanafikiri walivoambiwa wawe wasaidizi wanafikiri wnatakiwa kufua soksi kama vile sisi hatuji kufua
Na ndo usaidizi wenyewe huo ukitaka unaozidi hapo sasa ndo tatizo linapoanzia
 
Mtumishi ana nafasi yake,na muombaji ana nafasi yake.Kwani yule mama aliyekuwa anatokwa na damu kwa miaka 12 aliombewa na nani?,si alichukua hatua za imani mwenyewe na akapona?
Mtumishi ni Kiongozi anayekuongoza tu. Ila unaweza kuwa na Program zako mwenyewe Roho mtakatifu akakuongoza, ukaomba na ukajibiwa vizuri tu.

Shida watu wengi hawawezi kujisimamia wanapenda kuwekewa mikono na watumishi.

Ndio watumishi wengine wanawadanganya wanafunga kwa ajili yao,Mwisho wa siku unapigwa tukio.
 
Back
Top Bottom