Part Five A: In every life we have some trouble.
1993-1994
Baada ya mtihani wa kidato cha nne, nilirudi kwa mama Arusha. Nilikuta biashara zake zimechanganya hivyo basi akawa bize sana. Pia alikuwa ameshafanya maendeleo pale nyumbani pameboreka sana.
Siku zote nikiwa na mama alikuwa anapenda kunipa usia sana kuhusu maisha, kuheshimu watu wote, kusamehe, kutoa msaada pale ninapoweza , kushiriki vitu na wengine na kikubwa zaidi kumuomba Mungu.
Nilimpenda sana maana na yeye alinipenda sana kuliko watoto wake wote.
Pamoja na upendo alinifundisha kupika nikiwa mdogo sana, tena tunafanyiana zamu ya kupika na kuosha vyombo bila kujali huyu ni mama.
β¦β¦..
Nikawa niko mtaani tu nikisikilizia matokeo. Mzee alikuwa anamiliki nyumba za wapangaji mimi nikawa ndio bosi wao wa kufatilia kodi. Maisha nyumbani yalikuwa safi kiaina sio ile saana, ila pesa ya kutesea mtaani ilikuwa haikauki.
Nilikuwa na tabia ya kufanya jogging asubuhi saa 11 kila siku, natoka hapo nyumbani sakina mpaka pale chuo cha habari maalum.
Kama kawaida yangu sikuwa na marafiki wengi walikuwa wa nne tu na kati ya hao mmoja ndie nilikuwa nae karibu sana anaitwa Frank.
Jogging nilikuwa nafanya na huyu Frank wengine walikuwa wavivu nilikuwa nakutana na Frank pale sakina super market tunaliunga mdogo mdogo mpaka ngara mashamba ya serikali karibu na Habari maalum.
Siku moja nimetoka zangu home saa 11:00 nashuka mdogo mdogo, kuna semehu kulikua na shamba kubwa la migomba, huwa kuna giza sana hapo.
Nilipokaribia hilo eneo nikaona gari nyeusi imesimamishwa kwenye shamba la migomba.
Kipindi hicho Arusha ujambazi uko juu sana, sikuwa na hofu maana mida hiyo kuna watu wanaokwenda kufata nyama pale Arusha meat wanakuwa njiani.
Nika punguza mwendo ili nijue lile gari ni la nani na kwa nini liko migombani kama limefichwa, (ni shamba letu) lile shamba la migomba linapakana na nyumba za wapangaji wetu.
Sikufanikiwa kulikaribia gari maana nilihisi kama limeibiwa naweza pata matatizo na vyombo vya dola, au labda kuna mpuuzi kajificha pale ili kufanya ngono kwenye gari.
Ilikuwa kawaida sana kukuta mtu amepaki gari anafanya ngono maana njia yenyewe haikuwa busy sana na migomba ilikuwa mingi kwenye hilo eneo. Ikanibidi niendelee na safari zangu.
Nilikutana na Frank sakina supermarket, ilikuwa meeting point yetu. Tukaunga mpaka kwa idd akasema hajisikii vizuri ikabidi turudie hapo. Ikabidi nimwambie twende nyumbani maana ni karibu sana kuliko kwao.
Frank alikuwa anaishi jirani na 'Arusha Technical college' kama unaelekea mianzini. Wakati napandisha nikiwa na Frank tukalikuta lile gari pale pale, nikamwambia kuwa imekuwa pale toka nashuka.
Tukashauliana tusisogee maana tulihisi tu limeibiwa hatukutaka kujitafutia matatizo. Tukaenda nyumbani.
Ilikuwa 12:30 wakati tunarudi, kulikuwa kume pambazuka, Frank alioga akanywa paracetamol akalala.
Mimi nikatoka ili nikaangalie kama lile gari bado lipo, nikalikuta liko pale pale.kutokana na utundu niliotoka nao Songea boys ukiongeza mazoezi nikawa najiamini sana.
'kama pawa mabula au pawa suzuki vile,' .
Kutokana na tabia ya kufanya mazoezi nikapata ujasiri nikalisogelea maana tayari kulikuwa kume pambazuka na watu wako njiani wengi tu.
Nilipokaribia nikachungulia mbele nikaona mtu amekaa ananiangalia ila amefungwa kitambaa mdomoni. Alipo niona akawa anatikisa kichwa tu mwili umekaza nilitulia pale huku najiuliza nifanyeje.
Nikapata ujasiri wa kusogea karibu, nikamuona vizuri alikuwa ni mzungu ila amekuwa mwekundu kutokana na kamba alizofungwa. Akanipa ishara nikafungua mlango wa mbele, nilimkuta amefungwa kwenye siti ya dereva, miguu imefungwa kamba, amekalishwa kwenye siti na mikono imefungwa nyuma ya siti. Kamba zilipita karibu na mabega hivyo alishindwa hata kujitikisa kwa jinsi manila zilovyokuwa zimebana.
Usoni alifungwa kitambaa ili asipige kelele. Mpaka wakati huo akili ilisimama nisijue la kufanya, ghafla nikapata ujasiri wa kumfungua kitambaa cha mdomoni ndio akaanza kuongea ila kinyonge sana.
Baada ya kumfungua kamba zote, na yeye akajaribu kushuka kwenye gari ila akashindwa kusimama akajimwaga chini. Nilimsaidia kumkalisha akaegemea gari, akawa ananiambia
"Help my wife and my daughter pls. "
"Frankly, I was curious about what was happening there."
Today is Friday, Next later today