Mke kwenda kujifungulia kijijini, huu ni uchawi

Ndio maana tunakataa msipeleke wake zenu kuzalia vijijini, halafu vitovu vya watoto wote anavitunza shangazi. Anakaa kutwa nzima akiwaroga na kuwaharibia maisha
Hizo mila labda za kwenu ndio zinaruhusu kitovu kuchukuliwa na mashangazi mkuu. Kitovu kimila ni kitu sensitive sana na ukimpa mtu access ya kuwa nacho katika ulimwengu wa roho, mtu anaweza kumfanya chochote anachokipenda ndio maana kitovu siku sote hukabidhiwa mama wa mtoto. Akikifukia, akiamua kuwapa mbwa wale ni sawa tu

Hii ni kutokana na nilivyoelezewa
 
Ha ha ha Mwadada sio kila Kijiji kina huduma mbovu za afya. Nenda kule kwetu Igogwe kuna Igogwe Hospital, halau nenda kule Makete kwa ndugiu zako akina Sugu kuna Ikonda Hospital na Bulongwa Hospital ziko vizuri sana hizo hospitali kiasi kwamba watu wanatoka Muhimbili Hospital wanakimbilia zao Ikonda kutibiwa.
 
👏🏾👏🏾👏🏾👏🏾
Huduma za kiafya ni sawa ila kwa mtoto haswa wa kwanza ni vyema mtu akarudi kwao maana wale wazee hakuna kitu kinachoshindikana kwao haswa kwenye usumbufu wa watoto maana wana experience kubwa.
Kuna sister angu mmoja watoto wake wawili walipigwa na vipele, wakapelekwa hospitali ila dawa hazikuwasaidia ila kuongea na majirani zake vizuri, wabibi wa kisukuma wakampa majani ayachome kwenye jiko la mkaa halafu awafukize na huo moshi.. Siku mbili nyingi vipele vikapotea

I wish pharmacists wetu wafanye research na kuja na tiba asilia simple za kusaidia watu maana hawa wazee wakifariki na maarifa yao, tutakuwa wa kula vidonge na sindano endlessly
 
Na vijijii vingi vyenye missionary centres lazma ukute vina shule na hospitali nzuri tu

Na siku hizi baadhi ya sehemu hata usafiri hausumbui sana kwa hiyo kuna unafuu.. Cha msingi anaepeleka mkewe kijijini asiwatelekezee, huduma atume
 
Na vijijii vingi vyenye missionary centres lazma ukute vina shule na hospitali nzuri tu

Na siku hizi baadhi ya sehemu hata usafiri hausumbui sana kwa hiyo kuna unafuu.. Cha msingi anaepeleka mkewe kijijini asiwatelekezee, huduma atume
Hizo missionary hospitals ziko kwenye vijiji vichache sana
 
Ndugu yangu sijaoa mke ila nimeoa speaker mwanamke anaongea ana mdomo radio ikasome
Naomba niulize swali..nauliza tu. Wanaume mnapenda mwanamke mkimya?? Yani awe kimya kabisa no kuuliza, no what?? Mnajua expense ya ukimya lakin?? Bibi yangu alipoletewa mke mwenzake ndani hakuwezaga kuishi nae kwa sabbu ya visanga..kilichotokea akahama na watoto wake akaenda mahali pengine..ardhi nyingine ya babu na kulikuwa na nyumba huko hata kama si nzuri kama ile aliyoiacha pale pa mwanzo. Bibi hakua muongeaji yani watoto wake wanasema yeye ni shamba, nyumbani..akikaa hapo ni anaweza kaa masaa mawili hajasema chochote. Labda ile kutuma watoto basi..kilichotokea sasa..akaumwa ugonjwa wa moyo. Alianza na presha mwisho moyo umetanuka..na akapataga ugonjwa wa kuzimia tu..anazirai.

Kweli utapata mwanamke atakaa kimya hatakuhoji chochote..atafanya yale yanayotakiwa na kama ni kuumia ataumia ndani maana si hutaki akuulize chochote wala ahoji maana wewe ni mwanaume. Lakin nakuambia andaa pesa za kumtibu baadae..binafsi niko na mwenza wangu. Kuna nyakati naamuaga tu ngoja nisiseme chochote akosee apatie ni yeye. Nafanya majukumu yangu, namuheshimu kama mume wangu hata kama awe anakosea ninachowezaga ni kujifanya nasali..napiga magoti afu nalia sana kama vile nasali kwa Mungu ili ajue ninasali...lakin siwafichi..ndani nahisigi kabisa afya yangu ya moyo si salama na naishi kwa hofu ya kwamba kuna siku naweza kuja kuwa member pale JKCI. Yote haya ni nikae kimya mume apate amani kwamba mke wangu hanibugdhi, hana kelele lakini ndo ndani unaharibika little by little. Mwanamke asipoongea ajiandae, maana wanaume mnayo makwazo na wanawake pia tunayo makwazo. Tunaihitaji sana neema ya Mungu kuishi watu wawili tuliokutana ukubwani..bila Hekima tutafukuza upepo vibaya mno.
 
Kama unanisema mimi
 
Labda kwa ishu ya ukaribu wa huduma ikiwemo uangalizi wa ndugu mfano wazazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…