Memtata
JF-Expert Member
- Jul 27, 2013
- 587
- 1,863
Leo naomba mumsaidie rafiki yangu kumshauri, mimi ni nimeshashauri kwa upande wangu lakini nataka kuona fikra za watu zaidi.
Jamaa ana mke na watoto, hivi karibuni kaka yake alipoteza kazi ndugu wakamuomba asaidie kulea mtoto mmoja ambaye alikuwa kidato cha pili. Jamaa alimshirikisha mke wake kuhusu mgeni huyo mke akakubali lakini inaonekana alikubali kwa shingo upande.
Kwa sasa sio siri tena mwanamke kasema wazi kabisa hataki kuishi na huyo mtoto tena akaenda mbali zaidi kampigia simu mama wa mtoto kumueleza yeye hawezi kuishi na mtoto wake. Habari zikamfikia jamaa akashangaa sana aliporudi kumlaumu mwanamke kwanini amefanya hivyo mwanamke kaja juu na kusema hata yeye ana maamuzi kwenye familia na msimamo wake ndio huo, hataki kuishi na huyo mtoto.
Jamaa kabembeleza sana mke akawa kama kaelewa kumbe bado. Hivi juzi kalianzisha tena na sasa amefika mbali kamwambia mume wake achague moja aidha kuishi na yeye(mke) ama mtoto wa ndugu yake........
Mzozo uko hapo, mimi nilimshauri kama hana uwezo wa kumlea huyo mtoto amrudishe kwao lakini si kwasababu ya kukataliwa na mke wake maana hata yeye hajui kesho yake. Jamaa alinijibu uwezo anao maana mtoto anasoma shule za serikali halipi ada hata mia zaidi ya uniform na vifaa vya shule.
Kama nimekosea naombeni sababu, bado tuna nafasi ya kumsaidia jamaa. Kwa ndugu upande wa mume na narafiki zake wanashangaa sana maamuzi ya mwanamke lakini kwa ndugu wa mke anasema zaidi ya 80% wanamsapoti mwanamke 🤔