Memorandum ilifanywa kwa siri mpaka ilipo fichuliwa na wanaharakati wa kiislam ,serikali walikua wakikanusha kuwepo kwake mpaka ushahidi ulipotolewa.
Hakika katika nchi yenye madhehebu ya dini tofauti ambayo yamekumekuwa yakisababisha misuguano ya hapa na pale basi kufanya makubaliano au mikataba kama hii inaweza kuleta matatizo makubwa ya kutoaminiana basina ya serikali na waumini wa kislam na wakristo.ukweli hili lilikua ni kosa
Waislam wanaiona serikali yao imefanya upendeleo wa wazi kwa madhehebu ya kikristo,
NINI CHA KUFANYA
serikali makini yenye kufata katiba na kulinda misingi ya umoja walio jiwekea inatakiwa ifanye mambo yake bila ya upendeleo na "all inclusive" isiokua na upendeleo na viongozi wake wasiendeshe shughuli za serikali kwa misingi ya dini ,
basi kwa vile serikali inatambua umuhimu wa dini katika kuleta maendeleo ingeandaa kitu kama 'general policy on religious institutions and assistance'
hii ndio ingekuwa white paper kwa ajili ya kuzisaidia taasisi za dini kutoa huduma, mfano kama hii memorandum ingegeuzwa na kufanyiwa marekibisho ikawa sera ya kitaifa kwa dini zote,
na si vibaya serikali kuingiza katika bileteral talk kuomba misaada kwa ajili ya taasisi za dini.
umuhimu ni uwazi na kufanya haya kwa maslahi ya nchi, ikijulikana wazi faida itayopatikana ni kwa ajili ya taifa na sio kwa ajili ya taasisi moja kujifagilia dhidi ya mwenziwe.
leo tukiwa na white paper kama hii tungeona wakati rais labda alipoenda Oman juzi labda bakwata wangefatana na rais na wao wangeondoka na project ambayo serikali inairidhia , naamini ingetusaidia sana ,
ama Rais anapokwenda Germany angeweza kufatana na wachungaji wa kanisa nao pia wangekuja na project zao labda ya kujenga hiospital kule sumbawanga , basi naamini chance ya kupata ni kubwa.
Hivyo hata katika bilateral agreement serikali ingeingiza mipango na project za taasisi za dini .zingesaidia sana kuleta maendeleo katika nchii hii, haya lakini yanataka umakini na Utanzania kwanza.
hivyo ni jambo la kuimbia serikali kwamba ilichofanya sio kibaya lakini ni cha upendelo, hivyo ifute hii memorandum na badala yake itengeneze national policy ama sera kuhusu misaada kwa taasisi za dini
kwa waislam
Na upande wa ngugu zangu waislam , taasisi zetu ukweli zinahitaji kufanyiwa marekebisho makubwa ya kiutendaji.taasisi zetu nyingi zinaendeshwa na wanaharakati , sasa ni wakati wa wasomi wa kiislam kujitokeza na kupewa nafasi za kuongoza taasisi hizi.maulama na masheikh washughulike na mambo ya kiroho na propagation dini.mambo ya maendeleo wapewe wasomi .
Ama baada ya hapo tunaweza kuweka pressure au kuwa na constructive argument ili serikali iweze kubadili hii memorandum na badala yake itengeneze sera ya taifa kuhusu misaada ya taasisi za dini.
bakwata ambao mie binafsi ni mmoja kati ya wanaolipinga sana kutokana na uhafidhina na ubadhirifu wake basi at least wakati huu ambapo waislam wengi wamekosa na imani nalo likubali kubadilika.
Mpaka hapo tutapobadilika hakika kinyume chake tutakuwa tunapiga kelele ambazo hakuna ataetusikiliza