Mkasa wa kweli: Tulizichapa na member wa JF Tabata Shule

Mkasa wa kweli: Tulizichapa na member wa JF Tabata Shule

Mkuu kupigana mpka kuwe na motive halafu si muda wote ntashinda pengine unaweza kunidunda
Mm sio mgomvi mara ya mwisho kugombana ni miaka 20 iliyo pita nikiwa A_Level
Kwenye mpira jamaa alikua ananipiga rafu namwambia ananiomba msamaha nikipata mpira ananipiga kiatu alaf ananiomba msamaha aisee nikachoka NDIO nikageuka MikevTyson 😃😃😊😊😊🤓🤓🤓
 
Mm sio mgomvi mara ya mwisho kugombana ni miaka 20 iliyo pita nikiwa A_Level
Kwenye mpira jamaa alikua ananipiga rafu namwambia ananiomba msamaha nikipata mpira ananipiga kiatu alaf ananiomba msamaha aisee nikachoka NDIO nikageuka MikevTyson [emoji2][emoji2][emoji4][emoji4][emoji4][emoji851][emoji851][emoji851]

sasa huyu medicin alizidi.

hata kama ingekuwa wewe ungetaka kupigana
 
haina noma.

Ila atakayepigwa anaruhusiwa kukimbia ila naruhusiwa nibebe nyundo yangu wewe huruhusiwi
Ile nyundo kama ndio amekupa babu yako kujeruhi watu basi safari hii kwenye rematch kutakuwa na mashuhuda na nitawaambia wakukague kama unayo waichukue halafu tuone utaringia nini.
 
Jambo Jambo?

Hiki ni kisa cha kweli na kama mods wataniruhusu nitaweka PM screenshot za mimi na Jamaa jinsi tulivyochapana.

Jamaa anajiita “Medecin“ humu sijui alitokea wap ila nakumbuka alikuwa ananiqoute kwa matusi kweny nyuzi fulani na mimi bila hiyana nikawa namjibu mpka jamaa akahamia PM kwa matusi kedekede mpka tukapanga kuonana ili tuzichape na tukawekeana masharti ya kutokuenda na mtu pale tunapokutana.

Jamaa kweli alipanga location maeneo ya Tabata shule uwanjani na mida ya kukutana ilikuwa ni saa 12 jioni na tuzichape baada ya watu wa mazoezi n mpira kumaliza ratiba zao.

Ila kwa machale nilisogea pale saa 10 masaa mawili kabla ya kukutana ili nihakikishe kama hajabeba watu wengine na kunidhuru.

Kweli Jamaa mida ya saa 12:06 alisogea na kigari chake aina ya IST pearl white na nilimjua maana kila mtu alimwambia mwenzake atavaa vipi au ana usafiri gani ili iwe urahisi kwa kutambuana,Sasa yule Jamaa sijui Alijua pengine atakutana na mtu mwenye kitambi na miwani na boyaboya i don know ila ni kama alipigwa na butwaa baada ya kuniona na aliniona kirahisi maana nilisimama katikati ya uwanja namuangalia upande wa lami anakotokea.

Alivyofika akauliza wewe ndo nshomile nikamjibu ndio na haraka nikamwambia Hapa tunazichapa na atakayezidiwa anakimbia na hakuna kumkimbiza wala kufuatana wala polisi wala nini. Akajibu Poa.

Jamaa alikuwa kavaa traki nyeusi na jezi ya Arseno juu mimi nilikuwa nimevaa kadeti na shati la draft tu.

Kwa haraka haraka Tulianza kuzichapa hapohapo nilimtamdika ngumi 6 zikapenya 4 na 2 aliziblock huku yeye akirusha ngumi 3 na ikapenya moja.Jamaa akaanza kuhema sana kurusha ngumi 3 tu, nilimtime nikampa Upper cut 1 ambayo ilimpeleka chini na nikamsubiri ainuke na alipoinuka nili “swing”na Left Jab ya nguvu iliyompeleka chini mara ya 2 na kuanza kuvuja damu puani.

Mlinzi wa Shule ya Mtambani (jirani na tabat shule) alitoka anapiga mayowe kututaka tutoke hapo lasivyo atatuiitia wezi, wakati nahangaika kumjibu yule mlinzi jamaa akaanza kukimbia kuelekea lami kwenye gari lake alilopaki, nikijua anakimbia mazima kumbe kaenda kuchukua Sime kwenye gari na akaanza kuja kuelekea upande wangu kunikata, nilihamaki lakini nikajituliza ili nimzime nalo lasivyo anaweza kunidhuru.

nilimpokonya sime na mbinu ya Sei-Wong mi kwa umaridhawa naikalichukua sime bila yeye kujua namna nilivyolipora halafu nikamzima na Left swing back kick iliyompeleka chini na safar hii hakuinuka na alianza kulia kilio kikubwa akiomba msaada kwa watu.

Walinzi wakaitana wakaanza kuja upande wetu, nikaona jau hii nikachora mpka road na kudaka boda mpka njia panda chang'ombe.

Toka hapo [mention]Medecin [/mention] hajibu PM zangu, kama yumo akome na siku nyingine akirudia niko free kumkanda tena.

* Usiache kupiga pusha ups walau 100 na squats 50 kwa siku kwa mwanaume, siyo unakulakula na kuwa na likitambi la hovyo.

TUJIFUNZE KUHESHIMU WATU, KAMA HUWEZI UGOMVI TULIZANA.

AVOID EXPECTATIONS TO AVOID DISSAPOINTMENTS.

Nshomile,
kwa sasa Dar es Salaam.
Yaani Mimi sikubali mwana JF mwenzangu akandwe, lazima nimtetee.

naomba kuingilia kati huu ugomvi nimsaidie bwana medecin....

tukutane wapi tuzichape mkuu, najua huniwezi hata kwa dawa. 😄🤠🤠
 
Yaani Mimi sikubali mwana JF mwenzangu akandwe, lazima nimtetee.

naomba kuingilia kati huu ugomvi nimsaidie bwana medecin....

tukutane wapi tuzichape mkuu, najua huniwezi hata kwa dawa. [emoji1][emoji1783][emoji1783]
Mkuu asante kwa kunisaidia ila usikubali kupigana nae akiwa na hiyo nyundo.
 
Nshomile wa Muleba siku ile uliniotea mbwa wewe nilikuwa nimetoka bar nilishtua kidogo, nataka rematch nilipe kisasi. Halafu hukunipiga ngumi bali ulitumia nyundo na niliiona ndio maana nikakimbia. Kabla ya kuonana tulipanga tukikutana tutapigana ngumi sasa nyundo ilikuwa ya kazi gani.
Ilikuwa ni nyundo kweli mkuu? Au ngumi nzito? 😅😅
 
Hahahahaa! Kwa hiyo na wewe ukakimbilia sime [emoji1787][emoji1787][emoji1787] ilikua hatari siku hiyo na ungekufa kwa ajili ya ujinga na ubishi wa kipuuzi [emoji1787][emoji1787][emoji1787] dah! Umekandwa hadi michozi mwanangu [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Lile sime lilikuwa chini ya seat ya gari yangu, wakati naondoka baada ya kunipiga nyundo akawa ananifuata yeye na wenzie wanne wameshika fimbo, nyuma yao sijui alimkodi yule babu mlinzi kazi yake ikawa kupiga yowe tu ooh wanauwana! wanauwana! Walipokaribia nilipo kwenye gari ndio nikachomoa sime kuwatisha na kweli wakaogopa wakasimama, mimi huyo nikazama kwenye gari nikaondoka.
 
Ni nyundo kaka we muuize huyo mtu kama alikuja na nyundoau hakuja nayo. Halafu alishawapanga watu wake ili akizidiwa waje kumsaidia.

Sikuwa na nyundo wewe.

Ulileta zarau sana wewe PM.

Kama unabisha turudie pambano na naomba wakina [mention]Analyse [/mention] wawepo kama mashahidi ili waone kama nina nyundo au ngumi.
 
Back
Top Bottom