Mke aliomba talaka tugawane Mali, nilichomfanyia hajawahi kurudia tena

Mke aliomba talaka tugawane Mali, nilichomfanyia hajawahi kurudia tena

Ha ha ha n.....umekua muoga mno,
Mi wife baada ya kumtoa dukan kabaki kua mama wa nyumbani Hadi leo.

Sema ana mradi wa ngombe wa maziwa na kuuza maji ya kisima anausimamia na kupata Ela binafsi.

Yule kijna ndo lilimkabidhi kijiti,
Anaendesha vzur Lile duka na Hadi nae kaoa ana watoto wengi kuliko hata Mimi[emoji4]
Ndo maana hahangaiki na wewe kumbe Yuko busy busy kidogo
 
Usiruhusu mkeo awe na biashara ya kushika hela nyingi sana, unakaribisha matatizo kwenye ndoa...
Hii principal naitekeleza Sana
Saiv hajui nyumba zangu Mpya Wala miradi yangu anachojua ni hii gari na nyumba moja tunayoishi
Aliwahi kutamka tugawane Mali bas nilimtoa hapohapo kwenye akili yangu
 
Hii principal naitekeleza Sana
Saiv hajui nyumba zangu Mpya Wala miradi yangu anachojua ni hii gari na nyumba moja tunayoishi
Aliwahi kutamka tugawane Mali bas nilimtoa hapohapo kwenye akili yangu
Ulifanya Jambo la akili,
Wanaume Lazima tutumie akili kuliko hisia,
Mtu akishakuonesha redflag chukua hatua haraka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo mwenzo wako muache anyooke Kwanza, asipokaa sawa Itakua shida

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu namsikitikia kaponzwa na ndugu zake na nafahamu hilo nimeamua kimsamehe ila nothing can be the same, nothing can be fixed, huwezi kukaa na mtu ambae hakuna anaekuelewa kwao na yeye hakuna anaemuelewa kwetu japo haikua hivyo mwanzo na aliekua anategemewa saana kiweka haya mambo sawa alikua huyo kaka yake mchungaji maana mwanzo ya haya yote waliyaanzisha wadogo zake! Kuna swala walikua wanashinikiza nikalipangua na kuwafukuza nae akaja kuzamia humo humo kwa tiketi nyingine kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo mwenzo wako muache anyooke Kwanza, asipokaa sawa Itakua shida

Sent using Jamii Forums mobile app
Kiukweli anapitia wakati mgumu sana, namuhurumia sana mbali na kumpenda ila sina namna kabsa, kwanza binafsi sina amani kabisa hata nikikaa nae nusu saa, kila anachoongea hata kama anakimaanisha najikuta simuelewi japo najua anamaanisha kweli, hua nahisi kuna mtego anataka niuvae, haishi kuwalaumu ndugu zake haishi kujilaumu yeye mwenyewe kwa kuhama kwake na kwenda kupanga, anatamani arudi ila ndio hivyo dalali yupo kazini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata Mimi wangu alikuwa na hiyo tabia ugomvi kidogo tuachane na tugawane mali, ili kuepusha kelele na ujuaji mwingi toka hapo sijawahi mshirikisha kitu tena, nimenunua ardhi sana na kuna kiasi kizuri sana benki hajui na nilishaapa na kuweka nadhiri kuwa hatajua kitu chochote zaidi ya vile alivyokuwa ananiimbia wimbo tugawane, yeye siku pekee ambayo anakuja kujua ni siku ambayo mm nimetangulia mbele ya haki/kufa ndo hapo atapojua maana nategemea kuandika wosia alafu yeye hataridhi kitu toka kwangu zaidi ya vile alivyokuwa ananiimbia wimbo.
Duuuh hadi nimeogopa.
Poleni aisee na hizi changamoto za ndoa
 
SIKU YA SIKU IKAFIKA
Jirani na rafiki yangu akanipigia Simu kuwa mzigo duka kubwa ndo umeingia, na ile gari ndo imefika dukani inasubiri kufaulisha mzigo mwingine. Wee ukifika usifike dukani bana njia wanayotokea Kisha wakishatoka wafatilie uone mpk watakapofikisha mzigo husika.

Ikabd kuwatonya maaskari wawiki kupata backup na tuifatilie gari wanisaidie kuikamata pamoja na kaka wife Kama wezi wa dukani kwangu maana mizigo Yao ile itakuwa Haina risiti. Kweli wakakubali ile gari tumeiona na kuisubiri.

Ile gari imefaulisha mzigo Kisha kuondoka pale, tumewafatilia mpaka tukaona walipoifikisha.
Kaka wife kaja kuipokea, nikawatuma maaskari wakakague vitashuka vitu gani, kweli wakanitext kuwa njoo uone nikafika na kukuta mzgo wa pesa ndefu mno ulijazwa ile Gari.

Kaka wife akaanza kurusha Maneno mabovu nikawambia maaskari ile gari na mzigo wote na hao jamaa akiwemo Kaka wife waende polisi, maelezo mbele ya safari, Tutajua mbivu na mbichi kule kule kituoni. Kweli wote wamesombwa tumeelekea kituoni.

Tumefika polisi hata hatujaanza kutoa maelezo namuona wife kafika. Ghafla nawaona ndugu wa ukweni nao wamefika. Sikumsemesha yeyote pale. Kaka wife akatoa maelezo anasema ule mzigo Ni wa kwake kanunua duka Letu, Akaulizwa risiti iko wapi, akasema huwa wanapeana TU kwasababu wanaaminiana, kaulizwa khs ushahidi wa malipo akasema pesa wanatumiana kwny account ya benki ya duka. Anamuangizia pesa na sio kwamba kabeba TU vitu kiwizi wizi kutoka dukani kwetu kupeleka kwake.

Ikabidi maaskali wanambie nikafate bank statement wajiridhishe asemayo, nikawambia Kadi ya Hilo duka anayo wife nje, ngoja nimfate anipatie. Nikamfata wife nje anipe Kadi ya benki, nikafate statement akagoma. Nikarudi kuwaambia maaskari, wakamshurutisha Kadi ya benki akanipatia nikaenda benki kuchukua bank statement ya Miezi 6 page za kutosha nikaone hiyo miamala anayosema Kaka wife huwa anampa pesa amuagizie mizigo iko wapi.

BAADA ya kuichukua bank statement, na kuikagua Nikagundua hamna muamala wa maana Zaid ya fedha nyingi kuonekana wife ndo hutuma kwenye account ya Kaka yake kutoka kwenye account ya duka Na kibaya zaidi miamala mingine imefanyika kipindi ambacho marejesho ya benki yanakaribia hivyo kusababisha benki wakitaka kukata Deni lao la mkopo inashindikana wanakuta account Haina fedha za kutosha. Na wakiona siku zimepita pesa haziingii ndo wananipigia Simu Mimi.

Kwani akili ya haraka haraka maaskari na Mimi tukajua kumbe wife ananihujumu maksudi kabisa. Analalamika biashara hamna, marejesho yamegoma kumbe pesa zote anatuma kwa Kaka Yake afanye biashara. Huu Ni uhuni Hadi maaskari wakanishangaa nina MKE wa Aina gani, ndoa gani hii, hamna ndoa Hapa. Nnapoteza Muda, This is inside job.

Sijakaa sawa baba mkwe kafika pale na kuomba kesi ile akaimalize mwny kifamilia. Maaskari wakaniuliza Kama naridhia maana pale hamna kesi tunapoteza muda, mwenye tatizo Ni mkeo anaemtumia pesa sio Kaka yake. Ikabidi nikubali tuondoke pale tukayazungumze nyumbani kifamilia.

Tumetoka pale,
Baba mkwe akanambia nitangulie Magomeni yeye atakuja, alikuja gafla TU pale polisi, kaacha KAZI ya Watu, nikasema Haina shida ba mkwe.
Nmefika ukweni ikabd niwasimulie shangaz zake na wife nilowakuta khs yaliyojiri, wife na akasema yake, Kaka Yake nae akajieleza yake.

Cha kushangaza shangazi zake hao wakawa hawashtuki kilichotokea.
Wakadai yule ni mwanafamilia Kama alivyo MKE wangu, huo sio wizi Wala hujuma, bali pesa inarudishwa kwny familia, nikifariki wanangu watalelewa na hao hao wajomba zake ninaohangaika kuwapeleka polisi ili kuwafunga jela.
Kwanza pole kwa kuoa magomeni they don't like working or any hardship life
 
Duh asee kaka pole na hongera sana maana hili jambo lilinianza hata mimi nilipofungua kampuni yangu ilibidi nibadili shares sabab ilikua bado changa na imeanza kuleta mambo mengi ya mali acha tu nimesoma hadi nimejikuta nalia [emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]

Sent from my moto g power (2021) using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom