Mke wa Profesa Jay afunguka, familia yaomba msaada wa matibabu

Niliuguza mgomjwa wa figo 2018-2021 mkuu, nilijua mengi kuhusu huu ugonjwa. Nilitembea sana Muhimbili na Mloganzila hivyo najua kiasi chake.
 
Wasanii wakubwa wengi wakiwa kwenye pick maringo na nyodo, wakiumwa au kufulia wanakuwa wema na kutaka huruma za mungu.
 
Duh kwa kweli Mungu mwenyewe tu amsimamie na amponye tuchange kwa tulichojaaliwa hakuna aijuaye kesho maana hata jana alikuwa mzima kama sie.
 
Naona unatoa mipovu kama fisi, hata nikiwa ni mimi au ndugu yangu sitaomba msaada wa kutembeza bakuli, hayo sijui ya figo au nini sio yeye wa kwanza kuugua ,urafiki wako peleka huko kwani wangapi wana tatizo la figo na umewachangia?
 
Wangapi wanaugua figo na wanatembeza bakuli kwenye vyombo vya habari,wangapi wana wagonjwa mahututi wanatembeza bakuli,kuwa superstar hakufanyi wewe upendelewe zaidi ya wengine, nenda Muhimbili ndio utaona kila mtu anabeba msalaba wake kimya kimya, tunapokuwa na pesa tujue pia kuna kesho,nilichoandika sio roho mbaya bali ni kutuasa sisi sote, nadhani sote tunamkumbuka mzee Majuto pamoja na mikataba yote na hela nae ikawa hivi hivi, najiuliza ni kwanini bakuli liwe kwa watu maarufu tu tena wenye pesa na isiwe bakuli kwa malofa wenzetu ambao wapo hoi bin taabani mahosipitalini? mbona hatujifunzi?
 
"Wakati tunaanza kuuguza hatukutarajia kama itakuwa serious, tulijua ni kitu cha muda mfupi."

Nimewaelewa sana hapa.

Inauma. Ila msife moyo.

Wakati ni mgumu lakini mtashinda.

Na hamtaamini mmeshindaje.

Mungu ni wa ajabu sana.
Mimi nauguza baba yangu, wakati anaanza kuumwa tulijua tu ni kwa muda tu atakaa sawa, wanachokisema nawaelewa sana, hali hii isikie tu kwa wengine, get well soon Prof.. Mungu akufanyie wepesi upone haraka
 
Jamaa Tutamchangia Na Kumuombea Ila Ukweli Mchungu. Kuchomoka Ni Ngumu sanaa. Tunakupenda Legend. Hata Ruge Ilianza Hivi. Muhimbili wakikulaza Zaidi ya Wiki ni Ngumu kutoka.

Figo unavyozidi kukaa hospital ndio zinazidi kuwa Mbaya
 
Naona unatoa mipovu kama fisi, hata nikiwa ni mimi au ndugu yangu sitaomba msaada wa kutembeza bakuli, hayo sijui ya figo au nini sio yeye wa kwanza kuugua ,urafiki wako peleka huko kwani wangapi wana tatizo la figo na umewachangia?
Mwenzio ni public figure,sasa wewe utembeze bakuli nani anakujua ? punguza wivu mkuu...
 
Ruge aliwekeza nini na nini outside cmg?
 
Mkuu Unajua maana ya Privacy ? Kutaka mambo ya ndani kukaa ndani sio utamaduni wa kizungu hata huku tunao;

Faragha ni muhimu hata ukitoa pesa sio kwamba ndio una Haki ya kujua au kupewa daily feedback (utapata information panapobidi)
Ukisema unataka faragha maana yake uachwe kivyako, hutaki kufuatiliwa una hali gani, umeambukizwa na nani, uko wapi, unatibiwa na nani, unaletewa chakula na nani.

Lakini sisi Waafrika hatuko hivyo wakati wa shida!

Huyo mkewe au mwana familia aliyetoa tamko kwa umma alituletea mikogo ya kizungu, sasa mikogo imemtokea puani. Ajifunze na abadilike, kuiga kila cha mzungu utapasuka msamba.

Unataka privacy halafu unataka tushikamane na wewe, tushike lipi ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…