Mke wa Profesa Jay afunguka, familia yaomba msaada wa matibabu

Mtu wa watu!

Wakati mnasema mnataka privacy hamkujua Jay ni mtu wa watu? Kuiga tamaduni za kizungu ambazo hatuzielewi wala hazituhusu....

Walitoa tamko kwa umma Jay na familia wanaomba tuwape faragha zao wakati wakiuguzana.... leo wanasema tuungane nao kwa mchongo wa pesa na maombi.... tushike lipi ?

Wenzenu Ulaya huko wakisema gwiji fulani jamani linaumwa linaomba privacy yake hawawezi kurudi baada ya siku tatu kupiga yowe tumsaidie....
 
Boss,hawajapiga yowe, kama hujapendezwa na kitendo walichofanya kaa tu kimya haina haja ya kusema. wapo watu watatuma pesa hata jero jero jamaa atapona
 
Kila wakati huwa nasema hawa wasanii wawe wanaangalia na kujifunza kutoka kwa wenzao,hawa wasanii nyota ni kama hawajui kuna kesho, hawa wasanii wakiwa kwenye good time hawajui kesho na hawajuia kama kuna watu wana shida na kuwa kuna siku nao watakuwa hawana kitu.

Mimi nikiugua au ndugu yangu akiuugua siji mitandaoni kuomba msaada,ni mzigo wangu. Ukienda pale Muhimbili kuna mwembe unaitwa Mwembe mawazo huwa wanakaa watu mbalimbali kila mtu anahangaika na mgonjwa wake,utasikia huyu anapiga simu uza shamba,au muambie baba mdogo achangie , na wala hutawasikia kusema tuweke namba zetu mtandaoni tuwaombe watu.

Pamoja na umasikini wao, mzigo wangu ni wa kwangu, kila mtu abebe furushi lake! hawa wasanii hakuna wanaowasaidia wakiwa kilingeni wao ni starehe na watu wao.
 
Mungu afanye miujiza tu .Ila itakuwa katika terminal. Unamkumbuka kocha Mziray(R.I.P)Na yeye ilipofikia terminal ndo ikawa basi tena.
Dah umenikumbusha kocha Mziray dah umenipa simanzi sana. Alikua akinipa moyo sana na mara kwa mara nikienda ofisini kwake pale OUT Kinondoni. Mzee wangu huyu alikua muungwana sana. Wallah Allah amsitiri kaburini mja wake.
 
Tatizo la wasanii wanaishi maisha ya kifahari sana na kuwaona raia wa kawaida kama kinyesi ila wakiumwa haraka sana wanatembeza bakuli tuwachangie.
Prof siyo mtu wa matambo, ila hii imenifanya niwaze jinsi Watanzania wengi tulivyo na shida.

Kama Prof mtu ambaye amekuwa msanii kwa muda mrefu, akawa mbunge kwa miaka mitano imekuwa hivi, je kwa karundage tulio wengi!

Serikali ifanye namna aisee kwenye suala la matibabu ya wananchi wake.

Tumchangie Prof hasa sisi ambao ni generation ya kipindi cha chemsha bongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…