Jabakeke kwanza pole mkuu Kwa changamoto.
Ushauri mwingi humu nilio uona unatoka Kwa wavulana,unajua wavulana Wana Tabia ya kutishana tishana Sana,na kibaya Zaidi wanataka na kuwatisha wenzao
Wanaume huwa hawatishwi na matatizo ya wanandoa Fulani ambao kisa Tu eti masingle Maza Fulani wakiharibu basi masingle Maza wote ndio wabebeshwe msalaba? Hapana hiyo sio Sawa hata kidogo.
Si kila single Maza ana sex na mzazi mwenzake ,nakataa ingawa kuna wavulana watabisha Kwa hofu ambazo wanaishi nazo kila siku,lakini hao hao wanaishi na wanawake ambao hawakuwa single Maza lakin wamezaa na wanaume wengine na wao hawajui,inafikirisha Sana ujue!
Si kila wanachongea watu humu ni sahihi hata kama wako wengi kiasi gani,Bali wengi wao wamejawa na hofu Sana juu ya single Maza, ushauri wangu ukitaka kuoa single Maza uwe umepuvuka kimtazamo na kiakili,lkn kinyume na hapo utaishi na mashaka siku zote.
Ishu yako sijaona tatizo kwasababu mkeo alianza kumtafuta Baba mtoto kwasababu baada ya kuona matunzo Kwa mwanae hakuna,naamini kama ungesimamia hiyo show yasingetokea yote hayo.
Swali kwako dalili moja ya kuonyesha haikuwa tayar kuishi na single Maza ni kukataa mtoto wake asije ishi na wewe?
Kwanini huyo mtoto msikae nae,je unadhani mkeo anafurahi kukaa mbali na mwanae? Kama umeamua kumuoa single Maza basi ungekuwa tayar kuwa Baba WA huyo mtoto.
Namalizia Kwa kusema inahitaji akili kubwa kuishi na single Maza ikiwemo na kumpenda mwanae pia na kuchukua majukumu yote ya mtoto.
Kila la kheri