Mke wangu alibadilika baada ya kumfungulia biashara. Nifanye nini kuokoa ndoa yangu?

Karibu fazaa hawaa kenge bilaa hivyoo watatuchezea sanaa yani utatunza mafala watakulaa tuu
Tutoke huu uzi twende kwenye wazee wa kuweka mzigo [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Inaonekana mkeo sasahivi anataka kuingizwa mjini kwa nguvu za ndugu na marafiki. Na inaonesha hio biashara ilikuwa ina wasaidia mkweo na shemegi zako.

1 Mkataze wife kutoa namba yake binafsi na awe anawapa wateja namba ya biashara.
2 Mrejeshe wife kazini sababu akiwa busy na kazi hatokuwa na muda wa kuongea/text na wanaume mwengine sana kama akiwa nyumbani tu.
3 Ongea na wife juu ya rafiki yake(kuwadi) ili ajuwe nyendo zake, jiongeze kuongea na wife kama rafiki pia mtowe outing weekend ajuwe ana mume na aondokane na mawazo ya mwanaume.
4 Jenga familia yako usishuhulike na ukoo/familia ya mke wako.
5 Mwanaume ni general wa familia kuwa na mikakati ya kifamilia jinsi unavyotaka iwe.


Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
 
Mwambie achague moja kati ya ndoa au kuendelea na wanaume wengine, na Mwambie kabisa kuwa endapo ukija gundua issue yoyote ya usaliti anakwenda kwao....kuwa na sauti yenye maamuzi magumu.

Sent from my EVA-L19 using JamiiForums mobile app
Na maamuzi magumu yatahitajika maana mwanamke ukimlegezea anataka akuchukulie falaaa, sasa siku moja jamaa anatakiwa asale na huyo mwanamke akute mizigo nje na aambiwe ondokaa aone hao ndugu zake kama watakuwa nae karibu tena akiwa nyumbani m@maee
 
Hivyo nilifunga biashara for a while nikitafakari nini cha
Brother hakikisha huwi na wivu kumzidi mkeo itakugharimu ishi nae kwa akili,mimi niliwahi kuwa na demu nikamfungulia mgahawa akawa anatafutwa hadi usiku wa manane ikafika december krismas nikawa na simu yake ikaingia msg whatsap "mery chrismas my love" kutoka kwa jamaa anaitwa kevi...allow nikawaza niipasue au nifanyeje ila nikatumia hekima nikamwambia demu kama anataka nimfanye kitu mbaya huyo jamaa waendelee wala sikuhangaika nae tena akaona nna msimamo Nikaona tu yeye mwenyewe anawafokea..... mwanamke ukimganda sana atapigwa tuu maana wao wameumbiwa wivu,mpe uhuru pia mpe mipaka yenye kumgarimu
 
Mkuu kuhusu outing hilo ni jambo nilifanyalo angalau mara mbili kwa mwezi kutokana na ratiba za kazi zinavyo tubana wote wawili.

Ila kuhusu baishara kuwasaidia kwao hili pia nimelijua baada ya kutaka kuifunga biashara maana nilihitaji kujua hela jumla iliyopo ndio ananiambia kunahela amempa kaka yake kama laki 5 hivi .

Mengine nitayazingatia hasa hili la kuanzisha namba mpya ya biashara kwa ajili ya kuwasiliana na wateja wake.

Ahsante sana kwa ushauri mkuu.
 
Hii nitazingatia pia mkuu.

Ahsante sana.
 
Mkuu mimi mwanamke kutoa pesa bila kunishirikisha hapana, anampaje kaka yake bila kukushirikisha? Kuwa na sauti na msimamo uone huyo mwanamke atakavyokuwa hatafanya upuuzi huo, mwanamke ni msimamo.
 
Mkute huyo rafiki yake mpige marufuku aache tabia mbovu, najua kumuacha mke ni ngum aisee ukizingatia mnawatoto dah! Em kaa na huyo mwanamke mzungumze maisha yalivyo na jinsi kipindi akiwa single mother itakuwaje?
Fuata huu ushauri. Usiumie moyoni bila sababu.

Mleta mada eleza vyema msimamo wako auelewe. Atabadilika. Usifikirie kuachana. Tatizo dogo hilo linatatuliwa.
 
Yes, yes, he's the General of the family.

Ushauri mwingine wa kuufuata ni huu.
 
Masihara tu hayo boss jikaze
 
Mkuu mimi mwanamke kutoa pesa bila kunishirikisha hapana, anampaje kaka yake bila kukushirikisha? Kuwa na sauti na msimamo uone huyo mwanamke atakavyo kuwa hatafanya upuuzi huo, mwanamke ni msimamo.
Mkuu biashara niliiacha huru mikononi kwa wife sikutaka kuifuatilia hasa kwa jinsi alivyokuwa anaimudu wala sikutaka kuwa CAG kwenye hii biashara.

Hivyo hata alivyokuwa akitoa hela kwa ndugu zake nilikuwa sifahamu. Ila angetoa hela kwa kunishirikisha wala nisingemkatalia.


Ahsante
 
Big noooooh! Akianza kutoatoa hela kwa ndugu bila kukushirikisha atàanza kuhonga pia mpaka mtaji kwa wahuni! Hawa watu siyo wa kuwasusia shamba hivyo, lazima mahesabu uyajue, vinginevyo utakua unaombwa mtaji baada ya mtaji kalagabaho!
 
Mkuu usihangaike kumchunga mkeo kama ni wa kuchapwa atachapwa tu tafuta pesa kwaajili ya maendeleo ya familia yako
 
Pole sana kwa changamoto, huyo Mke wako kama ni mwaminifu anatakiwa kujua kuwa yeye ni Mke wa mtu hivyo anatakiwa kuwa ni msimamo na siyo vinginevyo, endelea kumpa mikakati yako atulie kwenye ndoa yake vinginevyo atajua hajui.
 
Sasa mkuu wewe humpi show kali kitandani au maana pesa ipo anatafutiwà bwana kwa nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…