Mke aliomba talaka tugawane Mali, nilichomfanyia hajawahi kurudia tena

Mengi mno ya kujifunza kaka. Whatever can be said ila wanawake wanachukua muda sana kusettle na kutuliza akili kwenye ndoa. Pia swala la kumweka wife na mama yangu nyumba moja ni mistake kubwa niliwahi kufanya, ilibidi nimkabidhi mama yangu nyumba niliyoijenga na kwenda kupangisha na kuanza upya na wife. Wanawake wawili ni vigumu sana kuishi nyumba moja.

Lingine ni wakati wa kuoa take into consideration swala la wakwe zako, hao watakusaidia sana kumshape mwenzako, haya mambo ya kukutana barabarani na kukubaliana kila kitu ni chanzo cha kwanza kabisa cha ndoa nyingi kuvunjika. Lazima wawe ni watu wanaojielewa na unawaona kabisa ni watu wenye uwezo wa kumkanya mtoto wao.

Biashara yangu ya kwanza ilikufa pia kwa ajili ya ukaribu wa mama na wife, ilikuwa hamna biashara kabisa ni mashindano tu ya kijinga, nikachukua mzigo wote nikauhamishia kwa mama, tukaanza upya tena....

Shukran sana mkuu.
 

Umeongea point muhimu kabisa mkuu, Sijui tatizo huwa nini, yaani hawakai chungu kimoja kabisa tofauti na sisi wanaume
 

Kweli kabisa, la kujifunza Hilo.
Magomeni alikokulia uswahili Ulikuwa mwingi, nashkuru upande wa mama ake Kimara ni wacha mungu na Wana maadili mazuri.

Wainisaidia kumshape wife mpaka Sasa Kama MKE Bora na mama wa kanisa.

Najivunia sana wakwe zangu upande wa mama ake, na mwaka Juzi kiukweli nmewapa zawadi
 
BOnge la Uzi mkuu. Kuna mengi sana nimejifunza hapa asee👏
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…