Habari zenu wakuu, nisiwachoshe sana ngoja niende Moja kwa Moja kwenye maada.
Mimi na mke wangu tangu tuoane hatujawahi kuwa na dada wa kazi nyumbani zaidi ya miaka 6 sasa.
Mwishoni mwa mwaka 2024 mke wangu aliomba atafute dada wa kazi ili awe anasaidia kazi za nyumbani kwasababu yeye anatingwa na majukumu
Tulifanikiwa kumpata dada wa kazi na tukaanza kuishi nae tangu mwezi wa kwanza 2025 mpaka sasa, kwakifupi ni kwamba dada wa kazi yuko vizuri na hana tatizo kwenye kufanya kazi
MKE WANGU KABADILIKA KABISA BAADA YA KUPATA DADA WA KAZI
1-Mke wangu hapiki chakula, anamuachia dada wa kazi ndio apike, yeye kupika ni mala Moja Moja sana.
2- Mke wangu sasa hakaliki nyumbani yaani ni misele ya kutosha, anajitafutia sababu ili tuu akapige misele isiyo na jambo lolote
3- Uangalizi kwa watoto umepungua sana , mtoto wetu wa pili ana miaka miwili tuu lakini naona kabisa uangalizi wa mke wangu ni hafifu sana
4- Nyumba ikiwa chafu ataiangalia tuu hivyo hivyo Hadi dada wa kazi atakapo Fanya usafi, dada wa kazi akichelewa basi nyumba itaendelea kuwa chafu mpaka nipige kelele
5-jukumu la kuhakikisha watoto wamekula chakula yeye amemuachia dada wa kazi
Siku za jumamosi na jumapili ni siku ambazo yeye haendi kazini lakin Bado hataki kubeba majukumu yake kama mama japo kwa siku za weekend.
Nimewaza nimuondoe huyu dada wa kazi ili akili ya mke wangu ikae sawa