Mke wa Dkt. Mwaka asema yuko tayari kumuachia Dkt. Mwaka kila kitu mradi apate amani

Mke wa Dkt. Mwaka asema yuko tayari kumuachia Dkt. Mwaka kila kitu mradi apate amani

Hizi ndoa za kina adriz Accumen Mo na Converter sijui zikoje? Yani full sarakasi. Bora tu kula kiti moto HADHARANI.
Sijafuatilia mgogoro wao , ila naamini sheria na misingi sahihi katika kila kitu uislamu umeweka wazi tatizo watu wenyewe tu ,hata chakula usipokukula na kukiandaa andaa katika misingi yake lazima kitakudhuru tu.
 
Huyu mwanamke kwa nini analazimisha talaka? kama kuna tatizo kati yake na mwenzie kwanini wasikae chini wayamalize, kama kweli anataka amani? iweje kwake amani iwe inapatikana tu kwa kutengana na mwenzie?

Hapo kuna jambo, huyu mwanamke ndio kati ya wale unamuacha saa sita mchana, ikifika saa nane, unasikia yupo sehemu nyingine anafunga ndoa.
Unatakiwa utambue fika; ndoa hailazimishwi! Ndoa ni makubaliano ya pande mbili. Kama ikitokea upande mmoja hauridhishwi, talaka haikwepeki.

Huwezi kumlazimisha huyo mwanamke kuendelea kumpenda mtu ambaye kwa wakati huu, hayupo moyoni mwake. Kama alivyosema; ni vizuri akasaidiwa ili aachane na huyo mume wake kwa amani, na hivyo kuendelea na maisha yake ya amani.
 
Huyu mwanamke kwa nini analazimisha talaka? kama kuna tatizo kati yake na mwenzie kwanini wasikae chini wayamalize, kama kweli anataka amani? iweje kwake amani iwe inapatikana tu kwa kutengana na mwenzie?

Hapo kuna jambo, huyu mwanamke ndio kati ya wale unamuacha saa sita mchana, ikifika saa nane, unasikia yupo sehemu nyingine anafunga ndoa.
Uhuru ni wake, kishamchoka. Na jamaa anaona mambo yake ya uganga na ushauri wa ndoa yataharibika pabaya.
 
Huyu mwanamke kwa nini analazimisha talaka? kama kuna tatizo kati yake na mwenzie kwanini wasikae chini wayamalize, kama kweli anataka amani? iweje kwake amani iwe inapatikana tu kwa kutengana na mwenzie?

Hapo kuna jambo, huyu mwanamke ndio kati ya wale unamuacha saa sita mchana, ikifika saa nane, unasikia yupo sehemu nyingine anafunga ndoa.

Kwani tatizo ni nini? Akiachwa haruhusiwi kuolewa tena
 
Sasa amejiingiza kwenye mtego wa Dr. Mwaka bila kutarajia.

Nadhani hakuwa anajua kwamba sio kama Dr. Mwaka haitaji waachane, ila ni mwamba hataki waachane kisha wagawane mali

Hii angeijua mapema angezichanga karata zake vizuri.
Nani alikudanganya hivyo kuwa eti kama akitamka hivyo tu na akapewa talaka kisheria hatakuwa tena na uwezo wa kudai mgawanyo wa mali?!!
kwa akili yako unafikiria mbele ya sheria ni ile karatasi tu ya talaka ndio inavunja ndoa?!! ni ndoa ngapi wanaume wanagoma kutoa talaka lakini kutokana na vipengere fulani kisheria vinajitoshereza kuvunja ndoa?!!mfano umemterekeza mke wako wa ndoa miaka 10 hujui anaishi vipi eti uje mbele ya mahakama udai ni mke wako kisa hujampa talaka?!!
 
Huyu mwanamke kwa nini analazimisha talaka? kama kuna tatizo kati yake na mwenzie kwanini wasikae chini wayamalize, kama kweli anataka amani? iweje kwake amani iwe inapatikana tu kwa kutengana na mwenzie?

Hapo kuna jambo, huyu mwanamke ndio kati ya wale unamuacha saa sita mchana, ikifika saa nane, unasikia yupo sehemu nyingine anafunga ndoa.

Talaka ni haki ya kila mmoja aliyepo ndani ya ndoa ikifikia hatua hiyo! Mamlaka ya Muumba yanaruhusu na hata mamlaka ya nchi yanaruhusu.

Kama kweli huyu dada anachokisema kinatoka moyoni na hana hatia juu ya hili, basi huyo Mwaka ajitafakari.

Hili jambo limeibua madhaifu mazito kwenye taasisi “nyeti” 2 ambazo kwa kiasi kikubwa ni mihimili muhimu katika ujenzi wa familia, jamii na taifa kwa ujumla!!

Ndoa na Uislam.

Tunaendelea kujifunza at the expense ya watoto! Mungu tuongoze.
 
Bi Queen apiga magoti na kusema anachohitaji zaidi yeye kwa sasa ni Amani, na kwamba yuko tayari kumuachia Mwaka kila kitu ili abaki na amani na kulea watoto wake.

Amesema kuwa anatamani mwisho wao uwe na amani, na kama kuna chochote Dkt. Mwaka anakihitaji basi amwambia ni njia zipi apite lakini vitendo vya kupelekana polisi kutengenezeana kesi na kudhalilishana kwenye mitandao si kitendo kizuri, mitandao isitumike vibaya kudhalilishana.

Akiongeza kuwa kauli ya Dkt. Mwaka alivyosema kuwa 'bado anampenda lakini hayuko tayari kuishi na yeye' imetosha kabisa kuonesha kuna sababu nyingi za kufanya wao wasibaki pamoja.

Amuomba Rais Samia, viongozi wa serikali na viongozi wa dini wamsaidie ili apate haki yake awe huru na kupata amani.
dini ya wisilamu inatambua kuwa kila kitu kina mwisho hata haya maisha tunayo ishi yana mwisho

hivio basi ndio katika wisilamu sio jela wala adhabu kama mwanamke anaone awezi endelea kuishi na huyo mume wake kutokana na sababu mbali

akaona akiendelea kuishi nae atomtii mume huyo hivio akaisi kupata dhambi sher,iya inampa ruhusa mwanake huyu kujivua yana kurudishia mumewe mahari yake hili hawe huru kama hana anaweza kupewa na kaka zake baba yake mama hata watoto wake

huo ndio ubora wa mwanamke kuolewa kwa kiasi kidogo hili akiona hana mume anamzingua anarudishia chake anasepa atakako

lakini kama mke huyo anafanyia hila hili aachike bila sababu mwanamke huyo akifa hawezi iona pepo ya allah makazi yake yatakuwa motoni milele

ifaamike talaka iko kwa dini wauwisilamu tu sio vinginevio sababu dini nyingine hazina mfumo huo
 
Ego and pride nadhani imesababisha haya yote. Kuna mdada hapa akandika wenye maneno mengi Kama manyara ,nwaka na sijui Nani vile
Hawakujua katika suala la ibaada hamna haja ya kuonyesha kwamba umeweza na umefanikiwa Allah kwamba ndoa hutunzwa na Allah, wengine tunapendana na ndoa zetu zimetulia sio kwa ujanja wetu laa. Manara na Mwaka msirudie hivyo vibri vyenu tena.
 
Huyu mwanamke kwa nini analazimisha talaka? kama kuna tatizo kati yake na mwenzie kwanini wasikae chini wayamalize, kama kweli anataka amani? iweje kwake amani iwe inapatikana tu kwa kutengana na mwenzie?

Hapo kuna jambo, huyu mwanamke ndio kati ya wale unamuacha saa sita mchana, ikifika saa nane, unasikia yupo sehemu nyingine anafunga ndoa.
ndio ni kitu kinacho fika mwisho kama mambo mengine pia ndoa katika iimani ya uwisilamu sio jela wala adhabu
 
Back
Top Bottom