Mke wa mtu ni Sumu ila Mume wa mtu ni Asali?

UMUGHAKA

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2021
Posts
2,753
Reaction score
12,932
Nsikuchoshe na Usinchoshe, Tusichoshane!

Kumekuwa na Video ya Binti mmoja inayozunguka mitandaoni ikionyesha namna anavyobakwa na kukawitiwa na Vijana kadhaa,Vijana hao ambao wamesikika wakitamka hadharani na kumshurutisha yule Binti akili hadharani na kumuomba radhi Afande.
Kwa akili ya kawaida,yaelekea yule Binti alitembea na mume wa huyo anayeitwa "Afande" ndipo huyo "Afande" akawatuma hao jamaa kumfanyia huyo Binti tendo la kikatili na ambalo halipaswi kuvumilika katika jamii ya wapenda haki na wapinga maovu!

"Inasemekana" na hao jamaa waliomfanyia huyo Binti huo ukatili ni askari au wanajeshi (Sina hakika).

Jambo ambalo limefanya nikaandika huu Uzi ni kwamba,inaonekana wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu huwa wanachukizwa na matendo mabaya pekee wanayofanyiwa wanawake ila tendo kama hilohilo akifanyiwa mwanaume kumekuwa na ukimya na wengi wao wakifurahia!

Akikamatwa mwanaume ambaye yawezekana amefanyiwa tukio kama alilofanyiwa huyo Binti,watu wengi wakiwemo hao wanaojiita wanaharakati na watetezi wa haki za Binadamu huwa wanasema "MKE WA MTU SUMU,MKOME KUTEMBEA NA WAKE ZA WATU"

Haohao watetezi wa haki za Binadamu na wanaharakati,wakikuta Binti amefanyiwa tukio hilo hilo baada ya kufumaniwa na mume wa mtu,husema "HUU UDHALILISHAJI HAUKUBALIKI NA TUNAUPINGA VIKALI"

Sasa,Mimi kama mtu mwenye akili timamu nimekuwa nikijiuliza maswali mengi sana ambayo mtu mjinga sidhani kama anaweza akawa na majibu,inawezekanaje mume wa mtu akawa asali hadi mwanamke aliyetembea naye atetewe wakati huohuo mwanaume aliyetembea na mke wa mtu aambiwe "Mke wa mtu sumu ?"

Mimi binafsi nachukizwa na kile kilichofanywa na hao wahuni na naliomba jeshi la polisi lichukue hatua Kali dhidi yao

Tunapoamua kutetea Utu wa mtu hatupaswi kuchagua upande,inapaswa tusimame na watu wote,matendo mabaya wanaofanyiwa Binadamu wenzetu yanawaumiza wote,siyo kwamba mwengine ana moyo wa chuma na mwingine ana moyo wa nyama!

Kama "MKE WA MTU NI SUMU" vile vile iwe "MUME WA MTU NI SUMU" siyo Mke wa mtu sumu halafu mume wa mtu iwe asali,hili halikubakiki!

USHAURI WA BURE

Unapomfumania mkeo Dili na mkeo,siyo mgoni wako,Kumpiga au kumfanyia vitendo vya kikatili mgoni wako,hakutabadili tabia mbovu za mkeo!

Pia,Unapomfumania mumeo na mgoni wako Dili na mumeo,kumpiga au kumfanyia vitendo vya kikatili mgoni wako,hakutabadili tabia mbovu za mumeo!

Yangu ni hayo tu Kwa Leo,niwatakie asubuhi njema!
 
Noma sana ila video sijaiona ,mwenye nayo anitumie inbox.
 
Kwa pande zote ukimfumania mmeo dili na mmeo,ukimfumania mkeo dili na mkeo,hiyo ndo akili otherwise ni upumbavu.
Unakuta mwanamke anadanganya hana mme,unakuta mme anadanganya hajawahi kuoa,mtu ambaye ana akili atadili na mtu wake,tofauti na hapo ni ujinga mtupu.
Mtu kama mmeshindwana si unaachana naye?
 
Njia bora usiangaike na binadamu kwa njia negative haijalishi ni mke wako au mme wako.
 
Hii ni chai tupu! Video ipo wap? Mnapiga keleeee video hamna ujinga mtupu.
 
Ni search nini ili niione
Mkuu Mimi nilikutana nayo kwenye komenti kwenye moja ya Uzi,Wewe nenda kwenye nyuzi zinazo zungumzia hiyo habari unaweza kukutana nayo kwenye Komenti Kwa wazee wa Engagement
 
Back
Top Bottom