Mkasa wa kweli: Tulizichapa na member wa JF Tabata Shule

Mkasa wa kweli: Tulizichapa na member wa JF Tabata Shule

Sijui niwaite wajinga au wapumbavu yaani midume mizima eti inapanga ikutane ikapigane, kwanza mpaka mtukanane pm wanaume ndo nini wapuuzu wakubwa kama ni kweli natamani mmoja angekufa kabisa ili mtu akikaa jela ajutie muda wake wa kwenda kwenye upuuzi aseme laiti ningejua.
 
Nshomile wa Muleba siku ile uliniotea mbwa wewe nilikuwa nimetoka bar nilishtua kidogo, nataka rematch nilipe kisasi. Halafu hukunipiga ngumi bali ulitumia nyundo na niliiona ndio maana nikakimbia. Kabla ya kuonana tulipanga tukikutana tutapigana ngumi sasa nyundo ilikuwa ya kazi gani.
Jambo Jambo?

Hiki ni kisa cha kweli na kama mods wataniruhusu nitaweka PM screenshot za mimi na Jamaa jinsi tulivyochapana.

Jamaa anajiita “Medecin“ humu sijui alitokea wap ila nakumbuka alikuwa ananiqoute kwa matusi kweny nyuzi fulani na mimi bila hiyana nikawa namjibu mpka jamaa akahamia PM kwa matusi kedekede mpka tukapanga kuonana ili tuzichape na tukawekeana masharti ya kutokuenda na mtu pale tunapokutana.

Jamaa kweli alipanga location maeneo ya Tabata shule uwanjani na mida ya kukutana ilikuwa ni saa 12 jioni na tuzichape baada ya watu wa mazoezi n mpira kumaliza ratiba zao.

Ila kwa machale nilisogea pale saa 10 masaa mawili kabla ya kukutana ili nihakikishe kama hajabeba watu wengine na kunidhuru.

Kweli Jamaa mida ya saa 12:06 alisogea na kigari chake aina ya IST pearl white na nilimjua maana kila mtu alimwambia mwenzake atavaa vipi au ana usafiri gani ili iwe urahisi kwa kutambuana,Sasa yule Jamaa sijui Alijua pengine atakutana na mtu mwenye kitambi na miwani na boyaboya i don know ila ni kama alipigwa na butwaa baada ya kuniona na aliniona kirahisi maana nilisimama katikati ya uwanja namuangalia upande wa lami anakotokea.

Alivyofika akauliza wewe ndo nshomile nikamjibu ndio na haraka nikamwambia Hapa tunazichapa na atakayezidiwa anakimbia na hakuna kumkimbiza wala kufuatana wala polisi wala nini. Akajibu Poa.

Jamaa alikuwa kavaa traki nyeusi na jezi ya Arseno juu mimi nilikuwa nimevaa kadeti na shati la draft tu.

Kwa haraka haraka Tulianza kuzichapa hapohapo nilimtamdika ngumi 6 zikapenya 4 na 2 aliziblock huku yeye akirusha ngumi 3 na ikapenya moja.Jamaa akaanza kuhema sana kurusha ngumi 3 tu, nilimtime nikampa Upper cut 1 ambayo ilimpeleka chini na nikamsubiri ainuke na alipoinuka nili “swing”na Left Jab ya nguvu iliyompeleka chini mara ya 2 na kuanza kuvuja damu puani.

Mlinzi wa Shule ya Mtambani (jirani na tabat shule) alitoka anapiga mayowe kututaka tutoke hapo lasivyo atatuiitia wezi, wakati nahangaika kumjibu yule mlinzi jamaa akaanza kukimbia kuelekea lami kwenye gari lake alilopaki, nikijua anakimbia mazima kumbe kaenda kuchukua Sime kwenye gari na akaanza kuja kuelekea upande wangu kunikata, nilihamaki lakini nikajituliza ili nimzime nalo lasivyo anaweza kunidhuru.

nilimpokonya sime na mbinu ya Sei-Wong mi kwa umaridhawa naikalichukua sime bila yeye kujua namna nilivyolipora halafu nikamzima na Left swing back kick iliyompeleka chini na safar hii hakuinuka na alianza kulia kilio kikubwa akiomba msaada kwa watu.

Walinzi wakaitana wakaanza kuja upande wetu, nikaona jau hii nikachora mpka road na kudaka boda mpka njia panda chang'ombe.

Toka hapo [mention]Medecin [/mention] hajibu PM zangu, kama yumo akome na siku nyingine akirudia niko free kumkanda tena.

* Usiache kupiga pusha ups walau 100 na squats 50 kwa siku kwa mwanaume, siyo unakulakula na kuwa na likitambi la hovyo.

TUJIFUNZE KUHESHIMU WATU, KAMA HUWEZI UGOMVI TULIZANA.

AVOID EXPECTATIONS TO AVOID DISSAPOINTMENTS.

Nshomile,
kwa sasa Dar es Salaam.
Sijui, lakini hii miandiko miwili yote inafanana.

Ukizingatia jambo lililofanyika, ukalipima kwenye utimamu wa akili ya binadamu, unagundua ni fiction, na miandiko kufanana ndo unapigia kabisa mstari kua ni fiction.

Sio mbaya, amedramatize
 
Ukisoma between lines, hawa hawakupigana kwa sababu hizi ID mbili ni za mtu mmoja. Ni kwa macho ya kijasusi tu utagundua hili.
Wasioijua tabata shule watakuamin ...lakin hyo shule imepakana na kituo Cha polisi kiasi kwamba mda wote polisi wapo hapo uwanjani ni ngumu kutokea ugomvi eneo Hilo haswa kwa mda uliosema ..acha kudanganya watu
Nilidhani nimegundua pekeangu
 
Mkuu naomba uwe promoter wa hii rematch, nataka kumuonesha mimi ni nani, sina kitambi kama anavyojinadi ila alikuja na nyundo akanipiga nayo mara nne kichwani na mbili nilizipunch zikatua mkononi, hala nilipo nauguza majeraha nikipona nataka marudio na wewe uwe shuhuda na ikiwezekana ulete mrejesho jukwaani.
Duh mpaka anabeba nyundo alitaka kukua au?? Hahaha nyie mnavutuko na wewe Iko sime vip
 
Duh mpaka anabeba nyundo alitaka kukua au?? Hahaha nyie mnavutuko na wewe Iko sime vip
Mimi sime hili ni kwa ajili ya kujihami, huwa linakaa chini ya seat ya ist yangu, ila yeye alikuja na nyundo ili akizidiwa anipige nayo ma kweli mwanzo nimtight kwelikweli ndio akanipiga nayo.
 
Ila wewe jamaa inaonekana mkorofi sana, Yani kweli unaweza panga mkutane kwa ajili ya kupigana tu pasipo chanzo chochote, Unfortunately mimi sina hulka ya ugomvi hata sikumbuki kama nilishagombana na mtu hadi kufikia hatua ya kupigana...
Hizi scenerio zimetokea several times hapa JF
Cc. NALIA NGWENA na yeye amewai kupanga occasion kuzichapa na mdau wa humu JF

😊😃🤓🤓
 
Sijui niwaite wajinga au wapumbavu yaani midume mizima eti inapanga ikutane ikapigane, kwanza mpaka mtukanane pm wanaume ndo nini wapuuzu wakubwa kama ni kweli natamani mmoja angekufa kabisa ili mtu akikaa jela ajutie muda wake wa kwenda kwenye upuuzi aseme laiti ningejua.

Hata wewe natakiwa nkukande vilivyo mpka mdomo huo uingie ndani.

Dume zima unajiita norah
 
Can not be
Angalia pattern yakupokezana..

Kinachoshangaza, ID moja kongwe miaka 12. Swali ni, huyu mtu alijiunga akiwa mdogo sanaa..[emoji848] kiasi kwamba bado hajamature mpaka leo au ndo wajinga nao huzeeka..[emoji848]

Watu kama nyie ndo huwa nawakanda vilivyo.

Toa komenti inatosha ila kwanini udhihaki?

Wewe ni mpumbavu sana we jamaa.
 
Huna maisha bro usingepata muda wa kuchezea [emoji23] eti Gily tuache kuwaza pesa tukapigane kweli,halafu mie sio dume mie jike tena lilokamilika.

unaweza kuta hapo ulipo umekaa kwa dada ako aliyeolewa unatype mikono juu unasubiri dada ako ajunjwe ili na mume wa dada ako aiombe aito.mbe na yako
 
Back
Top Bottom