Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Usie tate waonda chaonga iweMhhhh! Taarifa za huyo bi mkubwa kuzisagasaga hizo hela alizopewa na huyo Joseph ulizipata wapi?
INAENDELEA:
Kwa mujibu wa watu hapa kijijini hakuna mtu yeyote aliyehusisha ule msiba na dhana potofu ilionekana Kama vifo vingine vya kawaida.
Mambo yakaendelea kuwa mazuri zaidi kwa Gado, nakumbuka mwaka mmoja alikuja pale kijijini na Mimi nilikuwepo likizo nilishuhudia anafanya operation ya kuondoa vitanda vyote vya ngozi ama vile vya spring vilivyokuwa vinatumika sana kule kijijini kwenye nyumba za ndugu, jamaa na marafiki zake walikuwa ni wengi akawawekea vitanda vipya vya mbao na magodoro.
Huyu mwamba nadhani alijifunza kutokana na makosa ya Kaka yake, alikuwa hatoi pesa taslimu yeye alikuwa anawanunulia ndugu vitu au anampa pesa mtu mwingine akupe.
Kulingana na ukwasi aliokuwa nao akaoa Traffic mmoja wa kichaga hukohuko Arusha hiyo Harusi yao ilikuwa ni balaa madon na viongozi wa huko Arusha asilimia kubwa walikuwepo...mwamba akapewa jina la Kikwete wa pale kijijini.
Sasa pamoja na huyu jamaa kusaidia sana wazazi na ndugu wengine lakini akawa hasaidii kabisa mdogo wake huyu Sarah na kaka yake mkubwa aliyefirisika Joseph..yaani ukawa ni uhasama kwa huyu kaka mpaka mama yao mzazi anafikia hatua anasema nyumba iliyojengwa na Joseph ni takataka.
Maisha yalimpiga Sarah baada ya kifo cha mumeme ikabidi shemeji mtu (Kiringo) awe anaradhimika kumpa msaada kila mwezi ili ajikimu yeye na mtoto wake.
Hili suala likawa linamuuza sana sarah na istoshe kisa na mume wake kufa ni huyo Kaka yake Gado na alimshirikisha namna ya kufanikisha hilo zoezi kwa ahadi nyingi na yeye akalifanya kwa ustadi mkubwa mpaka kuwezesha mume wake kufa
Ikafika kipindi Gado akawa hataki kumuona kabisa huyu mdogo wake Sarah yaani akipita njiani kuelekea kwake lazma akutane na Dada yake akichoma mahindi pembenzoni mwa barabara...Jamaa alichokuwa akifanya anafunga vioo vyake vya V8 yake then anapita Kama hamuoni hata salamu alikuwa hataki
NARUDI.....
Kama bado unaripoti live kutokea baa mi nashauri kwa leo ungeishia hapo ili kesho ndio uimalizie hii storyBoss maji...naandika nikiwa bar hii inaisha leo...mods kesho wataviunga isha
Tupo sambamba mkuuINAENDELEA:
Pale kijijini ikawa ni kikwete, Kikwete, Kikwete ndilo jina pekee vijana walikuwa wakilihusudu kulingana na ukwasi aliokuwa nao, vijana nao wakaanza kutafuta waganga wengine walipitia Mikasa japo Kuna wengine walifanikiwa leo sitaki kuwazungumia hao.
Huyu jamaa alizidi kuchanua kipesa toka 2005 mpaka namaliza chuo bado jamaa Yuko juu...alikuwa na magari hayahesabiki...mama yake akahimishia makazi Arusha lakini bahati mbaya hawakuwezana na mke wake hivyo akajengewa nyumba nyingine ya ghorofa huko huko Arusha.
Cha kushangaza huyu mama akawa anaona binti yake anateseka na anaishi kwa kuchoma mahindi Wala yeye hakujali...Sarah akachukia hii hali sana.
Sasa ilikuwa Kama 201... Siku moja akapata taarifa Kikwete (Gado) ameenda kwa mama yake kumsalimia nae akaenda kwa kushtukiza...na kukawa na baadhi ya watu wa kule kijijini akiwemo mfanyakazi wa ndani alitolewa huko kijijini kwetu...Binti Sarah alifika pale amefura mno.
Mkononi alikuwa ameshika ukuni wa mbao..moja kwa moja kwa mama yake piga bao la kwanza kichwani ile watu kuhamaki akampa la pili wakamshika akiwa anahema Kama mtu anaetaka kuzimia...pale ndani pakawa ni patashika wageni walipkuwepo wanashangaa nini hiki...
Narudi...
OkJamiiForums ni zaidi ya habari, nami nimeona niweke hapa kisa ambacho kinaweza kuwa funzo/somo kwa vijana wengi watafutaji hasa wanaopenda shortcut. Mtanisamehe kwa uandishi wangu mbovu na mpangilio wa visa
Mwaka huu mwanzoni nilikuwa mkoani Arusha kwa jamaa yangu mmoja tuliyetoka nae Kijiji kimoja huko mkoani kwa baba wa taifa.
Siku moja katika matembezi mjini na huyu jamaa yangu, Ghafla nikasikia naitwa jina langu kwa kilugha changu na mchoma mahindi aliyekuwa pembeni yetu "Requal, Omwanono Ge zisiku..ndola ukulili igo" nikashangaa kidogo maana alikuwa mmama wa makamo na sikuweza kumkumbuka kabisa..ikabidi nimjibu "Mazomu", baadae akahamia kwa jamaa akawa anamuuliza umempata wapi huyu kiumbe maana sijamuona zaidi ya miaka 10, katika maongezi ndio nikaja kugundua ni Sarah...sio jina sahihi (Jirani yangu kabisa kule kijijini) ni kweli hatujaonana miaka 10 na zaidi ..Ule urembo wake umeisha kabisa na sasa anaonekana Kama bibi yangu japo amenizidi miaka 4 tu ya kuzaliwa.Kiukweli alikuwa amechoka sana na alionekana mtu aliyekata tamaa na maisha kabisa na hapa ndipo nilipoona Kuna haja ya kuweka hapa huu mkasa ili wengine wajifunze.
STORY YA FAMILIA YA AKINA SARAH.
Sarah ametoka familia ya watoto watano pale kijijini kwetu, wa kike wawili na wakiume watatu, mkubwa tumpe jina Joseph, anaefuata wa kiume "nyanza", na wa mwisho wa kiume aitwe "Gedo"..Hiki kisa kinamhusu zaidi Sarah, Gedo, mama yao pamoja na mume aliyekuja kumuoa Sarah..kabla hatujafika huko tutamzungumzia kidogo Joseph ili kupunguza maswali huko mbeleni.
Baba yao Sarah alikuwa na wake wawili na mama yao Sarah hakuwa kipaumbele Cha baba yao, mke mdogo ndiye aliyependwa zaidi na familia ya mke mkubwa ni Kama ilitelekezwa vile.
Baba yao Sarah alikuwa na ndugu mmoja tu wa tumbo moja wa kiume na wa kike mmoja pia walipenda sana, Hawa wazee ilikuwa ni mfano kijijini pale kwa jinsi walivyokuwa wanapendana..Huyu wa kiume ambaye ni baba yake mkubwa Sarah alikuwa na wake wawili na mke mkubwa alikuwa anasadikika ni mchawi mkubwa sana pale kijijini anasadikika kufuga misukule, kule kijijini watu wanamuogopa mno tukikutana nae porini mwenyewe huwa tunajificha ili apite, huwa havai viatu akitembea na haachi unyao anapokanyaga...nae atahusika kidogo kwenye huu mkasa.
MKASA WA JOSEPH.
Joseph ni mtu mzima kidogo amezaliwa miaka ya 70's, huyu jamaa ana asili ya roho nzuri sana, mcheshi na mkarimu mno alikuwa family friend wa ukoo wetu..alioa mwanamke mrembo sana kutoka Kijiji Cha jirani yule mke hata ukikutana nae leo ni vigumu kujua Kama ile ni product ya kijijini.
Nikiwa bado niko elimu ya msingi kipindi hicho, Joseph akapotea pale kijijini kwa vile alikuwa family friend ilikuwa rahisi kujua mahali alikoenda, tukaambiwa ameenda mgodini Arusha Merelani kutafuta maisha kwenye machimbo ya Tanzanite, mkewe alibaki na baada ya mda mkewe alimfuata na huko ndio yakawa makazi yao.
Maisha ya familia hii yalikuwa ya kawaida sana, mama yao alikuwa anaishi nyumba ya suit yaani imejengwa kwa mabati chakavu kuanzia chini mpaka juu..na wao walikuwa na nyumba za nyasi pembeni na zaidi walikuwa wanategemea kilimo Cha jembe la mkono ili kuendesha maisha.
Baada ya Kama miaka miwili Joseph akarudi pale kijijini na kabla yeye kurudi kusalimia taarifa zilikuwa zimeshazagaa kwamba Joseph Sasa amewin maisha, watu pale tukawa na hamu ya kumuona kama mnavojua maisha ya kijijini.
Jamaa alikuja kwa gari lake akiwa anaendesha mwenyewe alikuwa ni gumzo pale kijijini na isitoshe alikuwa anagawa pesa kwa kila mtu anaekutana nae, hili halikuwapa watu maswali kwa sababu ya roho yake nzuri toka mwanzo...aliwawezesha sana ndugu na akaanza ujenzi rasmi wa nyumba mpya na ya kisasa kabisa ya mama yake kuishi.
Baada ya kuanza ujenzi baba yao akahamishia kambi kwa mke mkubwa na akapewa kazi ya kusimamia ule ujenzi wa ile nyumba na Joseph akarudi Arusha kuendelea na kazi zake.
Joseph Ghafla akawa na maisha mazuri mno, na mke wake ule urembo ukang'ara zaidi , alikuwa ni zaidi ya mrembo yule mwanamke..walifungua miradi mingi na kujenga nyumba nyingi huko Arusha na wakawa wanakuja kijijini kusalimia mara kwa mara,..miaka ikaenda huku utajiri wao unazidi kukua.
Sasa Kuna mwaka kukawa na harusi ya ndugu yao inafanyika pale kijijini..bado niko S/M mpaka kipindi hicho..maandalizi yakaandaliwa na Joseph alitegemewa kama mgeni mahsusi na marafiki zake atakaokuja nao..basi bhana siku ya mkesha ilipofika kwa yale madisko ya kijijini kwa mnaoyafahamu tulicheza balaaa kunakucha unajikuta una vumbi kuanzia kwenye ukucha mpaka kwenye kope za uso.
Joseph na rafiki zake waliingia usiku huo wa mkesha..tulikula nyama za kutosha ile harusi, kesho yake ikawa ni siku ya kuzawadia, Joseph huohuo usiku akaanza kugawa pesa Kama kawaida yake.
Baada ya Joseph kuzawadia akaaga kuondoka pamoja na marafiki zake na walifanya kufuru ya kutisha kwenye kutoa zawadi kabla hajaondoka akaenda kumuaga mke wa baba yake mkubwa yule mchawi na akampa 50k.
Bwana eeeh Kumbe yule mama alikuwa anaona nongwa huyu Joseph kufanikiwa, alichokifanya akachukua zile 50k akazilowanisha then akazisaga zikawa ungaunga kabla ya kuzichanganya na madawa anayojua yeye ili kuuyeyusha utajiri wa Joseph..huku mbele utafahamu ni namna gani hii Siri ya huyu mchawi ilivuja.
Safari ya huyu Joseph na rafiki zake kurudi Arusha ikawa ya misukosuko sana walipotea sana huko njiani iliwachukua siku saba kufika Merelani na alipofika mambo yake yakaanza kuwa mabaya mno.
Baada ya ugumu wa miezi kadhaa akaanza kuuza kitu kimoja baada ya kingine, nyumba zote zikauzwa, gari na miradi yote ikafirisika akawa anaomba hata 500 na wanawake aliowajengea wakawa hawataki tena hata kumuona, mke wake pia akamkimbia..Joseph akarudi kwenye umaskini wa kutupwa..
Kwa mujibu wa wazee pale kijijini, Wanasema huyu Joseph Utajiri wake ulikuwa wa masharti nafuu kulingana na nyota yake na masharti yake ilikuwa ni kugawa pesa na mengine madogomadogo na Kama Ingekuwa sio huyu mama yake mkubwa kumuonea wivu na kumroga basi jamaa angekuwa mbali.
NITARUDI BAADAE
Nalazimika kuishia hapa kwa mda huu kutokana na hiki kisimu changu Cha tecno kupata Moto na kujitype maneno yasiyo na ridhaa yangu hivyo natumia mda mwingi kufuta badala ya kuandika.
Kumbuka Sarah na Gedo ndio wahusika wakuu wa huu mkasa ninaotaka kuueleza ambao ni halisi kabisa wa Utajiri wa ndagu nimeanza kumuelezea Joseph kwa sababu huko mbeleni pia atajitokeza.
Kijana, tafuta pesa kwa halali usijaribu huu Utajiri...kwa wale waliotoka kijijini kwangu huu mkasa wanaoujua vizuri sana pale utakapoisha kuulezea.
INAENDELEA:
Gado nae hakukaa mda pale kijijini akaenda Merelani kutafuta maisha pia .. Sasa pale kijijini Kuna mmama mmoja maarufu anaitwa Wasosi ni jina lake halisi, huyu mama alikuwa mcheshi sana kiasi kwamba vijana wengi waliotaka kuoa hasahasa waliokuwa nje ya pale kiutafutaji walimuomba awatafutie mke mwenye tabia nzuri ili waoe..yaani ilikuwa yeye anatafuta Mali inapelekwa halafu mwanamke anaenda kwa mume wake huko mikoani ili kupunguza gharama na wengi wao wanakuwa hata hawajuani.
Sasa huyu Wasosi alikuwa na kaka zake mkubwa nimemsahau jina lakini mwingine namjua kwa jina moja Kiringo ambaye ni mkuu wa Auxiliary police hapo Udsm...huyu ni mtu wa dini, mcha mungu hasaaa na mpenda haki na kwa mara ya kwanza nimeonana nae mwaka huu msibani hapa Dar.
Kaka yake mkubwa huyu Wasosi akatangaza nia ya kuoa, Dada mtu huyu Wasosi akamuambia kaka huku kijijini Kuna msichana mrembo sana na mpole mno anakufaa kuoa..kaka mtu akataka atumiwe picha ili ajiridhishe akatumiwa ... kweli Sarah alikuwa mzuri kaka mtu akajikuta amempenda akaruhusu wasosi apeleke ujumbe kwao Sarah na alipopeleka akakubaliwa taratibu za kaka kuja pale kijijini kuonana za sarah na familia yake zikafanyika na hatimae harusi ikafika wakaoana wakawa mke na mume.
Wakahamia Dar kimakazi, baada ya mda Gedo akarudi pale kijijini kusalimia vile na Mimi ndio nikawa namalizia Elimu yangu ya msingi..Kumbe jamaa alikuwa ameanza harakati za kuutafuta Utajiri wa giza.
Niko nyuma ya keyboard wakuu na pombe ishapanda kichwani inaendelea
NIMEENDELEA: POST #41
Imeendelea😛OST #66
Imeendelea: POST #78
Imeendelea: POST #85
Mi naona yupo sawa tu. Kwa unachosema inamaana story haitakuwa na contents.Story yako ni nzuri ila umeijaza vitu vingi ambavyo vingine ni unnecessary, mpaka story inakuwa ndefu na inaboa.
Unapoandika story humu usiandike kama unaandika kitabu, andika kama unaandika makala. Unahusisha vitu vya mhimu tu, mbwembwe za kujazia nyama piga chini.
Sijui nikala nyama, nikacheza disko nikapata vumbi, sijui akitembea haachi alama za unyayo ni unnecessary.
Mbona anaandika vizuri tu, kwani humuelewi?Siyo lazima sote tuandike jmn,wengine tubaki kuw wasomaji tuuu,umeandika kama mtoto wa la pili
Sent from my SM-N920F using JamiiForums mobile app
La WhatsAppGroup la nini mzee