Kuwa na genge ndani ya Serikali linalofanya uhaini sio jambo la kushabikia, hata mwalimu Nyerere kuna watu walikua wanamfanyia uhaini mpaka ikafikia muda akawaweka detention .
Kama ndiyo iko hivi kwa suala hili, Rais Samia Suluhu Hassan anasubiri nini kuwa - detain hao wenzake?
Na unadhani Rais Samia aweza kuji - detain mwenyewe? Yeye si ndiye mwanzo na mwisho wa ishu hii yote? Nani alisaini MoU? Nani alisaini IGA? Hakusoma kabla ya kusaini?
How come huu upuuzi uwe ni fault ya vyama vilivyo nje ya serikali a.k.a vyama vya upinzani?
Mimi nasema, HAPANA. Vyama vya upinzani viendelee kupiga kelele sana Kwa hili. Vitumie udhaifu huu wa Serikali na chama kinachoongoza Serikali kuwaambia hawafai kubeba dhamana hii.
Yaani lazima isemwe kuwa serikali yote kuanzia Rais Samia na chama chake ni wahaini..!!
Nani atam - detain mwenzake???
Pili, kuwa mpinzani sio kushabikia serikali iporomoke, bora ushabikie chama kiporomoke kwa maana ya CCM kama wewe ni CHADEMA,
Chama kinachoongoza serikali kikiporomoka na serikali yake huporomoka vivyo hivyo na siku zote hii huwa ni fursa na furaha kwa vyama vilivyo nje ya serikali. Na ndiyo siasa yenyewe..!!
lakini Serikali ikiporomoka ama isipoelewana kwa sababu ya uchu wa madaraka wa watu flani , wanaoumia ni ndugu zetu wanaotegemea kutibiwa kwa mkono wa serikali, kusoma kwa mkono wa serikali.
Obviously ndivyo ilivyo, nakubaliana na wewe kwenye hili. Lakini, kumbuka tena kuwa, kuanguka kwa chama kilicho madarakani tena kilicho kizee (kilichokaa muda mrefu madarakani) kama CCM, basi itakuwa ni kwa neema ya Mungu pekee iwapo kitang'oka au kung'olewa madarakani bila kuacha madhara ya aina fulani kwa nchi...
Vyama vya upinzani hasa CHADEMA kitendo cha kuwa tayari cheza ngoma yeyote ile ilimradi inadhoofisha nchi sio uzalendo.
Aisee likely wewe huijui siasa!!
Wewe unataka CHADEMA wafanye nini? Waanze awamu nyingine ya "
maridhiano" ili kiwapatanishe CCM wanaosalitiana wao kwa wao ndani ya chama na serikali yao?
Bro, mimi sio CHADEMA wala ACT Wala chama chochote kingine ikiwemo CCM. Lakini napenda tu ufahamu pia naichukia na siipendi CCM kama nisivyompenda shetani. Natamani hata leo kiondoke/kife na kutoweka kabisa..
Mr
poisonous, kwangu mimi it doesn't matter CCM itakufa na kutowekaje ktk uso wa Tanganyika. What matters ni kuwa iondoke bila kujali itaondokaje iwe ni kwa kifo cha kawaida ghafla au kuvurushwa Kwa nguvu..
Kumbuka hili:
Ili uvune mahindi mengi, basi lazima upande punje ya hindi moja, ioze chini ya ardhi/udongo, na kisha iote na kumea na kuzaa mahindi mengine mengi..
Huwezi kupata mazao usipokubali kufa kwanza ili baadae ufufuke kama mhindi, umee na kutoa mazao...!!
Tukubali tu CCM ife zake. Tunajua fika kuwa "Probably" wataondoka huku wakiacha makovu na maumivu kwa nchi na watu Kwa sababu ya mizizi waliyokwisha ichimbia.
Lakini ni heri hiyo, maana nchi hii itazaliwa upya Kwa mara ya pili ikiwa safi bila CCM...!