Mke hataki ndugu zako, utafanyaje?

Mke hataki ndugu zako, utafanyaje?

Angekuwa mtoto wa nduguyake either dada au kakayake alafu mumewe angekataa angejisikiaje
Kila mtu huona upande wa mwenzie
Kwanin watu wakioana tu wapewe ndugu wa kuwalea??zamani waliishi wapi ,mtu akioa au kuolewa unashangaa wanapelekewa ndugu kukaa nae watu wajifunze kuwaacha watu walooana waishi kwa amani
 
Wengi mnafurahisha sana! Hii kitu ni ngumu sana. Sijaona familia iliyosaidia ndugu akaondoka (baada ya mission completed) kwa kuishukuru. Mwisho wa yote huwa ni lawama tu.

Mtoto umejizalia mwenyewe akikua anakuita mchawi. Anakuua refer case za rombo, moshi mjini na hii ya kwimba ya juzi juzi.

Hivi humu ndani mnajua maana ya ndoa nyie? Unadhani ndoa ni mbususu? Ndoa unatafuta Rafiki wa ukweli, msaidizi wakati wa shida; mtu wa kukufichia madhaifu yako, mtu wa kukufariji etc,

Ndo maana Mie namchumbia To yeye ili Watoto awapeleke kwa Depal ili gharama ziwe kwa Demi na Antonnia awe Mchepuko
😘😘posa lini sasa
 
Kila mtu huona upande wa mwenzie
Kwanin watu wakioana tu wapewe ndugu wa kuwalea??zamani waliishi wapi ,mtu akioa au kuolewa unashangaa wanapelekewa ndugu kukaa nae watu wajifunze kuwaacha watu walooana waishi kwa amani
Lakini ukiolewa mume kulea wazazi na ndugu mwanamke ni jukumu lake ila sio nduguzake?
Mwanamke Hana utu pia watu wachoyo ndo wanahizo,busara angemshauri mumewe waone namna ya kumsaidia uyo kakaake Ili aweze kulea familia yake kama ni mzigo angeuepuka na baraka zao zingeongezeka usikute kaka ndo kamsomesha mdogowake sio et kukataa direct ukiolewa Tanzania ukubali tu familia zetu ni extended ilo lazima litokee
 
Leo naomba mumsaidie rafiki yangu kumshauri, mimi ni nimeshashauri kwa upande wangu lakini nataka kuona fikra za watu zaidi.

Jamaa ana mke na watoto, hivi karibuni kaka yake alipoteza kazi ndugu wakamuomba asaidie kulea mtoto mmoja ambaye alikuwa kidato cha pili. Jamaa alimshirikisha mke wake kuhusu mgeni huyo mke akakubali lakini inaonekana alikubali kwa shingo upande.

Kwa sasa sio siri tena mwanamke kasema wazi kabisa hataki kuishi na huyo mtoto tena akaenda mbali zaidi kampigia simu mama wa mtoto kumueleza yeye hawezi kuishi na mtoto wake. Habari zikamfikia jamaa akashangaa sana aliporudi kumlaumu mwanamke kwanini amefanya hivyo mwanamke kaja juu na kusema hata yeye ana maamuzi kwenye familia na msimamo wake ndio huo, hataki kuishi na huyo mtoto.

Jamaa kabembeleza sana mke akawa kama kaelewa kumbe bado. Hivi juzi kalianzisha tena na sasa amefika mbali kamwambia mume wake achague moja aidha kuishi na yeye(mke) ama mtoto wa ndugu yake........

Mzozo uko hapo, mimi nilimshauri kama hana uwezo wa kumlea huyo mtoto amrudishe kwao lakini si kwasababu ya kukataliwa na mke wake maana hata yeye hajui kesho yake. Jamaa alinijibu uwezo anao maana mtoto anasoma shule za serikali halipi ada hata mia zaidi ya uniform na vifaa vya shule.

Kama nimekosea naombeni sababu, bado tuna nafasi ya kumsaidia jamaa. Kwa ndugu upande wa mume na narafiki zake wanashangaa sana maamuzi ya mwanamke lakini kwa ndugu wa mke anasema zaidi ya 80% wanamsapoti mwanamke 🤔
Atoe chagua la kumwambia asepe mtoto abaki ,huo mda anaosepa atumie nguvu nyingi kufanya saving na kupambana na maisha hawa viumbe hawafai si ajabu anaesema hivo yeye analelewa watoto wa baba mwingine ila nigga hasemi
 
mi nilidhani ukipata manyanyaso ndo unakuwa na roho nzuri kumbe ni tofauti
Ukipata manyanyaso huwezi kuwa na roho nzuri, roho nzuri inatengenezwa ndani ya familia na wazazi jinsi wanavyoishi vizuri ndani na nje ya familia kwaiyo watoto wanaiga mfano Mama kwenye nyumba akiona wageni anaficha chakula au akiombwa vitu vidogo vidogo na jirani au rafiki anasema hana wakati vipo na wakati huo watoto wanaona, kwaiyo watoto wanakuwa na mazingira yale wanayo yaona ni hatari zaidi kwa watoto wakike bora watoto wakiume muda mwingi wanakuwa busy kucheza na watoto wenzao muda mwingi hawakai nyumbani na tabia za Mama wanakuwa hawazion sana.
 
Mkuu amua kama mwanaume kama kweli huyo mke yupo tayari kuachana na wewe sababu ya huyo mtoto mwambie mtoto lazima muishi naye kama anaondoka aondoke
Huu
Kama ingekua ni mimi huyo mwanamke angeondoka asubuhi saa 11 namuamsha tena akikataa kipigo kinahusika, mwanamke gani hana aibu na roho mbaya kiasi hiko?, mtoto kafiwa ni mipango ya Mungu hakupenda mzazi wake afariki. Tena jamaa awe makini huyo mwanamke atampa sumu oneday... yani mie wanawake wenye tabia za kipumbavu hata awe mzuri kama malaika sitaki ushenzi akafie mbele, unanyenyekea mke! mke! , hata nyau ina mke.
Kaka usiseme hivo hawa watu ukiwagusa mamlaka yamewapa ulinzi mkubwa sana juzi nimefanya wazo unalolitaja ila mwisho mimi ndio naonekana mbaya
 
Ni vizuri ulipoamua kuoa siulimuoa yeye Sasa ndugu wakazi gani??
Huo ni usumbufu hata wazungu baada ya ndoa wanaishi na ndugu zao Tena .??
Hapana Kwa sababu ulishakubali kuanza familia na umpendaye .
Sasa hivi ni utandawazi waende bhana kwani wamemuoa nani?

Mtu hata hupewi penzi Kwa Raha unaguna Guna kama mwizi kha nani kwako???

Halafu kazi kuja kuleta ushirikina , ulaghai, uchonganishi .

Ni Usumbufu
Walewale! Hoja za mabinti wa instagram ndio kama hizi. Mnadhani maisha ni kujipaka poda na make up kisha kujipiga selfie.
 
Kama ingekua ni mimi huyo mwanamke angeondoka asubuhi saa 11 namuamsha tena akikataa kipigo kinahusika, mwanamke gani hana aibu na roho mbaya kiasi hiko?, mtoto kafiwa ni mipango ya Mungu hakupenda mzazi wake afariki. Tena jamaa awe makini huyo mwanamke atampa sumu oneday... yani mie wanawake wenye tabia za kipumbavu hata awe mzuri kama malaika sitaki ushenzi akafie mbele, unanyenyekea mke! mke! , hata nyau ina mke.
Hahaaas eti ata nyau ana mke jmn ww
 
Loh! Ushauri wa hivi ukifuatwa waweza kuichana ndoa vipande viwili.

Ndoa inaunganisha ndugu wa pande mbili, sasa mkianza fukuza fukuza ya namna hiyo, mnakuwa mmejitengenezea kisiwa.

Ndugu hawatawasogelea kweli, lakini ndugu hao haao uelewe wana umuhimu wake katika maisha yetu, maana huwa hatuelewi kesho yetu itakuwaje.

Ninadhani busara tupu ni lazima ichukue mkondo kwa masuala kama haya.
Na ndoa ikichanika vipande ndo usalama wa muomba ushauri. Busara inayoonekana ni hii ya kutimua ndugu wa mume na karibisha ndugu wa mke. Hii ndo busara anayoitaka mke. Kwa harakaharaka bado mume yuko kisiwani tu
 
Hoja nzito hii!

Kuna mengi ya ndani hayasemwi. Hasa tabia za huyo anayekataliwa.

Kama ni senema, basi mhusika anayekataliwa haiba na silika zake hazijazungumzwa. Ni ngumu kumjaza na kumtambua kama ndio chanzo cha yeye kukataliwa.

Acha tusubiri kama mtoa mada ataleta data zaidi.
 
Leo naomba mumsaidie rafiki yangu kumshauri, mimi ni nimeshashauri kwa upande wangu lakini nataka kuona fikra za watu zaidi.

Jamaa ana mke na watoto, hivi karibuni kaka yake alipoteza kazi ndugu wakamuomba asaidie kulea mtoto mmoja ambaye alikuwa kidato cha pili. Jamaa alimshirikisha mke wake kuhusu mgeni huyo mke akakubali lakini inaonekana alikubali kwa shingo upande.

Kwa sasa sio siri tena mwanamke kasema wazi kabisa hataki kuishi na huyo mtoto tena akaenda mbali zaidi kampigia simu mama wa mtoto kumueleza yeye hawezi kuishi na mtoto wake. Habari zikamfikia jamaa akashangaa sana aliporudi kumlaumu mwanamke kwanini amefanya hivyo mwanamke kaja juu na kusema hata yeye ana maamuzi kwenye familia na msimamo wake ndio huo, hataki kuishi na huyo mtoto.

Jamaa kabembeleza sana mke akawa kama kaelewa kumbe bado. Hivi juzi kalianzisha tena na sasa amefika mbali kamwambia mume wake achague moja aidha kuishi na yeye(mke) ama mtoto wa ndugu yake........

Mzozo uko hapo, mimi nilimshauri kama hana uwezo wa kumlea huyo mtoto amrudishe kwao lakini si kwasababu ya kukataliwa na mke wake maana hata yeye hajui kesho yake. Jamaa alinijibu uwezo anao maana mtoto anasoma shule za serikali halipi ada hata mia zaidi ya uniform na vifaa vya shule.

Kama nimekosea naombeni sababu, bado tuna nafasi ya kumsaidia jamaa. Kwa ndugu upande wa mume na narafiki zake wanashangaa sana maamuzi ya mwanamke lakini kwa ndugu wa mke anasema zaidi ya 80% wanamsapoti mwanamke 🤔
Ni upumbavu mtoto ana mama yake afu alelewe na mama mwengne?

Mama yake akae na mwanae atasaidiwa pesa tu
 
Leo naomba mumsaidie rafiki yangu kumshauri, mimi ni nimeshashauri kwa upande wangu lakini nataka kuona fikra za watu zaidi.

Jamaa ana mke na watoto, hivi karibuni kaka yake alipoteza kazi ndugu wakamuomba asaidie kulea mtoto mmoja ambaye alikuwa kidato cha pili. Jamaa alimshirikisha mke wake kuhusu mgeni huyo mke akakubali lakini inaonekana alikubali kwa shingo upande.

Kwa sasa sio siri tena mwanamke kasema wazi kabisa hataki kuishi na huyo mtoto tena akaenda mbali zaidi kampigia simu mama wa mtoto kumueleza yeye hawezi kuishi na mtoto wake. Habari zikamfikia jamaa akashangaa sana aliporudi kumlaumu mwanamke kwanini amefanya hivyo mwanamke kaja juu na kusema hata yeye ana maamuzi kwenye familia na msimamo wake ndio huo, hataki kuishi na huyo mtoto.

Jamaa kabembeleza sana mke akawa kama kaelewa kumbe bado. Hivi juzi kalianzisha tena na sasa amefika mbali kamwambia mume wake achague moja aidha kuishi na yeye(mke) ama mtoto wa ndugu yake........

Mzozo uko hapo, mimi nilimshauri kama hana uwezo wa kumlea huyo mtoto amrudishe kwao lakini si kwasababu ya kukataliwa na mke wake maana hata yeye hajui kesho yake. Jamaa alinijibu uwezo anao maana mtoto anasoma shule za serikali halipi ada hata mia zaidi ya uniform na vifaa vya shule.

Kama nimekosea naombeni sababu, bado tuna nafasi ya kumsaidia jamaa. Kwa ndugu upande wa mume na narafiki zake wanashangaa sana maamuzi ya mwanamke lakini kwa ndugu wa mke anasema zaidi ya 80% wanamsapoti mwanamke [emoji848]

Polee sana kwa jamaa!!! Ila hapo akaze sauti yeye ni baba wa familia sauti yake ndo ya mwisho na hakuna wakupinga!!!!! Swala la ndugu kuja om sio jambo baya ila mwanamke asiyetaka ndugu hafai na kama ningeishi nae mimi huyo mwanamke angepata tabu sanaa
 
Wangejua kuwapenda ndugu wa mume inaongeza penzi wasingeendekeza choyo na chuki zao kwa ndugu wa mume
 
Mosi
Mimi naona msimamo mwanamke unawez kuwa sawa kama na yeye ataweza kukubali kuw familia yake isisaidiwe kwa ndugu kuja pale

Pili
Nazan jamaa kama mambo mengine na mkewake yanaenda sawa ni muda wa kumsaidia ndugu huyo juu kwa juu (popote alipo amsidie kwa akili bila kuja kuish nyumbn)

Tatu
Mshikaj ajiandae kisaikolojia kama kwenye ndoa bado wana umri mdogo na apime vzr safar iliyobak na alipofika ili ammue kuanua mapema hii au aendelee kuanika labda kutakauka.
 
Back
Top Bottom