Mke aliomba talaka tugawane Mali, nilichomfanyia hajawahi kurudia tena

Mke aliomba talaka tugawane Mali, nilichomfanyia hajawahi kurudia tena

Lakini pia braza DeepPond leo umejua kunishangaza. Leo nimekuona kwa namna ya tofauti sana. Hakika you are so true and real. Naamini ndoa yako ni ndoa flani kubwa sana na ina miaka mingi ahead.

Mmepita kwenye moto lakin mmetoka mnang'aa. Heko kwa baba zenu wote, hakika mmepata good parents wenye hekima na busara sana. Nimejifunza mengi sana kama mwanamke katika hiki kisa na natamani pale penye wrongs mimi nikawe right thou naweza nikawa nina yangu mabaya pia.

Nilichoona hapa na nadhan ndo kilichopo, wanawake weng tunapenda kuonekana victims, sisi ndo tunakosewa, sisi ndo tunatendewa ubaya, sisi ndo tunafanyiwa visa..lakin kumbe chimbuko kubwa la tatizo ni sisi.

Nimeona uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,husuda na ulafi wa mali. Haya yote ni matendo ya mwili ambayo yamepelekea uwepo wa Mungu atupaye hekima kuondoka. Utasoma zaid ktk Gal 5: 20-23.

Laiti kama kungekuwa na matunda ya Roho hapa..basi haya mambo yangepungua kama sio kutokuwepo. Upendo, Furaha, Amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi.. naamini hii shida ingekuwa solved mapema sana. Kuna mmoja alikosa uaminifu kumpelekea mwingine kupata hasira. No tunda la Roho, tendo la mwili likaingia na kupata nafasi kubwa. Ndo maana tunatakiwa tuisulubishe miili yetu sana pamoja na tamaa zake..kama tukiishi kwa Roho na tuenende kwa Roho. Life in Christ is better for me,and for you too.. nahisigi ningeshachizikaga kitambo au kuwa zaidi ya mama.G. We need God in our marriages and our families.
Huwa napenda Sana kusoma comments zako, zimejawa na Maneno ya ukweli bill unafiki.

Huwa ufichi Wala kujivunga dada angu.

Mungu akupe maisha marefu Sana jf,hasa mmu. Nikisomaga comments zako huwa kuna namna flan mwili want lazima usisimke maana Maneno unayaondika yanagusa Moja kwa moja.

Pa kujitafakari, najikuta nmejitafakari
Pa kueimisha,najikuta nmeelimika.

Wee Ni mfano Bora wa wanawake wanaojitambua Sana hapa jf.

Kongole Sana mkuu Juandeglo
 
IKAFIKA KIPINDI
Akawa anakuja dukan anakaa chini na mtoto mgongoni kibarazani analia anaomba msamaha sn nimsamehe sn kwa yote aliyonikosea. Anaahidi atajirekebisha Ni shetani alimpitia.simjibu chochote akichoka kuomba msamaha anaondoka zake.

Kuna siku kashinda dukan asbh mpk saa 11 jioni na mtoto mgongoni anabembeleza. Mpk nafunga anabembeleza anabubujikwa na machozi, nilivofunga nikaenda nyumbani. Usiku kaja, kakuta geti halijafungwa kasukuma kaingia ndani na kwenda dirishan kwangu chumban analia anabembeleza nimsamehe. Nikamkaushia.

Kaenda Hadi dirisha la bi.mkubwa analia kakosa anaomba asamehewe.
Bi mkubwa nae akakausha Ila alivoondoka nikashangaa na asivompenda huruma ikamuingia nae akawa ananisihi nimsamehe turudiane. Nikamwambia bi.mkubwa achana nae uyo,hafai.

Tumeenda ukimya juu ya ukimya,
Wife akadili na mzee, kumbe akawa Anaenda kuomba msamaha ofsin kwa mzee. Mzee alipoona imekua kero akaniita na kunambia uyu mwanamke kila Mara anakwenda ofsn kwake kumuomba msamaha na anadai shangaz zake ndo waliomponza anajutia kilichotokea. Naonaje suala la kumsamehe. Nikasema mzee Mimi simtaki tena. Mzee akasema sawa Kama nmeamua hivyo. Ikaisha.

Baada ya miez 3 tangu Lile vurugu. naendelea na shughuli zangu nishaanza msahau wife, mzee akanambia jumapili tutakua na kikao Cha familia saa 10 mchana usichelewe kurudi uwepo. Nikasema sawa. Nikajua yatakua mambo ya familia yetu tu. Kweli Nmefika nyumbani mapema.

Gafla Niko chumban bi mkubwa kaja nigongea kua MDA tayar nije seblen.
Ile Natoka nafika seblen,nawaona wale shangazi zake wameketi, ikanibidi kurudi zangu chumbani na kukaa kitandani nikajiinamia kwa uchungu. Ikawa Kama wamenitonesha upya kile kidonda .

Mzee kaja kaniinua na kunambia twende seblen kila kitu kitakua sawa.
Kweli nmeinuka kinyonge nmeenda seblen nmekaa na mzee kochi Moja kubwa la Watu watatu.

Gafla shangaz Yao mmoja aliekua na mdomo akaja niangukia chonde chonde nimsamehe kwa yaliyopita.
Mzee akaniangalia usoni, nikaona mzee kama anatuma ujumbe kua anajiskia viby jins mmama yule mtu mzima anavolia. Wale wengine wakawa wanasema samahani yaishe yaishe. Babamkwe nae akasema imefkia mahali wife mpk anataka kujiua nyumbani kwao, alishameza hadi vidonge Mara mbili kajifungia chumbani anataka kujiua yye na mtoto. Wakavunja mlango kumnusuru.

Kama familia wanaomba radhi, wametukosea Sana, wanaomba radhi Sana. Anawasiwasi wanakoelekea atampoteza binti Yake na mjukuu wake, binti yake anazurula kila siku mjini na mtoto mgongoni anasema anaaga kaja kuomba msamaha na hasamehewi na kichwa chake kishachanganyikiwa sahv kilivyo tusije kushangaa kagongwa na Gari yeye na mtoto wote wamefariki. Mzee kaniangalia usoni.

Sijakaa sawa, kumbe wife alijificha jikoni nae kaja analia Hadi kamasi macho yamevimba na mtoto wake mgongoni kaniinamia anaomba msamaha. Mzee kaniangalia Tena usoni Tena na kunipa ishara ya nimsamehe. Nikatikisa kichwa kukubali.

Mzee kamuinua wife na kumkalisha kushoto kwake, Mimi kulia kwake.
Akasema kua Hawa wote Ni wanangu. Nyie wote nendeni kila kitu kitakua sawa. Basi wageni wale wakatawanyika.

Tukabaki familia yetu, wife na mtt. nikawa ndani ya siku 2 simuongeleshi.
Bi mkubwa akanisihi yaishe niongee na mzazi mwenzangu, mzee nae akanisihi yaishe bhana. Basi siku ya 3 wife kaja chumbn kwangu kavaa kimitego analia anaomba msamaha.
Kwasababu moyoni nishamsamhe na nilivommiss siku nyng sijapiga show.
Basi ugomvi wetu ukaishia pale.

Baada ya wiki pale home,
Mzee akatutaftia nyumba nyingine kubwa zaidi na kutupangishia kua tukakae uko pale kwa wapangaji tuhame. Alivotupeleka kule tunakutana na vile vitu vyetu tulivosomba na canter vipo vimerundikwa TU sebleni. Wife akaanza kuvipanga upya na maisha yakarejea Kama zamani.

TANGU HAPO miaka mingi imepita na WIFE HAJAWAI TENA KUTAMKA KAULI ILE YA TUGAWANE MALI.

Na pia,
Tangu ugomvi huo alirudi kua mama wa nyumbani na Hadi leo hii nnapoleta Uzi huu hajawai tena kuuza duka langu lolote.

Pia,
Nilikata mguu kabisa na magomeni kule kwa mashangazi waswahili wale.
Japo wanadai ugomvi ulishaisha ila nmekua karibu na ndugu wa wife kule upande wa mama ake na upande wa baba ake, Maelewano mazur Nmebaki na baba mkwe wangu TU. wengine ni salamu TU,kila mtu kivyake.

Nihitimishe kwamba
kile kipind kilipita na kilikua Cha mafunzo sn kwetu kutukomaza na Siwez kumhukumu sn wife maana umri wake ulkua bado mdogo sn, afu mazingira ya uswahili alikokulia kwa mashangazi wale yalimharibu.
Nashkuru upande wa mama ake walinisaidia sn kumshape wife akatulia akawa mcha mungu na MKE mzur Sana.[emoji1431]

Kwasasa
MKE wangu kiumri na kitabia amekua sana. Naweza kusema Ni MKE bora kabisa maishani, naeweza kukaa mbele ya Wanaume wenzangu waliooa nami nakajivunia kua Nmeoa mke bora kabisa na pure wife material mama wa watoto wangu[emoji4]

Na huwa nawaza Sijui ningekaza ningempoteza kipind kile sijui ingekuaje maisha yangu, maana kila nnakogusa Ni chenga tupu. Michepuko wote nilonao, vichwa maji tupu, mamaJ inclusive.

KINGINE,
Najivunia Sana baba mkwe wangu nilie nae, Ni mkwe asiyependa mambo ya kipuuzi kabisa na alisaisaidia Sana kumshape wife miaka 5 ya changamoto ya ndoa yangu.[emoji1431]

SIKU NIKITULIA NTASHUSHA TENA KISA kingine KILICHONIFANYA NIJIVUNIE HUYU BABA MKWE WANGU KATIKA KUMNYOOSHA WIFE WANGU[emoji4]

ASANTENI SANA WAKUU[emoji1431]
#######mwisho######

NB:
Kuna la kujifunza Hapa wakuu
Uzi huu nmeuleta baada ya kuguswa na Uzi wa mdau mmoja mwenye kisa Kama changu, ugomvi wa kibiashara na mkewe, Kisha mkewe akadai talaka wagawane Mali.

NAWASILISHA[emoji1431]
Da! Huu UZI Nauita UziHalisi wa Nyakati na Mapito ya Ndoa katika Maisha. Uzi unaelimisha, unaburudisha, unakumbusha. Ila Mwamba ulikomaa kinoma. Wewe ni jabali ujue. Ulitia hishma. Mpongeze sana Baba yako Mzazi na Baba Mkwe. Wana busara sana. Nawatakia kila lenye heri katika Nyumba yenu.
 
.

Laiti kama kungekuwa na matunda ya Roho hapa..basi haya mambo yangepungua kama sio kutokuwepo. Upendo, Furaha, Amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi.. naamini hii shida ingekuwa solved mapema sana. Kuna mmoja alikosa uaminifu kumpelekea mwingine kupata hasira. No tunda la Roho, tendo la mwili likaingia na kupata nafasi kubwa. Ndo maana tunatakiwa tuisulubishe miili yetu sana pamoja na tamaa zake..kama tukiishi kwa Roho na tuenende kwa Roho. Life in Christ is better for me,and for you too.. nahisigi ningeshachizikaga kitambo au kuwa zaidi ya mama.G. We need God in our marriages and our families.

Maneno mazur Sana haya[emoji3516],
Unafaa kua mshaur mzur wa ndoa[emoji106]
 
Da! Huu UZI Nauita UziHalisi wa Nyakati na Mapito ya Ndoa katika Maisha. Uzi unaelimisha, unaburudisha, unakumbusha. Ila Mwamba ulikomaa kinoma. Wewe ni jabali ujue. Ulitia hishma. Mpongeze sana Baba yako Mzazi na Baba Mkwe. Wana busara sana. Nawatakia kila lenye heri katika Nyumba yenu.
Shukran Sana mkuu,
Namshkuru mungu nmepata mzee Safi na baab mkwe Safi. Tunaelewana Sana[emoji4]
 
Nianze kucomment hapa..nimejisikia vibaya sana kama mwanamke. Kuna muda tunaaminika af kumbe tunakuwa wase*** tu. Pia nimejifunza mwanamke ili uwe productive unatakiwa uwe na akili mingi sana. Na wisdom pia.

Hapa umeongea kitu muhimu Sana wanawake wengi wanapuuza.

Ujue mnapoolewa Kuna Watu nyuma hutukutumia Kama daraja kufanikisha mipango Yao binafs bila kuja usalama was ndoa yako.

Wanakuingiza unaanza kiburi na kuihujumu ndoa yako afu ukiingia matatizoni wanajiweka pembeni.

Wanawake mnapaswa kutumia akili Sana, na wisdom iwepo kubalance uku na huku.
 
tukio lako ni kama la bro. wangu mwanzoni nilishangaa ila badae nimekuja kuelewa

kwa ufupi bro na mke wake waliachana baada ya mke kumtuhumu bro kutoka nje.
mke akarudi kwao bro akagoma kumfata baada ya miezi 4 mke wake kaja na kenta 2 kubeba kila kitu

kilicho nishangaza ni bro kutoa hela ya kubeba mizigo yote na kukubali vyote kuchukuliwa

kwa hasira alienda vunja kibubu na kununua vitu vipya ndani ya siku 2, majirani wakampigia mkewe kumuuliza kama karudi maana wanaona vitu vinaingia

mke karudi kushuhudia na kuomba msamaha hadi leo n mwaka wa 5 hawako pamoja.

bro aligoma kumsamehe
Ha ha ha...
Kwa akili ya MKE alijua jamaa ndo kwisha habar yake atakuja anatambaa ukweni kuomba kurudishiwa vitu vya ndani[emoji1787]
 
Ila wanawake ni kama wamezaliwa na ujinga wa asili hivi

Ni nadra sana kumkuta mwanamke anawaza hata miaka 2 mbele.

Miaka 3 nyuma,wife kuna kipindi wakati naanza maisha nilisema nimshirikishe mke wangu kwenye mipango

Basi nikawa napiga deal mixer kazi kwa mwezi Nampa 700k mara M.1 sometimes 650k..

Hapo achana na budget ya emergency ambayo Kila mwezi nilikuwa naweka 250k.

Sasa siku nayopewa termination of contract najua kabisa emergency funds Nina km 5.8M huku kwingine najua nina kama 14M.

Nikajisemea hapa sitaki tena Ajira nitaendelea na mishe zangu, Sasa namwambia wife mkataba wangu umeisha hautaongezwa zilete zile hela tufanye mahesabu tujue tunaanza wapi..

Nashangaa mtu anatoa machozi, mimi moja kwa moja nikajua mke wangu kaumia kusikia Sina Kazi nikaanza kubembeleza mbona akiba tunayo na kazi zipo nyingi sana kwenye fani yangu!!Ni vile tu mi sina mpango wa kuajiriwa baada ya mda nikamwambia lete hela tufanye mahesabu akaenda kuchukua kama 650k kaweka kitandani,mi nikamwambia lete zote akasema ndo hizo zimebaki....

Kumbuka mi najua nina 20M. Kasoro hivi aisee hasira zilinipanda ghafla pumzi ikawa inakaba km nataka kupata presha hivi aiseeee pembeni kulikuwa na kastuli flani hivi napendaga kuwekea simu usiku nikiwa nalala, kuna roho iliniingia ya kikatili nilitamani nishike kistuli nimbamize nacho Cha kichwa bahati nzuri niligeuka kumuangalia sura yake na mke wangu ana sura ya kipole sanaaa na kamwili kake kalivyo kadogo plus mimi nishawahi kufanya mazoezi makali ya boxing nikisema nipige liver shot moja naweza hata kuua...

Nikatoka nikaenda kukaa sebuleni kwanza nawaza si ningemuumiza sana!!hivi presha ndo inashika vile!nilijiogopa sana kwakweli.Sijawahi kumpiga toka tumeanza mahusiano ila nikapata picha kwanini wanaume wanapigaga wake zao tena bora mwenye mkono wa kupiga makofi maana atakuwa anapiga kdg kdg,mimi niliwazA kumuumiza yaani ukimuona unasema eee huyu mwanaume kweli katili..nilijiogopa sana kwakweli.

Siku 3 sijui nifanye nini kusema popote naona aibu siwezi mwambia mama yangu siwezi kusema kwao siwezi mwambia rafiki yangu yaani nimekaa nalo moyoni natoka naenda kushinda Bar nikifika tu mlango wa nyumbani hasira zinawaka moto ,kazi sina akiba yangu ya mambo yangu ilikuwa ni 3.5M plus 650k tu Hela yote ndo wife kawapa ndugu zake wafungue biashara, nyingine kajenga choo Cha baba yake nyingine kanunua mavitu Yao ya kike.

Niliumia sana sanaaaaaa kilichokuwa kinaniuma ni mwanamke ambaye nimeoa aje anisaidie maisha ndo anakuja nishusha,mwanamke ninayemshirikisha kila kitu ndo anakuja kuwa adui yangu,nimemaliza mkataba na ndo hapo hapo napokea taarifa km hiyo.Sina mtu wa kumshirikisha kitu maana wakumshirikisha ndo huyo kazingua.

Mda wote nawaza ukatili tu sasa kimtu chenyewe hataukipiga kofi vzr kinazima.Nssf nilikuwa na 27M.pssf nilikuwa na 11M.Nikasema nianze kule kwanza.

Changamoto nilikuwa nayo kipindi kile ni nawezaje kukaa nae chini kupanga nae maisha mwanamke wa namna hii na je maisha nitapanga na nani? Nawezaje kumfungulia Biashara mwanamke wa namna hii??Nani nitaongea nae stress zangu za maisha?Nani atanifariji pale Mambo yakuwa yakienda mrama?Nani anayenionea huruma kama sio mke wangu?Kifupi alinitisha sana sababu niliamini nipo salama halafu nikagundua nahitaji kuwa makini maana sio kweli kwamba nipo salama.

Huyu mwanamke sijawahi kuprove kunisaliti na ana heshima kiasi chake nadhani hapo ndo alipoponea,mi nilikuwa willing kuvunja ndoa ila hivyo vitu viwili ndo deal breaker kwangu basi nikapata mafao nikaweka sehemu kazaa nikawa naingiza 3M. Per month Maisha yakarudi sawa.

Sijawahi kumwambia ila Nikampa adhabu kuu mbili sitakaa nikufungulie biashara,sitakaa na wewe kujadili maendeleo ya familia,tupige story tucheke tule tulale ila my next move itakuwa siri yangu siku zote...

Kiukweli hili jambo lilinifanye nisiwazingatie kabisa wanawake, Mungu aliposema tuishi nao kwa akili alijua kabisa hawa watu hajawapa akili ya utambuzi,Sasa km mwanaume nae huna akili basi familia inakosa mwenye akili...
Dah! Inaumiza Sana

Mi nilichojifunza wanamke ASILIMIA Kubwa wanajisahau sn kwny maswala ya pesa, Ni Kama wtot kila kukicha wakumbushwe. Lazima usimamie bampa-bampa

Kwanza Akiwa na pesa atataka shoga zake wajue.Afu wakishua hapo ndo wataanza kummwagia upupu na kumshaur UPUUZI.

Usiposimma imara kuvunja ile connection,
Matokeo Yake anakuja kutia huruma tayar keshakurudisha nyuma mno.

Story yako imenigusa mno,pole sn mkuu[emoji26]
 
Da! Huu UZI Nauita UziHalisi wa Nyakati na Mapito ya Ndoa katika Maisha. Uzi unaelimisha, unaburudisha, unakumbusha. Ila Mwamba ulikomaa kinoma. Wewe ni jabali ujue. Ulitia hishma. Mpongeze sana Baba yako Mzazi na Baba Mkwe. Wana busara sana. Nawatakia kila lenye heri katika Nyumba yenu.
Hiki tukio liliniheshimisha sana kule ukweni
Nowdays Hata nikikutana nao wale shangazi au kuja kwangu adabu ipo,

Wanajua lazima wakitaka kutamka neno, itabd wajitafakari maana wanajua sitolaza damu, wakizingua tunazinguana bila kupepesa.
 
Huyu kenge amenidhurumu usingizi wangu😂😂😂nimeshindwa kulala mpaka nimemaliza kusoma kila neno na kila nukta, hata kama ni stori tu ila ina elimu ya kutosha, stori kama hii ilimshatokea jirani yetu live kabisa japo hapo mazingira ni tofauti kwani hiyo ni Dar but hii ilikuwa mkoani huko mpakani mwa M7. Mpaka nikahisi yawezekana hii stori anaesimulia na mtoto mkubwa ambapo wazazi wake ndo walioathirika na hilo baada ya baba yao kufumaniwa na mkewe na mkewe akaona ni heri waachane.

Sema wife yeye aliamua kujigawia mali zote za nyumbani na dukani pamoja na watoto na kuzipeleka kwao.
Mume anarudi toka ugonini (Uganda)anakuta nyumba tupu,nmaduka tupu hakuna cha mtoto wala mama. Mzee akaamua kutulia ili aanze maisha mapya.

Kizaazaa kule ukweni ndo kilileta balaa baada ya babamkwe kukataa kupokea mali alizokuja nazo bintie na ulikuwa msimu wa mvua, fuso zimeshusha mzigo uwanjani kwa mzee (babamkwe)ni kunyeshenyewa mvua kwa kwenda mbele. Sema mzee akatumia busara ya bintie kuingia na wanae ndani kiubinadamu.

Baba akawa na msimamo kwa bintie kurudisha vitu vya watu na watoto kwamba kama maisha yamemshinda arudi kwake kama alivyoondoka.

Kule home jamaa nae akagoma kuifata familia na mali zake. Wakatuma wazee, viongozi wa dini na Serikali kumwombea msamaha mkewe, mwamba anawambia yeye amemsamehe mke wake ila akitaka kurudi kwake aje mwenyewe na watoto tu bila mali kusudi waanze upya kutafuta upya.

Anyway mimi sio good writter ila hiyo ndoa haijawahi kuvunjika tena hadi leo ni wazee sasa kipindi hicho nipo 15yrs sasa nina 45yrs na kijana wake alikuwa rika langu Nadhan kwa sasa yupo 43yrs. Ndo hii imenikumbusha mbali. Kuna baba mkwe wengine Mungu amewajalia hekima na busara😂😂😂😂😂😂😂😂
Aisee
 
Ha ha ha....wee jamaa ulimfanyia vituko vya ajabu lazima Kama alikua na wazo la ulozi ajitafakari upya[emoji1787]
Wanatibuaga akili hawa watu sijui hua wanakuaje! Kwa experience yangu hawa watu hua wanapotezana kwenye ushauri na wakisha yakanyagaga wale washauri hua wanapotea kabisa machoni pake na kumuachia msala yeye mwenyewe
 
Wanatibuaga akili hawa watu sijui hua wanakuaje! Kwa experience yangu hawa watu hua wanapotezana kwenye ushauri na wakisha yakanyagaga wale washauri hua wanapotea kabisa machoni pake na kumuachia msala yeye mwenyewe
Sahii kabisa,
Wapambe nuks hawafai
Lengo lao mwenzao aharibikiwe roho zao zifurahi. Sijui kwann wanawake hawapendagi mema.
 
Kabisa mkuu,
Wanatia huruma washakuingiza hasara sana, fikiria mwanamke anatoa pesa anampa Kaka ake na anajua Kuna rejesho benki na Hana wasiwasi kabisa.[emoji26]
Mm imefika pahala sasa hivi nikiwa na mwanamke hata awe bibi kizee hua namchukulia kama mtoto wangu wa kwanza wakike, kinacho tuponza ni kuwachukulia ni watu wazima wenzetu wenye akili sawa na sisi kua ukimuelekeza jambo ataelewa kumbe wao hua wanasikia ila kwenye kuelewa ndio ishu na bahati mbaya badala akuulize wewe ulie mueleza yeye anaenda kuuliza kwingine na hapo ndipo ma file yanapo gongana! Hao shangazi ndio walio mshauri kumfungulia duka kaka mtu kama kukulipa kisasi kwa kitendo cha kumuweka ndani
 
Marafiki,ndugu wasiojielewa na mashosti Ni sumu ya ndoa kabisa, hasa ndoa changa.
Na walivyo wapumbavu! Mf huyo nilie muelezea alikua analima mahindi, mihogo, bustani za mbogamboga, alikua anafuga kuku wa kutosha, hamna alipo kua analipia ama kulipa kodi na walio kuja kumvunjia nyumba yake hamna mwenye muelekeo na mmoja nilisha wahi msaidia kumpangia chumba mwaka mzima na nikampa na kazi flani kwny ofisi niliyokua nimemfungulia dada ake ili wasaidiane
 
Dah! Inaumiza Sana

Mi nilichojifunza wanamke ASILIMIA Kubwa wanajisahau sn kwny maswala ya pesa, Ni Kama wtot kila kukicha wakumbushwe. Lazima usimamie bampa-bampa

Kwanza Akiwa na pesa atataka shoga zake wajue.Afu wakishua hapo ndo wataanza kummwagia upupu na kumshaur UPUUZI.

Usiposimma imara kuvunja ile connection,
Matokeo Yake anakuja kutia huruma tayar keshakurudisha nyuma mno.

Story yako imenigusa mno,pole sn mkuu[emoji26]
Asante mzee baba

Ndo hivyo aisee tuishi nao hivyo hivyo kwa kupuuza Mambo maana tukisema tuwe serious nao

Mbona mwanamke hata mwaka huwezi kuishi nae unafukuza
 
Mm imefika pahala sasa hivi nikiwa na mwanamke hata awe bibi kizee hua namchukulia kama mtoto wangu wa kwanza wakike, kinacho tuponza ni kuwachukulia ni watu wazima wenzetu wenye akili sawa na sisi kua ukimuelekeza jambo ataelewa kumbe wao hua wanasikia ila kwenye kuelewa ndio ishu na bahati mbaya badala akuulize wewe ulie mueleza yeye anaenda kuuliza kwingine na hapo ndipo ma file yanapo gongana! Hao shangazi ndio walio mshauri kumfungulia duka kaka mtu kama kukulipa kisasi kwa kitendo cha kumuweka ndani
Walikua wapuuzi Sana,
Wife kwnyw maswala ya duka tangu hapo sijawai kumuamini tena,kabaki mama wa nyumbani.

Yule kijana wa Oda ninae mpk Leo tukakimbiza faranga Hapa Hapa mjini,
Keshaoa na Anafanya vzur sn kibiashara na Yale Maduka yote mawili anayasimamia vizur sn. Na amekua mwanafamilia wetu na sio mfanyakaz Tena Kama zamani.
 
Back
Top Bottom