Mkataba wa Bandari: Mbunge Aida Khenani akiri kupelekwa Dubai, lakini mpaka wanarudi hakujua walikwenda kufanya nini

Kuna shida gani kutafuta umaarufu kusema ukweli? Usilamishe aseme lini ukweli wake. Kaamua kusema leo mbele ya waandishi wa habari kuliko bungeni kwa wahuni.
Kwa nini huyo unamuona mkweli lakini akisema Msukuma unamuona muongo?

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Ila mheshimiwa Angekuwa amefanya vizuri kama angetusanua kabla ya kwenda Dubai.
Huyo Muheshimiwa aaminiki tangu kelele za bandari zilipoanza ndio anaongea leo je hizi kelele zisingekuwepo angeongea hayo aliyoongea? Au anatuletea mambo ya siasa ya kupima upepo na kutaka umaarufu?

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Ile mzazi ushakula kishika uchumba na mahari ya watu halafu bint yako hataki kuolewa
 
WABUNGE 30 walipelekwa kwa ndege binafis na kupokelewa as VVIP, wamefanya shopping kwa ajili yao na familia zao pamoja na posho ndefu kwa gharama za DP WORLD , wamerudi na kushawishi wenzao ila bado WASOMI wa kitanzania na wasio soma wakaona MANGONGO CONTRACT IS LAANA, wakagoma:

Wakatafutwa influencer, wa kwanza alikuwa DIAMOND PLATINUMZ na ZUCHU pamoja na OMMY DIMPOZ na SHEKHRAN wakagoma maana wangegawa mashabiki zao, madalali wakaona isiwe shida wakawanunua MAULIVI wa -KIKANGA na ZE-MBWELEE, wameshadalalia na shopping washafanya sasa wanarudi na kioo nyumbani baada ya kuacha almasi kwa mkoloni.
 
Hii sio hoja ila.ni miongoni mwa vioja , hivyo kutoa wanajumuia kwenue hoja kuu
 
Hii sio hoja ila.ni miongoni mwa vioja , hivyo kutoa wanajumuia kwenue hoja kuu
Kwa ufahamu wako, "hoja kuu" uijuayo wewe ni ipi kwani?

Nimekusoma, nimeona kuwa, umeandika kana kwamba umekurupushwa toka usingizini na bila kujua kinachojadiliwa, ukafyatua chochote kilicho kuja kwenye ufahamu wako!

Hata hivyo, nawe asante kwa kutia mguu kwenye mjadala kwa staili hii..!
 
huo mkataba umesainiwa lini? au unazungumzia makubaliano?
 
Kama hayo anayoyasema ni kweli na sikutaka umaarufu kwa nini akuyasemea bungeni na nafasi ya kuyasema aliipata?

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Na kwani kuyasema huku nje kuna ubaya gani? Au amevunja sheria gani kiasi cha wewe kuhoji na kupaniki?

By the way, huku nje kwa umma ndo kwenyewe maana hili ndilo bunge kuu la wananchi na halina figisu figisu za ki - CCM na za akina Tulia Ackson na hakuna cha kupewa dakika 5 au 10 za kuchangia...

Huku kwenye bunge la wananchi unamwaga Kila kitu hadharani na Kwa muda utakao wewe..

Kwa hiyo isikupe shida. Aida Khenani yuko sahihi. Jamii imemwelewa vyema na ujumbe umeeleweka kwa usahihi kwa umma wote isipokuwa labda wewe wa ukae..
 
huo mkataba umesainiwa lini? au unazungumzia makubaliano?
Kumbe unajadili kitu usichokielewa bitimkongwe?

Na kwa kadiri ya ufahamu wako wewe, unadhani ni ipi tofauti ya "mkataba" na "makubaliano?"..

Ukijibu vyema swali hili, uje tuendeele na majadiliano...
 
Kuwa na genge ndani ya Serikali linalofanya uhaini sio jambo la kushabikia, hata mwalimu Nyerere kuna watu walikua wanamfanyia uhaini mpaka ikafikia muda akawaweka detention .
Kama ndiyo iko hivi kwa suala hili, Rais Samia Suluhu Hassan anasubiri nini kuwa - detain hao wenzake?

Na unadhani Rais Samia aweza kuji - detain mwenyewe? Yeye si ndiye mwanzo na mwisho wa ishu hii yote? Nani alisaini MoU? Nani alisaini IGA? Hakusoma kabla ya kusaini?

How come huu upuuzi uwe ni fault ya vyama vilivyo nje ya serikali a.k.a vyama vya upinzani?

Mimi nasema, HAPANA. Vyama vya upinzani viendelee kupiga kelele sana Kwa hili. Vitumie udhaifu huu wa Serikali na chama kinachoongoza Serikali kuwaambia hawafai kubeba dhamana hii.

Yaani lazima isemwe kuwa serikali yote kuanzia Rais Samia na chama chake ni wahaini..!!

Nani atam - detain mwenzake???
Pili, kuwa mpinzani sio kushabikia serikali iporomoke, bora ushabikie chama kiporomoke kwa maana ya CCM kama wewe ni CHADEMA,
Chama kinachoongoza serikali kikiporomoka na serikali yake huporomoka vivyo hivyo na siku zote hii huwa ni fursa na furaha kwa vyama vilivyo nje ya serikali. Na ndiyo siasa yenyewe..!!
lakini Serikali ikiporomoka ama isipoelewana kwa sababu ya uchu wa madaraka wa watu flani , wanaoumia ni ndugu zetu wanaotegemea kutibiwa kwa mkono wa serikali, kusoma kwa mkono wa serikali.
Obviously ndivyo ilivyo, nakubaliana na wewe kwenye hili. Lakini, kumbuka tena kuwa, kuanguka kwa chama kilicho madarakani tena kilicho kizee (kilichokaa muda mrefu madarakani) kama CCM, basi itakuwa ni kwa neema ya Mungu pekee iwapo kitang'oka au kung'olewa madarakani bila kuacha madhara ya aina fulani kwa nchi...
Vyama vya upinzani hasa CHADEMA kitendo cha kuwa tayari cheza ngoma yeyote ile ilimradi inadhoofisha nchi sio uzalendo.
Aisee likely wewe huijui siasa!!

Wewe unataka CHADEMA wafanye nini? Waanze awamu nyingine ya "maridhiano" ili kiwapatanishe CCM wanaosalitiana wao kwa wao ndani ya chama na serikali yao?

Bro, mimi sio CHADEMA wala ACT Wala chama chochote kingine ikiwemo CCM. Lakini napenda tu ufahamu pia naichukia na siipendi CCM kama nisivyompenda shetani. Natamani hata leo kiondoke/kife na kutoweka kabisa..

Mr poisonous, kwangu mimi it doesn't matter CCM itakufa na kutowekaje ktk uso wa Tanganyika. What matters ni kuwa iondoke bila kujali itaondokaje iwe ni kwa kifo cha kawaida ghafla au kuvurushwa Kwa nguvu..

Kumbuka hili: Ili uvune mahindi mengi, basi lazima upande punje ya hindi moja, ioze chini ya ardhi/udongo, na kisha iote na kumea na kuzaa mahindi mengine mengi..

Huwezi kupata mazao usipokubali kufa kwanza ili baadae ufufuke kama mhindi, umee na kutoa mazao...!!

Tukubali tu CCM ife zake. Tunajua fika kuwa "Probably" wataondoka huku wakiacha makovu na maumivu kwa nchi na watu Kwa sababu ya mizizi waliyokwisha ichimbia. Lakini ni heri hiyo, maana nchi hii itazaliwa upya Kwa mara ya pili ikiwa safi bila CCM...!
 
Muungano wa ajabu sana huu
 
Hilo limama linakwendaje Dubai bila kujua limekwenda kufanya nini? Upuuzi mtupu.🀣🀣
 
Nami nikuulize aliyepeleka majina ya COVID-19 bungeni ni nani?

Mwanasheria mkuu wa Sirikali na Ofisi ya mwanasheria mkuu wa Sirikali ni vitu viwili tofauti.
Shehe, umewahi kupelekwa Dubayi weye.
Vipi, waonaje tufanye mpango upelekwe Dubayi? Usihofu gharama, yaani weye wapelekwa buure kabisa.
 
siwezi kujibu maana mimi siyo mwanasheria. Case closed
Afadhali umekuwa mkweli kwa nafsi yako mwenyewe...

Umekiri kuwa hujui kwa sababu wewe si mwanasheria..

Mimi na wewe, tumefunga mjadala. Endelea kuwasoma wengine na kujifunza toka kwao na mwisho utaelewa tu..

Case closed πŸ”’πŸ”’πŸ”’
 
Shehe, umewahi kupelekwa Dubayi weye.
Vipi, waonaje tufanye mpango upelekwe Dubayi? Usihofu gharama, yaani weye wapelekwa buure kabisa.
Yaani kupelekwa Dubai ndio sababu ya kuwasaliti Watanzania wenzako kwa kuwauza kwa Waarabu?? Huu ni UHAINI kabisa. Uzalendo kwa nchi yako ya kuzaliwa ni lazima iwe kipaumbele namba moja katika maisha ya binadamu yoyote yule hapa duniani.
 
Sipingi huja ya mbunge lkn Kuna shida nyingine naiona kwa sisi wa bongo.
Hivi mbunge atoke Tanzania hadi Dubai hajui alienda kufanya nn? Hatupo serious kiasi hiki kweli?

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app

Mkuu, inawezekana kabisa hata kama mnaambiwa sababu za kusafiri lakini hadidu za rejea na mwandishi wa ripoti ni mwenyekiti wa kamati. Mkifika kule mnafanya ziara kwenye bandari na kisha mnarejea.

Usichokumbuka ni kuwa sio ziara hii iliyokuwa chanzo za makubaliano. Makubaliano ya mkataba huu hakuna anayeweza kusema yalifanywa lini na kwa ushauri wa nani serikalini! Bunge lililetewa kuupa nguvu kisheria! Ulishakuwepo!!
 
Nakuelewa Sana shida ni kauli kuwa sikujua tunaenda kufanya nn

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…