HATUJAKAA SAWA
Kwnyw ule umati nikamuona jamaa mmoja Ni dalali namjua anapajua saiti kwangu, Nikamwambia nenda haraka sn katafute mteja Kwny ile nyumba yangu naijenga haijaisha, Nataka iuzwe leo leo pesa yote Mpatie huyu MKE wangu leoleo. Watu wakasema unachokifanya sio kizur.
Unamdhakioisha mkeo.
Nikawaambia huyu sio MKE wangu, ni muuaji ajae. Kwanza majirani mkisikia nmekufa ghafla fanyeni uchunguzi haraka, nmeuawa, nikimrudia huyu mwanamke atakuja kuniua ana tamaa sana na Mali. Bora niokoe maisha yangu kwanza, nimpe kila kitu aondoke, mimi bado kijana na Nguvu bado ninazo, ntatafuta tu vingine.
Hatukukaa Sana vijana wakawa wamemaliza kuijaza ile canter vitu vya ndani na wanarudishia turubai ili waondoke pale kuelekea Magomeni. Wife akaenda kumuinamia dereva anaomba Sana asitoe gari, amekosea saa, tena amekosea mno.
Nikamwambia dreva ngo'a gari usimsikilize huyo. Dreva kaiweka silencer kila akitaka kutoa wife anasimama mbele ya gari anasema Basi Leo Kama Gari hii inaondoka Hapa, basi nigonge na tairi nife kabisa. Sina maana kuishi. Basi dreva akawa anasita kuitoa gari.
Hatujakaa sawa,
Naona gari ya mzee wangu inaingia,
Mzee kashuka, kanifata na kunivuta mkono mpaka kwny Gari yake. Akanambia niingie kwenye Gari yake.
Nmeingia akaniuliza,
"Mimi Ni baba yako?" Nikasema "ndio"
Basi nakuomba usitoke humu ndani ya Gari mpaka ntakaporudi. Mzee akatoka na kwenda nje nikaona anazungumza na dreva wa Gari zote mbili canter na fuso.
Mzee akaenda kuzungumza na baba mkwe. Kisha akarudi ndani ya gari na kuwasha gari tukaondoka pale kuelekea Kimara nyumbani kwa mzee. Nikaona zile Gari mbili fuso na canter nazo kwa nyuma zinafata pamoja na gari nyngn mbili private na taxi Moja.
Tumefika nyumbani mzee kaingiza Gari yake ndani na kuamuru zile fuso na canter nazo ziingie ndani. Zile Gari nyingine zikataka kuingia, mzee akasema zibaki uko uko. Mzee akanifungulia na kunambia niende chumbani nikalale. Nikamwambia Wale vijana wa mizigo hawajalipwa bado.
Mzee akatoa pesa kawalipa vijana wa fuso na canter akawaambia watalipwa kesho, gari zao zitalala pale na ziko salama tuonane kesho asubuhi warudi na vijana wapakue mzigo wote Kisha watalipwa na usumbufu, wakasema POA wakaondoka.
Mzee kaenda nje kawaambia,
Kila mtu atawanyike aende nyumbani kwake anafunga geti lake hataki kuona mtu mazingira yake na kweli mzee akafunga geti Kisha kurudi kunishika mkono kunipeleka chumbani na kuniamuru nilale kwanza nipumzike. Kama kuna Chochote cha kuongea, basi tutaongea kesho, ikabid nitii amri ya mzee na kulala kutuliza kichwa pale pale nyumbani.
Kesho yake asubuhi nmeamka niko nakunywa chai, asubuhi nikaona dirishani kumbe baba mkwe kaja kuongea na mzee, wamekaa kwenye viti nje wanaongea Sana. Kisha nikaona baba mkwe anaondoka. Mzee nae Karudi ndani.
Nikamuuliza mzee alikuwa anasemaje huyo, akasema nipumzike kwanza Kama nmemaliza kunywa chai nirudi chumban kwangu kulala, sipaswi kutoka nje Wala kwenda popote pale bila ruhusa yake. Nikasema sawa mzee.
Kesho yake jioni,
Mzee kaiiita Kunisikiliza, nikamsimulia kila kitu. Mzee kasema kwa kilichotokea wameazimia na baba mkwe kuwa kila mtoto akapumzike nyumbani kwao. Mimi ntatulia Hapa kwetu na wife atarudi kwao. Kama kweli ndoa IPO basi itarudi Kama inafungishwa upya maana mpasuko uliokwishakuepo Kati ya familia hizi mbili Ni mkubwa sana, Ni Bora kila upande ukakae kivyake ukajitafakari kwa upya kwa kilichotokea.
Kweli ikawa nmerudi nyumban rasmi,
Baada ya wiki nikarudi normal na mzee akanisihi nikakae full-time kule duka kubwa, ofisi ijirudi kwanza ilipe madeni yake yote, ikitengamaa ndo niendelee na mirad Yake. Kwasasa nimuachie atapambana nayo mwenyewe. Kweli nikaanza kukaa duka kubwa mwnyw full time.
Gafla wife akaanza usumbuf anaomba sn radhi kwa yaliyopita.
Kila mtu wangu wa karibu anaemfahamu, anamfata anamwambia aniombee msamaha.
Anatuma Watu lukuki wanibembeleze.