Mkataba (MoU) kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini


Ndugu zangu wanaforum kwanza namshukuru Dr. Slaa kwa kutolea ufafanuzi suala la MOU maana limeibua mjadala na manungúniko mkubwa sana ktk makundi mbalimbali ya jamii wengine bila hata kulielewa vema. Mimi binafsi nimeshalieleza sana kwenye facebook mara nyingi sana. Lakini nachokiona kwa wengi pamoja na ufafanuzi wa Dr. Slaa bado wengi hawaelewi. Napenda kuongezea maelezo yafuatayo:-

(1) Watu wanasema hajaeleza juu ya pesa zinazotolewa na serikali kwenda kwenye uendeshaji wa hospitali. Ni kweli Dr. Slaa hajaeleza juu ya masuala ya pesa. Yeye ameeleza tu mazingira yaliyopelekea kuwepo kwa makubaliano yaani MOU kati ya serikali na Makanisa na si taratibu au kanuni zilizowekwa na serikali ili kutekeleza makubaliano hayo.


(2) Ikumbukwe kuwa ni jukumu la serikali kikatiba kutoa huduma za jamii kama afya kwa wananchi wake. Lakini baada ya hali ya kiuchumi kuwa ngumu hasa ktk miaka 80's baada ya vita ya Uganda na Tanzania 1979, serikali ilikosa uwezo wa kutoa huduma za kijamii kwa watu wake waliokuwa wameongezeka na kuzidi idadi ya hospitali na shule zilizokuwepo ikiwa ni pamoja na zile zilizokuwa zimetaifishwa hapo kabla. Ilishindwa kabisa kuendesha hata shule na hospitali walizokuwa wamezitaifisha na pia ikashindwa kujenga nyingine kwa hiyo huduma za elimu na afya zilizidi kuwa duni. Kama njia ya kutatua tatizo la wananchi kukosa huduma za afya serikali ikataka kuendelea kutaifisha hospitali za madhehebu ya dini zilizokuwa zimejengwa tena baada ya utaifishaji wa kwanza ili izitumie kuwahudumia wananchi. Lakini baada ya mvutano mkali na makanisa ilishindwa kuzitaifisha hizo hospitali ikabidi serikali ikubaliane na makanisa iwahudumie wananchi wake kupitia hospitali hizo za makanisa.


(3) Kuhusu Pesa: Kwanza napenda ieleweke kuwa sihospitali zote za makanisa zilizoko kwenye makubaliano ya serikali kuwahudumia wananchi wake kupitia hizo hospitali kwa kuzipatia ruzuku. Zinazopata ruzuku ni zile za wilaya na mikoa yaani Hospitali teule (District Disignated Hospitals –DDH) na zile za rufaa kama Bugando, KCMC na nyinginezo kama CCBRT. Ilibidi serikali iwe inatoa ruzuku ya 0%-50% ya gharama za uendeshaji ili gharama za huduma ktk hospitali hizo ziwe nafuu ukilinganisha na hospitali ambazo ni za binafsi kwa 100% huku makanisa yakitoa 50%-100% ya gharama za uendeshaji. Kwa maneno mengine makanisa hutoa pesa zake kugharimia huduma kwa watanzania wote bila kujali dini zao. Na mara nyingi serikali inapochelewa kupeleka hata hizo ruzuku makanisa hutoa gharama zote. Kwa maneno mengine makanisa huikopesha serikali bila hata riba yoyote kwa ajili ya kuwahudumia watanzania wote!

>>Ruzuku hizo za hadi 50% hutolewa kama fedha, madawa, misamaha ya kodi, mishahara, kuendeleza watumishi wa hospitali, vifaa tiba na vifaa vya maabala. Kumbuka gharama za uendeshaji ktk vipengere vyote hivyo nilivyotaja hutolewa kwa ubia yaani 0%-50% serikali na 50%-100% makanisa. Kwa maneno mengine tunaweza kusema uendeshaji wa hospitali hizo nusu ni wa umma na nusu wa binafsi. Makubaliano haya yamewekwa kwa lugha ya kisheria ktk MOU. Taratibu za utekelezaji wake hazipo kwenye makubaliano hayo (MOU) ndo maana watu hawaelewi wanadhani serikali hutoa tu hela na kupeleka makanisani. Bajeti za serikali ziko wazi zinaonyesha ruzuku zinazovyotolew. Na mtu akisoma kwenye MOU kwamba serikali itatoa support anadhani Pesa zinapelekwa tu na uendeshaji wote unatumia pesa ya serikali; HAPANA! Support hiyo ambayo ni ruzuku inatolewa ili gharama za matibabu ziwe nafuu na za chini zenye ulinganifu na hospitali za umma. Mfano ukiangalia gharama ktk hospitali za rufaa za Bugando na KCMC zina ulinganifu na zile za hospitali za rufaa za Mbeya na Muhimbili; za wilaya na mikoa hivyo hivyo. Na huduma nyinginezo kama za mama na mtoto hutolea bure tofauti na hospitali za binafsi mfano za Aga Khan. Magonjwa mengine kama Fistula na mengineyo kwa akina mama na wazee wagonjwa hutibiwa BURE (mfano CCBRT).

>>Sasa watu wanahoji kama serikali inatoa ruzuku za uendeshaji ktk hospitali za makanisa kwa nini huduma hazitolewi bure. Jamani ebu jaribuni kuelewa mfumo wa utoaji wa huduma za jamii hapa nchini. SERA YA SERIKALI NI KUCHANGIA HUDUMA ZA JAMII kama AFYA, ELIMU n.k. Hata kwenye hospitali za umma kama Muhimbili na nyinginezo ambako serikali hupeleka ruzuku ya kuziendesha kwa 100% kuna gharama za kulipia. Mfano mimi huwa naenda MOI na kumuona daktari bingwa (Specialist) au daktari wa mazoezi huwa natoa 30,000/= (Consultation fee) hapo bado madawa ambayo nayo inabidi uchangie na wakati mwingine unaambiwa hayapo kwa hiyo inabidi ukanunue kwenye maduka ya dawa binafsi. Na hata kama sio first track kumuona daktari bingwa (specialist) kwa kawaida inaenda hadi 20,000/=. Sasa swali la kujiuliza ni hili: Kama kuna uchangiaji kule ambako serikali imejenga kwa pesa ya wananchi na ambako inatoa pesa ya wananchi kama ruzuku ya uendeshaji kwa 100%, iweje gharama za huduma ziwe bure kule ambako serikali haikujenga na ambako hutoa ruzuku ya 0%-50% (si 100%) kwa ajili ya gharama za uendeshaji tu? Ebu wanaforum tuache jazba tufikirie na kuchunguza ukweli sahihi ili tupate uhalisia badala ya kuendelea kukaririshwa taarifa za uongo.

(4) Wengine wamehoji na kusema kuwa serikali inayaombea makanisa misaada toka nje. Ni upotoshaji mkubwa. Serikali haiombi misaada kwa ajili ya makanisa hata kidogo! Ikumbukwe kuwa Mashirika ya dini ya kikristo ya nje hata kabla ya uhuru yalikuwa yakitoa misaada na kutoa huduma za kijamii hapa nchini. Hata baada ya uhuru mashirika hayo yameendelea kutoa misaada kwa makanisa hapa nchini kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali na shule. Lakini kutokana na serikali ya Tz kubinafsisha shule na hospitali za makanisa ambazo zilijengwa kwa misaada ya Mashirika ya Kikristo ya nje yalijiondoa ktk kutoa misaada hiyo. Kwa hiyo makanisa ya TZ yakawa tena hayapati misaada toka kwa mashirika ya makisa yao huko nje, matokeo yake ujenzi wa shule na hospitali ukazorota. Baada ya hali hiyo ilibidi makanisa yajadiliane na serikali juu ya hali hii na serikali ya TZ ilibidi ikubali kuhusika ili kurejesha uhusiano na mashirika hayo ya Kikristo ya nje ili yaendelee kutoa misaada kwa makanisa ktk ujenzi wa shule na hospitali ili kuendelea kutoa huduma kwa jamii. Kwa hiyo kusema kwamba serikali inayaombea makanisa misaada toka nje ni kuelewa vibaya maelezo yaliyoko kwenye MOU au kuamua kupotosha ukweli halisi. Na kama kuna mtu ana ushahidi wa serikali kuomba misaada kwa ajili ya makanisa alete huo ushahidi. Misaada inayoombwa na serikali kusaidia bajeti yake inapokuwa ya wizara ya afya na kuipeleka kwenye hospitali zinazomilikiwa na makanisa ni katika mpango ule ule wa serikali kutoa hadi 50% ya gharama za uendeshaji wa hospitali hizo ili kuwahudumia wananchi wake. Isichukuliwe kwamba serikali inomba misaada kwa ajili ya kuendesha ibada au mambo ya kiimani ya makanisa! Bali ni misaada ya kusaidia bajeti yake ikiwemo wizara ya afya na hivyo kupelekwa kwenye hospitali. Na hii haina itikadi za kidini watu wote hutibiwa na kupata ajira ktk hospitali hizo kwa usawa.

(5) Kuhusu support ktk shule za mashirika ya dini naomba kuwaelewesha hivi: Support hiyo ktk shule haitolewi kama FEDHA! HAKUNA fedha inayotolewa na serikali kwenda kuendesha shule za makanisa. Support inayoongelewa hapo kwenye MOU ktk shule ni kupitia walimu waliosoma ktk shule na vyuo vya umma. Waalimu na watumishi wote waliosomea shule za serikali na vyuo vya serikali wamesomeshwa kwa pesa za wananchi aidha bila wao kuchangia (yaani waliosoma bure) au kwa huchangia karo na michango. Mfano karo ya shule za boding (sekondari) ni 70,000/= au day ni 20,000/=. Sasa hii si gharama halisi ambayo mwanafunzi alitakiwa kutoa bali ni gharama ambayo mwanafunzi huchangia tu, gharama kubwa kwa ajili ya kumsomesha hutolewa na serikali. Kwa hiyo wanafunzi hao wanapomaliza mafunzo yao mfano waalimu HAWAZUIWI kwenda kuajiriwa na shule za makanisa au za watu au mashirika binafsi kwa kuwalazimisha waajiriwe serikalini tu ili warudishe gharama. Bali serikali inawaruhusu waajiriwe hata kwenye shule hizo za makanisa au za watu na mashirika binafsi mengine kama huduma kwa jamii. Na wanapoajiriwa huko wanalipwa na makanisa. Hii ndiyo support inayoongelewa kwa upande wa shule za kawaida za makanisa. Hakuna hata senti moja inayopelekwa kuendesha shule binafsi. Makanisa huendesha shule zake kwa karo na pesa za sadaka na misaada toka mashirika ya kidini ya nje. Bajeti za serikali ziko wazi kama kuna mtu ana ushahidi huo anikosoe na asipotoshe!

>> Kwa hiyo suala la support watu walielewe vizuri iwe ni kwa Hospitali au shule. Liko kama nilivyolieleza. Pia ieleweke kuwa makanisa ni wamiliki tu wa hospitali na shule hizo. Hakuna ibada yoyote ktk hospitali hizo. Hospitali hizo hazihitaji mchungaji, padre au askofu wala kutumia msitari wowote wa biblia au kitabu chochote cha dini ili kutoa huduma. Lakini pia huhudumia na kuajiri watu wote bila kujali itikadi za kidini, kabila, kanda au hata uzanzibar na ubara. Vigezo vya ajira ni taaluma ya mtu na huduma kwa wagonjwa ni kwa watu wote. Tofauti na mahakama za kadhi ambazo huduma zake ni ibada kwa waislamu na huhitaji viongozi wa dini yaani Makadhi na kutumia mistari ya Quran na vitabu vingine vya kiislamu ktk kufanya kazi zake.

(6) Wengi wanajiuliza kwa nini serikali iliingia makubaliano na madhehebu ya dini ya Kikristo na si madhehebu ya dini nyingine kama Wahindu na Waislamu au hata mashirika mengine binafsi? Jibu lake ni kuwa makubaliano haya yana msingi wake kutoka kwenye utaifishaji uliofanyika miaka ya 70's ambapo waathirika wakubwa yalikuwa ni madhehebu ya dini ya Kikristo. Lakini pia baada ya serikali ya CCM kushindwa kutoa huduma za afya na elimu kulingana na uhitaji, miaka ya 90's madhehebu ya dini ya Kikristo yaliamua kuingilia kati ili kuokoa maisha ya watanzania na kuanza kujenga tena hospitali na shule. Lakini hofu na maumivu ya utaifishaji vilikuwa havijasahaulika. Hivyo madhehebu ya dini yalipoanza kujenga tena hospitali hizo na shule, Kwanza ilibidi yahakikishiwe na serikali kuwa haitataifisha tena hospitali na shule zao. Pili kulikuwa na suala la gharama. kumbukeni kuwa ni jukumu la serikali kutoa huduma za afya na elimu kwa wananchi wake. Sasa kwa hali halisi kutokana na gharama za uendeshaji kuwa kubwa, madhehebu ya dini yasingeweza kutoa huduma za afya bure au kwa gharama ya chini. Hivyo serikali ilibidi itoe ruzuku ili baadhi ya huduma kama kwa akina mama na watoto, wazee na kwa baadhi ya magonjwa kama kifua kikuu, fistula,n.k ziwe bure na kwa wengine huduma ziwe za bei nafuu kwa ulinganifu na hospitali nyingine za umma.
>>Sasa ili haya yote yatekelezeke, yaani ya kutokutaifisha hizo hospitali na kutoa huduma kwa bei kama hospitali za umma ilibidi yawekwe kwenye makubaliano, yaani MOU. Sasa kwa bahati mbaya Mashirika mengine ya binafsi, NGOs na madhehebu ya dini nyingine kama Wahindu, Waislamu n.k miaka hiyo ya 90's hawakuweka kipaumbele ktk huduma za kijamii kama afya na elimu. Hawakujihusisha na utoaji sana wa huduma za kijamii kama kujenga hospitali au shule. Kwa hiyo hawakuwa na hospitali zenye hadhi ya wilaya, mikoa na za rufaa ambazo zingewafanya wawe sehemu ya MOU. Ndo maana kwa miaka ya 90's wao hawakuhusika ktk MOU. Ila kwa miaka ya hivi karibuni NGO na madhebu ya dini nyingine yameanza nayo kujihusisha na utoaji wa huduma za kijamii ila kwa kiasi kidogo ukilinganisha na madhehebu ya dini ya Kikristo. Kwa hiyo hoja si kuchukia MOU au kuwachukia wakristo kwa sababu ya MOU. Lazima tuangalie na sababu zilizopelekea kuwepo kwa MOU na wengine kutokuwemo kwenye MOU.
>>Lakini pia kama hoja ni kupewa ruzuku za kuendesha hospitali, basi Waislamu, NGOs na dini nyingine nazo zijenge hospitali mahali ambapo kwanza serikali haina hospitali au zijenge hospitali kubwa ukilinganisha na hospitali za umma ktk maeneo husika ili ziingizwe kwenye mpango wa kupewa ruzuku ili zitoe huduma kwa bei nafuu kama hospitali za umma na za Makanisa. Lakini si kueneza chuku tu na uhasama wa kidini pasipo sababu. Au kama wanaoeneza chuki wana hoja wanipe hata hospitali kubwa yenye hadhi ya hospitali ya wilaya, mikoa na rufaa hata moja iliyojengwa na waislamu, NGOs au wahindu miaka ya 90's mahali ambapo serikali haikuwa na hospitali au ilikuwa na hospitali ndogo ukilinganisha na hospitali ya dini au NGO hizo ili waseme serikali iliwatenga kwenye MOU.
 

This in psychology is called projection - heaping your own garbage onto others - thinking the way you think and behave is also the same other people think and behave. Projection is a defence mechanism, a way of dealing with one's problems and shifting the blame to others so that the concerned person feels happy!
 
Si kutapatapa! ni wakati wa kuweka kila kitu mezani sasa!Wazungu wameshavitenganisha Kanisa na Serikali zamani sana!
Kodi unayoizungumzia ni ya Kanisa husika ambalo hutoza wanachama wake ili kuwasaidia kwenye shughuli mbalimbali ikiwemo kuzikana, serikali haina mkono wake! na ikitokea kuwa serikali ndiyo inayokusanya kodi ya Kanisa basi serikali huzikata kodi!

Kitu gani kinachotufanya leo tuambiwe kuwa SERIKALI ya Ujerumani inatoa pesa za walipa kodi wake waliokataa Kanisa na Serikali kuwa kitu kimoja na kuyapa Makanisa ya Tanzania mabilioni ya shilingi kila mwaka sielewi!

Ninakuambia bila ya wasiwasi kama ikidhihirika kuwa ni kweli (kitu ambacho siamini) serikali ya Ujerumani inatoa idadi hiyo ya pesa za walipa kodi wake na kuyapa Makanisa ya TZ kila mwaka basi mtikisiko wake utausikia kutoka kwa Wajerumani wenyewe huko Ujerumani, angalia tu sasa hivi serikali ya Ujerumani inavyosakamwa na Wajerumani wenyewe kuhusu kuipatia Ugiriki pesa ambazo ni kama kitega uchumi cha Ujerumani kwa baadaye, ije iwe kina Pengo wanaokinga mikono tu?
 
Wakristo wana mkataba na serikali kuwa taasisi zao hazitataifishwa.

Una uhakika gani wewe Muislamu baada ya kukusanya sadaka za wavuja jasho wenzako wa ndani na nje ya nchi na kujenga shule au Hospitali kuwa baadaye hamtaambiwa kuwa ni magaidi na kutaifishwa hayo majengo yenu?...think great!
 

kiruu!! kaka Mizambwa umemshusha mkuu wa meza, mbuzi katoliki live?! hii kitu wengine huwa tunakifaudu vizur wakt wa mfungo wa ramadhani, mfungo ukishaisha huwa hii kitu inakuwa adimu sana na bei inapanda sana bikozi ovo ze elastisite of demand...
 

Hujui unachokisema because you are in a cage! Serikali nyingi za Ulaya ziliingia makubaliano na Kanisa kwa sababu hizo hizo za kubinafsisha mali ya Kanisa (kuchukua bure mali ambayo imetokana na fedha za wanaKanisa bila kuwafidia). Kwa hiyo, hata Ujerumani wana makubaliano hayo. Ila kwa vile kwako ni kama usiku wa giza haya huwezi kuyaelewa na kama utayaelewa hutaweza kuyakubali maana unaona ni heri ubaki bila kuelewa kuliko kuelewa kama baadhi wanavyoamua wawe.
 
Labda Ulaya nyingine sio ninayoijua mimi.

by the way, makubaliano ya Serikali ya Ujerumani na Makanisa yalifanyika kimyakimya kama yalivyofanyika Tanzania?
 

Issue hapa ni wivu tu wa maendeleo unaotokana na approaches tofauti kuhusu uenezaji wa neno la Mungu: 1) Wakristo wao huwezi kutenganisha imani na ushiriki katika huduma za jamii (kumpenda Mungu ni pamoja kumpenda mwanadamu/kumkomboa kielimu, kiafya nk. 2) Waislamu approach yao ni tofauti (ni kushughulika zaidi na imani tu na si lazima sana mtu ashiriki katika huduma za jamii). Matokeo yake ni kwamba Wakristo wanajenga mashule na hospitali na Waislamu wanabaki kujenga tu misikiti zaidi na wanapojikuta wako nyuma ya wenzao wanaanza kuona wivu na kutunga uwongo na propaganda ili watu wengine wasiojua hali ilivyo waanze kuwaonea huruma. Hakuna atakaye waonea huruma kwa kutunga uwongo, my friends!
 
Labda Ulaya nyingine sio ninayoijua mimi.

by the way, makubaliano ya Serikali ya Ujerumani na Makanisa yalifanyika kimyakimya kama yalivyofanyika Tanzania?

Kutojua si sababu ya kubisha? Kwani ni makubaliano gani ya Ujerumani unayoyajua?
 
Labda Ulaya nyingine sio ninayoijua mimi.

by the way, makubaliano ya Serikali ya Ujerumani na Makanisa yalifanyika kimyakimya kama yalivyofanyika Tanzania?

Ulishasoma historia ya Ulaya na hasa namna gani serikali zilibinafsisha mali ya Kanisa?
 

nawe unajiita great thinker? unavuka mto kabla haujaufikia? unanunua mbeleko kabla mtoto hajazaliwa? zaa mtoto kwanza ndo ununue nepi. kwani mbona za kwetu tulijenga zikataifishwa ili na ninyi mzifaidi na baadaye mkazivuruga, zikawashinda mkatuomba mturudishie, lakini kwa sababu na sisi akili tunazo, na kwa sababu tunajua serikali yako ni babaishi na dhaifu, tukasema hapana, msiturudishie hiv hiv, tuwatwange mkataba ili kurudishiana huko kuwe kwa kisomi. siyo mnatudishia tu hiv hiv, tunapasua watu mabusha yao wanapona halafu kesho waje watunyang'anye insitutions zetu ambazo tumezitolea damu na jasho letu kuzijenga na kuziendesha. tulijua tusipokuwa wajanja na kuweka masharti lazima itaja kula kwetu kwa sababu tukiwaangalia wenzetu wa upande mwingine wao twaona wala tende tuuuuuuu na pilau, kaz hawafanyi kutwa kuchwa vibarazan...tukajua hawa wataja tuletea matatizo tu baadaye kwa sababu kuna siku watakuja kumbuka blanket lakini by the time wanalikumbuka hilo blanket kutakuwa tiyari ni asubuh.

unajua sadeeq theists wakristu japo skubalian na iman zao lakini nawapenda kwa maono yao ya mbali. hapo kilindi panapozungumziwa mimi nimefika na hiyo hospital wakti inajengwa nipo. wilaya ya kilindi wengi ni waislamu na hapo songe palipojengwa hiyo hospitali ni waislamu tupu. KKKT walipoionaga tu hiyo fursa walishukaga hapo kama mwewe nakwambia. hawa watu huwa wanafiikiri na kupanga kimkakati(strategically) 100 yers to come. ni theists ndiyo lakini pia wanao uwezo wa kufikiri nje ya box la dini zao, na hiyo ndo tofauti kati yao na ninyi...
 

na hivi nyerere aliyekuwa anawatetea kupitia ujamaa wake hayupo tena na ndiye huyo sasa wanamtukana, ngoja tuone dunia hii ya leo ya ushindani atawatetea nani. mnangojea eti rais mwislamu akiingia madarakani ndo apite anawagawia pilau, thubutu yake, mtabakia huko huko. sisi kwa sasa tunafikiria namna ya kukabiliana na soko la afrika masharki, yaan mawazo yetu ni juu ya wakikuyu na waganda huko, si ninyi wala tende wa kariakoo, kama tunawapa ushauri hamtaki shauri yenu, endeleeni kusikiliza propaganda za redio imani, watoto wenu watakuja kuwa matarishi wa wenetu, si tupo hapa hapa, mtaona.
 
blah blah tupu! tuhakikishiwe na sisi kuwa taasisi zetu hazitatifishwa au sisi Waislamu sio raia wa nchi hii?
 
blah blah tupu! tuhakikishiwe na sisi kuwa taasisi zetu hazitatifishwa au sisi Waislamu sio raia wa nchi hii?

lini uliomba ukakataliwa? lete document. kikwete mwenzako si keshakuambia wewe kazi yako unalialia tu ili uonewe huruma. mpelekeen basi MoU au bado ndo mnaiandika? tena katika kupeleka hiyo MoU mjue taratibu ni zip, mziunde vikundi vya wizi vya kuingiza majambia toka uarabuni mtegemee eti MoU itakubaliwa. Kuna utaratibu muujue. kwanza kabisa hizo institutions mnazo? je management yake ipoje? kwa sababu hatutakubali tuwape pesa kupitia MoU HALAFU KESHO NA KESHOKUTWA TUSIKIE VIJANA MUJAHIDEEN WA kiislam wameiteka hospital toka mikononi mwa wazee wa kiislamu. tunataka hospital hizo zitumike kupasua mabusha si kutekwa na mujahideen. Kwa kifupi mjue utaratibu ni upi, msifikir ni suala tu la ghafla bin vuuuuuuuuu. you will need to have a clear strategic plan, a blueprint, fikirini in terms of 100 years to come, msifikiri tu kesho.
 


Nilikuwa sijajua kwamba BAKWATA na waislamu wanadeni kubwa la kulipa kwa watanzania. Serikali ilikubaliana na taasisi zote za dini, TEC na CCT wakawachangisha watanzania kuchangia maendeleo wao sijui nini walifanya.
Mimi nadhani badala ya kuwalaumu wakristo waislamu inabidi watoe shukrani kwa majitoleo wa wakristo.

Sote tunaifahamu Hospitali ya Bugando. Hivi kweli hospitali kubwa kama ile eti ilikuwa ya Kanisa! Kwa wasiojua, Bugando ndio hospitali ya pili kwa ukubwa kwa mafunzo ya udaktari baada ya Muhimbili. Hivi hii hospitali ingekuwa chini ya kanisa, wakatoa huduma kwa gharama kama za Aga Khan kanisa si lingekuwa mbali. Nimeongelea mfano mmoja tu.

Jamani watanzania tuache kulalamika. Mimi ningekuwa mkuu wa TEC au CCT ningeshapendekeza kuvunja MoU, turudishiwe taasisi zetu na kudai faida kwa kutuhudumia wananchi kwa kipindi hicho chote pasipo faida. Ikumbukwe kwamba huduma za jamii iwe kwa mkristo au muislamu ni jukumu la serikali. Hata kama huduma
hizi zingekuwa zinaenda kwa dini fulani tu, bado ni jukumu la serikali kufanya hivyo.


 
Nimegundua wanaopinga MoU wala hawana hoja ya msingi pamoja na kwamba wanajitahidi kuja na data lakini wanashindwa hata kuelewa nini wanachokiandika. Serikali inatoa pesa kwa hospitali zinazomilikiwa na kanisa, serikali haitoi pesa ziende kanisani wakuu. Mahospitali haya yana uongozi wake na yako kwenye category ya Non-for-Profit Organizations. Zaidi ni kwamba mahospitali haya yote yanakuwa regulated na wizara ya afya. Kanisa halifanyi biashara, kanisa linatoa huduma. Kuna mantiki gani ya serikali kujenga hospitali ya rufaa Kilimanjaro wakati tayari ipo? Ingekuwa KCMC inafanya biashara ni haki serikali ijenge hospitali ya rufaa pale kuwapa wananchi unafuu, lakini sivyo. Badala ya kupoteza resources kujenga inasaidia kuimarisha kile kilichopo. Hela inayosave serikali inawekeza kwenye shughuli nyingine kama elimu, barabara etc.

Nimegundua kuna watu hawana ufahamu humu, wamekaza shingo zao hata wakielezwa hawawezi kuelewa. Ni sawa na mawe yaliyokaa mtoni, kila siku linapigwa maji, ukilipasua ndani ni kavu. Ndio watu hawa wanaopaza sauti humu. Nikifananishe na nini kizazi hiki? Ni nani aliyekilaani na kukinyanganya uwezo wa kufikiri? Watu wanapaza sauti kuhusu OIC lakini hata hawaijui OIC ni taasisi kwa ajili ya nini, poor Tanzanians! Lakini niwaeleze kwa uwazi hizi ni athari za umaskini, umaskini ulioshika mizizi ambao sasa umeanza kutafuna mpk uwezo wa watu wa kufikiri. Hamna lingine watu wanalopigania hapa, ni umaskini, umaskini, umaskini! Umaskini ndio unaofanya watu wajiingize kwenye ushirikina, vurugu za kugombea mali na mengine mengi yafananayo na hayo. Ole wa kizazi hiki, kimelaaniwa, kimekosa ufahamu na maarifa.
 
[/QUOTE]

kaka Mpenda.Haki umeeleza vizuri na kitaalamu sana, lakini naomba nikumbushe kitu kimoja ambacho najua hata wewe unakielewa. watu wasifkiri kina sadeeq, kina mzee mohamed Said na wengineo hawaujui ukweli huu bali ni kwamba wanaujua vema sana ila kwa kujua waislamu wengi hawajasoma sasa wanatumia mbinu ya blanketi la dini za kikoloni kuwachochea vijana wa kiafrika, wa kitanzania, kwa kuwalisha uongo, brainwashing, ili vijana wa kitanzania tuwachinje mama zetu na baba zetu, na wakati tunatumbua hayo matumbo ya mama zetu wao watapanda ndege kwenda saudia kula bata. kwa hiyo wanajua ila wameamua tu kutunyea uchafu wao kwa makusudi yao maalumu. ndo maana wengine humu tumeamua kuwa hawa hamna haja ya kupoteza mda kuwapa maelezo ya kitaalamu ila ni kuwangojea tu watunyee. wakitunyea mavi sahani moja sisi tunawanyea debe nzima, daadake..jino kwa jino tu. tumeshawageuzia shavu zote na makofi wametutwanga sana, sasa ni kuwapasukia tu waabudi fikra za kikoloni hawa...no cavity, enough is enough!
 
Unazungumza kitu ambacho hukijui. Jamaa watafurahi sana kama wakisikia misaada wanayotupa kupitia kodi yao inafanya kazi inayotakiwa.
Naona baada ya kupewa maelezo ya kina mnaanza kutafuta vijisababu vingine...sijui ugonjwa huu aliwapa nani!?
Germany


About 70% of church revenues come from church tax. This is about €9.2 billion (in 2010).
Article 137 of the Weimar Constitution of 1919 and article 140 of the German Basic Law of 1949 are the legal basis for this practice.

In Germany, on the basis of tax regulations passed by the communities and within the limits set by state laws, communities may either

  • require the taxation authorities of the state to collect the fees from the members on the basis of income tax assessment (then, the authorities withhold a collection fee), or
  • choose to collect the church tax themselves.
In the first case, membership in the community is entered onto a tax document (Lohnsteuerkarte) which employees must surrender to their employers for the purpose of withholding tax on paid income. If membership in a tax-collecting religious community is entered on the document, the employer must withhold church tax prepayments from the income of the employee in addition to other tax prepayments. In connection with the final annual income tax assessment, the state revenue authorities also finally assess the church tax owed. In the case of self-employed persons or of unemployed taxpayers, state revenue authorities collect prepayments on the church tax together with prepayments on the income tax.
If, however, religious communities choose to collect church tax themselves, they may demand that the tax authorities reveal taxation data of their members to calculate the contributions and prepayments owed. In particular, some smaller communities (e.g. the Jewish Community of Berlin) choose to collect taxes themselves to save collection fees the government would charge otherwise.
Collection of church tax may be used to cover any church-related expenses such as founding institutions and foundations or paying ministers.
The church tax is only paid by members of the respective church. People who are not members of a church tax-collecting denomination do not have to pay it. Members of a religious community under public law may formally declare their wish to leave the community to state (not religious) authorities. With such a declaration, the obligation to pay church taxes ends. Some communities refuse to administer marriages and burials of (former) members who had declared to leave it.
The money flow of state and churches is distinct at all levels of the procedures. The church tax is not meant to be a way for the state to directly support churches, but since expenses for church tax are fully deductible (as are voluntary expenses for the Church, for charity or a bundle of other privileged aims) in fact such support occurs on a somewhat large scale. The effort of collecting itself, done by the State, is entirely paid for by the Churches with a part of the tax income.
The church tax is historically rooted in the pre-Christian Germanic custom where the chief of the tribe was directly responsible for the maintenance of priests and religious cults. During the Christianization of Western Europe, this custom was adopted by the Christian churches (Arian and Catholic) in the concept of "Eigenkirchen" (churches owned by the landlord) which stood in strong contrast to the central church organization of the Roman Catholic Church. Despite the resulting medieval conflict between emperor and pope, the concept of church maintenance by the ruler remained the accepted custom in most Western European countries. In Reformation times, the local princes in Germany became officially heads of the church in Protestant areas and were legally responsible for the maintenance of churches. Not until the 19th century were the finances of churches and state regulated to a point where the churches became financially independent. At this point the church tax was introduced to replace the state benefits the churches had obtained previously.
Taxpayers, whether Roman Catholic, Protestant or members of other tax-collecting communities, pay between 8% (in Bavaria and Baden-Württemberg) and 9% (in the rest of the country) of their income tax to the church or other community to which they belong.[SUP][1][/SUP]
For example, a single person earning 50,000 euros may pay an average income-tax of 20%, thus 10,000 euros. The church tax is then 8% (or 9%) of that 10,000 euros: 800 (or 900) euros.
 
Wanasema ni afadhali umtendee wema mbwa atakulipa wema wako kuliko kuwatendea wema baadhi ya binadamu...
 
Wanasema ni afadhali umtendee wema mbwa atakulipa wema wako kuliko kuwatendea wema baadhi ya binadamu...

wee kaka acha tu. bibi yangu kule kijijini anayo kanga yake aipendaga kweli. maandishi yake yameandikwa "wema mtendee pweza binadam hutomweza"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…