Mkataba wa Lugumi wapelekwa kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama!

UVCCM TOENI MSIMAMO WENU KUHUSU LUGUMI ISSUE HUWA SIWASIKII KWENYE MAMBO YA MSINGI YANAYOPELEKEA TAIFA KUPATA HASARA MFANO HILI JAMBO
Suala hilo limeshafikishwa mahali husika, hatutatoa tamko kwani mambo ya kijeshi huwa hayajadiliwi hadharani, ni hatari kwa usalama wa nchi. Tuna kazi kubwa ya kujenga nchi na mambo ni mengi ya kuhusu maendeleo, jambo moja tu lisisababishe tuache kazi kubwa ya kutumbua majipu. PAC tunawapongeza kwa kazi nzuri, ila kwa sasa waendelee na hesabu za mashirika mengine kwani hapo watahatarisha usalama wa nchi.
 
hayaaaa kumekucha... hapa sasa ndo nataka nione FUNDI WA MAJIPU AKITUMBUA HILI JIPU UCHUNGU... maana yaonyesha uchungu wa hili jipu wakati linapasuliwa naona hata mpasuaji nae atakuwa anaskia uchungu zaidi lkn afanyeje inabidi tu lipasuliwe litumbuliwe ili maumivu yaishe.
akishindwa kulipasua sasa itabidi dharula itumike atumbuliwe yeye mtumbuaji.
 
unajua mimi kinachonikera sana kwenye serikali ya magufuli ni usanii.Kama kweli magufuli ni mwanaume,akamate madili yote ya kikwete na wengine waliosabisha hii nchi hasara kubwa.
Mimi naamini magufuli anafanya uonevu kwa watu wadogo wadogo,na badala ya kujenga kujituma,uadilifu na patriotism.Lakni tumbua tumbua hii,inawahusu watu wadogo sana,tena wale kutoka mikoa ya kaskazni zaidi na sio sehemu nyingine zozote.
Magufuli,hii vita unayotaka kuanzisha hutaiweza.Ukileta ubaguzi wa ukabila na ukanda hutaifikisha nchi popote.Be a leader and not a commander.Be a change but not a pervert.
tukiacha unafiki mkubwa alionao magufuli,mimi nasupport kwa kiasi kikubwa uwajibikaji na maadili katika sekta za umma,lazima tuwe na uwajibikaji la sivyo hatutafika.
 
....""IPO HAJA YA KUIPITIA MIKATABA YOTE YA JESHI HILO""
.....Inashangaza sana pale chombo cha Bunge kinapodharauliwa!....
 
***
Are you sure on that?
 
***
Are you sure on that?
 
Hoja yako ipo wapi sasa? Kwani ni makosa kwa DCI kuwa mbunge?
Hapana siyo makosa kuwa mbunge ila ni kosa kubwa la kiufundi kushughulikia ufisadi unaomhusu yeye bila kutangaza maslahi. Ajitanzaze kwanza ufisadi unaoletwa mezani kwake unamhusu hata yeye kwa namna moja au nyingine,kwamba wakati yakitokea hayo yeye alikua ofisini kama DCI.
 
Hakuna cha kujificha mbele ya Rais na serikali ya magufuli kwa ujumla tusubiri kila kitu kitakuwa ok.
Serikali zimejengeka kwenye msingi wa unyonyaji, uonevu, upendeleo na hata mauaji kwa kutumia kivuli cha usalama wa taifa.
Jambo hili lilikuwepo,lipo na litaendelea kuwepo.
Mabadiko hufanyika tu pale baadhi ya watawaliwa wanapochukua nafasi za watawala kwa kupitia sanduku la kura au mapinduzi ya nguvu.
Hata hivyo, hali hii haiondoi tabia ya asili ya serikali.
Itakuwa ni kujidanganya kufikiria kuwa serikali ya Magufuli ni ya kipekee itakayoweka kila kitu wazi.
 
Anayo hoja, nwaka huo 2011 mkataba ukiwa unaandikwa jee Adadi alikuwa kesha staafu u DCI?
Watu wanaandika mambo wasiyoyajua ili mradi tu tuwaone humu JF. Adadi Rajabu aliacha kuwa DCI miaka imepita 10 iliyopita na kuwa Balozi nchini Zimbabwe kuanzia mwaka 2008. Baada ya Adadi kustaafu msaidizi wake akachukua nafasi naye anaitwa Robert Manumba ambaye alikua mkurugenzi mpaka mwaka 2013 alipostaafu baaada ya kutimiza miaka 60. Sasa sielewi kitu gani kinamhusisha balozi Adadi na Lugumi wakati yeye alikua balozi huko Zimbabwe mpaka mwaka jana July. Watu wanatakiwa kufanya research kabla ya kuandika utumbo vinginevyo mtaishia kupelekwa katika kanisa la Mtakatifu Kisutu halafu mseme mmeonewa.
 
Hivi ukawa wako wapi.. John mnyika kimya katibu mkuu wa chadema kimya
 
mkuu hebu soma vizuri ile washamba yangu iko kwenye mabano , unajua hata kwenye maofisi ya umma , kama huibi au hupigi michongo ya kupata hela unaitwa fala .
Ujue hapa ni wachache sana wenye kuelewa haya mambo, vitu kama nukta, kiulizo, alama za funga na fungua semi, alama ya mshangao na nyinginezo wengi hawajui zina matumizi gani.
Lile neno "washamba" kwa namna ulivyoliandika watu hawakupaswa kukutolea povu hata kidogo. Nadhani ubadirishe namna ya kucomment kwa kuzingatia uelewa wa watu.
 
huyu jamaa anayeitwa chakaza ameuliza kama adadi alikwisha staafu huo mwaka 2011 , kwa hiyo badala ya kumtisha na mambo ya kisutu ulipaswa tu kujibu kama alivyouliza .
 
Adadi Rajabu ndiye mwenyekiti? Hapo tumeliwa
Huyu Adadi Rajabu akiwa DCI ndio waliokamata ule Mtambo wa kutengeneza Madawa ya Kulevya kwenye Nyumba moja, lakini mpaka leo hakuna ajuaye hatma ya ule mtambo na wahusika wake.
 



NIMEANZA KUIELEWA ILE MICHORO YA JANUARY MAKAMBA MALA MTU KAZUNGUSHIWA MINYORORO MALA NYANI ANARUKIA KILA TAWI RAIA WANAMCHORA TU LILE FUMBO TAMU SANA WA TZ TUMELIWA HAWA NI WALE WALE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…