Mke hataki ndugu zako, utafanyaje?

Mbona kama ni ishu yako na siyo ya rafiki yako mkuu. Humu hatujuani so ukiwa na tatizo lako sema tu kuwa ni lako inakuwa rahisi zaidi watu kutoa ushauri. Ikishasemekana ni ya third party watu hawaipi uzito sana.
 
Uzima wa Mtu haupo katika wingi wa Mali na vitu anavyovimiliki.
 

Baba yupo ila ameachishwa kazi, mama yupo
Binafsi sioni sababu ya kumhamisha mtoto hapo, waishi na mwanao wakikwama ndio waombe msaada wasaidiwe mtoto akiwa kwao wazazi wake. Ukiendekeza haya mambo yanaweza kugharimu sana uko mbele na ukashindwa kureverse situation.
 

umesema vyema kabisa, watoto wa umri huu kama hajaoewa malezi mazuri huko matokeo yake anakuja kuwachonganisha tu kwa kuepeleka maneno ya uongo, utakua atheshimu baba yake mdogo tu lkn mke wake anamwona na yeye kama wakuja tu ligi zinaanza. Haya mambo huwezi kuelewa hadi yakukute.
 
Mkuu amua kama mwanaume kama kweli huyo mke yupo tayari kuachana na wewe sababu ya huyo mtoto mwambie mtoto lazima muishi naye kama anaondoka aondoke

Mkuu kwa mtu mwenye busara na hekima, ushauri huu ni mbovu kabisa maana ni hatari kwa afya ya mtoto kama akilazimisha mtoto aende akae hapo kinyume na matakwa ya mke wake maana kuna mengi uyo mtoto anaweza kufanyiwa na uyo mwanamke akaharibikiwa kisaikolojia.

Wanawake wenye roho kma hiyo ni hatari sana kufanya uamuzi kama huo kwani unaweza mleta mtoto wa watu kwenye dimbwi la manyanyaso, na Mungu akaacha kutoa baraka kwenye familia yako ukabaki unatafuta mchawi kumbe ni mke wako.
 
Mimi binafsi niliwahi kuishi kwa ndugu sababu ya umasikini wa baba yangu na si kwa matakwa yangu nilikuwa mdogo lakini nakumbuka mengi siwezi kuruhusu mtoto wangu akaishi kwa ndugu kamwe ila tu kwa kulazimishwa na hali ikiwemo kifo.

Sisi pamoja na hali yetu duni tuliishi hivyo hivyo na wazazi baba yangu tangu zamani hakua anaruhusu kwenda kuishi kwa ndugu hata bibi, na tulikua na ndg wenye uwezo mzuri tu, ilikua kwenda kusailimia na kurudi, alitupambania mwenyewe na mama hadi tumefika, sasa namwelewa
 
Ushauri wangu achana naye.

Hawezi kuwa juu ya ndugu.

Kubla hujamjua yeye ndugu zako ndiyo waliokutengeneza hadi ukafikia kimo hicho hadi akakuona wewe.Hivyo yeye ni mpitaji TU. Hawezi kuwa na uchungu na wewe.
 

kwani amefiwa au ni baba yake ameachishwa kazi? anyway, mimi kwa umri huo kama mtoto ana nidhamu nitaishi nae vizuri tu ila kama ni yule wa kiburi na uchonganishi kwa ndugu wa mume sitaweza.
 

[emoji1][emoji1] unachekesha
ndio upate huyo atakayetambua kwamba hapo ni kama kwa wazazi wake ili a-assume majukumu ya nyumbani kama ambavyo angelia kwa wazazi wake. Anaweza akaja ambaye hagusi kitu na ukimwambia tu maneno yanafika ukweni mara moja unanyanyasa[emoji18] Haya mambo nyie yanahitaji busara sana.
 

kuliko ukamshauri afukuze mke wake ni bora ukamfungulia huu uzi ausome mwenyewe. Usimshauri mtu amwache mke/mume wake mwache aamue mwenyewe.
 
Mkuu andikishana mkataba na huyo Manzi, kama hataki wa kwako na wewe sema wa kwao basi! Muishi na watoto wenu tu! Siyo anakatwa wa upande wa mwanaume halafu wa kwake anasema sawa!
 
Sad story ambayo sikupenda kuiweka kwenye uzi huu; Huyo mwanamke wazazi wake walifariki kwenye ajali ya gari akachukuliwa na mjomba wake kasomeshwa hadi anaolewa ametokea kwa kaka yake mkubwa 😢
..........Basi huyo mwanamke ana matatizo ya akili.
 
Akikubali kulegea kwenye hili na ajiandae kwa litakalofata hapo ni kuwa mwanaume kamili.
 
Ujinga mkubwa alioufanya huyo jamaa yako ni kuoa. Ataendelea kutafta sana ushauri kwa mambo mengine mengi tu.
 
Arudi ukweni kuishi
 
Mkuu amua kama mwanaume kama kweli huyo mke yupo tayari kuachana na wewe sababu ya huyo mtoto mwambie mtoto lazima muishi naye kama anaondoka aondoke

Ni kweli tena zaidi kama anasema mwanaume kuwa walishawahi kuishi na mtoto wa ndugu wa huyo mwanamke, basi huyo mwanamke ni mbinafasi
 
Ushauri wangu achana naye.

Hawezi kuwa juu ya ndugu.

Kubla hujamjua yeye ndugu zako ndiyo waliokutengeneza hadi ukafikia kimo hicho hadi akakuona wewe.Hivyo yeye ni mpitaji TU. Hawezi kuwa na uchungu na wewe.

Shida kubwa Tanzania ni Upagani, Kikristu baada ya kufunga Ndoa Mke na Mume wanakuwa kitu kimoja, hivyo ndugu hawezi kuwa juu ya Mke (Kikristu) kwa maana wewe siyo mwili mmoja na ndugu yako isitoshe hata ndugu yako atakuja kuwa na kwake, …
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…