Mke hataki ndugu zako, utafanyaje?

Mke hataki ndugu zako, utafanyaje?

Mkuu amua kama mwanaume kama kweli huyo mke yupo tayari kuachana na wewe sababu ya huyo mtoto mwambie mtoto lazima muishi naye kama anaondoka aondoke
Unadhan ni rahisi?tena mi naona akikataa inakuwa rahisi hataki kuwa mnafiki amtese mtoto ,bora akalelewe kwa ndugu zake kuliko muda mwingi ashinde na mtu baki
Mim napenda ningekaa nae tu maana kuishi na watoto mama mjengo hutagusa mikazi ya vyombo sijui kudeki sijui uwanja mchafu ,we unaonaje 😂😂😂
 
Huyo mwanamke msimpuuze, ameamua kuwa mkweli.
Sio ukubali kinafiki alafu baadaye unaanza kumnyanyasa na kumnyanyapaa mtoto wa watu. Binti asaidiwe akiwa kwao kuepusha ugomvi usio wa lazima!
 
Kama nimimi ningemwondoa dogo faster. Ila sitoshiriki tatizo lolote la upande wa mke wangu. Yaani hata ukitokea msiba ataenda peke yake. Sitoruhisu mtu yeyote aje kwangu wa upande wao
Ntabadirika kitabia vibaya mno nikirudi mapema nisaa 6 usiku hapo nimewahi. Maji ya kunywa itakuwa ni bia. Yaani atapata tabu huyo
 
Kwenu wakuu,
Kwa muda mchache nimepata ushauri wa kutosha kazi iliyobaki ni kufikisha ujumbe.

Kuna majibu ya aina tatu hapa:
1. Kuna ambao wanakubaliana na maamuzi ya mwanamke, mtoto aondoke
2. Kuna ambao wanapinga tabia ya mwanamke, bora mwanamke aondoke.
3. Kundi la mwisho wanachukizwa na tabia ya mwanamke lakini wanashauri mtoto aondoke kuepusha ugomvi.

Binafsi naungana na kundi la pili, mwanamke asepe. Kuna sababu ya msingi kwa mfano aliotoa scolastika
nakataa sababu yoyote zaidi ya chuki na roho mbaya kwa sababu kama kuna changamoto yoyote angeongea na mume wake,
ok leo anakataa mtoto mmoja wa form two je akija kuuguliwa na mzazi kwake itakuaje?maybe kama mke ndo anatunza familia hapo ni sawa kulalamika lakini kama ni wewe basi mwanamke wa hivyo hakufai
N.B
hapa jirani kuna mwanamke yaani yeye ndugu wa mme huwa hawakai akijitahidi ni wiki mbili awe wa kike ama wa kiume sijui huwa anawafanya nini
Ukichunguza kwa umakini hapa mwanamke ana roho mbaya tu Hana sababu yoyote ya msingi. Kama alivyosema scolastika leo kafanyiwa mtoto kesho akimfanyia mzazi wako?!

Naenda kufunguka kwa jamaa akiona ushauri unamfaa auchukue akiona haufai auwache
 
asee,sema mambo ya mke na mme yana changamoto hasa ukute mtu kashikwa masikio mi naona ungempa haya majibu asome mwenyewe make usije ukaonekana kirusi ndani ya familia,wewe usiwe upande wowote pls
sema mpaka hapo ndoa ishaingia doa familia haimpendi tena mwanamke yaani vitu vidogo tena vya kupita vikufanye ukosane na watu?
nimependa ushauri wa jamaa hapo juu anasema unakubali aondoke ila unapiga pini kotekote hata ndugu yake akiomba kulala siku moja unafukuza,mbona atanyooka
 
1. mbona umefikia maamuzi mwanamke aondoke kwani wewe ni muhusika?

2. kama ana/una uwezo wa kumsaidia huyo mtoto akae kwa wazazi wake ila asaidiwe mahitaji ya msingi ili aweze kusoma.

3. ulioa/alioa kwa ajili yako/yake itakuwa ni upumbavu kuacha mke/mume sababu za ndugu.
 
Kwenu wakuu,
Kwa muda mchache nimepata ushauri wa kutosha kazi iliyobaki ni kufikisha ujumbe.

Kuna majibu ya aina tatu hapa:
1. Kuna ambao wanakubaliana na maamuzi ya mwanamke, mtoto aondoke
2. Kuna ambao wanapinga tabia ya mwanamke, bora mwanamke aondoke.
3. Kundi la mwisho wanachukizwa na tabia ya mwanamke lakini wanashauri mtoto aondoke kuepusha ugomvi.

Binafsi naungana na kundi la pili, mwanamke asepe. Kuna sababu ya msingi kwa mfano aliotoa scolastika

Ukichunguza kwa umakini hapa mwanamke ana roho mbaya tu Hana sababu yoyote ya msingi. Kama alivyosema scolastika leo kafanyiwa mtoto kesho akimfanyia mzazi wako?!

Naenda kufunguka kwa jamaa akiona ushauri unamfaa auchukue akiona haufai auwache
Wewe nawe acha ufala, unaona raha kuvunja ndoa ya watu, huyo mtoto kaingilia utaratibu wa watu hapo, kosa la mwanamke labda ni ile kukubali mara ya kwanza then kugeuka, mtoto wa form 2 tayar kakua, atasaidia ila sio lazima aishi hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo jamaa itakuwa ni yeye, eti ufukuze mke kisa unaforce ukae na ndugu ambaye wazazi wake wapo.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa sisi ambao tumekaa,tumesomeshwa na ndugu,hii ni changamoto kubwa, kwa maisha yetu ya kiafrika inatokea unajikuta upo kwa ndugu hata mwaka mmoja au miwili,hata huyo mwanamke once upon a time kuna uwezekano aliishi kwa ndugu,kwani maisha yetu yanashabihiana
suluhu hapo,kwa kipindi hiki cha likizo huyo mtoto aondoke hapo nyumbani,wakati huku nyuma mwanamke aulizwe shida nini anayoiona,endapo huyu mtoto atakuja kukaa hapo,wachambue hizo hoja kwa pamoja wafikie muafaka.
 
Hamna cha maana zaidi ya roho mbaya na hiyo tabia sio mila yetu sisi waafrica

nakataa sababu yoyote zaidi ya chuki na roho mbaya kwa sababu kama kuna changamoto yoyote angeongea na mume wake,
ok leo anakataa mtoto mmoja wa form two je akija kuuguliwa na mzazi kwake itakuaje?maybe kama mke ndo anatunza familia hapo ni sawa kulalamika lakini kama ni wewe basi mwanamke wa hivyo hakufai
N.B
hapa jirani kuna mwanamke yaani yeye ndugu wa mme huwa hawakai akijitahidi ni wiki mbili awe wa kike ama wa kiume sijui huwa anawafanya nini
 
Mambo yamebadilika..., huu wimbo sasa hivi unaleta maana kuliko hata zamani

ukitaka upendwe au ufurahiwe don't overstay your welcome....
 
Huyo jamaa itakuwa ni yeye, eti ufukuze mke kisa unaforce ukae na ndugu ambaye wazazi wake wapo.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ningekuwa mimi mapema angekuwa keshaondoka sababu hata alipokuja kuniomba ushauri wazo langu lilikuwa ni hilo na ndio msimamo wangu, aidha mwanamke akubali kuishi na mtoto au aondoke akitaka. Na huu utabaki kuwa ushauri tu kama ilivyotokea hapa muamuzi atabaki kuwa muhusika. Kumbukeni nimeleta hoja hapa kupima ushauri nilioutoa lakini kwa yote mtakayoongea hata nikimuonyesha hizi jumbe muamuzi wa mwisho ni mtu mmoja tu yeye mwenyewe.
 
Sad story ambayo sikupenda kuiweka kwenye uzi huu; Huyo mwanamke wazazi wake walifariki kwenye ajali ya gari akachukuliwa na mjomba wake kasomeshwa hadi anaolewa ametokea kwa kaka yake mkubwa 😢

Nilihisi tu huyo mwanamke kama kwao sio mafukara basi ashawahi pitia sosono ya akili...

Watu wenye tabia za chuki huwa na chanzo kutokea kwenye makuzi au maisha ya awali...
 
Wewe nawe acha ufala, unaona raha kuvunja ndoa ya watu, huyo mtoto kaingilia utaratibu wa watu hapo, kosa la mwanamke labda ni ile kukubali mara ya kwanza then kugeuka, mtoto wa form 2 tayar kakua, atasaidia ila sio lazima aishi hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sina uwezo wa kuvunja ndoa ya mtu, ushauri umekuja baada ya kuhitajika, nitatoa ushauri yeye ndio atapokea na kufanya maamuzi. Sitasema moja moja afukuze mke bali nitamuweka wazi kuwa mkewe ana roho mbaya na ana makosa
 
Kama ingekua ni mimi huyo mwanamke angeondoka asubuhi saa 11 namuamsha tena akikataa kipigo kinahusika, mwanamke gani hana aibu na roho mbaya kiasi hiko?, mtoto kafiwa ni mipango ya Mungu hakupenda mzazi wake afariki. Tena jamaa awe makini huyo mwanamke atampa sumu oneday... yani mie wanawake wenye tabia za kipumbavu hata awe mzuri kama malaika sitaki ushenzi akafie mbele, unanyenyekea mke! mke! , hata nyau ina mke.
Hajafiwa na we nae
 
Kwenu wakuu,
Kwa muda mchache nimepata ushauri wa kutosha kazi iliyobaki ni kufikisha ujumbe.

Kuna majibu ya aina tatu hapa:
1. Kuna ambao wanakubaliana na maamuzi ya mwanamke, mtoto aondoke
2. Kuna ambao wanapinga tabia ya mwanamke, bora mwanamke aondoke.
3. Kundi la mwisho wanachukizwa na tabia ya mwanamke lakini wanashauri mtoto aondoke kuepusha ugomvi.

Binafsi naungana na kundi la pili, mwanamke asepe. Kuna sababu ya msingi kwa mfano aliotoa scolastika

Ukichunguza kwa umakini hapa mwanamke ana roho mbaya tu Hana sababu yoyote ya msingi. Kama alivyosema scolastika leo kafanyiwa mtoto kesho akimfanyia mzazi wako?!

Naenda kufunguka kwa jamaa akiona ushauri unamfaa auchukue akiona haufai auwache
Memtata fanya hivi ndugu yangu... Chukua huyo mtoto mpelekee mkeo mkae nae. Mbna unalazimisha mwanamke kuachika?
 
Ajabu waliishi na mtoto wa ndugu wa mke hadi sasa yuko chuo na amani ilikuwepo
Hata tutowe ushauri upi huyo mtoto hawezi pendwa na huyo mwanamke, mkilazimisha atamtesa bule.baba yake mdogo amsaidie akiwa huko huko kwao. Kama ni ada atume maana umesema uwezo anao.

Unless utueleze kuwa kwao chakula ni shida.

All in all mtoto arudi kwao asaidiwe huko huko
 
Back
Top Bottom