Mke wangu alibadilika baada ya kumfungulia biashara. Nifanye nini kuokoa ndoa yangu?

Mke wangu alibadilika baada ya kumfungulia biashara. Nifanye nini kuokoa ndoa yangu?

Habari za jumapili wanajamvi.

Niende Moja kwa Moja kwenye mada inayoniumiza kichwa mpaka nakosa amani ya moyo kwa muda wa week sasa.
Mkuu kama ameisha ingia kingi kwenye mitongozo achana nae, wanawake hawafugiki...hata ukiamua kufunga biashara haisaidii, wakati upo Muhimbili miezi mitatu je una uhakika gani kama alikuwa haliwi na kama tayari ameshaliwa wewe ukimkaza unaona tofauti ya sasa na ya zamani? Kama huoni basi acha kumfuatilia, utaumia au kuumiza.

Wewe ishi maisha yako ukiwa naye, wewe sasa ivi huwezi mtimizia mahitaji yake ya mwili na familia.
Mwanamke hawezi kumlea mwanaume labda awe sugarmamy
 
Fanya hivii mdinye huyo rafiki yake alafu utengeneze mazingira mkeo ajue uyo rafiki yake ni msaliti anataka kumharibia ndoa yake
Samahani mkuu kwakukutag tena, ila huyu rafiki wa huyo mwanamke niwakupigwa mashineee.
 
Kukaa ndani kunamfanya asionekane kwa wanaume wengi. So kunapunguza kutongozwa

Kufanya biashara kunamfanya aonekane au akutane na wanaume wengi. So kunaongeza mitongozo. Na wanaume mbinu zetu unazijua. Swali la kujiuliza, je atakataa wangapi? Kukataa wote siyo rahisi

Mamamkwe na hao ndugu zake wengine lazima waje juu coz tayari alikuwa anawarushia visenti senti

Akili yako maamuzi yako
 
NDUGU WA WIFE:

Hawa watu walianza kuongea maneno ya hivyo sana kuwa mimi sitaki maendeleo ya ndugu yao baada ya kuona sasa hivi ameanza kufanikiwa ndio nataka kumrudisha nyuma bila kuangalia kiini cha tatizo.
nga akaze na biashara ili awe huru kutoka kwenye ndoa kiufupi hawafurahii hiyo ndoa
Umeongea vyema mkuu ingekuwa ni mimi kichwa kibovu wanaongea hivyo kuwa wamempa mtaji ningewaita baba na mama yake nikwaambia kama mnaona mtoto wenu simuhudumii leo hii afungashe muondoke nae unajaa sum kabisa huku nakipanga kilicho nolewa nyuma ya nyumba. [emoji23][emoji23]
 
Huyu mama ni mtu mzima wamejuana hapo Kwenye biashara ila yeye ni hawa wanawake wa kiswahili.

Nimeshachukua namba yake natafuta muda niongee naye pia huyu mama.

Ahsante kwa ushauri mkuu.
Mimi nikushauri tu; achana na huyu third party. Atapata sababu ya kusambaza mambo yako na mkeo eneo lote hilo, mkeo ataona biashara chungu. Anaweza kwenda hapo dukani akaanza kumbwatukia "kwahiyo umemwambia mumeo mimi ndo nakutaftia mabwana? Si ni umalaya wako" Tayari umefanya jambo dogo kuwa kubwa.

Zungumza na Mkeo kwa uwazi kabisa kuwa kuna vitu kama mume hutovumilia na vitapelekea kuvunja agano lenu. Kama huyo mama ndo kishawishi (i doubt this sana, nahisi huyu mama anatumika tu kama njia na mkeo) basi mwambie Mkeo akae naye mbali. Yeye atajua afanye nini. Hakuna mwenye jukumu la kulinda ndoa yenu zaidi ya nyie wawili.

All in all I pray mrudi katika hali ya awali.
 
Hana namba ya biashara wakati tunaanza biashara hatukufikiria haya mengine. Hivyo iwapo tutafikiria kuendelea na biashara hili litazingatiwa.

Kuhusu biashara ni kweli inatulipa sana kwa sababu kupitia hapo tunalipia ada ya shule watoto wawili.

Nashukuru kwa mawazo mkuu.

Ahsante.
Km ni hivyo usiifunge,Bali fanya km ambavyo mjumbe ameshauri.Mwekee restrictions za kutosha.
 
Habari za jumapili wanajamvi.

Niende Moja kwa Moja kwenye mada inayoniumiza kichwa mpaka nakosa amani ya moyo kwa muda wa week sasa.



Ahsante.
Ukiona mkeo hasumbuliwi sumbuliwi na wanaume wengine, ndugu, jua ulilamba garasa. Maadam anasumbuliwa basi atakuwa na viwango vya FIFA. Wacha kazi iendelee ila mbane bane asichepuke. Pia mdau upunguze wivu.
 
Ni vile unajiweka na ndivyo itakua. Mblna tunafanya biashara miaka sasa na hakuna tofauti kwny mahusiano?.yani mimi huwa sitaki mazoea ya kijinga na huwa straight kwny point nampa mtu ukweli wake akinuna anune akiendelea kuja aje tunaheshimiana. Sio kumchekea mtu kisa mteja mpk akugande kama ruba No. So ni vile mkeo alikua anawachekea chekea.
 
Ni vile unajiweka na ndivyo itakua. Mblna tunafanya biashara miaka sasa na hakuna tofauti kwny mahusiano?.yani mimi huwa sitaki mazoea ya kijinga na huwa straight kwny point nampa mtu ukweli wake akinuna anune akiendelea kuja aje tunaheshimiana. Sio kumchekea mtu kisa mteja mpk akugande kama ruba No. So ni vile mkeo alikua anawachekea chekea.
Mkuu kwa maelezo ya jamaa huyo mke hakua mpambanaji kama ilivyo kwa wanawake wengi wenye misimamo mikali hata kama ni wazuri, huyu yeye alikua goalkeeper akawekwa huru sasa hapo lazma awe na kiwewe cha uhuru tu, na kuna uwezekano akapokea mashauri mengi tu bila hata kuyachambua.

Mi namshauri mwamba aweke mtu kwenye hiyo biashara, yeye na mkewe wawe wasimamizi. Ama lah kama ataona jau kuajiri mtu basi awe ni mkaguzi mkuu wa hizo hesabu za mkewe. Trend ya biashara inaweza kukupa mashaka na ukiyafatilia ukapata jibu.

Kosa hapo ni kumpa uhuru uliopitiliza, hakuzoea hayo, ni mambo mapya kabisa kwake yaani ni kama vile form six wanapoingia chuo na kupewa boom(uhuru + pesa), lazma wengi wapagawe.
 
Huyu mama ni mtu mzima wamejuana hapo Kwenye biashara ila yeye ni hawa wanawake wa kiswahili.

Nimeshachukua namba yake natafuta muda niongee naye pia huyu mama.

Ahsante kwa ushauri mkuu.
Una hekima Sana! Ni kumpambania mke Safi sana
 
Mtafute mtu hawe anafanya kazi hapo kwa muda
 
Dah......huu use-ngerema siji kufanya.Yaani atoke akatoe chupi huko bila shuruti mi nijidhalilishe mbele ya mwnaume mwingine kuomba omba asimtie MKE WANGU?Kama kashindwa kuelewa nilipoongea nae si aende tu kwa amani?huku ni kujichoesha aisee!!
Siku ukioa utaelewa!
 
Habari za jumapili wanajamvi.

Niende Moja kwa Moja kwenye mada inayoniumiza kichwa mpaka nakosa amani ya moyo kwa muda wa week sasa.

Mimi na mke wangu tangu tufunge ndoa huu ni mwaka wa tisa . Hatukuwahi kuwa na migogoro mikubwa ingawa mikwaruzano ile midogo ilikuwepo.

Sasa katika kipindi cha miaka sita ya ndoa yetu nilimuweka tu nyumbani sikutaka ajishughurishe na biashara yoyote. Mwaka wa sita wa ndoa yetu nilipata ajali ya pikipiki iliyopelekea mimi kuvunjika baadhi ya viungo vya mwili. Hivyo nilikuwa admitted Muhimbili hospital kwa muda wa kama miezi 3 kabla ya kuruhusiwa.

Kutokana na uwekezeji wangu kwa kipindi chote hiki wakati naugua hatukuwahi kupata Shida ya mahitaji ya nyumbani. Baada ya lile tukio nikajiuliza hivi ikitokea nimefariki Huyu mama ataishije na watoto wangu. Nikamshirikisha nimfungulie biashara ili aanze kujifunza mbinu za utafutaji. Nilipopona tukafungua biashara ya kufanya miamala ya simu na kuuza soft drinks jumla na rejareja.

TATIZO:
Miaka mitatu ya hii biashara imeanza kuniletea matatizo Kwenye ndoa. Wanaume wamekuwa wanapiga simu mpaka juma pili Siku ambayo wanajua hafanyi biashara na mbaya zaidi kuna mmoja nilikuta SMS za mitongozo na wife alikuwa ameshaingia king. Sasa nilimtafuta yule kijana na kuongea naye ingawa alisema alikuwa hajui kama yule mke wa mtu tangu sasa hatomsumbua tena. Mke wangu yeye alijitetea kuwa alimwabia yule kijan kuwa yeye ameolewa lakini aliendelea kumsumbua tu.

Hivyo nilifunga biashara for a while nikitafakari nini cha kufanya.

NDUGU WA WIFE:

Hawa watu walianza kuongea maneno ya hivyo sana kuwa mimi sitaki maendeleo ya ndugu yao baada ya kuona sasa hivi ameanza kufanikiwa ndio nataka kumrudisha nyuma bila kuangalia kiini cha tatizo. Wengine mpaka wakadiri kwenda mbali na kusema wao ndio walimpa mtaji niliwauliza ni kiasi gani cha mtaji mlimpa wanasema laki saba. Niliishia kucheka tu kwa sababu hiyo lakini saba haitoshi hata kulipia kodi ya hilo eneo kwa mwaka.

NINACHOOMBA :

Wadau ninachoomba kutoka kwenu ni mawazo jinsi gani niweze kuliweka hili jambo sawa iwe kwa kufunga kabisa biashara yenyewe au vyovyote vile ili mradi ndoa yangu irudi Kwenye amani kama. Mwanzo. Mama mkwe amenikasirikia hivyo yeye sioni kama ni mshauri mzuri kwa mke wangu .

Mniwie radhi kwa maelezo marefu ila nitasoma kila comment ili niweze kupata suluhisho.

Ahsante.

Mwache afanye biashara, leeni watoto!
 
Kuna amani na utulivu. Inawezekana ndoa yako haikuwa na amani ila ilikiwa na utulivu sababu hukujua tabia ya mkeo. Tabia haina uhusiano na kumfungulia biashara au kushinda nyumbani. Ifahamu tabia ya mkeo, fanya maamuzi kulingana na tabia yake. Kufuga mke ndani hakubadili tabia.
Well said
 
Back
Top Bottom