SIKU YA SIKU IKAFIKA
Jirani na rafiki yangu akanipigia Simu kuwa mzigo duka kubwa ndo umeingia, na ile gari ndo imefika dukani inasubiri kufaulisha mzigo mwingine. Wee ukifika usifike dukani bana njia wanayotokea Kisha wakishatoka wafatilie uone mpk watakapofikisha mzigo husika.
Ikabd kuwatonya maaskari wawiki kupata backup na tuifatilie gari wanisaidie kuikamata pamoja na kaka wife Kama wezi wa dukani kwangu maana mizigo Yao ile itakuwa Haina risiti. Kweli wakakubali ile gari tumeiona na kuisubiri.
Ile gari imefaulisha mzigo Kisha kuondoka pale, tumewafatilia mpaka tukaona walipoifikisha.
Kaka wife kaja kuipokea, nikawatuma maaskari wakakague vitashuka vitu gani, kweli wakanitext kuwa njoo uone nikafika na kukuta mzgo wa pesa ndefu mno ulijazwa ile Gari.
Kaka wife akaanza kurusha Maneno mabovu nikawambia maaskari ile gari na mzigo wote na hao jamaa akiwemo Kaka wife waende polisi, maelezo mbele ya safari, Tutajua mbivu na mbichi kule kule kituoni. Kweli wote wamesombwa tumeelekea kituoni.
Tumefika polisi hata hatujaanza kutoa maelezo namuona wife kafika. Ghafla nawaona ndugu wa ukweni nao wamefika. Sikumsemesha yeyote pale. Kaka wife akatoa maelezo anasema ule mzigo Ni wa kwake kanunua duka Letu, Akaulizwa risiti iko wapi, akasema huwa wanapeana TU kwasababu wanaaminiana, kaulizwa khs ushahidi wa malipo akasema pesa wanatumiana kwny account ya benki ya duka. Anamuangizia pesa na sio kwamba kabeba TU vitu kiwizi wizi kutoka dukani kwetu kupeleka kwake.
Ikabidi maaskali wanambie nikafate bank statement wajiridhishe asemayo, nikawambia Kadi ya Hilo duka anayo wife nje, ngoja nimfate anipatie. Nikamfata wife nje anipe Kadi ya benki, nikafate statement akagoma. Nikarudi kuwaambia maaskari, wakamshurutisha Kadi ya benki akanipatia nikaenda benki kuchukua bank statement ya Miezi 6 page za kutosha nikaone hiyo miamala anayosema Kaka wife huwa anampa pesa amuagizie mizigo iko wapi.
BAADA ya kuichukua bank statement, na kuikagua Nikagundua hamna muamala wa maana Zaid ya fedha nyingi kuonekana wife ndo hutuma kwenye account ya Kaka yake kutoka kwenye account ya duka Na kibaya zaidi miamala mingine imefanyika kipindi ambacho marejesho ya benki yanakaribia hivyo kusababisha benki wakitaka kukata Deni lao la mkopo inashindikana wanakuta account Haina fedha za kutosha. Na wakiona siku zimepita pesa haziingii ndo wananipigia Simu Mimi.
Kwani akili ya haraka haraka maaskari na Mimi tukajua kumbe wife ananihujumu maksudi kabisa. Analalamika biashara hamna, marejesho yamegoma kumbe pesa zote anatuma kwa Kaka Yake afanye biashara. Huu Ni uhuni Hadi maaskari wakanishangaa nina MKE wa Aina gani, ndoa gani hii, hamna ndoa Hapa. Nnapoteza Muda, This is inside job.
Sijakaa sawa baba mkwe kafika pale na kuomba kesi ile akaimalize mwny kifamilia. Maaskari wakaniuliza Kama naridhia maana pale hamna kesi tunapoteza muda, mwenye tatizo Ni mkeo anaemtumia pesa sio Kaka yake. Ikabidi nikubali tuondoke pale tukayazungumze nyumbani kifamilia.
Tumetoka pale,
Baba mkwe akanambia nitangulie Magomeni yeye atakuja, alikuja gafla TU pale polisi, kaacha KAZI ya Watu, nikasema Haina shida ba mkwe.
Nmefika ukweni ikabd niwasimulie shangaz zake na wife nilowakuta khs yaliyojiri, wife na akasema yake, Kaka Yake nae akajieleza yake.
Cha kushangaza shangazi zake hao wakawa hawashtuki kilichotokea.
Wakadai yule ni mwanafamilia Kama alivyo MKE wangu, huo sio wizi Wala hujuma, bali pesa inarudishwa kwny familia, nikifariki wanangu watalelewa na hao hao wajomba zake ninaohangaika kuwapeleka polisi ili kuwafunga jela.