Mke aliomba talaka tugawane Mali, nilichomfanyia hajawahi kurudia tena

Mke aliomba talaka tugawane Mali, nilichomfanyia hajawahi kurudia tena

Habar wakuu,

Kwanza niseme TU kisa hiki ni Cha miaka mingi ya nyuma sn ilopita ya ndoa yangu na MKE wangu MAMA G.
Kiukweli miongoni mwa ndoa zilizopita misukosuko mingi miaka 5 ya kwanza ya kwangu naweza kusema ilikua mojawapo.

Misukosuko hii nashkuru iliweza kutujenga imara mpk Sasa naweza kusema sijutii kuoa na naweza kusema nmebahatika kupata MKE Bora kabisa maishani, yaliyopita Si ndwele. Tugange yaliyopo na yajayo.

Anyway,
Nawaletea kisa Cha misukosuko ya ndoa yangu ambapo MKE wangu baada ya ugomvi mkubwa alidai talaka na kutaka tufuate sheria ili tugawane Mali, sema nilichomfanyia nilimnyoosha alijuta na hatosahau maishani mwake na mpk leo Hata tugombane vipi.

Kauli ya "TUGAWANE MALI" ilikoma na hawezi Tena kurudia kuitamka Tena.

[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
5f
 
Wanawake wa siku hz wana tamaa sana. Ili kukwepa hlo,,, ntaoa mtoto wa mtoto wa shangazi yangu. Hata akitaka tugawane mali pw tu mana mali zangu najua haziend mbali!!!
Binamu yako Tena,
Imani yako inaruhusu[emoji848]
 
SIKU YA SIKU IKAFIKA
Jirani na rafk yangu aKanipigia Simu kua mzigo duka kubwa ndo umeingia, na ile gari ndo imefika dukan inasubiri kufaulisha mzgo mwngn.
Wee ukifika usifike dukani bana njia wanayotokea Kisha wakishatoka wafatilie uone mpk watakapofikisha mzigo husika.

ikabd kuwatonya maaskali wawiki kupata backup na tuifatilie gari wanisaidie kuikamata pamoja na kaka wife Kama wezi wa dukan kwangu maana mizigo Yao ile itakua Haina risiti. Kweli wakakubali ile gar tumeiona na kuisubiri.

Ile gari imefaulisha mzigo Kisha kuondoka pale, tumewafatilia mpk tukaona walipoifikisha.
Kaka wife kaja kuipokea, nikawatuma maaskali wakakague vitashuka vitu gan,kweli wakanitext kua njoo uone nikafika na kukuta mzgo wa pesa ndefu mno ulijazwa ile Gari.

Kaka wife akaanza kurusha Maneno mabovu nikawambia maaskali ile gari na mzgo wote na hao jamaa akiwemo Kaka wife waende polisi, maelezo mbele ya safari, Tutajua mbivu na mbichi kule kule kituoni. Kweli wote wamesombwa tumelekea kituoni.

Tumefika polisi hata hatujaanza kutoa maelezo namuona wife kafika. Gafla nawaona ndugu wa ukweni nao wamefika. Sikumsemesha yeyote pale. Kaka wife akatoa maelezo anasema ule mzigo Ni wa kwake kanunua duka Letu,Akaulizwa risiti iko wapi, akasema huwa wanapeana TU kwasababu wanaaminiana, kaulizwa khs ushahidi wa malipo akasema pesa wanatumiana kwny account ya benki ya duka. Anamuagizia pesa na sio kwamba kabeba TU vitu kiwizi wizi kutoka dukan kwetu kupeleka kwake.

Ikabd maaskali wanambie nikafate bank statement wajiridhishe asemayo, nikawambia Kadi ya Hilo duka anayo wife nje,ngoja nimfate anipatie. Nikamfata wife nje anipe Kadi ya benki, nikafate statement akagoma. Nikarudi kuwaambia maaskali, wakamshurutisha Kadi ya benki akanipatia nikaenda benki kuchukua bank statement ya Miezi 6 page za kutosha nikaone hiyo miamala anayosema Kaka wife huwa anampa pesa amuagizie mizigo iko wapi.

BAADA ya kuichukua bank statement, na kuikagua Nikagundua hamna muamala wa maana Zaid ya fedha nyingi kuonekana wife ndo utuma kwny account ya Kaka ake kutoka kwenye account ya duka Na kibaya zaid miamala mingine imefanyika kipind ambacho marejesho ya benki yanakaribia hivyo kusababisha benki wakitaka kukata Deni lao la mkopo inashindikana wanakuta account Haina fedha za kutosha. Na wakiona siku zimepita pesa haziingii ndo wananipigia Simu Mimi.

Kwan akili ya haraka haraka maaskali na Mimi tukajua kumbe wife ananihujumu maksudi kabisa.Analalamika biashara hamna ,marejesho yamegoma kumbe pesa zote anatuma kwa Kaka Yake afanye biashara. Huu Ni uhuni Hadi maaskali wakanishangaa Nina MKE wa Aina gani, ndoa gani hii,hamna ndoa Hapa. Nnapoteza Muda, This is inside job.

Sijakaa sawa baba mkwe kafika pale na kuomba kesi ile akaimalize mwny kifamilia.Maaskali wakaniuliza Kama naridhia maana pale hamna kesi tunapoteza muda, mwenye tatizo Ni mkeo anaemtumia pesa sio Kaka yake. Ikabd nikubali tuondoke pale tukayazungumze nyumbani kifamilia.

Tumetoka pale,
Baba mkwe akanambia nitangulie magomeni yeye atakuja, alikuja gafla TU pale polisi, kaacha KAZI ya Watu, nikasema Haina shida ba mkwe.
Nmefika ukweni ikabd niwasimulie shangaz zake na wife nilowakuta khs yaliyojiri, wife na akasema yake,Kaka Yake nae akajieleza yake.

Cha kushangaza shangaz zake hao wakawa hawashtuki kilichotokea.
Wakadai yule ni mwanafamilia Kama alivo MKE wangu, huo sio wizi Wala hujuma, bali pesa inarudishwa kwny familia,nikifariki wanangu watalelewa na hao hao wajomba zake ninaohangaika kuwapeleka polisi ili kuwafunga jela

[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
[emoji2962][emoji848][emoji1787][emoji1787][emoji1787] hivi kwanini hua wanafikiria kua sisi wanaume ndio tutawahi kufa!? Eti siku ukifa ........ Sijui fikra hizi hua wanazitoa wapi!? Maaa mae
 
Hatujakaa sawa,
Naona gari ya mzee wangu inaingia,
Mzee kashuka,kanifata na kunivuta mkono mpk kwny Gari yake. Akanambia niingie kwenye Gari yake.
Nmeingia akaniuliza,
"Mimi Ni baba yako?" Nikasema "ndio"
Basi nakuomba usitoke humu ndani ya Gari mpk ntakaporudi. Mzee akatoka na kwenda nje nikaona anazungumza na dreva w Gari zote mbili canter na fuso,
Nilipofika hapa machozi yamenilenga aisee nimemkumbuka mzee wangu Mungu amrehemu, kaka una baba bora mwenye hekima sana!

Asante kwa ku share nasi kisa chako, ubarikiwe.
 
IKAFIKA KIPINDI
Akawa anakuja dukan anakaa chini na mtoto mgongoni kibarazani analia anaomba msamaha sn nimsamehe sn kwa yote aliyonikosea. Anaahidi atajirekebisha Ni shetani alimpitia.simjibu chochote akichoka kuomba msamaha anaondoka zake.

Kuna siku kashinda dukan asbh mpk saa 11 jioni na mtoto mgongoni anabembeleza. Mpk nafunga anabembeleza anabubujikwa na machozi, nilivofunga nikaenda nyumbani. Usiku kaja, kakuta geti halijafungwa kasukuma kaingia ndani na kwenda dirishan kwangu chumban analia anabembeleza nimsamehe. Nikamkaushia.

Kaenda Hadi dirisha la bi.mkubwa analia kakosa anaomba asamehewe.
Bi mkubwa nae akakausha Ila alivoondoka nikashangaa na asivompenda huruma ikamuingia nae akawa ananisihi nimsamehe turudiane. Nikamwambia bi.mkubwa achana nae uyo,hafai.

Tumeenda ukimya juu ya ukimya,
Wife akadili na mzee, kumbe akawa Anaenda kuomba msamaha ofsin kwa mzee. Mzee alipoona imekua kero akaniita na kunambia uyu mwanamke kila Mara anakwenda ofsn kwake kumuomba msamaha na anadai shangaz zake ndo waliomponza anajutia kilichotokea. Naonaje suala la kumsamehe. Nikasema mzee Mimi simtaki tena. Mzee akasema sawa Kama nmeamua hivyo. Ikaisha.

Baada ya miez 3 tangu Lile vurugu. naendelea na shughuli zangu nishaanza msahau wife, mzee akanambia jumapili tutakua na kikao Cha familia saa 10 mchana usichelewe kurudi uwepo. Nikasema sawa. Nikajua yatakua mambo ya familia yetu tu. Kweli Nmefika nyumbani mapema.

Gafla Niko chumban bi mkubwa kaja nigongea kua MDA tayar nije seblen.
Ile Natoka nafika seblen,nawaona wale shangazi zake wameketi, ikanibidi kurudi zangu chumbani na kukaa kitandani nikajiinamia kwa uchungu. Ikawa Kama wamenitonesha upya kile kidonda .

Mzee kaja kaniinua na kunambia twende seblen kila kitu kitakua sawa.
Kweli nmeinuka kinyonge nmeenda seblen nmekaa na mzee kochi Moja kubwa la Watu watatu.

Gafla shangaz Yao mmoja aliekua na mdomo akaja niangukia chonde chonde nimsamehe kwa yaliyopita.
Mzee akaniangalia usoni, nikaona mzee kama anatuma ujumbe kua anajiskia viby jins mmama yule mtu mzima anavolia. Wale wengine wakawa wanasema samahani yaishe yaishe. Babamkwe nae akasema imefkia mahali wife mpk anataka kujiua nyumbani kwao, alishameza hadi vidonge Mara mbili kajifungia chumbani anataka kujiua yye na mtoto. Wakavunja mlango kumnusuru.

Kama familia wanaomba radhi, wametukosea Sana, wanaomba radhi Sana. Anawasiwasi wanakoelekea atampoteza binti Yake na mjukuu wake, binti yake anazurula kila siku mjini na mtoto mgongoni anasema anaaga kaja kuomba msamaha na hasamehewi na kichwa chake kishachanganyikiwa sahv kilivyo tusije kushangaa kagongwa na Gari yeye na mtoto wote wamefariki. Mzee kaniangalia usoni.

Sijakaa sawa, kumbe wife alijificha jikoni nae kaja analia Hadi kamasi macho yamevimba na mtoto wake mgongoni kaniinamia anaomba msamaha. Mzee kaniangalia Tena usoni Tena na kunipa ishara ya nimsamehe. Nikatikisa kichwa kukubali.

Mzee kamuinua wife na kumkalisha kushoto kwake, Mimi kulia kwake.
Akasema kua Hawa wote Ni wanangu. Nyie wote nendeni kila kitu kitakua sawa. Basi wageni wale wakatawanyika.

Tukabaki familia yetu, wife na mtt. nikawa ndani ya siku 2 simuongeleshi.
Bi mkubwa akanisihi yaishe niongee na mzazi mwenzangu, mzee nae akanisihi yaishe bhana. Basi siku ya 3 wife kaja chumbn kwangu kavaa kimitego analia anaomba msamaha.
Kwasababu moyoni nishamsamhe na nilivommiss siku nyng sijapiga show.
Basi ugomvi wetu ukaishia pale.

Baada ya wiki pale home,
Mzee akatutaftia nyumba nyingine kubwa zaidi na kutupangishia kua tukakae uko pale kwa wapangaji tuhame. Alivotupeleka kule tunakutana na vile vitu vyetu tulivosomba na canter vipo vimerundikwa TU sebleni. Wife akaanza kuvipanga upya na maisha yakarejea Kama zamani.

TANGU HAPO miaka mingi imepita na WIFE HAJAWAI TENA KUTAMKA KAULI ILE YA TUGAWANE MALI.

Na pia,
Tangu ugomvi huo alirudi kua mama wa nyumbani Hadi leo hii nnapoleta Uzi huu hajawai kuuza duka langu.

Pia,
Nilikata mguu kabisa na magomeni kule kwa mashangazi waswahili wale.
Japo wanadai ugomvi ulishaisha ila nmekua karibu na ndugu wa wife kule upande wa mama ake na upande wa baba ake. Maelewano mazur Nmebaki na baba mkwe wangu TU.
Hao wengine salamu TU,kila mtu kivyake.

Nihitimishe kwamba
kile kipind kilipita na kilikua Cha mafunzo sn kwetu kutukomaza na Siwez kumhukumu sn wife maana umri wake ulkua bado mdogo sn, afu mazingira ya uswahili alikokulia kwa mashangazi wale yalimharibu.
Nashkuru upande wa mama ake walinisaidia sn kumshape wife akatukia vizur Sana.[emoji1431]

Kwasasa
MKE wangu kiumri na kitabia amekua sana. Naweza kusema Ni MKE bora kabisa maishani, naeweza kukaa mbele ya Wanaume wenzangu waliooa nami nakajivunia kua Nmeoa mke bora kabisa na pure wife material[emoji4]

Na huwa nawaza Sijui ningekaza ningempoteza kipind kile sijui ingekuaje maisha yangu, maana kila nnakogusa Ni chenga tupu. mamaJ inclusive.

KINGINE,
Najivunia Sana baba mkwe wangu nilie nae,
Ni mkwe asiyependa mambo ya kipuuzi kabisa na huwa alinisaidia Sana kumshape wife miaka 5 ya changamoto ya ndoa yangu.[emoji1431]

SIKU NIKITULIA NTASHUSHA TENA KISA KILICHONIFANYA NIJIFUNIE HUYU BABA MKWE WANGU KATIKA KUMNYOOSHA WIFE WANGU[emoji4]

ASANTENI WAKUU[emoji1431]
#######mwisho######

NB:
Kuna la kujifunza Hapa wakuu
Uzi huu nmeuleta baada ya kuguswa na Uzi wa mdau mmoja mwenye kisa Kama changu, ugomvi wa kibiashara na mkewe, Kisha mkewe akadai wagawane Mali.

NAWASILISHA[emoji1431]
Umetisha mkuu...Wanawake hawa wakishaota mapembe na usipoonyeshabkwa vitendo kua uko tayari kumuacha for good asee watakufrustrate kwa viwango vya kimataifa.
 
Back
Top Bottom