Mke aliomba talaka tugawane Mali, nilichomfanyia hajawahi kurudia tena

Mbona unarudia mkuu

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Dah! Kuna watu ukiwabeba ni Kama gunia la misumari, hawabebeki kabisa yaan[emoji26]
 
Nimejifunza mengi sana kuhusu ndoa ..ila jamaa una uvumilivu sana mimi nisingeweza kwa kweli tusingerudiana
 
Nimejifunza mengi sana kuhusu ndoa ..ila jamaa una uvumilivu sana mimi nisingeweza kwa kweli tusingerudiana
Binfs pia nisingeweza,
I'll mzee alinihakikishia keshajirudi,
Anaamini funzo alilopata wife atakua MKE bora
 
Kabisa mkuu,
Wanatia huruma washakuingiza hasara sana, fikiria mwanamke anatoa pesa anampa Kaka ake na anajua Kuna rejesho benki na Hana wasiwasi kabisa.[emoji26]
So strange bro inashangaza sana yani
 
Asante sana sana sana lakin hizi sifa naomba tumrudishie Mungu wetu muumba wa mbingu na nchi. Kwa hakika miaka mitano nyuma sikuwa huyu. Nilikua mtu nisiyeeleweka pengine mtu mmoja gaidi sana mwenye roho iliojaa hila. Lakin kuna neema yake Bwana ikanitafuta, ikanipata. Namshukuru huyu Baba yetu wa mbinguni.

Lakini pia sisi bado ni wanafunzi tu. Kuna mengi najifunza sana JF na nakiri JF inanisaidia kubadilika sana mtazamo nikirelate my faith na some lessons ninazokutana nazo. Thanks for the heartfelt prayers...one love🙂
 
Kuoa familia yenye hali ya chini kuna changamoto zake.... Wifi yetu alitaka kusaidia familia yao wapate mafanikio ya haraka bila kujali familia yake.......

Mashangazi nao waliingia kiswahili kupambana na wewe wakidhani ungewaogopa kumbe ndo wanaharibu....

Baba mkwe katumia busara kubwa na hekima ambazo ndo wazazi wengi wanapaswa kuwa hivyo...

Mama yako pamoja na bifu zao za nyuma lkn alijirudi na kuanza kuwasupport...

Baba yako mzazi ndo kawabeba hapo...nilikuwa nasoma nikiwaza huyu mzee alikuwa mgonjwa,ila ilipofika pale kwenye kutoa vitu vya ndani akatokea,nikashusha pumzi... Huyu kamaliza kila kitu....

Tumalizie kwako, ulichukua maamuzi ya juu kabisa,hukutaka kupita kutafuta ushauri ila ni jambo jema lililo kupa heshima....hawatarudi tena kukuchezea...sio mashemeji wala shangazi.........

Hongera nimejifunza mengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…