Mke kwenda kujifungulia kijijini, huu ni uchawi

Naomba niulize swali..nauliza tu. Wanaume mnapenda mwanamke mkimya?? Yani awe kimya kabisa no kuuliza, no what?? Mnajua expense ya ukimya lakin?? Bibi yangu alipoletewa mke mwenzake ndani hakuwezaga kuishi nae kwa sabbu ya visanga..kilichotokea akahama na watoto wake akaenda mahali pengine..ardhi nyingine ya babu na kulikuwa na nyumba huko hata kama si nzuri kama ile aliyoiacha pale pa mwanzo. Bibi hakua muongeaji yani watoto wake wanasema yeye ni shamba, nyumbani..akikaa hapo ni anaweza kaa masaa mawili hajasema chochote. Labda ile kutuma watoto basi..kilichotokea sasa..akaumwa ugonjwa wa moyo. Alianza na presha mwisho moyo umetanuka..na akapataga ugonjwa wa kuzimia tu..anazirai.

Kweli utapata mwanamke atakaa kimya hatakuhoji chochote..atafanya yale yanayotakiwa na kama ni kuumia ataumia ndani maana si hutaki akuulize chochote wala ahoji maana wewe ni mwanaume. Lakin nakuambia andaa pesa za kumtibu baadae..binafsi niko na mwenza wangu. Kuna nyakati naamuaga tu ngoja nisiseme chochote akosee apatie ni yeye. Nafanya majukumu yangu, namuheshimu kama mume wangu hata kama awe anakosea ninachowezaga ni kujifanya nasali..napiga magoti afu nalia sana kama vile nasali kwa Mungu ili ajue ninasali...lakin siwafichi..ndani nahisigi kabisa afya yangu ya moyo si salama na naishi kwa hofu ya kwamba kuna siku naweza kuja kuwa member pale JKCI. Yote haya ni nikae kimya mume apate amani kwamba mke wangu hanibugdhi, hana kelele lakini ndo ndani unaharibika little by little. Mwanamke asipoongea ajiandae, maana wanaume mnayo makwazo na wanawake pia tunayo makwazo. Tunaihitaji sana neema ya Mungu kuishi watu wawili tuliokutana ukubwani..bila Hekima tutafukuza upepo vibaya mno.
Unajua hii concept ya mwanamke mkimya haimaanishi mwanamke asiongee kabisa ila aongee tu panapostahili na ajue kipi cha kuongea kwa wakati upi.

Shida ya wanawake wengi ambao wamekosa maadili au kulelewa na mama pekeyake wakalishwa sumu kuhusu baba zao katika mazingira mabovu huwa wana ile tabia ya ujuaji. Mwanamke anakuwa mropokaji yani hawazi anachoongea anafyatua mineno kama chizi. Intention yake ni wewe ukerekwe tu sababu ya kauli zake zisizo na staha. Mara nyingi wanawake wa hivi wanapenda ku contest/compete na waume zao mtajibizana mwishowe unamzaba kofi anyamaze.
 
Kwanini mamamkwe asije mjini akawacare mama na mtoto huku?? Kwanza mara nyingi kumpeleka mama aliyejifungua ugenini unamuongezea na msongo wa mawazo maana anakuwa na upweke zaidi ya kichanga chake tuu anazungukwa na ndugu asiowazoea.

Akiwa uwanja wa nyumbani kwa mume wake atlist anakuwa na ile uhuru na amani ya moyo hata atarecover mapema.

Sent using Jamii Forums mobile app
mWanamke ni kiumbe kinachozoea mazingira mageni haraka tofauti na unavyofikiria

Huwa ni vizur zaidi akienda kwa mama ake mzazi huko kijijini kama hayupo hata kwao bwana ake sio mbaya
 
Unajua hii concept ya mwanamke mkimya haimaanishi mwanamke asiongee kabisa ila aongee tu panapostahili na ajue kipi cha kuongea kwa wakati upi.

Shida ya wanawake wengi ambao wamekosa maadili au kulelewa na mama pekeyake wakalishwa sumu kuhusu baba zao katika mazingira mabovu huwa wana ile tabia ya ujuaji. Mwanamke anakuwa mropokaji yani hawazi anachoongea anafyatua mineno kama chizi. Intention yake ni wewe ukerekwe tu sababu ya kauli zake zisizo na staha. Mara nyingi wanawake wa hivi wanapenda ku contest/compete na waume zao mtajibizana mwishowe unamzaba kofi anyamaze.

Mkuu unatumia kinywaji gani mkuu?
 
Naomba niulize swali..nauliza tu. Wanaume mnapenda mwanamke mkimya?? Yani awe kimya kabisa no kuuliza, no what?? Mnajua expense ya ukimya lakin?? Bibi yangu alipoletewa mke mwenzake ndani hakuwezaga kuishi nae kwa sabbu ya visanga..kilichotokea akahama na watoto wake akaenda mahali pengine..ardhi nyingine ya babu na kulikuwa na nyumba huko hata kama si nzuri kama ile aliyoiacha pale pa mwanzo. Bibi hakua muongeaji yani watoto wake wanasema yeye ni shamba, nyumbani..akikaa hapo ni anaweza kaa masaa mawili hajasema chochote. Labda ile kutuma watoto basi..kilichotokea sasa..akaumwa ugonjwa wa moyo. Alianza na presha mwisho moyo umetanuka..na akapataga ugonjwa wa kuzimia tu..anazirai.

Kweli utapata mwanamke atakaa kimya hatakuhoji chochote..atafanya yale yanayotakiwa na kama ni kuumia ataumia ndani maana si hutaki akuulize chochote wala ahoji maana wewe ni mwanaume. Lakin nakuambia andaa pesa za kumtibu baadae..binafsi niko na mwenza wangu. Kuna nyakati naamuaga tu ngoja nisiseme chochote akosee apatie ni yeye. Nafanya majukumu yangu, namuheshimu kama mume wangu hata kama awe anakosea ninachowezaga ni kujifanya nasali..napiga magoti afu nalia sana kama vile nasali kwa Mungu ili ajue ninasali...lakin siwafichi..ndani nahisigi kabisa afya yangu ya moyo si salama na naishi kwa hofu ya kwamba kuna siku naweza kuja kuwa member pale JKCI. Yote haya ni nikae kimya mume apate amani kwamba mke wangu hanibugdhi, hana kelele lakini ndo ndani unaharibika little by little. Mwanamke asipoongea ajiandae, maana wanaume mnayo makwazo na wanawake pia tunayo makwazo. Tunaihitaji sana neema ya Mungu kuishi watu wawili tuliokutana ukubwani..bila Hekima tutafukuza upepo vibaya mno.
Wanawake wa hivyo ndio kero. Jambo dogo la kuelekezana atalifanya ligi akujibize ilimradi unywee ajione anakuweza. Mwisho wa siku migogoro ndio inakuwa mtindo wa maisha.

Tazama Ile clip ya jana ya yule nesi aliokuwa anamjibiza mwenzie kuhusu vipimo vya MRDT kisha angalia namna ambavyo yule mwanamke alikuwa anamjibu jamaa utaelewa hasa nachojaribu kukuelewesha hapa. Thats a typical example of wanawake waongeaji kama spika ambao ni kero kwenye ndoa.
 
Wengine hawana lolote
Wanaogopa zile adha za Ujauzito
Mambo ya Kuamshwa Saa 8 za usiku 'Mume wangu nipeleke sheli nataka Harufu ya petrol
Duh mke wangu kwani, Unazaa Bodaboda???

Enewei kama ni kufata Care ya Mama ni heri huyo mama Akaletwa mjini ili kwenda bega kwa bega na mama mjamzito
Kama umepanga chumba kimoja au viwili huyo mama mkwe itakuaje?
 
Mjini ndiko kwenye huduma bora za afya halafu unataka mkeo akajifungulie kijijini ambako huko huduma za afya ni duni. Miundombinu sio rafiki, maji safi na salama hakuna.

Unampeleka huko ili mtoto akizaliwa kitovu chake kichukuliwe na kuungamanishwa na mashetani. Huu ni ushetani daraja la kwanza.

Mambo mengine hayana maana, mkeo akipata changamoto anakimbizwa tena mjini. Hebu tubadilikeni.
Kama anakwenda kwa baba mkwe ni sahihi. Lakini kama anakwenda kujifungilia kwao Kuna walakini na familia Yao. Mtoto lazima azaliwe kwenye asili ya baba yake ili aweze kuungwa kwenye ukoo wa asili yake.

Kwa wale wanaofuata Mila za kiarabu ambazo mjomba ana maamuzi kwenye ukoo hawatanielewa
 
Mtoto anaungwaje kwenye ukoo? Naomba ufafanuzi
 
Back
Top Bottom