Mke aliomba talaka tugawane Mali, nilichomfanyia hajawahi kurudia tena

Mke aliomba talaka tugawane Mali, nilichomfanyia hajawahi kurudia tena

MZOZO UKAENDELEA,
watu wakinisihi tuyamalize pembeni Hapa mjini tunawafaidisha Watu, nikawambia Sina MDA wa kupoteza kwenda mahakamani
Na Hilo pagale analodai tugawane Kama Kuna mtu anapesa Hapa aseme naliuza cash pesa yote mpeni huyu Mwanamke akaanze maisha yake. Kama hamna Basi niitieni dalali liuzwe leo leo silazi damu Mimi. Watu wakamsihi wife ashuke pale aombe radhi anadhalilika yeye. Wife akaanza kujishusha nimsamehe Lile neno lilimponyoka TU bahat mbaya. Nikasema maamuz yangu Ni hayo hayo. Sirudi nyuma. Kazi iendelee.

Hatujakaa Sana,
CANTER tupu ikaingia, nikawaambia vijana wapande twende nyumbani nako tukapakie kila kitu vitu vya ndani navyo vipelekwe magomeni. Vijana wakasema utatuongezea hela, nkwambia hamna shida ntawaongezea. Vijana wakapanda, CANTER ikang'oa tukaelekea nyumbani. Tulipofika hatukua na muda wa kupoteza vijana wakaingia ndani haraka na kuanza kusomba vitu kuingiza kwny Gari.

Ghafla wife na baadhi ya wafanyabiashara wenzangu wakafika pale nyumbani kunisihi niache vile nilikua nakifanya, namdhalilisha wife.
Wife akawa analia na kuwazui vijana wasitoe vitu kwenye Gari. Vijana wanaingiza, kwny Gari wife anatoa anarudisha ndani. Vijana wanamsukuma pembeni kua wao wako kazini asiwaingilie.

Mzozo ukawa mzozo majirani mtaani pale wakajaa, nikawaambia pale,
"Wote Mmemuona uyu shemej yenu, tumegombana tu anasema tugawane mali. Sasa Mimi Sina MDA mchafu wa kwenda kukaa mahakamani kupotezea ili kugawana mali,Nampa kila kitu Hadi kijiko nisikione ndani kwangu, Leo rasmi naanza upya. Kule dukan, fuso tayar lishapakia mzigo wote wa Dukani linaelekea kwao magomeni Kwenda Kufungua duka ukweni.Na Hapa Hii canter mnayoiona itasomba mzigo wote wa vitu vya ndani na kuelekea kwao kule kule magomeni. Kwaiyo Nataka Akafungua duka lake magomeni na akaanze yake maisha mapya magomeni. Sina Muda mchafu wa kugawana Mali na mwanamke Mimi" wote wakabaki na mshangao.

Hatukukawia Sana mwenyekiti wa mtaa akafika na kunisihi tukayaongee ofsn ya mtaa, nikamwambia mzee nakuheshimu Sana Ila tutayaongea tayari nishampatia huyu mwanamke anachokitaka. Hapa niache tu nimalizie hili zoezi langu afu ntakuja uko ofsin tuyaongee.

Mwenyekiti akaanza kuniletea habar za kuniitia polisi nakaidi agizo lake. Basi nae mwenyekiti Tukajibizana mbovu sana, ugomvi karibu uibuke nimchape ngumi maana alianza kuminyooshe vidole. Baadhi ya Watu wakaamulia na kumtoa mwenyekiti eneo Lile akaondoka.

Wife akazidi kububujikwa na machozi anaomba yaishe, kelele zile Ikawa Kama nmeufunga mtaa sasa maana zilikua kelele kibao Sana pale. Sijakaa sawa nikaona ile fuso yenye mzigo wa duka inarudi na kusimama pale nyumbani. Kwenye fuso anatoka kijana wa dukani na baba mkwe. Sijakaa sawa taxi nyeupe nayo inafika iko na wale shangazi zake na wife wale walionitukana sana kipindi kile.

Baba mkwe kanifata na kuniomba radhi yaishe, chonde chonde nitulize jazba. Nikamwambia mzee kua unawaona hawa walokuja na taxi, walionitukana Sana nilivokuja ukweni kusuluhiahwa. Wakanitusi sifai na kusema niwarudishie binti yenu,Sina msimamo,mzee wa kusemelea nna kiherehere , najipendekeza kwenye ukoo wenu, binti yenu mzuri sana na matusi mengine lukuki.

Sasa mzee wangu nmeamua kutimiza haja yenu,nmemuacha rasmi binti yako na kila kitu hapa nampa Kama unavoona ili akaishi kwa amani. Tena nampa mbele ya umati huu mtaa mzima unashuhudia Ili mbeleni uko Asije Sema nimemtelekeza, mimi ni katili Sana Kama shangaz zake walivodai.

Umati wote ule ukawageukia wale shangaz zake na mzee wao waliulizia ilikuaje. Ikabd kuwasimulia matus yote na kejeli zote nilizotukanwa ukweli siku ile nilipofata suluhu.
Umati ule ukawa unawashangaa na kuwanyooshea vidole wale wakwe zangu, inakuaje mkwe wao anakuja wayazungumze kistaarabu mnamtukana matusi, kinachotokea Hapa mkwe wenu msimlaumu, mmeyataka weyewe na mmejidhalilisha Kama familia.

Baba mkwe akasema chonde chonde yeye hakuepo siku ya matusi, nisimjumlishe tuyaongee. nikamwambia mzee Mimi hatuwez kuongea chochote km nawaona Hawa hapa walonitusi matusi ya nguoni mbele yangu. Ikabd waambiwe warud kwnyw Taxi yao na kuondoka eneo Lile. Maana Hali ya hewa ishachafuka.

Wife akabaki analia machozi Hadi kamasi,kapiga magoti mbele ya umati kumuomba baba ake msamaha kakosea yaishe. Baba ake kwambia hajamkosea yeye kaniskosea Mimi.
Kaja anatambaa anaomba msamaha yaishe nnachofanya namdhalilisha yeye na familia yake pale. Amekiri makosa yake yote tuanze upya. Nikasema HAPANA Hapa mpk kieleweke.

[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
Mbona unarudia mkuu

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Na walivyo wapumbavu! Mf huyo nilie muelezea alikua analima mahindi, mihogo, bustani za mbogamboga, alikua anafuga kuku wa kutosha, hamna alipo kua analipia ama kulipa kodi na walio kuja kumvunjia nyumba yake hamna mwenye muelekeo na mmoja nilisha wahi msaidia kumpangia chumba mwaka mzima na nikampa na kazi flani kwny ofisi niliyokua nimemfungulia dada ake ili wasaidiane
Dah! Kuna watu ukiwabeba ni Kama gunia la misumari, hawabebeki kabisa yaan[emoji26]
 
Nimejifunza mengi sana kuhusu ndoa ..ila jamaa una uvumilivu sana mimi nisingeweza kwa kweli tusingerudiana
 
Nimejifunza mengi sana kuhusu ndoa ..ila jamaa una uvumilivu sana mimi nisingeweza kwa kweli tusingerudiana
Binfs pia nisingeweza,
I'll mzee alinihakikishia keshajirudi,
Anaamini funzo alilopata wife atakua MKE bora
 
Kabisa mkuu,
Wanatia huruma washakuingiza hasara sana, fikiria mwanamke anatoa pesa anampa Kaka ake na anajua Kuna rejesho benki na Hana wasiwasi kabisa.[emoji26]
So strange bro inashangaza sana yani
 
Huwa napenda Sana kusoma comments zako, zimejawa na Maneno ya ukweli bill unafiki.

Huwa ufichi Wala kujivunga dada angu.

Mungu akupe maisha marefu Sana jf,hasa mmu. Nikisomaga comments zako huwa kuna namna flan mwili want lazima usisimke maana Maneno unayaondika yanagusa Moja kwa moja.

Pa kujitafakari, najikuta nmejitafakari
Pa kueimisha,najikuta nmeelimika.

Wee Ni mfano Bora wa wanawake wanaojitambua Sana hapa jf.

Kongole Sana mkuu Juandeglo
Asante sana sana sana lakin hizi sifa naomba tumrudishie Mungu wetu muumba wa mbingu na nchi. Kwa hakika miaka mitano nyuma sikuwa huyu. Nilikua mtu nisiyeeleweka pengine mtu mmoja gaidi sana mwenye roho iliojaa hila. Lakin kuna neema yake Bwana ikanitafuta, ikanipata. Namshukuru huyu Baba yetu wa mbinguni.

Lakini pia sisi bado ni wanafunzi tu. Kuna mengi najifunza sana JF na nakiri JF inanisaidia kubadilika sana mtazamo nikirelate my faith na some lessons ninazokutana nazo. Thanks for the heartfelt prayers...one love🙂
 
Kuoa familia yenye hali ya chini kuna changamoto zake.... Wifi yetu alitaka kusaidia familia yao wapate mafanikio ya haraka bila kujali familia yake.......

Mashangazi nao waliingia kiswahili kupambana na wewe wakidhani ungewaogopa kumbe ndo wanaharibu....

Baba mkwe katumia busara kubwa na hekima ambazo ndo wazazi wengi wanapaswa kuwa hivyo...

Mama yako pamoja na bifu zao za nyuma lkn alijirudi na kuanza kuwasupport...

Baba yako mzazi ndo kawabeba hapo...nilikuwa nasoma nikiwaza huyu mzee alikuwa mgonjwa,ila ilipofika pale kwenye kutoa vitu vya ndani akatokea,nikashusha pumzi... Huyu kamaliza kila kitu....

Tumalizie kwako, ulichukua maamuzi ya juu kabisa,hukutaka kupita kutafuta ushauri ila ni jambo jema lililo kupa heshima....hawatarudi tena kukuchezea...sio mashemeji wala shangazi.........

Hongera nimejifunza mengi
 
Back
Top Bottom