Mpenda.Haki
Member
- Jan 14, 2013
- 59
- 31
Tunachosema hapa ni kuwa MoU ilitengeneza upendeleo maalum kwa wakristo over and above hizo nafasi za watanzania wengine. Issue sio kufaidika waislamu watupu, kwani kwenye hizo shule za kanisa waislamu wanasoma bure.
Huu ufisadi hautofautiani na ufisadi mwingine ambao unapigwa vita. Inabidi ukomeshwe hata mkijitetea vipi.
Ndugu zangu wanaforum kwanza namshukuru Dr. Slaa kwa kutolea ufafanuzi suala la MOU maana limeibua mjadala na manungúniko mkubwa sana ktk makundi mbalimbali ya jamii wengine bila hata kulielewa vema. Mimi binafsi nimeshalieleza sana kwenye facebook mara nyingi sana. Lakini nachokiona kwa wengi pamoja na ufafanuzi wa Dr. Slaa bado wengi hawaelewi. Napenda kuongezea maelezo yafuatayo:-
(1) Watu wanasema hajaeleza juu ya pesa zinazotolewa na serikali kwenda kwenye uendeshaji wa hospitali. Ni kweli Dr. Slaa hajaeleza juu ya masuala ya pesa. Yeye ameeleza tu mazingira yaliyopelekea kuwepo kwa makubaliano yaani MOU kati ya serikali na Makanisa na si taratibu au kanuni zilizowekwa na serikali ili kutekeleza makubaliano hayo.
(2) Ikumbukwe kuwa ni jukumu la serikali kikatiba kutoa huduma za jamii kama afya kwa wananchi wake. Lakini baada ya hali ya kiuchumi kuwa ngumu hasa ktk miaka 80's baada ya vita ya Uganda na Tanzania 1979, serikali ilikosa uwezo wa kutoa huduma za kijamii kwa watu wake waliokuwa wameongezeka na kuzidi idadi ya hospitali na shule zilizokuwepo ikiwa ni pamoja na zile zilizokuwa zimetaifishwa hapo kabla. Ilishindwa kabisa kuendesha hata shule na hospitali walizokuwa wamezitaifisha na pia ikashindwa kujenga nyingine kwa hiyo huduma za elimu na afya zilizidi kuwa duni. Kama njia ya kutatua tatizo la wananchi kukosa huduma za afya serikali ikataka kuendelea kutaifisha hospitali za madhehebu ya dini zilizokuwa zimejengwa tena baada ya utaifishaji wa kwanza ili izitumie kuwahudumia wananchi. Lakini baada ya mvutano mkali na makanisa ilishindwa kuzitaifisha hizo hospitali ikabidi serikali ikubaliane na makanisa iwahudumie wananchi wake kupitia hospitali hizo za makanisa.
(3) Kuhusu Pesa: Kwanza napenda ieleweke kuwa sihospitali zote za makanisa zilizoko kwenye makubaliano ya serikali kuwahudumia wananchi wake kupitia hizo hospitali kwa kuzipatia ruzuku. Zinazopata ruzuku ni zile za wilaya na mikoa yaani Hospitali teule (District Disignated Hospitals DDH) na zile za rufaa kama Bugando, KCMC na nyinginezo kama CCBRT. Ilibidi serikali iwe inatoa ruzuku ya 0%-50% ya gharama za uendeshaji ili gharama za huduma ktk hospitali hizo ziwe nafuu ukilinganisha na hospitali ambazo ni za binafsi kwa 100% huku makanisa yakitoa 50%-100% ya gharama za uendeshaji. Kwa maneno mengine makanisa hutoa pesa zake kugharimia huduma kwa watanzania wote bila kujali dini zao. Na mara nyingi serikali inapochelewa kupeleka hata hizo ruzuku makanisa hutoa gharama zote. Kwa maneno mengine makanisa huikopesha serikali bila hata riba yoyote kwa ajili ya kuwahudumia watanzania wote!
>>Ruzuku hizo za hadi 50% hutolewa kama fedha, madawa, misamaha ya kodi, mishahara, kuendeleza watumishi wa hospitali, vifaa tiba na vifaa vya maabala. Kumbuka gharama za uendeshaji ktk vipengere vyote hivyo nilivyotaja hutolewa kwa ubia yaani 0%-50% serikali na 50%-100% makanisa. Kwa maneno mengine tunaweza kusema uendeshaji wa hospitali hizo nusu ni wa umma na nusu wa binafsi. Makubaliano haya yamewekwa kwa lugha ya kisheria ktk MOU. Taratibu za utekelezaji wake hazipo kwenye makubaliano hayo (MOU) ndo maana watu hawaelewi wanadhani serikali hutoa tu hela na kupeleka makanisani. Bajeti za serikali ziko wazi zinaonyesha ruzuku zinazovyotolew. Na mtu akisoma kwenye MOU kwamba serikali itatoa support anadhani Pesa zinapelekwa tu na uendeshaji wote unatumia pesa ya serikali; HAPANA! Support hiyo ambayo ni ruzuku inatolewa ili gharama za matibabu ziwe nafuu na za chini zenye ulinganifu na hospitali za umma. Mfano ukiangalia gharama ktk hospitali za rufaa za Bugando na KCMC zina ulinganifu na zile za hospitali za rufaa za Mbeya na Muhimbili; za wilaya na mikoa hivyo hivyo. Na huduma nyinginezo kama za mama na mtoto hutolea bure tofauti na hospitali za binafsi mfano za Aga Khan. Magonjwa mengine kama Fistula na mengineyo kwa akina mama na wazee wagonjwa hutibiwa BURE (mfano CCBRT).
>>Sasa watu wanahoji kama serikali inatoa ruzuku za uendeshaji ktk hospitali za makanisa kwa nini huduma hazitolewi bure. Jamani ebu jaribuni kuelewa mfumo wa utoaji wa huduma za jamii hapa nchini. SERA YA SERIKALI NI KUCHANGIA HUDUMA ZA JAMII kama AFYA, ELIMU n.k. Hata kwenye hospitali za umma kama Muhimbili na nyinginezo ambako serikali hupeleka ruzuku ya kuziendesha kwa 100% kuna gharama za kulipia. Mfano mimi huwa naenda MOI na kumuona daktari bingwa (Specialist) au daktari wa mazoezi huwa natoa 30,000/= (Consultation fee) hapo bado madawa ambayo nayo inabidi uchangie na wakati mwingine unaambiwa hayapo kwa hiyo inabidi ukanunue kwenye maduka ya dawa binafsi. Na hata kama sio first track kumuona daktari bingwa (specialist) kwa kawaida inaenda hadi 20,000/=. Sasa swali la kujiuliza ni hili: Kama kuna uchangiaji kule ambako serikali imejenga kwa pesa ya wananchi na ambako inatoa pesa ya wananchi kama ruzuku ya uendeshaji kwa 100%, iweje gharama za huduma ziwe bure kule ambako serikali haikujenga na ambako hutoa ruzuku ya 0%-50% (si 100%) kwa ajili ya gharama za uendeshaji tu? Ebu wanaforum tuache jazba tufikirie na kuchunguza ukweli sahihi ili tupate uhalisia badala ya kuendelea kukaririshwa taarifa za uongo.
(4) Wengine wamehoji na kusema kuwa serikali inayaombea makanisa misaada toka nje. Ni upotoshaji mkubwa. Serikali haiombi misaada kwa ajili ya makanisa hata kidogo! Ikumbukwe kuwa Mashirika ya dini ya kikristo ya nje hata kabla ya uhuru yalikuwa yakitoa misaada na kutoa huduma za kijamii hapa nchini. Hata baada ya uhuru mashirika hayo yameendelea kutoa misaada kwa makanisa hapa nchini kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali na shule. Lakini kutokana na serikali ya Tz kubinafsisha shule na hospitali za makanisa ambazo zilijengwa kwa misaada ya Mashirika ya Kikristo ya nje yalijiondoa ktk kutoa misaada hiyo. Kwa hiyo makanisa ya TZ yakawa tena hayapati misaada toka kwa mashirika ya makisa yao huko nje, matokeo yake ujenzi wa shule na hospitali ukazorota. Baada ya hali hiyo ilibidi makanisa yajadiliane na serikali juu ya hali hii na serikali ya TZ ilibidi ikubali kuhusika ili kurejesha uhusiano na mashirika hayo ya Kikristo ya nje ili yaendelee kutoa misaada kwa makanisa ktk ujenzi wa shule na hospitali ili kuendelea kutoa huduma kwa jamii. Kwa hiyo kusema kwamba serikali inayaombea makanisa misaada toka nje ni kuelewa vibaya maelezo yaliyoko kwenye MOU au kuamua kupotosha ukweli halisi. Na kama kuna mtu ana ushahidi wa serikali kuomba misaada kwa ajili ya makanisa alete huo ushahidi. Misaada inayoombwa na serikali kusaidia bajeti yake inapokuwa ya wizara ya afya na kuipeleka kwenye hospitali zinazomilikiwa na makanisa ni katika mpango ule ule wa serikali kutoa hadi 50% ya gharama za uendeshaji wa hospitali hizo ili kuwahudumia wananchi wake. Isichukuliwe kwamba serikali inomba misaada kwa ajili ya kuendesha ibada au mambo ya kiimani ya makanisa! Bali ni misaada ya kusaidia bajeti yake ikiwemo wizara ya afya na hivyo kupelekwa kwenye hospitali. Na hii haina itikadi za kidini watu wote hutibiwa na kupata ajira ktk hospitali hizo kwa usawa.
(5) Kuhusu support ktk shule za mashirika ya dini naomba kuwaelewesha hivi: Support hiyo ktk shule haitolewi kama FEDHA! HAKUNA fedha inayotolewa na serikali kwenda kuendesha shule za makanisa. Support inayoongelewa hapo kwenye MOU ktk shule ni kupitia walimu waliosoma ktk shule na vyuo vya umma. Waalimu na watumishi wote waliosomea shule za serikali na vyuo vya serikali wamesomeshwa kwa pesa za wananchi aidha bila wao kuchangia (yaani waliosoma bure) au kwa huchangia karo na michango. Mfano karo ya shule za boding (sekondari) ni 70,000/= au day ni 20,000/=. Sasa hii si gharama halisi ambayo mwanafunzi alitakiwa kutoa bali ni gharama ambayo mwanafunzi huchangia tu, gharama kubwa kwa ajili ya kumsomesha hutolewa na serikali. Kwa hiyo wanafunzi hao wanapomaliza mafunzo yao mfano waalimu HAWAZUIWI kwenda kuajiriwa na shule za makanisa au za watu au mashirika binafsi kwa kuwalazimisha waajiriwe serikalini tu ili warudishe gharama. Bali serikali inawaruhusu waajiriwe hata kwenye shule hizo za makanisa au za watu na mashirika binafsi mengine kama huduma kwa jamii. Na wanapoajiriwa huko wanalipwa na makanisa. Hii ndiyo support inayoongelewa kwa upande wa shule za kawaida za makanisa. Hakuna hata senti moja inayopelekwa kuendesha shule binafsi. Makanisa huendesha shule zake kwa karo na pesa za sadaka na misaada toka mashirika ya kidini ya nje. Bajeti za serikali ziko wazi kama kuna mtu ana ushahidi huo anikosoe na asipotoshe!
>> Kwa hiyo suala la support watu walielewe vizuri iwe ni kwa Hospitali au shule. Liko kama nilivyolieleza. Pia ieleweke kuwa makanisa ni wamiliki tu wa hospitali na shule hizo. Hakuna ibada yoyote ktk hospitali hizo. Hospitali hizo hazihitaji mchungaji, padre au askofu wala kutumia msitari wowote wa biblia au kitabu chochote cha dini ili kutoa huduma. Lakini pia huhudumia na kuajiri watu wote bila kujali itikadi za kidini, kabila, kanda au hata uzanzibar na ubara. Vigezo vya ajira ni taaluma ya mtu na huduma kwa wagonjwa ni kwa watu wote. Tofauti na mahakama za kadhi ambazo huduma zake ni ibada kwa waislamu na huhitaji viongozi wa dini yaani Makadhi na kutumia mistari ya Quran na vitabu vingine vya kiislamu ktk kufanya kazi zake.
(6) Wengi wanajiuliza kwa nini serikali iliingia makubaliano na madhehebu ya dini ya Kikristo na si madhehebu ya dini nyingine kama Wahindu na Waislamu au hata mashirika mengine binafsi? Jibu lake ni kuwa makubaliano haya yana msingi wake kutoka kwenye utaifishaji uliofanyika miaka ya 70's ambapo waathirika wakubwa yalikuwa ni madhehebu ya dini ya Kikristo. Lakini pia baada ya serikali ya CCM kushindwa kutoa huduma za afya na elimu kulingana na uhitaji, miaka ya 90's madhehebu ya dini ya Kikristo yaliamua kuingilia kati ili kuokoa maisha ya watanzania na kuanza kujenga tena hospitali na shule. Lakini hofu na maumivu ya utaifishaji vilikuwa havijasahaulika. Hivyo madhehebu ya dini yalipoanza kujenga tena hospitali hizo na shule, Kwanza ilibidi yahakikishiwe na serikali kuwa haitataifisha tena hospitali na shule zao. Pili kulikuwa na suala la gharama. kumbukeni kuwa ni jukumu la serikali kutoa huduma za afya na elimu kwa wananchi wake. Sasa kwa hali halisi kutokana na gharama za uendeshaji kuwa kubwa, madhehebu ya dini yasingeweza kutoa huduma za afya bure au kwa gharama ya chini. Hivyo serikali ilibidi itoe ruzuku ili baadhi ya huduma kama kwa akina mama na watoto, wazee na kwa baadhi ya magonjwa kama kifua kikuu, fistula,n.k ziwe bure na kwa wengine huduma ziwe za bei nafuu kwa ulinganifu na hospitali nyingine za umma.
>>Sasa ili haya yote yatekelezeke, yaani ya kutokutaifisha hizo hospitali na kutoa huduma kwa bei kama hospitali za umma ilibidi yawekwe kwenye makubaliano, yaani MOU. Sasa kwa bahati mbaya Mashirika mengine ya binafsi, NGOs na madhehebu ya dini nyingine kama Wahindu, Waislamu n.k miaka hiyo ya 90's hawakuweka kipaumbele ktk huduma za kijamii kama afya na elimu. Hawakujihusisha na utoaji sana wa huduma za kijamii kama kujenga hospitali au shule. Kwa hiyo hawakuwa na hospitali zenye hadhi ya wilaya, mikoa na za rufaa ambazo zingewafanya wawe sehemu ya MOU. Ndo maana kwa miaka ya 90's wao hawakuhusika ktk MOU. Ila kwa miaka ya hivi karibuni NGO na madhebu ya dini nyingine yameanza nayo kujihusisha na utoaji wa huduma za kijamii ila kwa kiasi kidogo ukilinganisha na madhehebu ya dini ya Kikristo. Kwa hiyo hoja si kuchukia MOU au kuwachukia wakristo kwa sababu ya MOU. Lazima tuangalie na sababu zilizopelekea kuwepo kwa MOU na wengine kutokuwemo kwenye MOU.
>>Lakini pia kama hoja ni kupewa ruzuku za kuendesha hospitali, basi Waislamu, NGOs na dini nyingine nazo zijenge hospitali mahali ambapo kwanza serikali haina hospitali au zijenge hospitali kubwa ukilinganisha na hospitali za umma ktk maeneo husika ili ziingizwe kwenye mpango wa kupewa ruzuku ili zitoe huduma kwa bei nafuu kama hospitali za umma na za Makanisa. Lakini si kueneza chuku tu na uhasama wa kidini pasipo sababu. Au kama wanaoeneza chuki wana hoja wanipe hata hospitali kubwa yenye hadhi ya hospitali ya wilaya, mikoa na rufaa hata moja iliyojengwa na waislamu, NGOs au wahindu miaka ya 90's mahali ambapo serikali haikuwa na hospitali au ilikuwa na hospitali ndogo ukilinganisha na hospitali ya dini au NGO hizo ili waseme serikali iliwatenga kwenye MOU.