Sitaki kuamini hili lakini uvumi huu umeeneea
sana kiasi cha kwamba umenifanya niwe na shauku kutaka kujua yaliyojiri kwenye kusign hiyo memorandum
maana naona kwa taarifa nilizokuwa nazo
malalamishi ni kuwa serikali imeipa CCT na TEC nguvu kubwa ajabu na matokeo yake leo watu watu wanaanza kulalama kwa nini serikali haiipi nguvu hizo NGO zingine kama walivopewa na serikali.
Na under this memorandum seriali inatoa nafasi za kazi kwa Church candidates kwenye chuo chake cha Teachers Training College
Hakuna ubaya hata kidogo kwa serikali kusign hii memorandum
lakini nataka kujiuliza je ni sawa serikali kufanya agreements kama hizi na taasisi za kidnini?
na Je imefanya gareement kama hii na taasisi za Kisslam au wahindu au ni Kanisa tu ndio walifanya nao?
Je hamuoni hapo mambo ya bilateral negotiations wakaachiwa wataalam wa mambo hayo?
a)Huyu jamaa kaleta mikataba ya kanisa na serikali =Upendeleo dahiri ulaaniwe!
b) kama kuna mtu ameona kuna mkataba kati ya serikali na Wailamu aulete ndio tujadili
lakini kwa sasa evidence iliyopo ni kwamba "serikali inapendele wakrsto" kwa kuweka mkataba wa siri,
Wachangiaji wakristo wanaona raha kanisa kunyonya walipa kodi==Huo unaitwa "Unafiki"
GT,
Mkuu ndio hapo naposema kila siku watu wanakataa OIC bila kujua wala kufikiria kwa sababu tu kuna jina la Uislaam lakini ni serikali hiyo hiyo imeweka mikataba kibao na Taasisi za Kikristu kwa kutumia jina la Vatican ambayo ni Taasisi ya kidini vile vile.
Fundi Mchundo,
Mkuu unakataa hili kwa sababu kiingereza kilichotumika ni kibovu au?..Hivi katika akili yako unafikiri watu hawafdahamu mikataba ambayo serikali imekwisha ingia na taasisi za kidini?..Au kwa sababu hazitangazwi isipokuwa inapofikia za Kiislaam basi kila mtu hupiga kelele hata mwenye kulala huamka..Mkuu hatusemi tuu na mjue kwamba Waislaam ni watulivu sana kiasi kwamba ingekuwa maswala mengi yametokea upande wa pili sidhani kama nchi ingekalika..
Fundi.. swali jingine ambalo liko wazi kabisa ni juu ya uanzishwaji wa Chuo Kikuu cha Waislamu kutoka katika majengo yaliyokuwa Chuo cha Tanesco (cha serikali).
"The University shall be used solely and exclusively for the education of the Muslim community" tutaanza kujadili kipengele hicho kwa jazba zote!
Ok.. tutaujadili at face value.
Hii MoU ilisainiwa lini, na nani, na wapi? tuweze kujua msingi wake.
taarifa gani hizo?
kwa hiyo hii CCT na TEC walisaini hiyo MoU pamoja?
Hiki Chuo cha serikali cha Teachers Training College kiko mkoa gani?
Kama hakuna ubaya, hakuna malalamishi! Kuna malalamishi hivyo kuna ubaya.
that is a huge leap! tuestablish kwanza without a doubt that there is such an agreement. Kwa sababu jambo kama hilo ni kinyume na Katiba, period.
Unazungumza kana kwamba this is an established fact. Kama kuna mkataba wa aina hiyo kati ya serikali na Kanisa lolote inabidi kesi ya Kikatiba ifunguliwe kwani ina vunja "non-discrimination clause" ya Katiba yetu, haijalishi ina lengo zuri kiasi gani. Na kwa vile kuna wasomi wengi tu wa Kiislamu na maprofesa wa sheria nina uhakika taasisi za Kiislamu na za dini nyingine zinaweza kufungua kesi ya Kikatiba kwanini serikali iingie mkataba wa aina hiyo.
Kwani tumeambiwa waliosaini au watakaosaini hizo "bilateral negotiations" siyo wataalamu wa mambo hayo? Hiyo inference umeipata wapi kwenye huo "mkataba"?
Kama hamtuwekei full MoU, mjadara ufungwe maana inawezekana tunajadiri kitu kisichokuwepo. Isije kuwa ni janja ya watu kututoa katika mijadara mizito ya Cheyo na Spika, Selelii na Spika, Zitto na Spika nk.
Kwa ufahamu wangu sirikali ya Tanzania haina dini, kwa hivyo suala la kusaini MOU with any religion is incorrect. Kama ikiwezekana waweke kinaga ubaga kwamba dini zote zitapata misaada based on the MOU signed with Muslims or Chrisitians - this is my thought
Interesting...mbona yapo mengine mengi tuu ambayo ni kinyume na katiba?
mfano Anti terrorism Act ya 2002 ni Kinyume na katiba au kama huna then waweza soma "Bill supplement No.11" ambayo pia ilinakiliwa na Gazette of the United Republic of Tanzania.2002. 83.40 pp1-39
Mkuu achana naye huyo,hana lolote.Ni udini tu ndo unamsumbuaNi kinyume na Katiba vipi?
Kwani huu mjadala unaoendelea haujaonyesha kuwa hata hili limekuwa nongwa?...ngekuwa waislamu wamefanya hivi ingekuwa NONGWA.
makubwa tena haya. Ingekuwa waislamu wamefanya hivi ingekuwa NONGWA.
Kwani Waislam kuanza kutoa taaluma kuhusu uchaguzi kila mtu anapiga kelele japo malengo ake ni sawa na a kanisa
Kutoa elimu ya uraia na uchaguzi dini zote zinaruhusiwa,ila kinacho gomba ni pale taasisi ya kidini inapotumika kumpigia kampeni mtu wa dini isiyo yao. hapa wakristo hawajasema asichaguliwe muislama au pagani, bali uzuri au faida za kumchagua kiongozi aliye bora awe muislamu/pagana au mkristo etc awe wa ccm au wa vyama vingine, sasa hofu ni ya nini? au huyu aliyepo hafai hivyo wafuasi wake wanahisi anafuatwa kwa kuwa ni Mkristo/muislamu? kama aliyepo ni kiongozi bora basi wafuasi wake au mashabiki wake hawana haja ya kuwashwa washwa maana atapita tu kwa sifa zake, lakini kama si hivyo tutayaona ya Mabuto ambaye hakuwa muislamu bali hakuwa kiongozi Bora.makubwa tena haya. Ingekuwa waislamu wamefanya hivi ingekuwa NONGWA.
Kwani Waislam kuanza kutoa taaluma kuhusu uchaguzi kila mtu anapiga kelele japo malengo ake ni sawa na a kanisa
The fact kwamba mmekasirika na kutetea mkataba kwa nguvu zote inaonyesha jinsi mlivyo.....biased (one sided thinkers)Mkandara. Huu unaoitwa mkataba ni forgery. Hii haihusiani na kuwepo au kutokuwepo kwa makabuliano kya kushirikiana kati ya serikali katika nyanja mbalimbali. Mbona serikali ina shirikiana na Bakwata (institution ya waislamu), na Hindu Mandal (hospitali ya wahindu), Aga Khan ( taasisi ya kiislamu ), Chuo Kikuu cha Tumaini ( taasisi ya wamisheni), hospitali ya KCMC (taasisi ya wamisheni) n.k.? Ninachopinga ni kutuwekea kitu ambacho ni blatantly forgery kwa nia ya uchonganishi. Tukiangalia tena mada iliyo mbele yetu:
1) mwandishi anadai katika hiyo MoU kuna makubaliano ya kupewa upendeleo wa AJIRA kwa wakristu katika vyuo vya walimu vya serikali! CCT na TEC wataanzaje kuwaombea nafasi za KAZI (sio elimu) kwa watu wao (ambao ni sehemu kubwa ya wamisheni wote ) katika taasisi za serikali yao! Hao ambao mwandishi anadai ni watu wa CCT na TEC si raia wa nchi hii na wana kila haki ya kupata ajira huko? Au mwandishi anataka kutuambia kuwa CCT na TEC wameona kuna vizuizi kwa wamisheni kuajiriwa hadi waombe upendeleo maalum? Hivi kweli kuna upungufu wa wamisheni katika vyuo vya ualimu nchini?
2) CCT haina watu wake. Hiki ni chombo kinachounganisha baadhi ya madhehebu ya wamisheni. Hayo madhehebu ndiyo yana watu (tukichukulia kuwa hii ina maana ya wafuasi wake). Kwa hali hiyo upendeleo huo utakuwa vigumu kuutekeleza maana kila dhehebu litataka watu wake ndio wapate upendeleo! Au mwandishi anataka kutuambia kuwa upendeleo huo wa ajira utakuwa kwa wafanyakazi wa CCT? Hauoni ni upuuzi kwa CCT waombe ajira kwa waajiriwa wao! Ili iwaje?
3) Tunaposema serikali katika upuuzi huu tuna maanisha nani? Mnataka kutuambia Rais wa nchi ndiye amesaini mkataba huu? Au Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha? Au waziri wa Fedha? Au Hawa Ghasia? Nani basi ndiye ataiwakilisha serikali katika utekelezaji wa MoU?
Aliyeuweka huu unaodaiwa kuwa ni MoU ni Agent Provocateur. Na wengine wenu kwa vile kila wakati wanapenda kuona kuwa wameonewa wameingia mkenge! Mbaya zaidi hamkawii ( hasa wewe Mkandara) kuja na lugha ya vitisho. Kwani ni waislamu peke yao walioonewa na serikali yetu? Mbona wamisheni na wahindu hawakulalamika wakati rasilmali zao zilipopokonywa na serikali? Si walijua nia na makusudi ilikuwa kutoa nafasi kwa raia wote wa nchi hii kufaidika na rasilmali hizo. Ndivyo inavyotakiwa.
Kama nilivyosema awali. Tuoneeni huruma raia wa nchi yetu.
Amandla........