Mke adai talaka na kugawana mali kwa kumzuia kutoenda msibani Hadi nitakapo rudi, nimemwambia chukua Kila kitu

Mke adai talaka na kugawana mali kwa kumzuia kutoenda msibani Hadi nitakapo rudi, nimemwambia chukua Kila kitu

Just imagine unaishi ww na mke na watotowako pekee mpo Dar es salaa umepata janga kama hilo ni rafiki au jirani gani utamwamini umwachie watoto,katika nyakati hizi.Huyo ndugu naye ni mpaka umuandae aje hapo tayari siku 2-3 zimisha katika hapo ni sawa angamsubiri tu jamaa arudi.

Bado kuna maeneo mwngine kwenda msibani na watoto ni zaidi ya hatari,mfano sisi vijijini kwetu kwenye msiba ndio watu wanawekeana sumu-utaanzaje kuwalinda watoto 3 wote wakati wa msiba.

Sisemi sana but hadi jamaa kufikia hayo maamuzi ya kumwambia mke wake amusibiri kuna factors nyingi kazingatia.

Fact​

 
Kwa upande wangu naona kauli ya mwanamke kusema waachane hapo ameenda mbali sana

Huenda ndio kauli ambayo huitumia mara kwa mara kumtishia mume wake kuwa usipofanya hili au kunifanyia hili basi tutaachana,hapo ameshajua udhaifu wa mumewe kuwa hayupo tayar kuachwa,ndio maana huenda katumia kauli hiyo hiyo,ila this time mume kawa ngangali kamwambia chukua kila kitu na uondoke,ndio maana kwa maelezo ya mtoa mada wife kaanza kujirudi kwa kutuma msg kuomba msamaha kwakuwa ameona mbona leo homeboy amekaza na sio kawaida yake

Au ni jambo ambalo tayar mwanamke ameshadhamiria siku moja kuja kuachana na homeboy kutokana na tofauti zao,lakini kiuhalisia neno kuachana haliwezi kuja kibahati mbaya lina sababu maalumu
 
Lakini unamzuiaje mtu kwenda kuzika bibi yake jamani? Kama kuna arrangement nzuri ya kuacha watoto hakuna sababu ya kumzuia baada ya siku tatu atakuta wameshazika
kwani ikitokea wamezika akiwa hayupo kinabadirika kitu gani au kinapungua kitugani?
 
Mkuu matendo ya mtu ni jinsi alivyolelewa,wazee wetu huko kijijini tulikuwa tunawaona -sasa unapo kutana na utandawazi ambao umewabadilisha wadada tabia ambazo sio kama zile za Mama yetu ndio shida zinapoanzia.

Upo sahihi kabisa,wanaume bado tuntaka kuishi ki uafrika ilihali wenzetu wanawake wanataka kuishi kimagharibi.
Can u clarify this? Maybe with vivid examples.. 🤔
 
Wewe Seran punguza hiyo mioto yako coz umefanya hadi nimekua addicted na hiyo mioto
 
Gentleman,
ukiona mke wako anakuonyesha kiburi hivyo, ujue nyuma ya hicho kiburi kuna mchepuko unakipa nguvu na jeuri zaidi.

In fact,
umetumia surrender tactic vizuri sana gentleman, na umempa ushindi utakaomtikisa kisaikolojia na kujitafakari zaidi juu ya jeuri hiyo ya kulazimisha kwenda kuzika mkoani hali yakua msiba hua hauishi, anaweza kwenda kuhani hata mwaka ujao.

Hivi kweli kufiwa na bibi tu , kunaweza kumsababisha afosi kuiacha nyumba yake na watoto wadogo na kulazimisha kwenda kuzika tu? Hakuna kitu behind the scene kinachomfosi?

No, kuna kitu kingine gentleman ,amepanga kwenda kufanya huko kwa kisingizio cha kwenda kuzika ndio maana analazimisha hivyo.

Na,
Gentleman,
hebu jaribu kama vile nawe unataka kuambatana nae kumsindikiza kwenda huko mkoani mazishini kumzika huyo bibi yake, halafu utagundua kitu, anaweza kuahirisha, kwasababu utakua tayari umeinterfear mipango yake ovu alikua ameikusudia katika ipindi hicho cha msiba.

Pole sana gentleman na hongera kwa ujasiri,
Kumbuka,
wanamke mjinga anaivunja nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe.
Tuishi nao kwa akili 🐒
Tlaatlaah maoni yako yamebeba uhalisia wa jamii ya kwenu manyara maana sio kwa maoni ya kibabe hivo gentleman👀🤣
 
Kwenye milion 10 siamini ila huko juu ndio bado nashangaa waoaji na waolewaji wa siku hizi hekima ni 0 kabisa!!
Hakuna hekima kabisaa mkuu na ndio kinachoangusha ndoa nyingi na ndio maan wengi wao hawapendi /hatupendi kuoa




KATAA NDOA TUPO

KATAA NDOA TUPO

KATAA NDOA TUPO

#TUTAENDELEA KUWEPO👊
 
Taratibu za kisheria zipi ndo maana sijataka kuchukua kitu chochote vyoote avichukue,sitaki usumbufu wa mambo ya mahakamani
malembeka18 umekunywa maji ,kama hujapata just do it alafu ufikirie maamuzi yako kwa makini
Though inaonekana hiyo ndoa inakabiliwa na mgogoro wa muda mrefu sanaa thus why maamuzi yamefanyika haraka sanaa em jaribuni kushirikisha wazee wa busara hata viongozi wako pande zote serikali na dini myamalize kwa amani hakuna mkamilifu gentleman
 
Habar wakuu nima mke na watoto 3Niko safarini kikazi,gafla ikatokea dharura nyumbani mke Wangu kafiwa na bibi yake mkoa mwingine akanitaarifa,nikamsihi asubiri ndani ya siku3 ntakua nimerud ila watoto wawe salama,

Mke akagoma akasema hawezi akasubiria Hadi nije haiwezekani lazma ataenda na kama akasema sitaki basi atakaporudi tuachene na tugawane mali kila mtu aendelee na maisha yake,

Nikamwambia kama umenikaidi amri yangu we chukua Kila kitu safisha nyumba nzima usiacha kitu chochote,chukua hati zote za viwanja usiache hata kimoja nkaenda mbali Zaid nikamuonesha nakadi ya bank ilipo inakiasi Cha pesa kidogo kama 10m nikampa namba ya Siri akatoe nazo aende nazo
Kunyimwa kwenda Msibani sio jambo zuri, lakini kunyimwa kwenda Msibani hadi mtu anasema Bora tuachane inatia wasi wasi kama kweli alikuwa anaenda Msibani Tu au kuna mambo mengine, au hii stori ni ya kutunga au kuna mgogoro mwingine unaendelea ambao wewe hujaeleza hapa.
 
Ukiachwa na hilo tatizo lako la nguvu za kiume ndiyo basi tena!!😀😀 Komaa tu na hicho kimeo chako kinachokustiri.
 
Back
Top Bottom