Ni kwenye PC yake ya juzi kwa vyombo vya habari alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari..
Your browser is not able to display this video.
Wasio na bundle, hizi hapa πππni baadhi ya quotes za kauli zake
β’ "Haya makubaliano ndiyo mkataba. Kwa jinsi mkataba huu ulivyo haurekebishiki na ukabaki", Tundu Lissu
β’ "Kwa jinsi mkataba huu ulivyo, naamini hakuna mtanzania aliyeandaa mkataba huu. Ni wazi Rais alikubaliana nao huko alikokutana nao huko akawaambia, andaeni mtuletee, akaletewa draft yake na kusaini tu", Tundu Lissu.
β’ "Ukimpelekea mkataba huu au document hii mwanasheria mkuu wa serikali au mwanasheria yeyote makini, kabla ya yote atakuambia, umeliwa". Tundu Lissu..
β’ "Kama Rais au waziri Mbarawa angewapelekea mwanasheria mkuu huko serikalini, lazima wangemwambia 'mh. Waziri, hili hapana, hebu subiri kidogo'..." Tundu Lissu
Ni kwenye PC yake ya juzi kwa vyombo vya habari alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari.. View attachment 2664711
Wasio na bundle, hizi hapa [emoji116][emoji116][emoji116]ni baadhi ya quotes za kauli zake
β’ "Haya makubaliano ndiyo mkataba. Kwa jinsi mkataba huu ulivyo haurekebishiki na ukabaki", Tundu Lissu
β’ "Kwa jinsi mkataba huu ulivyo, naamini hakuna mtanzania aliyeandaa mkataba huu. Ni wazi Rais alikubaliana nao huko alikokutana nao huko akawaambia, andaeni mtuletee, akaletewa draft yake na kusaini tu", Tundu Lissu.
β’ "Ukimpelekea mkataba huu au document hii mwanasheria mkuu wa serikali au mwanasheria yeyote makini, kabla ya yote atakuambia, umeliwa". Tundu Lissu..
β’ "Kama Rais au waziri Mbarawa angewapelekea mwanasheria mkuu huko serikalini, lazima wangemwambia 'mh. Waziri, hili hapana, hebu subiri kidogo'..." Tundu Lissu
Kwa hiyo, njia pekee ya kuuvunja mkataba, wenye "utukufu wa Kikatiba", ni kwa Bunge kurekebisha huo "utukufu wa kikatiba", yaani shera ya kurekebisha "Katiba"?
Na urekebishaji huo ni wakati wowote, na Bunge lolote, siyo lazima liwe hili la CCM.
Hiyo haitoshi.
Hawa wanao ukwasi wa kutosha kuweka jeshi lao pale.
Na kumbuka, miradi hiyo yote itakuwa inawaingizia faida kubwa sana, kiasi kwamba hawa matumbi wenzetu wanaotuuza huko utumwani, ndio litakalokuwa jeshi lao.
Kwa hiyo, tutakuwa tunapambana sisi kwa sisi, huku jamaa wakifaidi matunda.
Ukisikia nchi zenye vurugu, usidhani sisi hatuwezi kuwa miongoni mwa nchi hizo, kwa 'instigation' za watu kama hawa.
Na bado usisahau, Wagner wa Urusi, na 'contractors wa huko Marekani 'blueprint kwa vinchi vidogodogo kama hivi vilivyo na ukwasi mkubwa. hata havijui viutumie wapi ukwasi huo.
Tunacheza na kiberiti mbele ya tanki la mafuta linalovuja hapa!
Bunge, (siyo lazima liwe hili la mafisadi), warekebishe "masharti ya kimkataba yenye utukufu wa kikatiba", kama vile tunavyoweza kurekebisha Katiba yetu.
Tukishafanya hivyo, hatfungwi tena na mkataba wa kitumwa. Wakileta chokochoko, na kuleta u'Wagner' wao hapa, nasi tutawaleta hata kama ni waChina, watusaidie kuikomboa nchi yetu.
Tutakuwa na haki ya kupigania uhuru wetu, kama walivyofanya wengine wote duniani walipokuwa wakidai uhuru wao..
Kwa mfano, Msumbiji, na Afrika Kusini, n.k.
Sitaki kuamini kwanini tusubiri mpaka atakapokuja kiongozi mwingine, au bunge lingine, ndio tuvunje huu mkataba, binafsi nataka huu mkataba uvunjwe na huyu msaliti mwenyewe aliyeuleta.
Hatuwezi kuishi hata mwezi mmoja zaidi mbele tukiwa chini ya huu mkataba, kufanya hivyo ni sawa na kujikubali tumekuwa watumwa wa mwarabu ndani ya nchi yetu, huu ni ujinga na upumbavu mkubwa sana kutokea karne hii.