Mkataba wa Bandari: Mbunge Aida Khenani akiri kupelekwa Dubai, lakini mpaka wanarudi hakujua walikwenda kufanya nini

Mkataba wa Bandari: Mbunge Aida Khenani akiri kupelekwa Dubai, lakini mpaka wanarudi hakujua walikwenda kufanya nini

Sipingi huja ya mbunge lkn Kuna shida nyingine naiona kwa sisi wa bongo.
Hivi mbunge atoke Tanzania hadi Dubai hajui alienda kufanya nn? Hatupo serious kiasi hiki kweli?

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
Amejieleza vizuri Sana labda kama hutaki kumuelewa Kwa makusudi. Anasema wakati wanaondoka aliuliza akaambiwa wanakwenda ziara ya mafunzo ili kuona wenzetu wanavyoendesha bandari ili waje waishauri serikali. Baada ya kurudi ndo anakutana na mikataba iliyosainiwa mwaka mmoja nyuma Kwa hiyo kwake ni kama alikwenda hajui Nia halisi ya ziara maana hata barua rasmi ya ofisi ya Spika ilieleza mwaliko pekee wa ziara bila maudhui ya ziara.
 
Kasema baada ya kuuliza wanaenda fanya nini alijibiwa na Mbalawa wanaenda kujifunza namna wengine wanavyoendesha bandari ili waje kuishauri Serikali.
Na kwanza safari yenyewe ilikuwa ya ghafla tu maana alikuwa jimboni kwake...

Ghafla akapigiwa simu ajiandae kwa safari kwenda Dubai..

Baada ya muda kidogo akapata barua rasmi ya bunge kumtaka kujiandaa kwenda huko..

Mpaka hapo alikuwa hajui lengo la safari hiyo ni nini specific ukiondoa statement ya jumla jumla tu ya kuwa "wanakwenda kujifunza"

Posho zao za safari kwanza walilipwa na TPA Kwa pesa za kitanzania na huko Dubai wakalipwa na Dubai Ports World Kwa pesa ya huko... Lakini cha ajabu na cha kushangaza mbunge anasema "Kwa kufuata utaratibu wa malipo ya bunge".

Swali kubwa ni hili:
Hivi TPA na DUBAI PORT WORLD ambao ndiyo wanataka washauriwe na bunge juu ya mkataba wao wanawezaje kufadhili safari kama hiyo wabunge kwa jambo lao ambalo wabunge ndio wanapaswa kulipitia waone ni zuri linafaa au baya halifai Kwa maslahi ya taifa?

JIBU NI RAHISI SANA HAPA: Hiyo ni rushwa, wabunge wamehongwa ili wakubali mkataba huu mchafu, mbaya na hatari Kwa nchi yetu...!

Kwa hili, Rais Samia Suluhu Hassan katukosea sana Watanganyika. Aombe radhi na aachane na kitu hiki. Kama amepewa hongo, arudishe vitu vya watu alivyochukua. Watanganyika tumekataa...!

Mbunge wa Nkasi ameviambia vyombo vya habari Mwanasheria mkuu wa Serikali hadi MKATABA wa milele wa bandari ya Tanganyika na waarabu unaletwa bungeni kesho yake hakuwa na taarifa.

"...hilo jambo lililetwa kwa uharaka wa ajabu na nikuhakikishie ndugu WAANDISHI hadi jioni ya kuamkia kesho ya MKATABA ule kuletwa bungeni AG hakuwa na taarifa yeyote!"

Mbunge Aida Khenani.
Siasa za majitaka na kujitafutia umaarufu tu!! Kama ilikuwa hivyo kwa nini hakusema hayo wakati alipata nafasi ya kuchangia bungeni kuhusu huu mkataba?

Alipata nafasi ya kuchangia akaishia kumtetea Mbowe na kuweka clip ya Mbowe tuseme hili halikuwa na umuhimu wa kulisema bungeni wakati ana kinga anapoongea?

Hizi kisheria tunaziita after thought. Anajitafutia umaarufu tu
 
Mkataba huu ni BATILI, FAKE.

Naamini unavunjika kirahisi ikiwa CCCM itaondoshwa madarakani.
 
Mbunge wa Nkasi ameviambia vyombo vya habari Mwanasheria mkuu wa Serikali hadi MKATABA wa milele wa bandari ya Tanganyika na waarabu unaletwa bungeni kesho yake hakuwa na taarifa.

"...hilo jambo lililetwa kwa uharaka wa ajabu na nikuhakikishie ndugu WAANDISHI hadi jioni ya kuamkia kesho ya MKATABA ule kuletwa bungeni AG hakuwa na taarifa yeyote!"

Mbunge Aida Khenani.
Endapo kama hii ni kweli basi Mkataba huu ni BATILI (Null and Void ab initio) kwa sababu Sheria za nchi hii zinataka Mikataba yote ya Kimataifa ambayo Serikali inaingia, ni lazima ipitiwe kwanza ( yaani ifanyiwe Vetting) na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kabla ya kusainiwa.
Aidha, hata mikataba ya ndani ya nchi yenye thamani ya fedha kuanzia Tshs 1 bilioni na zaidi, lazima na yenyewe ipitie kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili ifanyiwe Vetting kabla ya kusainiwa.
 
Siasa za majitaka na kujitafutia umaarufu tu!! Kama ilikuwa hivyo kwa nini hakusema hayo wakati alipata nafasi ya kuchangia bungeni kuhusu huu mkataba?

Alipata nafasi ya kuchangia akaishia kumtetea Mbowe na kuweka clip ya Mbowe tuseme hili halikuwa na umuhimu wa kulisema bungeni wakati ana kinga anapoongea?

Hizi kisheria tunaziita after thought. Anajitafutia umaarufu tu
Alikuwa anaongea kila saa akawa anakatishwa na miongozo isiyo na kichwa wala miguu. Cha kushangaza spika akawa anataka mjadala ufanyike kwa utashi wake na anayelinda nafasi yake.
 
Alisema waziwazi bungeni na alipinga azimio hilo waziwazi tena ndani ya Bunge
 
Alikuwa anaongea kila saa akawa anakatishwa na miongozo isiyo na kichwa wala miguu. Cha kushangaza spika akawa anataka mjadala ufanyike kwa utashi wake na anayelinda nafasi yake.
Kwenye hayo aliyokatishwa akiwa anaongea hakuna sehemu aliposema mwanasheria mkuu hakushirikishwa? Kwa nini tuamini maneno yake saivi?
 
Tupe uthibitisho wa Mwanasheria Mkuu kutoshurikishwa?

Alafu unajua anayewasilisha nyaraka za Serikali za kisheria Bungeni ni nani?
Nami nikuulize aliyepeleka majina ya COVID-19 bungeni ni nani?

Mwanasheria mkuu wa Sirikali na Ofisi ya mwanasheria mkuu wa Sirikali ni vitu viwili tofauti.
 
Back
Top Bottom