Mke wa Profesa Jay afunguka, familia yaomba msaada wa matibabu

Mke wa Profesa Jay afunguka, familia yaomba msaada wa matibabu

Kumsaidia mtu matibabu ya ugonjwa unao msumbua ili ujue unatoa kiasi gani. Kuna watu labda wangependa kujitolea viungo vyao au kwenda zaidi ya hapo.
Wakikutajia gharama bila kutaja ugonjwa utachanga? Maana unaweza ukaambiwa matibabu yanataka Tshs. 1B, lakini ugonjwa usitajwe, UTACHANGA?
 
Boss,hawajapiga yowe, kama hujapendezwa na kitendo walichofanya.... wapo watu watatuma pesa hata jero jero jamaa atapona

Ndio, watu watatoa chochote kwa sababu Waafrika tukiuguliwa tunakuja pamoja....

Wataacha kujifanya wazungu, eti tunataka privacy yetu....

Sasa privacy imewatokea puani, wanapiga yowe...

Sio kila anachofanya mzungu ni umaridadi wa kuiga jamani...

Huwezi kukuta Mwarabu anaiga mila za mzungu, atajilipua bomu kabla hajaiga
 
Kila wakati huwa nasema hawa wasanii wawe wanaangalia na kujifunza kutoka kwa wenzao,hawa wasanii nyota ni kama hawajui kuna kesho, hawa wasanii wakiwa kwenye good time hawajui kesho na hawajuia kama kuna watu wana shida na kuwa kuna siku nao watakuwa hawana kitu, mimi nikiugua au ndugu yangu akiuugua siji mitandaoni kuomba msaada,ni mzigo wangu. Ukienda pale Muhimbili kuna mwembe unaitwa Mwembe mawazo huwa wanakaa watu mbalimbali kila mtu anahangaika na mgonjwa wake,utasikia huyu anapiga simu uza shamba,au muambie baba mdogo achangie , na wala hutawasikia kusema tuweke namba zetu mtandaoni tuwaombe watu pamoja na umasikini wao, mzigo wangu ni wa kwangu, kila mtu abebe furushi lake! hawa wasanii hakuna wanaowasaidia wakiwa kilingeni wao ni starehe na watu wao.
Acha roho mbaya mkuu binafsi jamaa alipiga hela ila majanga yalikuwa mengi! Imagine uvunjiwe nyumba ghafla unafikiri kujenga same house ni bei gani?

Naskia pia mbowe alikusanya hela toka kwao ku fund kampeni za lissu mwaka 2020. Sasa hebu imagine una 150M na unevunjiwa nyumba. Ujenge nyumba mpya labda 60M hivi na makorokocho ya ndani 75M kuna hela tena humo?

Hapo bado kuna mke na mtoto wa kum support haya kingine akakosa ubunge term iliofata. Nilipoona mkewe kaanza tu kuwa MC nilihisi tayari kuna tatizo kwenye ile familia.

Kwa stage ya maisha aliyofikia hakuwa mtu wa kuunga show au kutafta kazi ya utangazaji. Let the nigga fight for his life jamani tum support sababu mitihani ni sehemu ya maisha hakuna mtihani mgumu kama kuumwa. Mungu amjalie afya aweze kuendelea ku support familia yake tuache kiburi cha uzima na mabezo.

Ipo siku na sisi tutapitia kuumwa tu wala sio swala la kumbeza mtu na kumkejeli. We would all need help in some way.

Hata uwe na million 100 jiulize dialysis kila week ni laki 3 unafikiri ni hela kiasi gani utatumia ukilala kwa week 20 tu? Bado gharama za kitanda kwa VIP daily kulala unaweza pigwa laki au zaidi. Matibabu sio rahisi tuache kiburi cha uzima jamani!

Bima tulizonazo nyingi ni za janja janja inakutibia magojwa ya malaria tu na UTI magonjwa mazito inakuacha upambane na hali yako nyie acheni tu!
 
Tatizo la wasanii wanaishi maisha ya kifahari sana na kuwaona raia wa kawaida kama kinyesi ila wakiumwa haraka sana wanatembeza bakuli tuwachangie.
Unaweza ukawa sahihi ila sio kwa Jay wa mitulinga.

1. Profesa Jay ndo alinifanya nipewe ruhusa ya kugusa radio ya mkulima kwa kumsikliza dj abubakari sadick au do diary warungu nikitoka shule...
2. Muda mwingine wasanii maisha ya show off hakuna watakachovutia jamii ndogo ambayo inataka kuwa kama wao.. mfano msanii kama harmorapa
 
Mungu afanye miujiza tu .Ila itakuwa katika terminal. Unamkumbuka kocha Mziray(R.I.P)Na yeye ilipofikia terminal ndo ikawa basi tena.
Dah ila Ngoma ni mtihani sana aisee noma yani kwa kweli. Kama ni mkono wa Nyani itakuwa mbaya sana aisee. Figo na ini huwa lazma zikate moto chap.
 
Miafrika matatizo matupu sasa ugonjwa nao ni wakuficha,binafsi yangu nilikuwa tayari kuchangia ila kama hawaweki wazi ni uhonjwa gani basi wacha waendeelee.
 
hakuna sababu ya msingi kutaja ugonjwa wa mtu. Tuheshimu faragha za watu.
Basi kama Hamna sababu unaomba msaada wa nini? Hela zinatafutwa kwa jasho hazitoki kama njugumawe kama unahitaji msaada huna budi kusema kinachokusibu
 
Kila wakati huwa nasema hawa wasanii wawe wanaangalia na kujifunza kutoka kwa wenzao,hawa wasanii nyota ni kama hawajui kuna kesho, hawa wasanii wakiwa kwenye good time hawajui kesho na hawajuia kama kuna watu wana shida na kuwa kuna siku nao watakuwa hawana kitu, mimi nikiugua au ndugu yangu akiuugua siji mitandaoni kuomba msaada,ni mzigo wangu. Ukienda pale Muhimbili kuna mwembe unaitwa Mwembe mawazo huwa wanakaa watu mbalimbali kila mtu anahangaika na mgonjwa wake,utasikia huyu anapiga simu uza shamba,au muambie baba mdogo achangie , na wala hutawasikia kusema tuweke namba zetu mtandaoni tuwaombe watu pamoja na umasikini wao, mzigo wangu ni wa kwangu, kila mtu abebe furushi lake! hawa wasanii hakuna wanaowasaidia wakiwa kilingeni wao ni starehe na watu wao.
Kitu usichokijua ni bora ukae kimya mkuu,hivi yeye anapotoa msaada kwa wengine wewe utawezaje kujua au ulitaka awe anatangaza kila anaposaidia!,tenda wema nenda zako.

Tetesi ni kuwa ana shida ya figo,hiyo kitu inaitwa dialysis isikie tu kwenye bomba wala usiombe ukapata mgonjwa kwenye familia akahitajika kufanyiwa hiyo kitu,kama tajiri Luge ilifikia mahali kuombewa michango,Prof J ni nani,weka akiba ya maneno mkuu,kesho yako huijui...
 
Prof siyo mtu wa matambo, ila hii imenifanya niwaze jinsi Watanzania wengi tulivyo na shida.
Kama Prof mtu ambaye amekuwa msanii kwa muda mrefu, akawa mbunge kwa miaka mitano imekuwa hivi, je kwa karundage tulio wengi!
Serikali ifanye namna aisee kwenye suala la matibabu ya wananchi wake.
Tumchangie Prof hasa sisi ambao ni generation ya kipindi cha chemsha bongo
Tunaishi kwa kudra tu,kiuhalisia Watanzania wengi ni zaidi ya maskni
 
Back
Top Bottom